SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Nikiwa ninaendelea kunywa juisi yangu kuna wasichana wawili warembo wakaja kukaa kwenye kitanda kilichopo pembeni yangu huku wakianza kuvua nguo zao kwa ajili ya kuogelea katika swimming pool hiloSASA ENDELEA...
Wakabaki na nguo zao za ndani na kujitosa ndani ya maji na kuanza kuogelea.Wakiwa wanaendelea kuogelea mmoja anayeonekana si mzoefu sana katika kuogelea akaanza ku-piga kelele ya kuomba msaada wa kuokolewa.
Nikanyanyuka haraka haraka na kuvua viatu na kuitoa wallet yangu yenye pesa pamoja na simu mfukoni na kujitosa ndani ya maji.Nikaogelea hadi katika eneo alilo kuwepo nikamsubiria maji ya mlegeze kwanza kwa sekunde kadhaa nikihofia enedapo nikimuokoa akiwa katika hali yake ya kuwa na nguvu anaweza kunizamisha na mbaya zaidi sehemu waliyopo katika swimming pool hilo kuna kina kirefu kwenda chini.
Nikamshika vizuri na kwenda naye njee na kumlaza katika ukingo wa swimming pool hilo huku nikianza kumminya minya kifuani ili atapike maji aliyo yanywa nikaanza kumpa pumzi kwa kumpulizia mdomoni kwake.Wahudumu wa kiume wa hotel wakawa tayari wameshafika katika eneo hilo na kunisaidia katika zoezi la kumtapisha msichana huyo huku mwenzake akiwa pembeni akilia
Baada ya muda kidogo akastuka na kila alipo kohoa akawa anayatapika maji aliyoyanj-wa.Nikawaachia wahudumu wa Hoteli waendelee na hudumu nyingine zaidi.Nikarudi katika sehemu yangu niliyokuwa nimekaa nikavikuta vitu vyangu vipo katika usalama kama nilivyo viacha.Nikawa na kazi ya kusubiri nguo zangu zikauke,Yule muhudumu aliye niletea chakula chumbani akanifwata na kunisalimi
“Pole mwaya kaka yangu”
“Asante”
Akaaki kimya huku akionekana amekosa cha kuzungumza na akabaki anajing’ata ng’ata vidole vya mikononi
“Vipi unatatizo lolote?”
“Apana kaka yangu”
“Basi chukua hii ukanywe soda”
Nikapatia elfu ishirini akazipokea ila kwa haraka haraka nikawa nimeitambua dhamira yake ni ipi.Akapiga hatua kama kumi akasimama na kurudi nilipokuwa
“Samahani kaka yangu sijui ninaweza kuipata nambaya yako ya simu?”
“Powa”
Nikamtajia namba yangu ya simu kisha akanibip na akaondoka kwa furaha akijumuika na wahudumu wengine waliokuwa wakishuhudia yule msichana aliye taka kuzama kayika swimming pool.Nikamuona Rahma akija kwa hatua za haraka eneo nililokaa huku akionekana kuwa na wasiwasi
“Baby upo salama?”
“Ndio mbona umekuja haraka haraka kiasi hicho?”
“Wee acha tu kuna rafiki yangu yupo hapa amenipigia simu na kuniambia umezama kwenye swimming pool yaani amenifanya mpaka hapa mapigo yangu ya moyo hayapo sawa”
“Amekudanganya kuna wasichana wawili walikuwa wakiogelea hapa mmoja akaomba msaada wa kuokolewa ndio maana na mimi nikamuokoa.Ila sikuzama”
“Pole sana mpenzi yaani bado nusu presha ipande”
“Imekuwaje huyo rafiki yako anijue wakati hujawahi kuniambia kwamba kuna rafiki yako anayatambua mahusiano kati yangu na wewe?”
