BIKRA YANGU (23)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Alijikuta kaingia mzima mzima mpaka ndani ya kibanda kile bila kujali na kumuinua mganga Yule kwa kumshika manywele yake kisha kumtupa pembeni huku akimshambulia na mateke, hakua yeye wakati huo alikua amejawa na hasira sana, alimfuata Mganga na kumtandika ngumi iliyo mpeleka mpaka chini chali akiwa vile vile uchi wa mnyama.

SASA ENDELEA...
Alimgeukia Heather ambaye alikua kama amechangayikiwa baada ya kumuona Enock mahali pale na kumzaba kofi zito lililomfanya arudi nyuma kabla ya kukaa sawa alimpiga kofi aina ya kelbu na kumzaba kofi lingine na kumfanya adondoke juu chali. Kitendo cha sekunde sabini Heather na Mganga Yule walianza kuvuja damu.

“umekosa nini ku*** la mama yako, umekosa nini, ku** wewe, Malaya una kuja unato*** na waganga yaaa…”

Enock alikua akitetemeka kwa hasira sana, hakuwahi kukasirika na kutukana matusi ya nguoni kama yale machozi ya hasira yalimlenga lenga, moyo wake ulimwenda mbio, na kufanya kifua chake kupanda juu na kushuka akihema kwa jazba nyingi!, alikunja ngumi na kumtwanga Heather ya mdomo alimvuta na kumtupa upande wa pili.

Alisogea kwenye vibuyu vilivyokua pembeni na kuvipiga teke kisha kumuendea mganga na kuanza kumtwanga vichwa.

“nita kugeuza uwe kunguru kijana, embu wacha wacha wacha!”

Mganga Yule alifoka na kuanza kuchukua vibuyu huku akiongea maneno yasiyo eleweka ila Enock alikipiga kibuyu kile teke na kuanza kumshambulia Mganga Yule, alivyoona hali ile isha kua tete kwake alibeba nguo zake na kutoa mbio ndefu,

Zahara alishafika tayari na kuanza kumshika Enock ambaye alikua akimpiga Heather kwa hasira ila alitupwa pembeni nayeye kupigwa kofi lililo mpeleka chini, hali ilikua isha badilika tayari upepo ulikua mchafu, hasira zilikua ziki mzidi sana Enock na kumfanya atetemeke kwa kitendo kichafu cha kumkuta mke wake akifanya mapenzi na mganga.

“Mume wangu nisamehe uta niua, uta ua mtoto aliye tumboni”
Aliongea Heather akiwa amepiga magoti analia sana.
“fuc*** you, keep quit mother fuc**”

Licha ya kuongea hayo yote bado aliendelea kumpiga Heather ila aliteleza kidogo, kitendo cha Enock kuteleza na kudondoka, hapo ndipo Heather alipata mwanya wa kushika gauni lake na kukimbilia gari lake lililokua nje, aliingia haraka haraka na kulitia funguo huku akimuonna Enock akija kwa nyuma akilikimbilia.

“leo ata nikoma, bado nina hasira nae, Yule mganga yuko wapi”?

Enock aliongea kwa hasira huku jasho jingi likimtoka laiti kama angekua na bastola angeshaua mtu pale pale, alivua shati lake na kubaki na vest huku akikiendea kibanda kile, aliona kibiriti na kuwasha moto na kuweka juu ya shuka na kibanda kile kuanza kuteketea na moto,.
“Enock punguza jazba, usichukulie hasira utakua una fanya makosa”

Kwa upande wa zahara alionesha wazi kujuta kwa kitendo cha kumwambia Enock ukweli uliosababisha fujo na kumpiga rafiki yake kipenzi kipigo cha mbwa mwizi,katika akili yake hakudhani kama mambo yange kua kama ivyo, hakuwahi kumuona Enock akiwa na hasira kama izo aliongea nae huku akiwa mwenye hofu nyingi sana.

“hapana nitamuuwa leo, bora usingenionesha”
“usifanye ivyo”
“nawewe una mtetea”?
“hapana”
“kumbe, au nikuzibue nawewe, kwanza ulisema nawewe ulikua una kujaga huku huyu mganga kakutia”?
“mimi, mimi hapana , mimi nilikataa”

Enock alimkata jicho kali Zahara huku mkono wake ukiwa juu ambapo angeushusha unge mpata juu ya shavu lake. alianza kutembea huku nyuma yake Akiwa zahara na shati la Enock mkononi, baadae walikutana na boda boda na kupanda sababu gari ile waliokuja nayo ilikua haina mafuta, waliliacha na

walivyo fika mjini Bagamoyo walitafuta taxi na safari ya kuelekea kwake kuanza, zahara alishuka Mwenge na Enock kubaki na hasira nyingi kooni,picha ya mganga yule kizee akiwa mchafu akifanya mapenzi na mke wake Heather vilizidi kujijenga ndani ya akili yake na kuzidi kupandwa na hasira ndani ya moyo wake!.

