TANGA RAHA (34)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Nikashindwa kumjibu na kila nilipo mtazama sauti yangu haikuweza kunitoka kaisa nikabaki nikiwa nimemtazamaSASA ENDELEA...
“Basi nimekuja kuitimiza ahadi yangu ya kuja kukuchukua”
Mwili mzima ukaanza kumwagikwa na jasho na katika siku amazo nimepatikana hii kwangu leo nimepatikana tena kwa asilimia kubwa na sikuona dhamani yoyote ya pete niliyo ivaa kunisadia,Akaunyosha mkono wake mmoja na kujikuta nikinyanyuka kitandani na pasipo kupenda.
Akaniamrisha kuzunguka kwa kutumia kidole chake kimoja cha mkono wa kulia na kujikuta nikizunguka zaidi ya mara saba kisha akanishika mkono na tukapiga hatua hadi kwenye kona ya chumba changu na kujistukia tukipita bila wasiwasi na tulipo tokea si nje kwangu bali kuliwa makaburini na nikakuta kuna chungu kikubwa kilicho zungukwa na watu walio uchi wakiwemo wakubwa na wazee,wanawake na wanaume.
Bibi akanipaka unga kwenye uso wangu na kuniambia kuwa watu hao itakuwa ni ngumu wao kuniona
Tukapita kati kati yao huku nikijitahidi kuchungulia kwenye chungu kikubwa walicho kizungukana sikuona ni kitu gani wanacho kichemsha,Tukasimama pembeni kwenye kaburi lililopo kwenye eneo ilo kisha tukaanza kushuhudia wale watu walio fariki kwenye ajali wakipita mmoja baada ya mwengine huku wakiwa wamepanga mstari mmoja kama wanajeshi walio tekwa huku mikono yao wakiwa wameinyoosha juu na moja kwa moja
Wakaenda mpaka kwenye moja ya kaburi lililo wazi na wakaanza kusukumwa na Yule mzee ambaya jamaa aliniambia kuwa ni mchawi kikongwe na karibia watu thelathini na saba wakadumbukia ndani ya shimo moja kisha wale wachawi wali zunguka chungu wakasimama na kuanza kucheza ngoma iliyo tibua vumbi jingi kiasi kwama hata sikuweza kuwaona vizuri
“Bibi pale wanafanyaje?”
“Mjukuu wangu pale wanasherekea kuwa wamewapata vibarua wapya”
“Vibarua vipya kivipi?”
“Ni wafanyakazi wapya wa kuwalimia kwenye mashamba yao na kuwafanyia kazi nyingine za utapeli kama kukopera”
“Kukopera ndio nini?”
“Kukopera ni ile hali kwamba mtu anakuja na kiasi kidogo cha pesa ila anapo kupa pesa yake na ukazichanganya na pesa zako kwa mfano dukani basi kuna misukule yao huwa wanaituma na kuja kuzichukua pesa karibia zote ikiwemo na ile pesa ambayo wamekupatia na huwa wakati wanazichukua huwaoni”
Nikabaki kimya nikiwa ninashangaa jinsi wanavyo tolewa mmoja mmoja kwenye shimo na kunyweshwa kitu kilicho kuwa kikichemshwa kwenye chungu a kila aliaye nywesha alionekana kupata shida sana japo sauti zao zilitoka mara moja tuu
“Ndio wananyweshwa nini pale?”
“Ile ni dawa inayo wakata kauli”
“Inayo wakata kauli kivipi?”
“Inayo wafanya washindwe kuzungumza kabisa na hata wakikutana na watu wana wajua hawawezi kuzungumza kitu cha aina yoyote”
“Bibi mimi nilisikia kwamba wanakatwaga ulimi?”
“Ndio walikuwa wakikatwa ulimi ila mambo yanabadilika kwani kwenye ulimwengu wa kawaida kuna mfumo wa kidigital basi hata katika ulimwengu wa wachawi kuna udigital kama wenu”
Nikatamani kucheka ila nikajikuta nikiwa nimeuziba mdomo wangu kwa kutumia kijanja changu,Shuhuli ikaendelea na bibi akaniomba kunirudisha nyumbani kwangu na kutokana kumekaribia kupambazaku.
Tukafika nyumbani kwangu na bibi akatoa kichupa kidogo kwenye kiuno chake na kunikabidhi
“Humo ndani kuna mafuta ambayo ukijipaka usoni mara tatu hata ukitembea mtu hawezi kukuona”
“Nikijipaka kwa mtindo gani?”
“Jipake vidoti vitatu kwenye paji la uso kidoti kimoja kwenye kila shavu utajipaka mara moja moja”
“Sawa bibi nimekuelewa”
Kama tulivyo toka mara ya kwanza ndivyo bibi alivyo toka kwenye chumba changu na kutokana na uchovu mwingi nikajitupa kitandani na kulala.
Mida ya saa tano asubuhi nikaamka huku mwili ukiwa umechoka sana kiasi kwamba nikabaki nikiwa ninajifikiria jinsi ya kuamka kitandani,nikakitazama kichupa alicho nip bibi jana usiku na kujikuta nikiachia tabasamu kubwa sana huku nikijifariji moyoni mwangu
“Kitanisaidia kumrudisha Rahma kwenye himaya yangu”
Nikanyanyuka kwa furaha huku nikicheka cheka na nikaingia afuni kwangu nikaoga na kurudi tena kitandani kwangu na kujifuta maji vizuri na kuvaa pensi kisha nikaingia jikoni kwangu na kukuta ile hali ya maunga niliyo jimwagia siku nikiwatoroka wazazi wa Rahma ikiwa vile vile.
Nikaanza kufanya usafi na ndani ya dakika kumi na tano mazingia ya ndani kwangu yakawa yamekaa safi.Nikajipikia uji na kunywa ili kuuweka mwili wangu vizuri kisha nikarudi chumbani na kuchukua kichupa changu chenye dawa na nikajipaka kama alivyo niambia bibi na nikatoka nyumbani kwangu na kuanza kutembea barabarani kwa majaribia
Kusema kweli hapa ndipo nikaanza kuamini kuwa uchawi upo na unafanya kazi kwani kila nilipokuwa ninapapita ikawa ni ngumu sana kwa watu kuniona na hata baadhi ya watu ninao wajua nilipo pita karibu yao hawakuweza kustuka wala kuniona.
Nikapata wazo na nikalifanyia kazi mara moja na sikutaka kulilazia damu.Moja kwa moja nikachapusha miguu yangu hadi kwenye jumba la kina Rahma na kukuta geti lao liliwa wazi na kuna gari moja imesimama katikati ya geti ikijiandaa kutoka,Dereva wa gari hii sikumjua kwani ni kijana mdogo wa kiarabu na anazungumza na mwanamke mwengine ambaye analifwata gari lilipo akitokea ndani
Nikapishana nao na kuzidi kushangaa kwani hawakuweza kuniona,Nikafiaka mlangoni na kutizama huku na kule na sikuona mtu na kwa tahadhari kubwa nikashika kitasa cha mlango na kuufungua kisha nikaingia sebleni na kukakuta kazee
Kale kaliko kuja sehemu niliyo tekwa kakiwa kameshika tama huku mkononi akiwa na picha kubwa iliyo tengenezwa kwenye jifremu kubwaa na ikionyesha sura ya yule mzee mwenzake aliye zikwa akiwa hai,Nikasimama karibu yake na hakuweza kuniona na kila nilipo mpitishia kiganja mbele yake wala hakuweza kustuka.
Mlango ukafunguliwa na akaingia baba Rahma akiwa ameongozana na daktari wa kiarabu na wakasalimiana na babu aliye shika piacha
”Mumefika wapi juu ya mdogo wangu aliye potea?”
“Bado tunaendelea kumtafuta ila tutampata”
“Bada usiniambie kwamba utampata nakupa siku yaleo nataka kumuona mdogo wagu”
“Lakini baba unavyo niambia mimi hivyo ni kana kwamba mimi ndio niliye mpoteza”
“Haswaaaa wewe ndio umempoteza mdogo wangu ingekuwa sio hilo jiroho lako baya wala haya matatizo yasinge fikia huku kwa maana mimi nilisema muacheni mtoto wa watu nyinyi mukaniona mimi mjinga umeona sasa hayo yote yamehamia kwa mwanao hapo alipo lala hajielewi wala kujitambua”
“Lakini baba hayo yote yametokea wapi?”
“Sitaki ujinga nasema namtaka mdogo wangu hapa leo la sivyo nitakuachia laana na wewe ukawehuke kama weu wezako”
Mzee alizungumza kwa uchungu huku machozi yakimwagika kiasi kwamba nikabaki nikiwa ninamuonea huruma na laity angejua kuwa mdogo wake amezikwa kikatili kiasi kile nahisi angejaza machozi sehemu nzima aliyo kaa.
Baba Rahma akaanza kupandisha ngazi za gorofani huku akiwa yupo na daktari na mimi nikaanza kuwafwata kwa nyuma na sote tukafika kwenye moja ya chumba na baba Rahma akaufungua mlango na akaanza kuingia ndani na ikanibidi nimpige kikumbo daktari na nikawa wa pili kuingia
“Vipi dokta mbona unayumba?”
“Ahaa nimejikwaa hapa”
“Pole sana”
Nikamkuta Rahma akiwa amelala kwenye kitanda kikubwa cha sita kwa sita huku pembeni kukiwa na mashine za kupumulia pamoja na mtungi mkubwa wa gesi,Macho yake bado hayakuwa na nguvu ya kufumbuka na wala hakuweza kujitingisha na yupo sawa na mfu aliye hai kwani kuhema kwake kwa mbali kuliidhihirisha kuwa hali yake sio mzuri kabisaa.
Daktari akaanza kumtazama tazama na kumpima pima kisha akamgeukia baba Rahma
“Hali yake kusema kweli bado ni mbaya”
“Sasa tutafanya nini dokta?”
“Kama nilivyo kushauri ni vyema ukampelea katika hospitali kubwa ili akapatiwe matibabu zaidi ya haya tunato mpa hapa nyumbani”
“Sawa dokta hilo nimekuelewa ila woga wangu unakuja hapa endapo madaktari watataka kujua kuwa ni nini kilicho mpa je itakuwaje?”
“Hilo ni swala la kuwahonga wao wasihitaji udhibitisho kutoka polisi wewe unapesa hembu tumi hizo pesa zako katika kuyaokoa maisha ya mwanao na usipo angali utampoteza kiurahisi”
“Sawa nimekuelewa ila…….Mmmmm”
“Mbona unaguna?”
“Nina mtihani kama ulivyo kuwa ukimsikia baba pale akifoka foka akimuhitaji mdogo wake”
“Kwani huyo mdogo wake ni mtoto?”
“Ni mtoto wapi wakati ni mtu mzima kabisa na mimi ninamuita baba kabisa anakaribia miaka 60”
“Duu sasa atapoteaje…..?”
Kabla hakazungumza chochote akaingia shangazi wa Rahma ambaye anajifanya ni mganaga na wote tukamgeukia kisha mimi nikapiga hatua za haraka hadi nyuma ya mlango na kujibanza,
“Vipi mbona unahema juu juu kuna nini?”
“Ngojeni kwanza”
Akaanza kunusa nusa ndani ya chumba huku akizunguka zunguka na akaipiga hatua hadi sehemu niliyo simama na akaiangalia sehemu niliyopo kwa muda huku macho yake akiwa ameyatoa kiasi kwamba nikahisi ananiona ila nikaendelea kujikausha kimya na nikawa nipo tayari kwa lolote na kama ataniletea shida ya aina yoyote nitamtandika ngumi kali itakayo mpotezea hata uwezo wa kunusa nusa.
Nikajianda kuivuta ngumi na kabla sijaiachia akawageukia baba Rahma na daktari
“Kaka kuna askari wamekuja na wapo sebleni na huyo baba usipo angalia ataanza kuzungumza hata mambo yasiyo husiana na atakacho ulizwa”
“Wee wapo wangapi?”
“Wapo wanne wewe nenda kazungumze nao”
“Ohhh Mungu wangu”
Baba Rahma akaanza kubabaika kiasi kwama nikaanza kumuona akitetemeka akatoka huku akiwafwatiwa na shangazi wa Rahma na wakamuacha daktari akiwa anamtazama tazama
Rahma,Simu ya daktari ikaanza kuita na kumfanya afungue mlango na kutoka ndani ya chumba na kwenda kuzungumza na simu nje.Kwa haraka nikapiga hatua hadi kitandani mwa Rahma na kumshika kifuani na kuyasikilizia mapigo yake ya moyo jinsi yanavyo na nikaanza kumuita
“Rahma……Rahma……Rahma”
Nilimuita huku mdomo wangu ukiwa upo karibu sana na sikio lake ila hakuweza kunisikia,Nikaelekea hadi mlangoni na kufungu mlango na kumuona daktari akishuka kwenye ngazi na nikachungulia kwa chini walipo kaa askari na wazazi wa Rahma na kuwaona wapo kimya huku wakisubiria swali la askari mmoja kujibiwa,
Nikarudi ndani na nikahisi Rahma hanisikii kutokana na dawa niliyo jipaka,nikaingia kwenye bafu lililopo ndani ya hichi chumba na kunawa uso kisha nikarudi kitandani kwake na kuanza kumuita karibu na lilipo sikio lake na nikarudia mara kadhaa na kumuona
Akiiunyanyua mkono wake mmoja wa kushoto huku akiyafumbua fumbua macho yake na nikazisikia sauti za watu wakija karibia na mlango na kunifanya nikimbilie bafuni na nikajifuta maji usoni na kukitoa kichupa cha dawa na kujipaka usoni na kusubiri kwa muda
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni