TANGA RAHA (6)

0
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Wakapokelewa na mwalimu wa zamu na kuelekezwa katika ofisi za waalimu.Furaha yangu yote ikapotea nikajikuta nina shauku ya kutaka kujua ni kwanini Rahma ameletwa shule tena akiwa katka hali ya unyonge
SASA ENDELEA...
Wanafunzi walipo tawanyika nikaelekea ofisini na kuwakuta Rahma na Mama aliyemleta huku wakiwa wanazungumza na mwalimu wa zamu

“Malimu hii toto kuwa jinga sana……yeye chelewa chelewa rudi nyumbani chelewa amka yeye leo fanya tia yeye makofi awai amka ndio lete mimi hapa shule”

Mama aliye mleta Rahma alizungumza kwa Kiswahili kibovu ila niliweza kumuelewa,Rama akawa ananitazama kwa macho ya kuuiba iba huku akiwa amenunu

“Sawa mama tumekuelewa ila mwanao si jeuri na tabia yake ni njema labda hiyo tabia ya ku-chelewa awe ameianza siku za hivi karibuni”

“Sawa malimu ila jana yeye danganya mimi na baba yake kwamab kwenda kwa nyanya yake ila nyanya yake dai yeye akukaa hata saa moja akaondoka hata jui alikuwa wapi na yeye rudi nyumbani saa tatu usiku”

“Rahma jana ulikuwa wapi?”

Mwalimu wa zamu alimuuliza Rahma na kunifanya nianze kuogopa kwani sikujua Rahma atajibu kitu gani kwani kili nilipomtazama usoni nikahisi ataitoa siri

“Sir jana mimi nilikwenda kwa bibi ila nikawahi kuondoka wakati ninarudi nikakuta kuna ajali ile barabara ya Mwahako basi pale nilitumia kama masaa mawili tukisubiri wagari yaliyopata ajali yatolewe barabarani…….Baada ya hapo nikaendelea na safari yangu….Nikiwa njiani gari ikapata pancha sikuwa na jinsi zaidi ya kumpigia fundi ninayemjua atoke huku mjini hadi sehemu mimi nilipo kufika kwanza akawa hana vifaa ikamlazimu arudi tena mjini ndio aje na kifaa cha kugungulia tairi za gari nililo kuwa nalo.Mpaka tunamaliza ni saa mbili usiku”

Uongo wa Rahma ukafanania na ukweli nikajikuta nikishusha pumzi kidogo nguvu zikaanza kunirejea.
“Jana nimemuelewesha baba akanielewa sasa sijui kwanini mama yeye amekuwa mbishi….”
“Malimu hii toto anza tabia ya vivu leo hadi amsha na makofi si kazi ndogo”
“Sawa mama hilo tutalifanyia kazi”
“Mimi malimu taka huyu kula bakora tano za nguvu kesho yeye menyewe atakumbuka wahi shule”
“Sawa”
“Taka ona mbele yangu wewe chapa hii toto zembe”

Mwalimu wa zamu akanyanyuka na kufungua kaati ambalo tunahifadhia fimbo akatoa fimbo moja ya mti wa mpera ambayo imekaukavizuri na kukaa katika kiti chake.
“Rahma chukua hii fimbo nenda pale kwa Sir Eddy akakuchape mimi mkono wangu unani-uma.Sir Eddy hembu nichapie huyo mualifu kwa niaba yangu”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwani tangu nianze kazi yangu ya uwakimu sikuwahi kumchapa mwanafunzi wa aina yoyote na mbaya zaidi mwanafunzi ninaye anza kumchapa ndio kiburudisho cha roho yangu.Rahma akanipa fimbo huku akinikonyeza
“Wewe kijana taka chapa Rahma fimo za nguvu usimlezee kabisa”

Mama Rahma alizungumza na kuzidi kuigopesha.Nikimtazama Rahma usoni ananiambia nim-chape kidogo kidogo kwa sauti ya chini sana ambayo haikuwa rahisi kwa wengine kutusikia huku sura yake ikiwa imejaa huzuni,nikimuangalia mama Rahma ninamuona jinsi alivyo na shauku ya kuona mwanae ninamchapa
“Wee weka mkono vizuri ukikwepesha ninafuta ninaanza upya”

Nilizungumza kwa kujikaza huku Rahma akionekana kuwa muoga wa kuchapwa.Akanyoosha mkono wake,Nikashusha fimbo ya kwanza kwa nguvu kwenye kiganja chake na ku fanya Rahma kutoa kelele ya maumivu na kuanza kulia
“Weka weka vizuri mkono wako”

Rahma akauweka huku akinitazama kwa jicho la hasira,Nikashusha fimbo ya pili ikiwa na jazo wa nguvu kama fimbo ya kwanaza.Rahma akavivikicha viganja vyake kisha akaweka tena huku akionekana kununa na sura yake kubadilika na kujawa na hasira.Fimbo ya tatu ikatua katika kiganjani Rahma hakuosogeza 