Alifika kwake na kufungua geti kwa nguvu zote ila alishangaa baada ya kuwaona polisi nyumbani kwake, ila hakuwasalimia aliingia mpaka ndani na kumkuta Heather akilia, alimvaa na kuanza kumpiga tena huku akizidi kumtukana, polisi wale walifika na kumshika Enock ambaye pia alianza kuwapiga baadhi ya polisi, hakukua na jinsi ya kumtuliza zaidi ya kutumia virungu wakimpiga miguuni na kumfanya akae chini.

“una jifanya bondia, jinga wewe, kwanza una kesi kubwa sana kisheria, alafu una pigana na polisi, umepiga mkeo tena ni mjamzito”

“embu naicheni, nyie wote wase**** niachie nimuuwe kabisa ili mkanifunge kihalali, Heather naomba utoke kwangu”

Enock aliongea huku akipigwa pingu kwa nyuma, cha kushangaza Heather alitabasamu na kumfanya Enock ashindwe kuelewa.

“mpumbavu nini wewe Enock, nitoke niende wapi, wewe ndo utoke, kwani hapa kwako”?

“jinga hili, kumbe lina lelewa alafu lina jifanya kidume”

Aliongea askari mmoja kwa kejeli.

Heather hakutaka kuongea mengi aliingia ndani kisha baadae kutoka na Makaratasi matatu na kuweka mezani.

“MIMI KWA AKILI ZANGU TIMAMU KABISA MBELE YA MASHAHIDI ZANGU NIME MUANDIKA MKE WANGU WA NDOA HEATHER ENOCK MWASHA KAMA MRITHI WA NYUMBA HII

ENDAPO NIKIFA KILA KITU ATARITHI YEYE PAMOJA NA WATOTO WANGU, MIMI ENOCK KWA MKONO WANGU NIMEANDIKA MANENO HAYA BILA KULAZIMISHWA NA MTU YOYOTE YULE “

Maandishi hayo yalisomeka juu ya karatasi hiyo yakiwa na mwandiko wa Enock, Aliitizama karatasi ile kiumakini sana na kuvuta kumbu kumbu za nyuma, hakukumbuka hata siku moja kama alishawahi kuandika kitu kama hiko, alicho kumbuka ni kua alimuhaidi angempa nyumba hiyo endapo atakapo jifungua, bado alizidi kuunga unga vitu kichwani kwake akijaribu kufikiria,

Chini ya karatasi hiyo aliona sahihi yake na kushindwa kuelewa nini kime tokea, moyo ulimwenda mbio na kujikuta anakaa kimnya na kushindwa kuongea lolote, nyumba kubwa aliyoghaarimia mamilioni ya pesa ilikua ikitaka kuondoka kirahisi!,
“Heather”!
“sasa nani atoke, askari mpelekeni kituoni, mumpige kisawa sawa, amenitesa sana, alikua akinipiga kila siku navumilia tu,”

Kwa hasira Heather alisimama na kumtandika Enock kofi la shavu kisha askari wale kuondoka nae na safari ya kituoni kuanza na kumuacha Heather akicheka kwa sauti sana!.

Kitendo cha fujo ile kutokea Kway aliamua kuwashika mikono kushoto Sabrina kulia kwake Catherine na kuwapakia ndani ya gari usiku huo bila kuongea chochote kile, macho yake yalionekana dhahiri kabisa ni mtu aliye kereka sana, na kufanya sura yake ijikunje kunje.. aliwasha gari na kuliondosha eneo hilo.
“kwanini umeamua kuniaibisha”?
“abee”!
“hujanisikia, Cate kwanini umeamua kuniaibisha vile, ndiyo nini kusababisha fujo”?
“anco sio mimi,”
“sio wewe nini,? Wakati niliona una msukumiza Yule mzee pale”?
“Anco alinifanyia kitu ambacho kilinikera hata unge kiona usinge kubali mimi nifanyiwe”
“kakufanya ninii?”
Sabrina mama yake mzazi alidakia huku akigeuza shingo yake na kumtizama mwanae
“Mama”
“kakufanya nini, kama sio umalaya wako,?”
“Mama, mimi sio Malaya”
“kaa kimnya, nita kuzabua sasa hivi, muombe msamaha mjomba ako!”
“anco naomba unisamehe,”
“sawa usijali”!

Gari lilizidi kutembea kisha baadae walifika posta chuo cha CBE na Catherine kushushwa chuoni hapo na kway kugeuza gari akielekea bunju ili akamshushe Sabrina kisha yeye akakae baa aendelee kunywa pombe, hakuona raha yoyote ya kurudi nyumbani, sababu kila aliporudi nyumbani alizidi kuikumbuka familia yake iliyo tekwa nyara, ambapo aliamini kua MKE WAKE Julia au Mama Natu ameuwawa kwa kupigwa risasi.

Alimfikisha Sabrina mpaka nyumbani kwake na wote kuingia ndani walipiga stori za hapa na pale kisha yeye kurudi ndani ya gari.!
“nimesahau simu yangu”

KWAY alijisachi mfukoni na kugundua kua alisahau simu yake ndani nyumbani kwa sabrina, alirudi ndani na kufungua mlango, ila aliangalia pembeni kwa aibu baada ya kumkuta Sabrina ametoka kuoga akiwa na kanga moja iliyolowa na kumchoresha umbile lake zuri lenye mvuto wa hali ya juu!.
“nimesahau simu yangu”
“hiyo hapo”.

Sabrina aliiichukua simu ile na kumkabidhi Kway ila katika kasi ya umeme aliuvuta mkono wa kway na kumuendea mdomoni na kuanza kumlamba lips zake huku mikono yake laini ikiwa nyuma ya shingo yake, aliendelea kumlegeza Kway huku wakizidi kusogea sogea mpaka mlango wa chumbani na wote kuingia huku wakiendelea kunyonyana midomo yao yaani denda na Sabrina kuzima taa, huku wakizidi kupapasana sehemu tofauti miilini mwao huku wakiwa wamegandana midomo yao, kilicho fuata hapo Sabrina alitupa kanga yake kule na kumvua Kway nguo hapo kila mtu alibaki kama alivyozaliwa na kuvunja amri ya sita juu ya kitanda huku kila mtu akimburudisha mwenzake usiku huo!.

“Catherine fanya haraka basi, anti yangu kanipigia simu tumsindikize kituo cha polisi, kuna sijui bosi wake ameshikiliwa, ameniomba nika msaidie kutoa maelezo yeye hawezi”

Alikua ni rafiki mwingine aliye itwa Suzi, walivaa na kumuaga Betty kisha wao kutafuta bajaji mpaka magomeni mapipa, baadae alikuja mwana mke mmoja mnene kiasi na kuwasalimia.
“Anti huyu rafiki yangu anaitwa Catherine, Catherine huyu ndiye anti yangu anaitwa Zahara, au mwite Anti Zuu”!

Baada ya utambulisho huo mfupi waliingia ndani ya taxi na safari ya kuelekea urafiki kituo cha polisi kuanza , Ndani ya dakika kadhaa walikua teyari wamesha fika kituoni hapo Urafiki na kumpa dereva taxi pesa yake ndani ya akili ya Zahara alimuonea sana huruma Enock hakutaka aendelee kukaa kituoni akijua hastaili kabisa,sababu alishakaa siku mbili teyari.

Walianza kutoa maelezo ambayo yalimfanya Catherine abaki kumuangalia Suzi machoni. Zahara alionesha hali ya kua mwenye wasi wasi mwingi sana sababu aliitwa kutoa maelezo ambapo alimuomba Suzi amsaidie kwa niaba yake, kutokana nayeye Alisha muelezea kila kitu.!

“huyu jamaa, jina lake lime nitoka alimkuta mke wake huyo ambae ni Heather kwa mganga wa kienyeji, akifanya nae mapenzi, kwa hasira akampiga vibaya sana kiasi kwamba akampasua na kumuumiza vibaya sana,”

Suzi alizidi kutoa maelezo hayo kiumakini huku askari huyo akimsikiliza kwa utulivu sana kabla ya kuyaandika maelezo yake.
“Beatrice”!

Sauti hiyo ili washtua wote waliokuwemo ndani mule na kumfanya Catherine ageuze shingo yake nyuma na kumuona mzee aliye kua na funguo za gari mkononi mrefu kiasi, alikua ni mzee Mwasha baba yake na Enock teyari kesha fika kituoni hapo baada ya kusikia mwanae kipenzi yupo kituoni, ivyo alikuja kwa nia moja tu kumtolea dhamana.

“Halloo, nani wewe?”

“Kway Mume wangu mimi Julia, njoo nisadie siyuwe nilipo, nimetoroka sijui nipo fasi gani, bananikimbiza!”

“Julia upo wapi,Natu, Natu upo nae?”

“mutoto nipo nae, kuja ni twala basi saa hii”

“wanakuya al… titititi”

Kway asubuhi ya siku hiyo akiwa anavaa shati lake huku kitandani akiwepo Sabrina bado amejifunika shuka sababu ya uchovu mwingi,

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)