“Hapana Sir sikutaka kukuambia kwani nilijua utakasirika ila ni rafiki yangu mmoja yu ndio nimemuamia kuwa wewe ni mpenzi wangu ila yeye amekuja huku na bwana yake”
“Rahma kuwa makini bwana isije ikafikia hatua ukasababisha nikafugwa si unajiju wewe bado ni mwanafunzi”
“Nimekuelewa Sir ila nakuomba unisamehe kwani sipendi ukasirike mpenzi wangu”
“Powa ila sitaki hii siri ivuje pale shule kwani itanigharimu sana”
Tukachagua eneo jengine la kwenda kukaa na kuanza kuzungumza mambo mengi juu ya maisha yetu huku tukisimuliana maisha ya nyuma.Nikaanza kumsimulia Rahma historia ya maisha yangu
“Kusema ukweli mimi nimezaliwa katika familia ya kimasikini mkoani Morogoro na wazazi wangu walifariki na kuniacha nikiwa na umri wa miaka kumi huku mdogo wangu anaye fwatia ni wa kike ambaye kipindi wazazi walipo fariki walimuacha akiwa na miaka saba.Kitu ambacho wazazi wetu walituacha nacho ni shamba la heka kumi pamoja na ka-jumba kamoja ka matofali ya kuchoma.Kutokana na uroho wa mali wa ndugu upande wa baba wakatupokonya shamba la mpunga tulilo achiwa mimi na mdogo wangu na wakali-uza
Hawakuishia hapo wakatufukuza katika nyumba ambayo tulikuwa tunaishi na mdogo wangu na kutokana ni kijijini na ilikuwa ni miaka ya nyuma hatukujua ni wapi kwa kwenda kushtaki.Usiku ambao sinto usahau ni usiku wa tarehe 24 mwezi wa 12 ambapo tulikuwa tunatoka na mdogo wangu katika mkesha wa krismasi,
Kutokana hatukuwa na makizi maalumu ya kuishi sisi kila sehemu kwetu ilikuwa ni kambi.Tukiwa tunajiandaa kulala nje ya duka moja lililokuwa kijiji cha pili kutoka katika kijiji chetu ambacho ndugu wa upande wababa walitufukuza na walituambia tusionekane kabisa katika kijiji hicho la sivyo watatufanyia kitu mbaya.Sungusungu wapatao wanne walituzingira na walinishika mimi na kunifunga kamba katika miguu na mikono kisha mdogo wangu wakambaka na kumuingilia kinyume na maumbile huku wakipokezana kwa zamu na kusababisha kifo cha mdogo wangu mbele ya macho yangu.”
Sikuweza kuimalizia story ya maisha yangu na nikajikuta ninalia kama motto mdogo mbela ya Rahma huku naye kwa kunionea huruma machozi yakaanza kumdondoka taratibu huku akijaribu kuninyamazisha kwa kunibembeleza.Rahma akatumia kama dakika kumi na tano kunibembeleza hadi nikanyamaza
“Eddy pole sana mpenzi wangu”
“Nimepowaa ila katika maisha hiyo ni hali ya kawaida na huwakumba wanadamu wengi”
Kutokana muda ulishakwenda sana tukaondoka na kuingia katika gari na safari ya kurudi Tanga mjini ikaanza
“Baby hivi unaweza kuendesha gari?”
“Hapana siwezi kuendesha.Alafu Rahma uwe unaniita Sir Eddy kwani siku unaweza ukajisahau shule na kuniita Baby mbele ya watu ikawa ni balaa jengine”
“Sawa usijali kwahilo na siku tukipata muda nitakufundisha gari sawa mpenzi wangu”
“Nitashukuru”
“Alafu Sir kuna kitu nitakuambia pale kitakapo kamilika”
“Huwezi kuniambia wakati huu?”
“Hapana nataka nikufanyie surprise”
Tukafika Tanga mjini na akanipeleka katika bustani moja inaitwa Forozani ambayo ina mjumuiko wa watu mbali mbali wanopata chakula na vinywaji huku wengine wakipiga story zao,Tukashuka kwenye gari huku nikiwa nimevalia kofia ya Rahma iliyo niziba uso ili hata kama kuna mtu anaye nifahamu isiwe ni rahisi kunitambua vizuri.
Rahma akaagizia chakula kikaletwa na muhudumu tukaanza kula.Tulipomaliza tukaingia tena kwenye gari na safari ya kwenda kwangu mtaa wa Chuda ikaanza,haikuchukua muda kufika kwangu.Rahma akalisimamisha gari sehemu ambayo alilisimamisha asubuhii nikashuka kabla hajafika simu yeke ikaita na akaonekana kustushwa na simu hiyo.Akaipokea na kuanza kuiogea nayo kwa upole huku akitumia lugha yao ya kiarabu.
Rahma akiwa anaendelea kuzungumza na simu kwa mbali nikamuona Mama Fe-ty(Fatuma) akija katika eneo la ninapoishi hokum akiwa ameongozana na mwanamke mwengine ambaye sikuweza kumtambua mara moja kwani bado wapo mbali kidogo na nilipo simama mimi
Rahma akamaliza kuzungumza na simu akashush kiio cha gari katika upande nilio simama mimi
“Baby wala siingii ndani hapa baba amenifokea kama nini kwa jinsi nilivyo chelewa”
“Sawa tutaonana kesho shule?”
“Powa.Nakupenda Sir Eddy”
“Hata mimi ninakupenda pia”
Rahma akawasha gari na kuondoka.Nikabaki nimesimama huku nikiwaona Mama Fety na mwenzake wakija nilipo simama
“Mambo Eddy?”
“Powa vipi?”
“Safi mida ya mchana nilikuja sikukuta ulikwenda wapi?”
“Kuna sehemu nilikwenda kufwatilia mambo yangu ndio ninarudhi hivi”
“Ahaa vipi chai ulikunywa”
“Ohhh yaani mwanao alipokuwa anaileta yaani nilikuwa ndio naondoka ikanibidi niiweke ndani na sasa hivi kama unavyo niona ndio ninarudi”
Nikamuona rafiki wa Mama Fety akimminya Mama Fety kiunoni kama anapeana ishara ila si-kujua ni ishara ya nini
“Karibuni ndani”
Tukaingia chumbani kwangu nikawakaribisha na kuwawashia video waangalie wanachopenda kuangali.
“Baby huyu ni rafiki yangu anaitwa Saumu…..Saumu huyu kama nilivyo kuadisia anaitwa Eddy ndio mahabuba wangu”
Utambulisho alio ufanya Mama Fety haukunifurahisha hata kidogo japo ninajitahidi kuweka sura ya furaha usoni kwangu
“Nashukuru kukufahamu Eddy”
“Na mimi pia nasg=hukuru kukufahamu”
Nikachukua Laptop yangu na kuanza kupangilia mada nitakazo fundisha shuleni siki itakayo fwata.Wakaendelea kutazama Video baada ya muda Mama Fety akanyanyuka kutoka katika sofa alilo kaa hadi kwenye sofa nililo kaa mimi.
“Baby”
“Mmmmm”
“Mbona upo kimya jamani hata huzungumzi na sisi?”
“Kuna kazi hapa nina ifanya si unajua kesho ni Jumatatu inanibidi kupangilia kila kitu cha ku-fundisha mapema ili kesho nisipate tabu”
“Utamaliza saa ngapi?”
“Kwani munataka kuondoka?”
“Hapana ila nilitaka kujua ni saa ngapi utamaliza kwani mimi na rafiki yangu tunataka tukupe-leke ukashangae shangae mji”
“Kwa hili best itakuwa ngumu”
“Kwa nini jamani?”
“Hap nilipo nimechoka kiasi kwamba nikimaliza tu hii kazi nalala ili kesho nisichelewe kazini”
“Jamani Baby si tunakwenda mara moja mida ya saa tano tano tunarudi”
“Yaani kweli kwa hapo nisamehe baby hembu tufanye siku nyingie”
“Mama Fatuma kweli shemeji Eddy anaonekana amechoka muache apuumzike kwani si yupo kila siku”
“Shemeji umeona eheeee”
“Haya bwana mumeamua kunishambulia watu wawili basi sina jinsi inabindi nikubaliane na nyini”
Nikashukuru Mola kwa shemeji Saumu kunitetea.Mama Fety akarudi alipokuwa amekaa awali na kuendelea kutazama video,baada ya dakika kumi wakaaga na kuondoka mimi nikashukuru Mungu.Nikamaliza kufanya kazi zangu nikaingia bafuni nikaoga na kupanda kitandani na kuaanza kuulazimisha usingizi huku kumbukumbu za
Maisha yangu ya nyuma zikianza kunijia akilini.Machozi yakaanza kunimwagika nilipokumbuka jinsi baba na mama walipokufa siku moja wakiwa shambani wakilima.Inasadikika kuwa radi ya kimiujiza iliwapiga na kuwaua na chakushangaza jua lilikuwa ni kali katika siku hiyo na hapakuwa na dalili yoyote ya mvua kushusha.Sura ya mdogo wangu ikaanza kunijia nikakumbuka kipindi mdogo nilipokuwa nina cheza naye hadi siku anafariki kwa kubakwa mbele ya macho yangu
Nikakumbuka jinsi nesi mmoja laiyejitolea katika kunisaidia akanipeleka katika kituo vha kulelea watoto yatima kilichopo Iringa ambapo nilipata fursa ya kuendelea na elimu yangu ya msingi na kufanikiwa kufaulu vizuri na kuendelea na eleimu yangu ya sekondari hada kidato cha sina na kufanikiwa kuingia chuo na kusomea ualimu.Na hapo ndipo nikaajiriwa Tanga Mjini na katika maisha yangu yote nilitokea kuwaogopa wasichana hadi Rahma aliponitoa uoga wangu siku mbili za nyuma.Kwa msongamano wa mawazo nikapitiwa na usingizi na kulala.
Nikastushwa nn sauti ya mlio wa saa yangu ya ukutani ikiniashiria ni asubuhu,Nikajiandaa na kwenda zangu shule kuwajibika.Nikafika shule moja kwa moja nikaongoza hadi ofisini na ku-wakuta baadh ya wanafunzi waalimu wakiendele na na maandalizi ya masomo yao tukasali-miana nao na kukaa katika sehemu yangu.Kendelea ya wanafunzi kukusanyika ikawadia kama kawaida yangu nikaenda kwenye mkusanyiko huo wa wanafunzi ambao mara nyingi waalimu tunautumia katika kutoa matangazo.
Wanafunzi wakiwa wanaendelea kuwepo mstaarini nikaliona gari alilo kuja nalo Rahma jana nyumbani kwangu.Akashuka mwana mama wa kiarabu huku wakiongozana na Rahma anayeonekana mnyonge kama mtu aliyetoka kupigwa muda mchache ulio pita.Wakapokelewa na mwalimu wa zamu na kuelekezwa katika ofisi za waalimu.Furaha yangu yote ikapotea nikajikuta nina shauku ya kutaka kujua ni kwanini Rahma ameletwa shule tena akiwa katka hali ya unyonge.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA