TANGA RAHA (33)

0
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Tumbo likaanza kunikoroga kiasi kwamba nikaanza kuhisi kichefu chefu na kila nilivyo jikaza ili kukipotezea kisije nikajikuta kikiongezeka hadi mwishowa wa siku nikajikuta nikitapika hadi nikaanza kutapika vidonge vidogo vidogo vya damu iliyo ganda
SASA ENDELEA...
“Mama weee ninakufaa”
“Hufi ndio unasafisha uchafu hivyo endelea kutapika”

Bibi alizungumza huku akinipiga piga mgongoni na nikazidi kutapika hadi ikafikia kipindi nika-kosa cha kutapika zaidi ya kutema tema mate chini.

Bibi akachukua kikopo kidogo kilicho fungwa na kifuniko na kuanza kukitingisha sana kisha akakisogeza karibu na pua yangu na kukifungua na vumi jingi likatoka ndani ya kikopo na kuingia puani mwangu na kujikutani nikianza kupiga chafya kwa kiasi kwamba makamasi yaliyo changanyikana na damu damu yakaanza kunimwagika hadi ikafika kipindi zikakatika.

Bibi akaniletea chakula cha miogo ya kuchemsha na kuanza kunilisha taratibu na kuokana na njaa kali ikanilazimu kumuomba bibi aniongoze chakula
“Utakula jioni kwani inabidi usishibe sana ili dawa uliyo kunywa ifanye kazi vizuri mwilini”
“Kweli bibi”
“Ndio na utapona tuu jipe moyo”

Nikaendelea kuishi ndani ya kibanda cha bibi kwa skiku mbili mfululizo pasipo kutoka nje huku akiwa aninipaka dawa zake za asili hadi baadhi ya vidonda vikaanza kukauka kauBibi akanipa ruhusa ya kitoka nje kukitazama kijiji na akamuomba 

Kijana mmoja kunitembeza sehemu mbali mbali za kijiji.Wanakijiji wengi kila sehemu ninayo pita wakaanza kunong’onezana huku wakimuuliza maswali jamaa niliye naye kwa kutumia kilugha na jamaa akawa anawajibu vizuri
“Wanasemaje?”
“Wananiuliza kuwa wewe ni nani na ninawajibu kuwa wewe ni ndugu yetu”
“Si waliniona ile siku nimebebwa nakumbuka kama tulipia njia hii”
“Ndio ila achana nao kwani hichi kijiji watu wake tunawajua sisi wenyewe”
“Wana nini?”
“Wapo watu wema na wabaya na si kila anaye kuchekea usidhani anakupenda na kijiji hi-chi kina wachawi kama nini”
“Mmmmm
“Ndio na wamekuwa wakiyaangusa magari yanayo pita barabara kubwa?”
“Kwa nini wanafanya hivyo?”
“Ni roho mbaya tuu kwani unadhani mchawi akiamua lake anakuwa na roho nzuri...Tena ile nyumba pele ya yule mzee aliye kaa pale nje...Unaweza ukasema pale hawezi kutembea ila yeye ndio gwiji la wachawi na ndio anaye fuga majoka yanayo maliza ndama na mbuzi wa watu hapa kijijini”
“Eheee sasa kama munamjua si mukamuue na yeye?”
“Mmmm asikuambie mtuu ukiwa na lengo au wazo tu la kutaka kumuua huyo mzee ukienda kwake anapote mbele yako”
“Mmmm ulisema kuwa kuna barabara?”
“Ndio hiyo barabara inakwenda Tanga na Dar,Arusha”
“Kwahiyo siku nikitaka kuondoka ninaweza kupata usafiri vizuri”
“Ndio unapata.....Mmmm kuna nini tena?”

Jamaa aliniuliza swali ambalo nikashindwa kulijiu hii ni baada ya kuwaaona watu wakikikimbi-lia sehemu moja watoto,wamama na wanaume.

Ikamlazimu kumuliza kijana mmoja anaye onekana yupo kasi akikimbilia sehemu ambayo watu wengine wanakwnda
“Kuna gari mbili zimegongana na moja ni ya unga na mafuta ya kula watu wanawahi viroba vya unga na vindoo”
“Kaka twende”
“Ni mbali na hapa kwani bado sipo sawa ninajihisi maumivu”
“Nahisi ni hapo juu”

Tukaanza kutembea kwa mwendo wa haraka na tulishingwa kukimbia kutokana na bado mau-mivu kadhaa yametawala kwenye sehemu za mwili wangu japo nimevaa shati kubwa kiasi ila kitu kingine nikaofia kukimbia kwani jasho likinitoka ni lazia dawa niliyo pakwa itatatoka na jasho litapelekea pia shati kunasa kwenye vidonda.

Tukapishana na watu wakiwa wamebeba vindoo na viroba vya unga huku kila mmoja akijitahidi kubeba kwa uwezo ambao anauweza yeye mwenyewe kitu kilicho nishangaza hadi watoto wadogo nao wanajitahidi kubeba wanacho kiweza
“Naona leo neema imeingia kijijini”
“Wee acha tuu tuwahi na mimi nipate hata kijindoo na kiroba cha unga”
“Wahi mimi ninakuja taratibu taratibu”
“Hapo umenena ndugu”

Jamaa akachomoka kwa kasi na kutokana na watu ninao pishna nao ni wengi wanao toka na kuelekea eneo la ajali haikuwa ngumu kwangu kupotea.

Nikafika sehemu ya ajali na kukuta gari aina ya ‘Scan’i lenye tela la nyuma likiwa limeanguka kichwa chini miguu juu ambalo ndilo linashambuliwa na wanakijiji katika kutoa vindoo na viroba vya unga na huku mbele kukiwa na basi dogo la 

Abiria aina ya ‘Rosa’ likiwa halitamaniki kwa kubonyea na likiwa limemelala mtaroni kiubavu na damu nyingi za abiria zikiwa zimetapakaa kwenye eneo lilipo,IkanibIdi na mimi kwenda kusaidiana na watu wanao wachomoa abiria waliomo kwenye gari hili.

Nikajitahidi kumchomoa dada mmoja kupitia dirishani aliye funikwa kichwa kwa baibui lake na nikafanikiwa na kumburuza mbali kidogo na dari lao lilipo

Nikamfungua baibui lake kichwani na kujikuta nikistuka baada ya kumkuta ni madam Zena am-baye aliniaga kuwa anakwenda kwa mama yake.

Ukimya wake ukazidi kunipa wasiwasi kwani sikujua kama amefariki au amepoteza fahamu kwani hata hakuwa anahe-ma.Nikaanza kmminya kifuani kwake kama kuyastua mapigo yake ya moyo,

Nikiwa ni-naendela kumminya nikashuhudia jamaa wawili wakigombania kidoo cha mafuta huku mmoja wao akiwa na kipisi cha bangi mdomoni.

Wakaanza kupigana na ikamlazimu mwenye kipande cha bangi mdomoni kukitema pembeni huku kikiendelea kuwaka na ki-kaangukia kwenye mafuta ya pretroli yanayotoka kwenye tanki lililo pasuka la gari aina ya 

Scani ambayo yamesambakaa barabarani na ndani ya dakika mlipuko mkubwa ukatokea na kusababisha idadi kubwa ya watu wanao gombania viroba vya unga na vindoo vya mafuta kurushwa mbali na wengine kupoteza maisha

Moshi mwangi na harufu kali ya moshi wa mafuta aina ya Petrol ikatawala katika eneo zima la eneo rulilopo huku vilio vikianza kutwala kwa wale walio wapoteza ndugu zao kwenye ajali ya moto.Ikanilazimu kumsogeza madam Zena pembeni zaidi ili kuepuka kuunguo kwa moto unaosambaa kwenye hili eneo kwa kupitia upepo mkali.

Gari za Polisi mbili zikafika katika eneo la tukio na sikujua ni nani aliye wataarifu na baada ya muda gari za zima moto na gai ya wagonjwa ikafika katika sehemu ya tukio na kuanza kupakiza baadhi ya wagojwa mahututi ikiwemo madam Zena na wakawahishwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga iitwayo Bombo. 

Msongamano wa magari mengi yaliyo simama kutokana na ajali ikazidi kuongezeka na kusababisha msongamano mkubwa wa magari mengi yanayotoka mkoani na yanayokwenda mkoani.

Maiti za wanakijiji walio ungua katika mlipuko zikaanza kukusanywa eneo moja na nikajikuta nikitafuta sehemu nikisimama kutokana na kushindwa kuiangalia miili ya watu wengine kwa maana imeharibika kiasi kwamba inatisha.

Hadi inafika saa tatu usiku magari yakaanza kuruhusiwa kuendelea na safari baada ya magari yaliyo pata ajali kusogezwa barabarani.

Nikarudi kijijini na kukuta nyumba nyingi zikiwa zimetawaliwa na vilio kiasi kwamba hata raha ya viroba vya unga na vindoo vya mafuta ya kupikia ikawa imetoweka miongoni mwa wanakijiji wengi,Kutokana sikuwa mwenyeji 

Kwenye kijiji hichi mojo kwa moja nikafikizia kwa bibi aliye nihudumia kipindi nikiwa nimeokotwa porini,akanipatia chakula nikala na kwenda kuoga kasha nikarudi ndani na kumkuta akichanganya changanya dawa zake kama kawaida
“Unajisikiaje sasa mjukuu wangu?”
“Kdogo afadhali bibi yangu”
“Mshukuru Mungu kwa yale yote yaliyo tokea na ameweza kukuokoa hadi ukafikia kuwa na hali kama hiyo”
“Ni kweli bibi na vipi mbona hauendi kwenye misiba?”
“Mbona hiyo sio misiba mjukuu wangu”
“Sio misiba kivipi bibi?”
“Mjukuu wangu kwenye ulimwengu huu kuna mambo mengi sana ambayo wanadamu huwa tunayapitia na kuyafanya,Yakiwemo mazuri na mabaya”
“Ni kweli bibi ila sijakuelewa ni kwanini umesema kuwa sio misiba?”
“Watu hao hawajafa kilicho tokea kwenye hiyo ajali ni kiini macho tu ila watu wanao sadikika kufa kwenye hiyo ajali wote wapo hai”

Nikajihisi kama mwili ukiwa umesizi kidogo huku nikifikiria cha kumuuliza bibi kwa maana ninacho kisikia hapa ni kama vile nipo ndotoni vile na ikanilazimu kuamini ninacho ambiwa hapa ni kweli na wala sio ndoto
“Kwa nini bibi?”
“Kwa malezo zaidi nitakufwata usiku nikakuonyesha hao watu sehemu walipo”
“Usiku kivipi?”

Bibi akanyanyuka na kuingia ndani kwake na kuniacha na alama ya kuuliza huku mapigo ya moyo yakiaanza kunienda mbio hata hamu ya kulala ikaanza kunitoweka.

Nikatoka nje kwa kunyata na nikafanikiwa na kukuta bado wenye misiba wakiendelea kupiga makalee ya kuomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

Nikaanza kutembea kuelekea barabarani na kukuta na watu wengine wakiendelea kusafisha safisha barabara huku gari aina ya Rosa iliyo pata ajali ilinyanyuliwa na gari maalumu lenye winchi na kuwekwa barabarani
“Kaka hili gai lenu munalipeleka wapi?”

Nilimuuliza mmoja wa wafanyakazi walio kuwa wakijishuhulisha na jinsi ya kuinyanyua gari hii ya abiria
“Tanga mjini”
“Samahani kaka sijui ninaweza kupata japo kanafasi ka kujishikiza na hadi huku munapo elekea?”
“Kwani wewe unakwenda wapi?”
“Mimi ninakwenda Tanga mjini?”
“Sasa huku ilikuwaje ukaja?”
“Niliacha na basi niliingia porini kuchimba dawa kurudi ninakuta basi nililo lipanda likiwa halipo”
“Powa ngoja nizungumze na suka”

Sikuwa na ujanja ilinibidi kudaganya kwa maana pasipo kufanya hivyo ingekula kwangu na jamaa niliye zungumza naye akazungumza na dereva wake kasha akaniita na sote tukaingia kwenye gari lao kubwa na safari ikaanza huku ililivuta gari la abaria lililo pata ajali.

Japo bibi amenisadia ila kusema kweli alivyo niambia atakuja usiku kunichukua nikapoteza amani kabisa ya kukaa nyumbani kwake.

Ndani ya lisaa na nusu tukafika Tanga mjini na mimi wakanishusha maeneo ya Reilway na nikawashukuru na jamaa wakaelekea barabara ya sita anapoishi mmiliki wa gari hiyo.Nikakodi bodaboda japo mfukoni sina hata senti moja ikanipeleka hadi nyumbani kwangu.

Sikuwa na woga kutokana ninahisi kuwa baba Rahma anaamini kwa wakati huu nitakuwa ni maiti.Nikalikuta geti la nyumbani kwangu likiwa limerudishiwa na moja kwa moja nikaingia ndani kwangu huku nyumba yangu nikiwa nimeichungaza vya kutosha

Nikaaza kutafuta kikadi changu cha benki na kwa bahati nzuri nikiwa ninakagua kwenye mifuko yangu ya suruali nikakuta noti mbili za elfu tano tano kwenye suruali yangu ya jinzi,nikatoka nje na kumlipa boda boda na kufunga geti langu na kurudi ndani na moja kwa moja nikajitupa kitandani na kutokana na uchovu mwingi usingizi mwingi ukanipitia.

Nikaanza kuhisi hali ngumu kila nilipojaibu kuvuta pumzi nikajikuta nikishindwa kiasi kwamba nikaanza kutumia nguvu nyingi katika kupambana na kitu kilicho nikaba kooni ambacho sikioni na kadri muda ulivyo zidi kwenda nikajikuta ninazidi kukabwa,

Gafla bibi akasimama pembani ya kitanda changu huku akiwa amevalia kaniaki nyeusi huku mkononi mwake akiwa ameshika unyonya wa simba pamoja na kijikibuyu kidogo
“Eddy mbona ulinikimbia pasipo kuniaga?”

Nikashindwa kumjibu na kila nilipo mtazama sauti yangu haikuweza kunitoka kaisa nikabaki nikiwa nimemtazama

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)