Kiganja chake,Fimbo ya nne na ya tano zote zikamwingia katika kiganja chake huku zikiwa na ujazo sawa.Akaushusha mkono wake akaniangalia kwa sekude kadhaa huku akinipandasha na kunishusha pasipo waalimu wala mama yake kuona kwani aliwapa mgongo kisha akaondoka sehemu yangu na kurudi alipokuwa amesimama mwanzoni
“Nenda zako darasani”

Mwalimu wa zamu alimrihusu Rahma akaondoka na kuniacha nikiwa ninajiuliza sijui nitatu-mia mbinu gani kumtuliza Rahma kwani tayari nimesha jichafulia C.V.Mama Rahma akasima-ma na kuja nilipokuwa nimekaa na kunifanaya nistuke kidogo
“Malimu wewe onekana upo serious na kazi yako.Omba wewe fwatii nyendo zote za huyu binti na ngoja patie wewe namba yangu ya simu.Chochote mbaya anafanya julisha mimi ”
“Sawa”

Mama Rahma akanipa namba yake ya simu kisha akatuaga na kuondoka zake laity kama ange-jua ameniachia msala wala asingenipa hata hiyo nambay yake ya simu.Nikabeba vitabu vyangu na kuelekea darasani kwa kina Rahma ambapo kipondi cha somo langi la Biology ndia cha kwanza.Nikamkuta Rahma ameegemeza 

kichwa kwenye meza huku rafiki yake akimbembeleza.Wanafunzi wote wakasimama kunisalimia ila Rahma hakusimama zaidi ya kubaki kama nilivyo mkuta.Nikafundisha nilichopamga kukifundisha katika siku hiyo kisha nikatoka darasani huku nikumuavha Rahma akiwa katika hali yake

Kabla sijafika mbali kutoka darasa la kina Rahma mwanafunzi ambaye alikuwa anambembele-za Rahma aliniita na kuja hadi nilipo simama
“Sir kuna mzigo wako nimepewa na Rahma nikupatie”

Akanipa kikaratasi pasipo mtu yoyote kuona.Nikaondoka na kwenda ofisini nikaweka vitabu vyangu kisha nikaelekea chooni ili niweze kukisoma kikaratasi hivyo kwa shauku.Nikafunga malango wa chooni nikakitoa kikaratasi nilicho pewa na kuanza kukisoma
{EDDY…..EDDY……EDDY}

Nimekuita jina lako kama lilivyo ili ujue nimekasirishwa na use**e ulionifanya.Wewe si mtu wa kuninyanyulia mkono wako na kunipiga mimi kisa umemuona mama yangu na ukajaa siifa hadi hilo bichwa lako likakaribia kupasuka.

Tambua nimekuokoa katika mengi nilikuwa sishindwi kuwaeleza wazazi wangu kuwa wewe ndio unaye nit***a na ndio hapo ungejua kuwa baba yangu ni mtu wa aina gani.Umeona haitoshi ukanichapa mafimbo yako hadi hapa kiganja kilipo kimevimba.

SASA WEWE SI UMEIANZISHA VITA BASI UMEIPATA NITAKUFANYIA KITU KIBAYA AMBACHO HUTOKUJA KUNISAHAU KATIKA MAISHA YAKO WEWE JANA SI ULINAIMBIA MDOGO WAKO ALIBAKWA NA KUFA MBELE YAKO SASA NA MIMI NITAHAKIKISHA NINATUMIA KIASI CHOCHOTE CHA PESA ILI NA WEWE UBAKWE MBELE YA MACHO YANGU NA WANAUME WEZAKO NA MIMI HIYO NDIO ITAKUWA MALIPO YANGU
BY:ONE ARMY LADY(msichna wa jeshi moja)}

Hadi ninamaliza kusoma kikaratasi nikajikuta mwili mzima ukimwagikwa na jasho huku mi-kono ikinitetemeka kama nimepigwa na shoti ya umeme.

Sikujua hata nifanyenye niaanza kumlamu mwalimu wa zamu ni kwanini hakumalizana na Rahma yeye mwenye.Nikarudi ofisini kila story iliyokuwa ikipigwa ndani ya ofisi hiyo na waalimu wengine wala sikuzielewa kabisa na nikajikuta msongamano wa mawazo ukinipelekesha puta
“Sir Eddy una tatizo gani?”

Madam Zena aliniuliza na kuwafanya waalimu wote kuniangalia wakisubiria jibu langu
“Ahhaa kichwa kina nisumbua kidogo nahisi ni homa”
“Fanya ukapime kwani mbu wa Tanga hawana masihara kabisa katika kunyonya damu”
“Sawa”
“Madam nimekuelewa”
“Eddy au timu yako jana imefungwa ndio umekosa raha”

Mwalimu mwengine alinitania na kuwafanya wengine wacheke
“Wee Sir Sm hembu muache mwenzako si unaona anaumwa….Mwaya Eddy ukizidiwa sema nikupeleke kwako”

Kauli ya mwalimu Zena ikawafanya waalimu wengine kugua na kuanza kucheka na wakaendelea kutaniana.Nikapata wazo la kwenda darasani kwa kina Rahma kwani muda wa mapumziko bado haujafikia.Nikamuomba mwalimu niliye mkuta akifundisha aniitie Rahma.Jibu alili nipa likazidi kunichanganya
“Rahma aliniomba ruhusa kama dakika 20 zilizopita kwa jinsi anavyo onekana anaumwa sana”
“Asante mwalimu”

Nikarudi ofisini huku mawazo yakizidi kuniandama sikujua hata nifanyanye.Nikakusanya viti vyangu ambavyo ni muhimu nikaviweka kwenye begi langu na kuomba ruhusa kwa mwalimu mku.Madam Zena akaniomba anisindikize kwa kutumia gari yake ndogo.

Sikuwa na kipingamizi zaidi ya kumkubalia.Nikamuelekeza hadi tukafika kwangu tukaingia ndani nikamkaribisha kinywaji Madam Zena taratibu akaanza kunywa
“Ehee Eddy kwako ni kuzuri mtu akiingia anaweza akasema umeanza kazi miaka mingi kumbe hata mwezi mwenyewe huna”
“Asante…”
“Unaishi na nani?”
“Peke yangu”
“Duu hongera sana ndugu yangu”

Simu yangu ikaingia meseji na namba iliyoleta meseji hito imeandikwa PRIVETE.Taratibu ni-kaanza kuisoma meseji hiyo

{NIPO NJE NAKUFWATILIA KILA HATUA NA HUYO MALAYA ZENA ULIYE NAYE NDANI KWA-KO NITAMUUA UKISHUHUDIA}

Nikatamani ardhi ipasuke nidumbukie.Nikazidi kuchanganyikiwa pale Madam Zena aliponiaga anataka kuondoka ili akawahi kipindi chake cha kufundisha baada ya mapumziko ya saa nne asubuhi
“Madam ninakuomba usiondoka please”
“Kwa nini Eddy wakati nimesha kuleta hadi nyumbani?”
“Na penda tu leo unipe kampan yako ya kukaa hapa kwangu nakuomba”

Madam Zena akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akatoa simu yake na kupiga kwa mtu ila si-kujua ni nani
“Sir Barongo”
“Nakuomba unishikie vipindi vyangu kaka yangu kama huto jali kidogo nimepata dharura”
“Nashukuru kaka yangu haya Mungu akipenda kesho”

Madam Zena akakata simu kisha akairudisha kwenye begi lake na kuniangalia huku aikitabasa-mu
“Sasaa hapa ninaweza kukaa kwa amani….Ehee mgonjwa una CD gani nzuri nzuri za movie”
“Kwa CD tu hapa utakesha”

Madam Zena akachukua makasha ya CD yaliyopo chini ya meza ya kioo na kuanza kuangalia kasha moja hadi jengine hadi akakuta kasha lililoandikwa PIRATE ON BLACK SEE akaitoa CD yake na kuiweka ndani ya deki kisha akarudi kwenye sofa na kukaa.

Madam Zena akaanza kuguna baada ya CD hiyo kuanza kwani imeshamiri mambo ya kikubwa yanayo onyeshwa live bila chenga
“Sir Eddy hivi hizi CD unazitolea wapi?”
“Kwa nini?”
“Huwa ninazitafuta ila sizipati”
“Kuna maeneo ya pale forozi karibu na benki ya NMB kuna jamaa best yangu anaziuza”
“Bei gani?”
“Elfu tatu”
“Basi kuna vijana walinipitishia wakaniuzia kwa elfu ishirini”
“Dooo wamekutapeli hao”
“Tena wamenitapeli sana kwani CD lenyewe lina scratch kama nini”
“Basi nitakutafutia”

Madam Zena akaendelea kutazama CD huku akionekana kunogewa kwa jinsi watekaji wa meli katika CD hiyo wakipeana mambo matamu,Nikatazama Wallet yangu na kukuta nina pesa ya kutosha.
“Zena ngoja nikanunue chakula cha mchana”
“Haupiki?”
“Sijisikii kupika”
“Lakini mimi si nipo ninaweza kupika”
“Utapika siku nyingine ila nakuomba kama mtu yoyote akigonga usimfungulie hadi usikie sauti yangu”
“Sawa ila ni kwanini?”
“Watu wa mtaa huu ni wasumbufu sana na wamesha anza kunizoea vibaya”
“Sawa au unaogopa vimanzi vyako vitakuja?”
“Sina manzi wala nini wewe fanya kama nilivyo kuambia……………Nikuletee kinywaji gani?”
“Kwanza unakwenda kununua nini….”
“Alafu sikukuuliza nikuchukulie chakula gani?”
“Mimi niletee chipsi yai na kuku nusu nikipata na castel mbili baridi utakuwa umeifanya siku yangu ikawa powaaa”

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)