TANGA RAHA (48)

0
SEHEMU YA IROBAINI YA NANE
ILIPOISHIA...
Rahma ukazidi kuongezeka, kila anacho nifanyia ninakiona kipya kutoka kwake.Mechi ikatawaliwa na furaha na matusi ya nguoni kwa kila mmoja alipojisikia kutoa tusi lake aliweza kufanya hivyo ili mradi kuongeza utamu wa mechi yetu.Hadoi tunamaliza kila mmoja, akabaki akiwa na tabasamu usoni
SASA ENDELEA...
“Mume wangu, mbona umekuwa mtamu, umeutolea wapi?”
“Nikuulize wewe mke wangu, umekuwa zaidi ya kipindi cha nyuma”
“Ahaaa, ila asante sana mume wangu”
“Hata wewe asante mke wangu”
“Mume wangu, niliweza kuvumilia kwa kipindi chote ambacho wewe ulikuwa hospitalini, japo nilikutana na vishawishi vingi, ila Mungu aliweza kunisaidia hadi leo hii nakutana tena na wewe”
“Asante sana mke wangu, kwa maana niwanawake wachache sana wenye roho na moyo kama wako”
“Kweli mume wangu, mimi sikukutamani, nilikupenda na ninaendelea kukupenda.Kwenye maisha yangu sikuwahi kufikiria kumpenda mwanaume kama wewe, amini usiamini wazazi wangu wanakupenda tena sana, ile chuki kwao imekwisha kabisa”
“Kweli?”
“Ndio, hadi baba ametoa mamilioni yake kuijenga hii nyumba, ujue kweli kakupenda”
“Ehaaa, alafu nimekumbuka”
“Umekumbuka nini baby?”
“Naomba uniambie siri ambayo uliniambia inakusumbua?”

Rahma akanitazama usoni, sura yote ya tabasamu ikapotea nasura ya huzuni ikaaanza kuchukua nafasi yake, jambo ambalo likaanza kunipa wasiwasi wakujiuliza kuna kitu gani amabcho kimempata, Akaniachia mwili wangu na kutoa bafuni, ikanilazimu kumfwata nyuma.Sote tukakaa kitandani
“Mke wangu kuna, tatizo?”

Rahma hakunijibu na taratibu akaanza kumwagikwa na machozi, nikabaki nikiwa nimemtum-bua mimacho sijui ni kitu gani kinacho mwaga machozi
“Mume wangu, unanipenda?”
“Rahma ni swali gani ambalo unaniuliza, wakati unajua fika mimi ninakupenda kuliko kitu cho-chote kwenye maisha yangu”
“Eddy, sijui hata nianzie wapi?”
“Kivipi?”

Rahma akanitazama huku machozi yakiendelea kumwagika, hadi sura yake ikaanza kujawa na uwekundu fulani kwa mbali
“Eddy, nakupenda sana mume wangu, sipo tayari kukuona unakufa pasipo....”
“Pasipo kufanya nini?”

Rahma alizidisha kulia, na wasi wasi mwingi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na kubaki nikiwa nimemtazama mke wangu huku kigugumizi kizito kikinijaa.Rahma akakiweka kidole kimoja kwenye lipsi zangu, kisha akanipiga busu zito la taratibu sana kisha akaendelea kuzungumza
“Eddy, na uzuri wangu wote huu.Ila sinto weza kukuzalia mtoto, sina kizazi mimi”

Nikabaki nikiwa nimeduwaa, kiasi kwamba kuzungumza ninatamani, kukaa kimya ninatama-ni.Taratibu nikajikuta nikinyanyuka kitandani na kuanza kutembea tembea ndani ya chumba bila ya kuwa na kituo maalumu
“Baby, siku ambayo nilipata mimba yako ya kwanza.Olvia alinitoa kizazi changu, na aliniambia kwamba sinto zaa maisha yangu yote”

Rahma alizungumza huku akisimama, akanishika mkono na kunitazama machoni huku akiendelea kuniangalia.Kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga, sikuamini kama Rahma anaweza kukosa kizazi isitoshe mtoto wa kwanza hakuwa binadamu aliye kamilika
“Nisamehe mume wangu”
“Hupaswi kuniomba msamaha mke wangu, tumuombe Mungu”

Nilizungumza huku machozi yakinimwagika, taratibu.Rahma akanikumbatia na kulala kifuani kwangu taratibu kisha akanipiga busu jengine la mdomoni, ambalo nikashindwa hata kulipokea vizuri
Siku nzima nikashinda nikiwa ninamawazo, japo usoni mwangu nikawa na kazi ya kuilazimisha furaha yangu kujengeka ila nikashindwa kufanya hivi nilivyo tegemea.Hata chakula sikukila kwa raha kabisa
“Mume wangu, nakuomba usiwaze sana juu ya kuta kupata mtoto”
“Ahaaa, usijali baby”

Rahma akawa na kazi ya kunifariji
“Hivi kipindi chote ninaumwa maisha yalikuwa yapo vipi?”
“Baby nilipitia sana maisha ya shida, nilihangaika huku na huku kutafuta njia ya kuweza kuyaokoa maisha yako, kusema kweli nilipata tabu sana kutokana hospitalini waliniambia kuwa wewe ni.....”

Rahma akanyamaza na kuniangalia kwa macho ya kuiba kisha akanitazama tena
“Waliniambia kuwa mimi nini”
“Waliniambia kuwa wewe ni mfu aliye hai”
“Kivipi, mbona sijakuelewa?”
“Waliniambia kuwa, ulisha kufa siku nyingi”

Nikabaki nikiwa nipo kimya, kama nimemwagiwa maji ya baridi, swali la kwanza kujiuliza kich-wani ni mbinu gani waliyo itumi hadi mimi leo nipo hai.Nikiwa ninaendelea kuliwazia ninalo liwaza nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama nyuma ya Rahma huku macho yake yakimwagikwa na machozi ya damu

Nikabaki nikiwa nimeduwaa, pasipo kuzungumza kitu chochote, Olvie akaanza kutingisha kich-wa taratibu huku machozi ya damu yakiendelea kumwagika kwa wingi, akauinua mkono wake mmoja na kuanza kuniita taratibu, hapa ndipo nilipoiona mkono wake ukiwa umejaa damu nyingi.
“Walipo niambia kwamba umekufa, ikanilazimu kufanya kitu ambacho kingeurudisha uhai wa-ko, kutokana sikuhitaji uweze kupotea kiurahisi maishani mwangu, wakati bado sijaisha nawe vya kutosha”

Hata Rahma alicho kizungumza sikukitilia maanani kwa maani macho, na akili yangu zote zili-kuwa zipo kwa Olvia aliye simama nyuma ya mke wangu Rahma.Olvia Hitler akaunyanyua mkono wake wa pili juu na kuendelea kuniita kwa ishara kiasi kwamba nikazidi kuchanganyikiwa kwa vitendo vyake
“Niliamua kwenda, India kwa wanganga wanao tumia nguvu za kienyeji.Ambapo kuna mganga mmoja ambaye ni maarufu sana aliweza kunisaidia sana, hadi akaurudisha uhai wako”

Nikayahamishia macho kwa Raham, kisha nikayarudisha tena macho yangu kwa Olvia Hitler
“Mganga yule, alikupandikiza roho ya nyoka, na kila katikati ya mwaka na mwisho wa mwaka nilazima ugeuke kuwa.......”

Rahma alisita kidogo kuzungumza kitu anacho kizungumza na nikabaki nikiwa nimemtazama kwa umakini
“Utageukuwa kuwa nyoka mkubwa, na ninatakiwa kukupa watu wawili, uwale ili uweze kuon-geza maisha ya kuishi la sivyo utakufa kabisa na nitakukosa mume wangu”

Rahma alizungumza huku akimwagikwa na machozi, nikaanza kujitazama kiungo kimoja baada ya kingine kwa maana sikuamini kama hapa mimi nilipo nimekuwa na pumzi ya nyoka.Olvia Hitler akapiga hatua moja nyuma kisha akasogea hatua nyingine moja kushoto, hapo ndipo nikamshuhudia utumbo wake ukiwa umechomoza nje, na ameushika na mkono mmoja ili usiguse chini
“Eddy”

Olvia Hitler aliniita pasipo Rahma kuisikia sauti yake kwani, Rahma hakutikisika wala kugeuka nyuma.
“Nisaidie, tafadhali”

Olvie Hitler alizungumza kwa shida, huku machozi ya damu yakizidi kumwagika kwa wi-gi.Nikasimama kwenye kiti na kuanza kupiga hatua za kuelekea alipa simama Olvia Hitler, huku Rahma akibaki akiduwaa
“Eddy unakwenda wapi?”

Sikujiu swali la Rahma zaidi ya kumuacha akinishangaa, kabla sijamfikia Olvia Hitler, Rahma akanyanyuka kwa haraka na kinishika mkono
“Eddy, unakwenda wapi?”
“Eheee”

Nilizungumza huku macho yangu yote nikiyaelekezea alipo simama Olvie Hitler
“Baby, niangalie mimi”

Rahma akanigeuza kichwa changu na nikiwa ninamtazama yeye, akanishika mashavuni kwa viganja vyake vilaini na taratibu akajivuta, karibu yake na kunibusu mashavuni
“Eddy mume wangu, nimefaya hivyo kwa sababu ninakupenda sana.Sikuweza kuishi peke yan-gu, kama ningeishi peke yangu naamini hadi sasa hivi ningekuwa marehemu”

Rahma aliendelea kuzungumza huku machozi yakimwagika, Olvier Hitler akapotea kwenye uwepo wa macho yangu
“Eddy forgive my husband, I did not mean to get you to be so bad you are, But all is because of love”(Eddy nisamehe mume wangu, sikuwa na maana mbaya ya kukufanya wewe kuwa hivyo ulivyo, Ila yote ni kwasababu ninakupenda)

Rahma alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu, na kuuminya mwili wangu.Sikujua hata cha kumjibu zaidi ya mimi machozi kunimwagika, nikamnyanyua na kumbeba Rahma hadi chumbani kwetu.Tukapanda kitandani, kutokana na mawazo mengi kichwani mwangu sikuwa na hata hamu ya kumsogelea Rahma.Taratibu Rahma akanisogelea na kichwa chake kukilaza kifuani na sote tukapitiwa na usingizi mzito

Siku zikazidi kwenda mbele huku nikiwa ninafurahia maisha yangu ya ndoa nikiwa na mke wangu Rahma, nikaanza kusahau hata yale mambo magumu ambayo niliyapitia.Siku ya mkutano kati yangu na waandishi wa habari ikawadia.Waandishi wa habari wapatao ishirini kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakafika nyumbani kwangu huku wote wakiwa na furaha kubwa ya kuhitaji kuzungumza na mimi

Rahma akishirikiana na wafanyakazi watatu wa ndani, wakaandaa eneo zuri la kufanyia maho-jiano katika bustani yetu ya maua, iliopo katika eneo la jumba letu la kifahari, Rahma akanitolea suti nzuri iliyo nipendeza na kuniomba nivae, huku akinisaidia kuweka weka sawa sehemu za kola ya shati langu jeupe pamoja na tai nzri aliyo ichangua
“Mume wangu umetoka chikopa”
“Wacha wee”
“Eheee, ila kuwa makini kuna waandishi wa habari wadada wazuri wamekuja hapo sema tuu ndio hivyo tena”
“Acha wivu mke wangu”
“Wivu lazima, tena sana”
“Haya baby, wangu vipi wewe huojiwi?”
“Hapana, mimi nitasimama nyuma ya kamera zao”

Tukatoka, huku tuomeongozana na Rahma na kuwakuta waandishi wa habari wakiwa wamekaa kwenye viti wakinisubiria, huku kamera zao wakiwa wameziweka tayari za kuchukua kila tukio ambali litakalo tokea eneo hili
“Habari zenu”

Niliwasalimia, na wote wakaitikia kwa furaha.Nikakaa kwenye kiti changu ambapo mbele yake kuna meza ndogo ilio na maji pamoja na glasi, kisha na kuwatazama wote na wakatabasamu kwa mmoja mmoja
“Jamani karibuni, hapa ndio nyumbani kwangu na mpenzi wangu, mahabuba wangu, chocolate wangu, utamu wangu, pumzi yangu, ubavu wangu, chakula changu, mke wangu Rahma”

Maneno yote ya kumsifia mke wangu Rahma yakawafanya waandishi wa habari kupiga makofi kwa furaha
“Yaaa ninamependa sana mke wangu, na popote nikiwa nilazima nimtaje mke wangu kama mtu muhimu sana kwenye maisha yangu, japo hata wengine pia ni muhimu sana kwenye maisha yangu”
“Sasa ninakaribisha maswali”

Akanyoosha kidole muandishi wa habari mmoja na nikampa ruhusa akasimama huku akiwa ameshika kikaratasi kidogo mkononi mwake
“Kwa jina mimi ninaitwa Godwin ninatokea kituo cha habari ITV, kwanza ninashukuru sana bwana Eddy kwa kuweza kutujali na kutupa nafasi ya kuzungumza na sisi waandishi wa haba-ri.Kwana ninapenda kutanguliza pole kwa yale yote ambayo yalikupata, pia hongera kwa kuweza kujitoea kwa hali na mali katika kukuokoa mji wako”
“Swali ambalo ninapenda kukuuliza, ni jinsi gani uliweza kupambana na jola kubwa ambalo ku-sema kweli lilikuwa ni tishio kubwa sana kwa mji pamoja na dunia hii,ASANTE”

Godwin akakaa kwenye kiti chake
“Kwana, asante kwa pole ulizo nipa, nimezipokea.Hata asante pia nimezipokea.Niende kwenye jibu lako, kitu ambacho kilinisaidia ni Mungu tuu kwa maana kwa uwezo wangu wa kibinadamu nisingeweza kufanya kitu cha aina yoyote mbele ya joka hilo”
“Lilikuwa linafananiaje”

Dada mmoja aliniuliza na kuwafanya wezake kumgeukia
“Linatisha na lilikuwa na vichwa kumi na mbili”
“Kabla ya hapa nyuma, ninasikikia ulikuwa unamiliki majini, kuna ukweli wowote katika hilo”

Jamaa mmoja aliniuliza, nikamtazama kwa muda kisha nikamjibu

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)