Notifications
  • MY DIARY (12)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...Niliamua kufanya ziara ili nijue pakoje na mwisho wa siku niliamini kuwa kutokana na umaarufu wa marehemu baba yangu isingekuwa kazi sana kulipata shamba lake..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilitembea kijiji hadi kijiji huku nikijaribu kuuliza kwa wenye viti wa mtaa kama walikuwa wakimjua marehemu Bura. Kwa kweli kazi ilikuwa ngumu sikuweza kuvimaliza vijiji…
  • MY DIARY (11)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA MOJATULIPOISHIA...Wakati akiongea maneno hayo mara mtarimbo ukaanza kusimama nikajisemeha nimeshakosea nilitakiwa niondoke nilivyoona kimelele tu, nikajua hapo lazima atanitafuuna bila huruma. Basi akaingia bafuni akachukua sabuni akajipaka ili kujisisimua ngoma isimame vizuri.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Yaaani nilichanganyikiwa na huko bafuni nilisikia maneno ambayo yalinichekesha…
  • MY DIARY (10)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMITULIPOISHIA...Nikamwambia Joyce ndo maana mimi nakupendaga. Nikamwambia “nitakuapa feedback ngoja nimpigie asije akaja na makufuli yake leo hii. Nikampigia baba mwenye nyumba eti kwa kujiamini kabisa akapokea nakusema “ Halow mrembo” Nikamwambia Yes mpenzi kitu ambacho kilimfurahisha sana..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuokoa hela ya vocha nikamwambia nimekubali ombi lako alafu nikakata…
  • MY DIARY (9)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TISATULIPOISHIA...Basi Dj wangu aliendelea na mautundu yake akaniwekea mambo ya pwani na hapo ndipo uvumilivu ulipomshinda akaja kunibambia na mimi sikuona haja ya kumbania kwa kuwa ni mali zake mwenyewe. Nilizungusha nyonga na kiuno mpaka nikachoka nikajitupa kitandani ili nipumzike. Nafsi yake ilikuwa imeridhika kwani hakutka tena penzi bali alichukua lap top yake na kuanza kunionesha picha na vitu vingine ambavyo vilinipa raha.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (8)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA NANETULIPOISHIA...Sijui hata haya maneno yalitoka wapi, fahamu zilinitoka na Ticha aliamua kuninyanyasa maana nilishajikojolea zaidi ya mara tano. Basi na yeye kwa kutafuta mbwembwe alianza yale mambo yao ya katerero, siunajua tena mwalimu John alitokea pande za Bukoba.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alinichezea sana na baadaye nilishangaa kukuta jamaa ameshaingiza kunako. Sikujielewa kwa…
  • MY DIARY (7)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA SABATULIPOISHIA...Kwaito zilivyonoga uzalendo ulinishinda nikajikuta na mimi nashuka ngazi kuelekea chini sehemu ya kuchezea.Nilizijua kwani shuleni tulikuwa tunazicheza sana hasa kwenye yale madisco yetu ya mwisho wa mwezi.John wangu alibaki juuu akiniangalia jinsi nilivyokuwa nikicheza vizuri.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Yeye alishindwa kushuka akiofika kile kitu kukaliwa na watu…
  • MY DIARY (6)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA SITATULIPOISHIA...Akanambia kuwa wamemwambia wapo East Africa Pub na tayari wamaeshaagiza mkuu wa mbuzi. Mmmmhhhh kusikia mguu wa mbuzi mate yalinijaa mdomoni. Basi kwa harakaharaka nikamwambia naomba niende niende nyumbani nikachukue viwalo vya club kisha nitawakuta hapo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alinambia mbona hizo nguo ulizofaa zipo poa tu wewe twende hivyo bhana si upo na…
  • MY DIARY (5)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TANOTULIPOISHIA...Akanisimamisha na kuanza kuiuliza maswali mengi yasiyo na maana huko akionekana kutojiamini. “samahani dada, sijui unaelekea wapi”? Nikamjibu dukani. Akavuta pumzi ndefu na kuniambia ok, nisaidie namba zako za simu. Nikamwangalia juu na chini nikwambaia nimezisahau na simu nimeiacha ndani nikirudi ndani nitakuletea..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Akaishiwa pozi akanambia,…
  • MY DIARY (4)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA NNETULIPOISHIA...Uchambuzi huu ulinigusa sana kwani hata mimi nilijihisi kuwa sikuwa na utando huo yaani bikira japo nilikuwa sijawahi kujamiana na mwanaume wa aina yeyote zaidi ya ile michezo ya utotoni ya kula mbakishie baba au ile ya kibabababa na kimamamama. Alianza kunishika mapajani na kunifanya nianze kusisimuka ajabu kwani japo alikuwa ni mwanaume mikono yake likuwa ni milani sana kama ya mtoto wa kike.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media…
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…

BIKRA YANGU (73)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA SABINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Hakutaka kupoteza wakati alisimama mpaka sehemu walipokuwepo Dorothea na Naomi.
“Habari zenu”
Alisalimia Enock na kumkataka jicho kali Dorothea aliyekua anatetemeka kwa hofu!

SASA ENDELEA...
KITENDO cha Enock kumuona Dorothea akiwa na Naomi kilimtibua sana akili yake,hakuelewa walijuana vipi isitoshe walikuwa wakicheka na kufurahi wote ki ujumla ilionekana ni watu waliofahamiana kwa kipindi kirefu.

“Karibu bosi”

Alisema Dorothea huku akitabasamu kuashiria kuwa kila kitu kilikuwa sawa lakini bado Enock alikunja sura yake,ki ukweli alimchukia Naomi na kila mtu aliyekuwa karibu yake, dalili zilionesha kuwa hata Dorothea angeenda kuchukiwa na Enock.

Mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea yalimfanya Naomi asiseme lolote aliwatizama tu na kukaa kimnya kabisa!

“inakuaje unaongea na adui yangu ambaye ni muuaji asiyestaili kuishi mna mikakati gani?”

“Sina mikakati naye yoyote ile, nimeamua tu kuja kumsalimia leo bosi,hata mimi ninamchukia kwa kitendo alichofanya ….”

“Hujajibu swali langu”

“Ndio naenda huko bosi. Ni hivi Naomi ni rafiki yangu tulizoeana sana kipindi cha nyuma sasa kuna mambo Fulani tunazungumza ya kawaida bosi”

Dorothea alizidi kumshawishi Enock ili asiweze kuhisi chochote kinachoendelea, hususani mipango yao.

Kitendo cha Enock kugundua kuwa Naomi na Dorothea ni ndugu kingesababisha kikwazo kikubwa na hawakutaka hilo litokee, ilibidi Dorothea ampumbaze na kumzuzua akijaribu kuibadili akili ya Enock taratibu sana, ni kweli alifanikisha hilo, uwaminifu wake na ukaribu wake ndiyo uliyonunua akili ya Enock jumla na kuachana na kwenda kuendeleza mazungumzo na Baba yake.

Hakuna walichozungumza zaidi ya kutafuta njia za kumnasa Catherine popote alipo ili mradi yupo hai, Mzee Mwasha alimuhakikishia mwanae kuwa Catherine ni lazima apatikane kama yupo kwenye sayari inayoitwa Dunia.

“Kama yupo Duniani hapa lazima apatikane,Nadhani sina haja ya kuongea mengi sana Enock, nafikiri unanifahamu kuliko mtu yoyote Yule”

Aliongea Mzee Mwasha kwa kujiamini.

“Nina hasira naye sana Dad!, sijui nimfanye nini”

“Usiwe na hasira hizo, mambo mazuri hayataki haraka wewe nenda, nadhani wiki ijayo tutakua wote uraiani huko, tutapanga lakini ibaki kuwa siri yako”

Maneno ya Mzee Mwasha yalimfariji kiasi kwamba alitabasamu na moyo wake kuwa mweupe, alijawa na furaha mno, alivyopita kwenye meza ya Naomi na Dorothea hakuwaona tena!

Karandinga lililobeba Wafungwa ishirini na tano lilizidi kusonga mbele usiku wa saa mbili kuelekea mkoani Mwanza,Huku nyuma yake likisindikizwa na Difenda zilizobeba askari kumi wakiwa na mitutu mikononi mwao kwa ajili ya usalama.

Baadaye Waliimaliza Chalinze sasa walikuwa wakiitafuta Morogoro Msamvu!

“Bwana Mapua, leo naenda kuonana na Yule kigoli mtoto wa kisukuma Mwanza nilikuwa nina hamu sana kuchaguliwa na hii safari”

“Inabidi namimi unitafutie kasichana kamoja kazuri sio unakula mwenyewe, nikwambie kitu Fupi?”

“Nambie”

“Mimi na utu uzima wangu wote huu sijawahi kuonja watoto wa kisukuma nasikia wanajua sana mapenzi”

“Kweli nakwambia wewe subiri ufike uwone”

“Wacha we”

“Ndio Mapua usifanye mchezo, nakumbuka huyo mtoto wa kisukuma nilimpa mambo vibaya mno,ki ufupi nilimpania,sema nayeye alinipeleka sana puta, Mtoto ana pumzi kama mcheza mpira”

Maongezi hayo yalifanyika ndani ya Difenda wakiwa katika msafara wa kuwafikisha wafungwa Mkoani Mwanza wakiwa katika mwendokasi!.

Lisaa limoja lizima walikuwa wakiitafuta Msamvu hapo walivuka na baadaye kuanza kupita Mbuga ya mikumi, Dereva wa karandinga alianza kushusha gia kidogo na kupunguza mwendo baada ya kuona kuna gari kubwa mbele yake lililobeba mafuta, tena limetanda katikati ya barabara, alipiga honi ili apite lakini gari hilo lilijongea mwendo wa kobe!

“Huyu jamaa mbona analeta mambo ya kihuni”

Alifoka Dereva wa karandinga lililobeba Wafungwa.

Ivyo ndivyo ilivyokuwa hata nyuma ya difenda kulikuwa kuna gari kubwa pia aina ya Canter likitembea taratibu sana kisha kupita mbele yao, bila kuchelewa watu saba walitoa nyuso zao wakiwa wamevaa ninja na mitutu mikononi, walianza kumwaga risasi wakishambulia difenda za polisi.

Askari walikuwa bado hawakujiandaa, haikuchukua hata dakika saba Diffenda zote mbili zilikuwa Porini zinawaka Moto kisha kuriamuru karandinga lisimame kwani wasingefanya ivyo polisi Wote wangeuwawa.

“Shukeni chini ya gari mlale kwenye majani haraka iwezekanavyo”

Askari walitii amri na kushuka ndani ya karandinga mikono yao hewani wakiwa chini ya ulinzi.

“Masela tumekuja kuwakomboa, kuanzia leo mpo huru kama vipi sepeni”

Kila mfungwa alifunguliwa, Mzee Mwasha tayari alikuwa huru ndio sababu iliyowafanya majambazi hao walifuatilie gari hilo, mipango ilipangwa tangu siku nyingi sasa ilitimia.

“Inukeni”

Polisi mmoja wapo alikuwa teyari amejikojolea kwa uwoga. Kilichosikika hapo ilikuwa ni milio ya risasi kisha majambazi kutokomea na mzee Mwasha kurudi Dar es salaam.

“Kakunguru safi sana. Wewe ni jembe”

Mzee Mwasha aliwapongeza vijana wake.

“sisi ndio wazee wa kazi,usicheze na sisi hii ni kazi ndogo kama ya kuuwa mbu ndani ya neti,kila kitu kitaenda sawa, tukifika mbele hapo tunatia magari kiberiti tunazama ndani ya ndinga ingine Mzee”
Mzee Mwasha alijawa na Furaha sana kurudi tena uiraiani hakuamini kabisa.

Taratibu za kumtafuta Catherine zilianza mara moja, picha yake ilipelekwa mpaka polisi wakisingizia kuwa ni jambazi ivyo akamatwe haraka iwezekanavyo,Enock alichukua wazo hilo kutoka kwa baba yake na kuzidi kumwaga pesa nyingi akitaka swala hilo lipelekwe mpaka CNN na Aljazeera, aliamini kupitia njia hizo hata kama Catherine angekuwa nchi gani angekamatwa tu, ndani ya wiki moja picha ya Catherine ilikua katika kila chombo cha habari ikirusha picha zake kuwa ni gaidi kutoka katika kikundi cha Al shaabab, ivyo alitafutwa kwa wudi na uvumba, mbali na hapo Enock aliweka kiasi cha dolla elfu tatu endapo watafanikiwa kumtia mikononi Mwanamke huyo.

Polisi waliingia kazini sasa na kuacha shughuli zao. Habari zake ziliruka nchi zote na kutapakaa dunia nzima kwa ujumla.

“Ndio namfahamu,anajiita Elizabeth”

“Wewe ulimuona wapi?”

“Mama Milanto Yule Mama muuza chakula”

“ una uhakika ndiye mwenyewe?”

“Asilimia elfu moja kwanini nidanganye wakati nataka hiyo midola”

“Ole wako tusimkute utajiweka kwenye matatizo”Polisi alisema.

Unoko huo ulitolewa na Ismigo alienda mpaka kituo cha Polisi mjini, baada ya kuona picha ya Catherine kwenye magazeti pamoja na Aljazeera. Taarifa za Catherine zilifika mpaka visiwani Madagascar na ndipo alipokuwa.

Askari watatu waliwasha magari yao wakiwa na Ismigo kwa safari moja tu ya kwenda kumkamata Catherine.

Uonevu ulitulia tabia hiyo ilikomeshwa na Catherine kila mtu alimuheshimu,lakini kila mtu alitaka kujua Catherine au Elizabeth ni raia wa wapi,hakuna aliyetegua kitendawili hiko hata siku moja!

Catherine alikuwa ni mwenye furaha muda wote,alishayazoea mazingira na kupata baadhi ya marafiki. Siku hiyo akiwa anapika na Mama Milanto walisikia muungurumo wa Magari walivyochungulia tu dirishani waliwaona askari tena wakiwa wana picha zake mikononi, hakuelewa ni kwanini, mpaka mmoja wa maaskari alivyotoa bastola na kumuweka chini ulinzi.

“Weka mikono yako juu binti upo chini ya ulinzi”

Askari alifoka huku akimsogelea Catherine karibu.

Ndoto za kuchapwa na Mama yake huku wakati mwingine akimkaba zilizidi kumtesa Enock kila kukicha, hakuelewa ni kwanini Mama yake ana mjia ndotoni na kumkaba kohoni tena wakati mwingine akimkimbiza na visu kutaka kumuuwa, hakuweza kupata usingizi wa raha mustarehe kama binadamu au wanyama wengine waishio nchi kavu na majini,kila usiku aliweweseka.

“Mom, usiniue tafadhali Mom nisamehe sana, nini nimefanya Mamaaa?”

Alikurupuka kitandani baada ya kuweweseka kwa lisaa limoja lizima, majasho yalilowanisha mwili wake, hakuwa na utofauti na mtu aliyemwagiwa ndoo ya maji.

Mapigo ya moyo yalimwenda kasi sana kama aliyetoka kukimbia riadha. Kilichomchanganya haswa ni baada ya kusikia maumivu makali sana shingoni, dalili zilionesha ni kweli alikuwa akikabwa na wala haikuwa ndoto.

Alipitisha mkono wake kwenye kitanda na kuwasha taa, alitizama huku na kule lakini hakuona dalili ya kuwa na mtu yoyote Yule kuingia chumbani kwake, kwani hata mlango wa chumba chake ulifungwa na funguo! Hakulala mpaka kunakucha.

Siku hiyo hakuamua kwenda ofisini wala kwenda kwenye vyombo vya habari ili kujua walifikia wapi kuhusu Catherine, alinyoosha mpaka kwa Shekh Mohamedi Omary aliyesifika kwa kutafsiri ndoto, huyu alizipata habari zake siku nyingi sana nyuma,japokuwa hakuwa na imani na watu hao kutokana na elimu aliyokuwa nayo lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda Magomeni Mwembe chai ili akajue nini maana ya ndoto hiyo inayomsumbua kila kukicha, Ndoto ilimtisha sana moyoni alihisi kuna kitu Fulani alitakiwa kukijua.

“Samahani ndugu”

Enock alimuuliza mpita njia Baada ya kufungua kioo cha gari alivyohisi amepotea.

“Bila samahani kaka”

“Naomba kuuliza”

“Uliza tu”

“Namuulizia Shekh Mohammedi Omary ni wapi?”

“Mbona ushafika, ni nyumba hiyo hapo yenye nguzo”

“Ahaa aise asante sana,sikuwa nina uhakika napo ndiyo maana”

“Basi ndiyo hapo”

Enock alisogeza gari mbele na kuliweka kando ya nyumba ya Shekh Mohammedi Omary kisha kushuka na kugonga geti jeusi,Ki ukweli alitaka kujua nini maana ya ndoto hiyo iliyomuanza muda mfupi kabla na kumfanya akose usingizi mnono!

“Karibu”

“Aaasalam Aelekuy”

Enock alimsalimia mwanamke aliyetoka amevaa ushungi na kuziba nywele zake baada ya kumfunguliwa mlango,

“Waalekuy Muislam, karibu sana”

“Samahani, nimemkuta Shekh Mohamedi”

“Ndio yupo pita ndani”

Ndani ya nyumba hiyo kulinukia harufu ya wudi na ubani.

Mwanamke aliyevaa ushungi aliingia chumbani kisha baadaye Shekh Mohammedi Omary alitokea, Enock alimtambua sababu humuona kwenye runinga mara kadhaa akiwa anatafsiri ndoto na kutabiri vitu mbali mbali, alisimama na wote kupeana mikono kisha Enock kuanza kusema shida yake kuhusu ndoto inayomsumbua, alitaka kujua maana yake.

“Bora umewahi kuja mahali hapa, maana ungeweza kufa hizi siku za karibuni”

Alisema Shekh Mohammedi kisha kusimama na kwenda kuchoma wudi, nyumba nzima ilijaa Moshi, alichukua karata zake kisha kuziweka mezani.

“Nipe mkono wako wa kulia”

Enock aliuweka mezani.Shekh Mohammedi alianza kuongea kwa lugha ya kiarabu na kumtizama Enock kwa macho makali.

“Hii ndoto imeaza lini?”

“ina wiki sasa”

“Mama yako anakupenda sana”

“Una maana gani?”

“kuna kitu anajaribu kukuonesha, kuna moja wapo kati ya haya mawili kuna jambo ambalo unataka kulifanya yeye halipendi au kuna watu wabaya wanataka kukuangamiza, tena inaelekea huyo mtu au hao watu ni wa karibu sana nawewe, kwenye ndoto huwa anasemaje?”

“Huwa ananikaba namuona analia sana anatoa machozi, haongei kitu”

“Basi siku akiongea ujue ndiyo unakufa,na ndiyo mwisho wako utakuwa”

Enock alistaajabu sana, alishindwa kuelewa ni mambo gani anaambiwa, ndani ya akili yake alishindwa kuchanganua pumba au mchele.

“Mzimu wa mama yako bado unakulinda inaelekea kuna mengi sana kakuepusha nayo na bado anakupigania”

“Unaweza kunitajia hao watu?”

“Mimi siyo kazi yangu hiyo, kazi yangu mimi nishaimaliza tayari”

Maneno ya Shekh Mohamedi Omary yalizidi kuukoroga ubongo wa Enock na kumfanya ayatoe macho yake akitafakari.

Mama Catherine kila kukicha yeye alilia mfululizo hakuamini kuwa leo hii Mwanaye anatangazwa kwenye vyombo mbali mbali kuwa ni Alshabab na alihusika kwenye mauaji mengi.

Aliumia moyoni na kusononeka lakini licha ya kulia sana alijua hizo ni njama za Enock na wala sio mtu mwingine, alimkombatia mwanaye Christopher huku akiwa mwenye machungu!

Hakuna siku ambayo Mzee Mwasha alifurahi kama siku hiyo ya kuwa huru mambo yaliyo mfurahisha ni mawili moja, kuwa uraiani mbili kumpata Catherine na Enock kiurahisi kisha baadaye Sabrina ili afanikishe zoezi lake la kutaka kuwauwa! Kuwauwa watu hao watatu kwake ilikuwa kama ndoto ya miaka mingi ambayo ilikuwa ni lazima itimie, hatimaye yupo huru na Catherine kutangazwa kwenye vyombo vya habari mbali mbali, alichukulia huo ndiyo ushindi tosha.

“Bwana Masawe,wiki ijayo itabidi niondoke zangu kwenda mbali nikajifiche kuna kitu nakisubiri kwanza hapa”

“Hakuna tabu wewe kaa hapa, hakuna hata mmoja atakaye jua upo mahali hapa”

Mzee Mwasha alijificha kwenye nyumba ya mchaga rafiki yake aliyemiliki magorofa mawili kariakoo.
Alifichwa gorofa namba kumi hapo Kariakoo Mtaa wa Gerezani, akisubiri tu Catherine akamatwe ili akamuuwe wakiwa pamoja na Enock hilo ndilo lilikuwa kusudi la kumfanya asubiri na kujificha Kariakoo Mtaa wa Gerezani.

Catherine Kidhirwa alikuwa chini ya Ulinzi mkali anasafirishwa kurudishwa nchini Tanzania ili akahukumiwe tayari, alikamatwa na kesi ya mauaji ili mkabiri, hakuelewa mambo yanayotokea!
Saa kumi ya jioni ndipo alipanda ndege na maaskari wawili ili kumlinda kisha kupaa mpaka Doha, hapo walichukua ndege nyingine iliyotuwa moja kwa moja Mwalimu Nyereere Jijijni Dar es salaam nchini Tanzania. Kitendo cha Ndege kukanyaga ardhi ya Tanzania Catherine alilia machozi alikumbuka mengi sana yaliyotokea akiwa Tanzania, mtu wa kwanza kumkumbuka alikuwa Mama yake mzazi kisha picha ya Enock kumjia hapo hapo!

Taratibu walianza kushuka ngazi za ndege mpaka nje, Waandishi wa habari walikuwa wengi wamejaa wakipiga picha za mnato sababu ya muhalifu aliyekuwa akitangazwa kukamatwa huko Visiwa vya Madagascar.

Watu wa Mwasha hawakucheza mbali walipewa amri ya kummaliza Catherine hapo hapo uwanja wa ndege mwalimu Nyerere kabla ya kwenda kituoni, aliamini kitendo cha Catherine kupelekwa rumande ingekuwa vigumu kumtia mikononi mwake.

Jerry na Tyson walipaki gari yao kwenye maegesho kisha kushuka kuweka viwamba kwenye bastola zao ili zisiweze kutoa milio.

Enock naye alifika kimnya kimnya, habari za Catherine kufika Tanzania alizisikia ivyo alitamani kumuona, alipaki Marced Benz yake kando na kushuka akitembea kwa haraka akifuata watu waliokuwa na kamera waandishi wa habari.

Kamera za mnato zilimulika kila wakati, Catherine alikua amefungwa pingu kwa nyuma kichwa chake kakiinamisha,taratibu alikiinua na macho yake kugongana na Enock aliyekuwa nyuma kabisa.
Moyo ulimdunda sana, alivyogeuka pembeni aliona mwanaume aliyevaa koti jeusi na Miwani,
alimkazia macho,alivyoangalia kulia kwake alimuona mwanaume mwingine mfupi pia amevaa miwani kisha wakapeana ishara.

Kengele ililia kichwani mwake kuwa kuna kitu kibaya kinafuata.

Ni kweli mawazo yake yalikuwa yana ukweli, alimshuhudia Mmoja wa wanaume waliovaa nguo nyeusi anatoa gazeti huku ndani yake kukiwa na bastola.

“Pyuu pyuuuu”

Risasi zilitoka kwa mlio wa chini bahati nzuri zilimkosa Catherine baada ya kuinama na kuwapiga askari wa nyuma yake,watu walianza kutawanyika huku na kule.Mambo yaliharibika.

“Shiit, Nimemkosa Catherine, mtafute hawezi kwenda mbali”

Alifoka Mwanaume mfupi mweusi huku akizidi kumtafuta Catherine.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

MWISHO

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

15 Bikra Yangu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni