SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Kway asubuhi ya siku hiyo akiwa anavaa shati lake huku kitandani akiwepo Sabrina bado amejifunika shuka sababu ya uchovu mwingi,SASA ENDELEA...
Alikua teyari amechanganyikiwa baada ya kupigiwa simu na mke wake, hakujua simu ile imepigwa kutokea sehemu gani,alivyojaribu kuipiga iliita bila kupokelewa kisha baadae ikawa haipatikani, moyo wake ulizidi kwenda mbio na kushindwa kujua ni wapi aanzie ili aipate familia yake, aliamini mke wake huko alipo ana pokea mateso na ana hitaji msaada wake,kama baba wa familia ilikua ni lazima afanye jambo.
“Kway”!
Sabrina aliita huku akikaa vizuri kitandani kiuchovu.
“naam”
“kwanini usifanye kama ulivyofanya kipindi kile ulivyofanya Na Loydah kumtafuta Marehemu Ramsey?”
“enhee nime kumbuka ngoja nimpigie simu jamaa angu yupo I.T anafanya kazi kampuni ya simu ya fabbycom”
Haraka haraka kway alitafuta namba za rafiki yake huyo huku akiwa mwenye mawazo mengi alimuonea huruma sana mke wake,alijua ni jinsi gani alivyo kua akiteseka huko alipo na ujauzito alioubeba ambapo muda mfupi alitakiwa kujifungua, baada ya simu ile kupokelewa upande wa pili kutoka kwa Victor Marton, alimtumia namba iliyo mpigia muda mfupi ulio pita kisha kuambiwa asubiri kidogo, aziingize kwenye kompyuta.
“MWENYE IYO SIMU YUPO TANGA LUSHOTO,
JINA LAKE ANAITWA REHEMA NASSORO”
“ASANTE VICTOR”!
Kway alitoka mbio mbio baada ya kujibu ujumbe ule na kubeba funguo za gari huku akimuacha sabrina akimuita ila hakutaka kumsikiliza, alichowaza yeye ni kuikomboa familia yake iliyokua ikipata sana shida, alitaka jambo lile alifanye mwenyewe bila kuwashirikisha polisi,alimkumbuka mtoto wake mdogo Natu mwenye miaka mitatu na roho kumuuma sana.aliendesha gari mpaka kariakoo ofisini kwake na kumkuta Hussein Molito.
“kaka niazime gari yako”
“Kway vipi”?
“niazime gari yako, nina dharura”
“embu kaa kwanza”
“sina muda wa kukaa,unaniazima huniazimi, niende kwa khalfani sudi”!
“poa funguo izo hapo”
Kway alimtupia funguo za gari lake kisha kuchukua za gari la Molito na kutoka nje mbio mbio na kumfanya Molito asimuelewe Kway kilicho kua kina mkimbiza.
Aliingia ndani ya landcruser vx na kulitia moto pale pale, aligeuza na nusura amgonge muuza maji aliye kua akiuza maji pembeni yake, hakujali wala kugeuka nyuma alizidi kukanyaga mafuta kwa lengo moja tu awahi Tanga Lushoto akiamini kua uwezo wa gari lile kukimbia ita mchukua masaa kadhaa kuliko vitz yake ndogo.
ALivuta mkanda na kuufunga vizuri kwa usalama wake huku akizidi kukanyaga mafuta na kufanya gari izidi kuchanganya, aliushika usukani kwa mikono yote miwili akiyatoa macho yake mbele akizidi kutoka mbio.!
Julia akiwa na Natu mgongoni mwake alizidi kukimbia asipopajua ndani ya msitu huo uliokua mzito wenye miti mingi na mabonde makali, huku nyuma yake akiwa anakimbizwa na watu waliokua na silaha za moto mikononi mwao, hakutaka kurudi tena alipo toka baada ya kupokea mateso huko alipo kua ametekwa na watu asio wajua,tayari alikua kesha choka tumbo likiwa kubwa lime mchosha sana huku akiwa na mtoto wake Natu mgongoni na kuamua kujificha ili akusanye nguvu nyingine,
Kitendo cha kukaa chini ilikua ni kosa kubwa sana la jinai pale pale jitu moja lilitokea na kumkamata na kuanza kurudi nae,.
“pumbavu,ongoza mbele, sasa ulidhani ungeweza kukimbia na huyo mtumbo wako?”
Julia aliongoza mbele akiwa amesalimu amri, ila alivyo fika mbele alijidondosha na kuinuliwa, katika akili yake alikua na mahesabu alivyo jidondosha alikua ameokota jiwe kubwa bila jitu lile kuona, kama umeme aligeuka na kumtwanga nalo kichwani na kufanya jitu lile lidondoke chini alimfuata na kuendelea kumtwanga na jiwe lile kichwani mpaka alivyo muona katulia anavuja damu,alichuka bastola iliyokua chini na kuzidi kusonga mbele, ilikua ni lazima afanye vile ili aokoe maisha yake na mtoto wake, akiamini kuwa mume wake yupo njiani anakuja sababu Alisha mpigia simu muda mchache uliopita.
“MAMA NJAA”!
Alilalamika Natu akiwa mgongoni, njaa ilishaanza kutafuna kuta za tumbo lake baada ya kukaa masaa mengi bila kuingiza chochote mdomoni,
“subiri tuta kula saa hii hii, chunga kwanza”!
Alizidi kusonga mbele, bila kujua anapokwenda mpaka giza lilipo ingia, ila kwa mbali alihisi miungurumo ya magari na kuzidi kusogea akiamini kua atapata msaada, alitokea bara barani na kuanza kusimamisha magari ili apewe msaada, haikuwa kazi rahisi kwa gari kusimama katika msitu huo wenye mlima sababu ulisifika kwa kuwa na majambazi, ivyo kila alipopunga mkono magari yalimpita mbali kabisa na kukoleza mwendo,
Alisha kata tamaa akiwa ameshika tumbo lake lililokuwa kubwa lililohitaji matibabu maalumu kwa wakati huo, ila yeye leo hii alikua porini akiteseka na mtoto wake mdogo Natu.alizidi kutembea pembezoni mwa bara bara akiwa amechoka sana.
“BADO KILOMITA 93 kufika Dar es salaam”!
Aliona kibao kilichoandikwa ivyo na kukaa chini, ulikua ni mwendo mrefu sana mpaka kufikia jiji la Dar es salaam
alizidi kuchanganyikiwa na kukata tamaa huku njaa ikizidi kumtesa, Natu alishaanza kulia akilalamika njaa ina muuma pia,
Magari yalizidi kumpita sasa tumbo lilianza kumsumbua la uchungu na kuanza kulia akigala gala chini, PRADO nyeupe ilimpita ila baadae aliliona likirudi kinyume nyume mpaka mbele yake kisha kioo cha mbele kufunguka na sura mwana ume kuonekana.
“Mama una tatizo, mbona upo hapa usiku huu”?
“ndiwo naomba unisaidie kuni fikisha mujini”
“unaenda wapi”?
“Dar es saalam,”
“hata mimi naelekea huko, ingia ndani twende”
Jamaa Yule alifungua mlango wa gari , Julia na Natu waliingia kisha kuondoa gari kwa kasi alimuonea sana huruma, shukrani alizotoa Julia hazikuelezeka kabisa, jamaa Yule aliye jitambulisha kwa jina la Baba Faraji alitoa mfuko wa mikate na kuwa kabidhi wale,
“merci(asante)!”
“wewe ni mtanzania”?
“hapana mimi natokea Congo”
“congo sehemu gani, mimi nimeishi sana Kinshasa pale, nilikua nauza madini ya almasi”
“mimi nime tokea Bukavu”
“sasa huku umefuata nini”?
“nimeolewa na bwana wa kitanzania”
“huku porini ulikua una fuata nini?”
“nili….”
Kabla ya kumalizia maneno yale ulisikika mlio mkubwa mithili ya bastola na kufanya hofu kutanda na gari kuanza kupoteza uelekeo wake, ila baba Faraji alikaza mkono wake na kuliweka gari sawa, ilikua ni pancha ya tairi la mbele na gari iyo kusimama pale pale porini,
BADO KWAY alikua barabarani akiendesha gari akimtafuta mke na mwanae alishaanza kukata tamaa sasa alishuka na kutoa picha ya Julia akiwauliza watu, lakini kulikua hakuna dalili yoyote ile ya kumpata,
Usiku sasa ulishafika na giza totoro kuingia lakini hakukata tamaa aliapia ni lazima arudi Dar es salaam akiwa na familia yake mkononi, akiwa ana endesha gari mbele yake aliona PRADO ya rangi nyeupe imepaki pembeni ambapo kulikua kuna msitu mzito,mbele yake alimuona mzee wa makamo akimpungia mkono kuwa asimame, alivyoangalia msitu ule aliona una tisha sana na kulikua hakuna usalama,alipunguza mwendo ili asimame ila baada ya kuweka mkono wake kiunoni alijikuta hana bastola yake na kukumbuka vizuri aliiacha chini ya mto chumbani kwa Sabrina, kwa hofu alikanyaga mafuta na kulipita gari lile bila kujua kuwa Mke wake alikua ndani ya ile prado,
“samahani naomba telefoni yako”
Alizungumza Julia kisha baba Faraji kutoa simu yake, Julia alibonyeza bonyeza namba za simu kisha kuiweka simu sikioni akimtafuta mume wake Kway.
“Uko wapi Julia, uko wapi Mama Natu, upo salama”?
“nipo fasi sijui ipi, nipo salama cheriee”
“kama upo na mtu mpe simu anielekeze mlipo”
Baba Faraji alipewa simu ile na kuanza kutoa maelezo wapi walipo, Na kumfanya Kway ageuze gari lake kurudi alipotokea, lakini baada ya kufika kwa mbali aliona vijana wengine wakiwa na piki piki wamewaweka chini ya ulinzi Julia na baba faraji,hakua na chaguo lingine zaidi ya kukanyaga mafuta na kuongeza mwendokasi wa gari, aliwa fikia watu walioshika bastola na kuwagonga na kuwafanya wadondoke upande wa pili, aliwasogelea na kupandisha matairi ya gari juu ya vichwa vyao kwa hasira kisha kufungua mlango kutoka nje,
Julia alimkimbilia mume wake kway kama mtoto mdogo ambaye hakumuona mama yake siku nyingi sana sasa alimuona na kumrukia nusura wadondoke chini. Alilia sana na kutokuamini kama amepona,
Kway aliwakombatia wote na kumbusu mwanae Natu na kumuendea mzee aliye kua pembeni akimshukuru sana.,
Waliliendea gari la Baba Faraji na kusaidiana kubadilisha tairi, kisha badaae Kway kuchukua familia yake na safari ya kurudi Dar es salaam kuanza, ila alivyokua anaendesha gari alimsikia mke wake akipiga kelele za uchungu huku akilitizama tumbo lake,
Macho yalizidi kumtoka kway baada ya kuangalia mapajani mwa mke wake. aliona damu nyingi ziki mvuja na nyingine kuchuluzika kati kati ya mapaja yake,mapigo ya moyo yalizidi kumwenda mbio, sababu kulikua kuna kila aina ya dalili ya mimba ile kuwa imeharibika!
“Julia, Cherie, Cherie. Mama Natu”
“tumboo, tumboooo , tumbo”!
Alilalamika Julia huku akipiga piga mapaja yake na kuzidi kumchanganya Kway aliyekuwa katika mwendo wa kasi sana spidi mia moja ishirini na kujisahau kuwa anaendesha gari, na mawazo yote kuhamia kwa mke wake huyo ambaye alikua akipiga kelele nyingi sana za uchungu!..
Mwasha bado hakuelewa kwanini Catherine yupo kituoni pale, bado alichanganua akili yake huku akimtizama cate jinsi alivyopedeza na mwenye mvuto ambao kila mwanaume aliye kamilika ilikua ni lazima umuangalie mara mbili.
“Beatrice,mbona upo hapa kuna tatizo gani,”?
“nimemsindikiza rafiki yangu,anti yake ana matatizo, na wewe je”?
“kuna kijana wangu hapa, ameshikiliwa na polisi nime kuja kumuwekea dhamana”
“pole sana”
“ahsante”
Kila askari aliye muona Mzee Mwasha alimchangamkia na haraka haraka kuanza kujipendekeza kwake sababu walijua lazima angewapa posho,
“namuomba kijana wangu basi”
Kila mtu alikua kimnya wakati huo akimtizama mzee Mwasha hata kwa Catherine pia, askari wale waliachana na Zahara na wote kuhamia kwa mzee Mwasha ambaye alitoa burungutu la pesa na kuwakabidhi askari wale,
Baada ya muda mfupi hawa kuamini mtu aliyetoka ndani akiwa amechakaa hana shati juu yake,akiwa amelowa damu macho mekundu sana, Kitendo cha kumuona mwanae yupo katika hali ile kilimshangaza sana,
Enock kitendo cha kutoka macho yake yalitua moja kwa moja kwa Catherine na kutoamini aliye muona mbele yake, moyo ulimwenda mbio na kuzidi kumkazia macho,
“Catherine”!
“Enock”!
“Enock”!
Zahara na Catherine walijikuta wakiita kwa pamoja jina hilo, Mzee Mwasha alishindwa kuelewa na kubaki kuwatizama wote wawili na kushindwa kuelewa mwanae amemjuaje mwana mke huyo na kumuita jina jingine ambalo yeye hakulizoea.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA