TANGA RAHA (49)

0
SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Dada mmoja aliniuliza na kuwafanya wezake kumgeukia
“Linatisha na lilikuwa na vichwa kumi na mbili”
“Kabla ya hapa nyuma, ninasikikia ulikuwa unamiliki majini, kuna ukweli wowote katika hilo”
Jamaa mmoja aliniuliza, nikamtazama kwa muda kisha nikamjibu
SASA ENDELEA...
“Ukweli huo upo, nikweli nilikuwa ninawamiliki majini ila ni kutokana na kurisithwa”
“Ulirisithwa na nani?”
“Nikizungumza watu wengi hamuta amini ila, ndio ukweli wenyewe.Nilirithishwa na mfalme Suleiman”

Waandishi wa habari wakatazama
“Ila mfalme huyo si alifariki kipindi kirefu cha karne za enzi hizo, kabla ya kristo?”
“Ndio, ila yeye mwenyewe alidai kwamba hajafariki, ila watu wengi walizani kwamba amekufa”
“Ulikutana naye wapi?”
“Kwenye moja ya handaki la msitu ambao hadi sasa hivi siujui jina lake”
“Pia niliwahi kusikia kwamba mke wako alibeba ujauzito na kujifungua kiumbe cha ajabu”

Swala lamuandishi huyu wa kiume likanifanya nimtazame Rahma ambaye baada ya macho yetu kuyakutanishwa kwa pamoja akayaiinamisha kichwa chake chini
“Hapana, hakuwahi kubeba ujauzito”
“Kwa habari ambazo zinaendelea huko mtaani, kwamba wewe ulisha kufa siku nyingi?”
“Nani kakuambia?”

Sikujibu swali zaidi ya kumuuliza huyu muandishi wa habari, kwani swali lake limeanza kunikera moyo wangu
“Hii nikutokana na wajibu wa madaktari walio kupokea na kukupima vipimo vyote na kusadikika kwamba wewe ulikuwa mfu”

Nikakaa kimya kama dakika mbili, nikikosa jibu la kujibu
“Bwana Eddy?”

Muandishi mmoja aliiniita na kunifanya ninyanyue sura yangu kumtazama
“Sio kweli, laiti kama ningekuwa mimi ni mfua sidhani kama leo mungekuwa munanihoji, nina-hisi hao madaktari akili zao hazina akili”
“Je nasikia mke wako, alikuwa ni mwanafunzi wako?”
“Nani?”
“Rahma”
“Kwani kua ubaya?”
“Hapana”
“Basi ni ndio”
“Kutokana na kupendwa, sana na kujipatia umaarufu kwa wananchi wako wa mji wa Tanga, je unampango wa kugombania Ubunge kama wananchi wanavyo hitaji?”
“Siipendi siasa, na sidhani kama ninaweza kuwa mbunge”
“Je kuna ukweli wowote kwamba wewe umepandikizwa roho ya nyoka?”

Swali la muandishi huyu wa habari likanifanya niiname chini ya meza kwani nilijikuta nikikasi-rika sana jambo ambalo taratibu nikanza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wangu, ubaridi mkali ukaanza kunitawala, huku ukiambatana na mikono yangu kuanza kubadilika jambo lililo anza kuniogopesha

Nikastukia nikifunikiwa na taulo mgongoni, kuangalia vizuri nikamkuta ni Rahma ndio amenifunika na taulo ambalo limelowana maji, kidogo nikaanza kujihisi vizuri hata ubaridi mkali na mabadiliko kwenye mikono yangu vikaanza kuputea taratibu hadi nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida
“Unajisikiaje mume wangu?”

Rahma aliniuliza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza sana, ambayo sio rahisi kwa mtu yoyote kusikia
“Nipo powa”
“Twende basi ukapumzike ndani”
“Sawa”
“Jamani wapendwa Mr kidogo hali yake sio nzuri sana, ninawaomba mummpe muda kidogo, na mahojiano yataendelea jioni kwenye tafrija ndogo niliyo waandaliaa”

Rahma alizungumza na waandishi wa habari, taratibu akaninyanyua kwenye kiti, tarataibu tukaanza kuelekea ndani, Rahma kwa utaratibu akanilaza kitandani na kuniwashia feni lililopo pembeni ya kitanda changu
“Eddy vumilia, mume wangu”
“Mbona imekuwa hivi, sielewi?”
“Mume wangu pumzika kwanza nitakujibu baadaye”

Rahma alianza kunibembeleza taratibu, akaniacha na kwenda nje kuendelea na maandalizi ya tafrija fupi aliyo iandaa, nikaanza hihisi harufu ya tofauti ndani ya chumba changu, na taratibu nikaanza kunyanyuka kitandani mwangu, huku nikiongozwa na pua zangu, kunusa ni wapi harufu hiyo inapo tokea.Nikaanza kusikia vikopo vya kuwekea ,afuta vilivyopo bafuni vikianguka,
“Ni nini?”

Nilijiuliza kwa maana ndani kwat hakuna panya wala paka anayeweza kufanya uharibifu kama huo.Nikaendelea kutembea kwa umakini hadi bafuni na kukuta vikopo vyote vya mafuta na sabuni zikiwa chini, harufu nayo sikuihisi ndani mwangu tena.

Nikaanza kuokota kimoja baada ya kingine, nikiwa nimeinama nikastukia kuiona miguu ya mwanake nyuma yangu, kupitia kioo kilichopo mbele yangu ikiwa inavuja damu nyingi, nikasimama na kugeuka na kukutana na binti wa miaka kama kumi na nane akiwa anavuja damu mwili mzima

Macho yake ameyatoa kiasi kwamba anaonekana kubanwa na kitu kwenye koo lake,
“Ni…nisa..idie”

Alizingumza kwa shida sana kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeshangaa kwani sikujua ameingiaje ingiaje ndani kwet na istoshe sikujua ni kitu gani kilicho mpata
“Wewe ni nani?”
“Ni…saaa iii..dieee”

Aliendelelea kuzungumza kwa shida sana, nikajaribu kuuinua mkono wangu ili nimpe, nikajihisi uzito mkubwa sana kutoka kwenye mkono wangu
“Ed….ddy nisai…diee”

Nikaanza kuulazimisha mkono wangu wa kulia kunyanyuka ila nikajikuta nikishindwa, kuunyanya na zaidi nikabaki nikiwa nimesimama kama namba moja, Gafla upepo mkali ukaanza kutawala ndani ya bafu na kunirusha na kuniangusha chini.Nikamuona 

Olvia Hitler akiwa amesimama katikati ya upepo unaozunguka mithili ya kimbunga kikali, gafla nikastukia Olvia Hitler akimvuta binti huyo na kumuingiza katikati ya upepo na kupotea mbele ya macho yangu
“Mmmmm”

Nilibaki nikiwa nimeguna tu kwani sikuelewa kitu kinacho endelea kati ya mtoto huyo na Olvia Hitler ambaye kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa katika hali mbaya sana kwenye mwili wake, ila ujio wake wa sasa upo tofauti sana.Nikajinyanyua kwa msaada wa kishika kuta za kioo zilizopo bafuni mwangu, kisha nikaelekea chumbani na kujitupa kitandani

Hadi unafika wakati wa tafrija sikuwa na furaha moyoni mwangu, japo usoni mwangu ninajikaza kutabasamu mbele ya wageni waalikwa, akili yangu yute inakazi ya kumfikiria binti niliye muona bafuni mwangu
“Habari yako kaka Eddy”

Msichana mmoja aliye valia suti nyeusi alizungumza huku akinipa mkono
“Salama tu mambo vipi?”
“Salama tu, Mimi ninaitwa Rejina, nimuandishi wa vitau vya story kama huto jali ninaomba kuzungumza mimi na wewe”
“Sawa, tunaweza kuzungumza”
“Ombi langu kubwa ambalo ninahitaji kukuomba kwako ni kwamba, ninaomba niiandike story ya maisha yako ninaimani kitabu chako kitauza sana”
“Kwa nini umeamua au umependela kuandika kitabu cha maisha yangu na sichawatu wengine?”
“Wewe, umepitia mambo mengi sana kwenye maisha yako japo sisi watu tunatambua machache ila kusema ukweli wewe kama wewe utakuwa na mambo mengi sana ya kuniadisia na mimi nikayaweka kwenye maandishi na kuwa kumbukumbu nzuri hata kwavizazi vijavyo”
“Nipe muda nilifikirie hilo”
“Ila kaka Eddy, kuna kitu nakuona kinakukosesha raha?”
“Hapana, nipo sawa tu”
“Sawa hii ni kadi yangu inanamba za simu ukiwa tayari ninaomba uwasiliane na mimi”
“Poa”

Nikapokea kadi ya mawasiliano ya Regina na akanikumbatia na kuondoka zake, na kuniacha nikiangalia jinsi watu wanavyo sakata mziki, nikaanza kukisoma kikadi alicho nipa Regina na kukuta maandishi ya jina lake na kampuni anayo 

Ifanyia kazi, nikakuta namba zake mbili za simu za mitandao tofauti.Nikakiingiza mfukoni mwangu na kugeuka upende wa kushoto na kumkuta Rahma akiwa amenitazamakwa macho makali, baada ya macho yetu kukutana Rahma akaachia msunyo mkali nakuondoka kwa hasira
“Anataka nini naye huyu?”

Nilijiuliza swali mimi mwenyewe, sikutaka kumfwatilia sana Rahma zaidi ya kumuwazia msichana niliye muona akiniomba msaada bafuni.Nikatafuta kiti nakukaa, wakaja baadhi ya wageni waalikwa wakakaa na mimi na tukaanza kupiga stori za hapa na pale, wengine wakinipongeza kwa kazi niliyo ifanya

Gafla nikamuoma msichana aliye nitokea bafuni akiwa amesimama kwenye geti la kuingialia ndani kwangu,
“Samahani jamani, ninakuja sasa hivi”
“Sawa muheshimiwa”

Nikaanza kunyanyuka na kupita pembezoni mwa bwala la kuogelea walilo jaa baadhi ya wageni waalikwa wakiburudika, sikutaka kuyakwepesha macho yangu sehemu yoyote zaidi ya kumfwata binti aliyepo mbele yangu,huku akiwa katika 

Muonekano wake ule ule wa kuvunjwa na damu mwili mzima.Cha kustaajabisha nikaanza kumuona akiingia ndani, huku akipishana na watu wengine pasipo wao kumuona, nikazidi kuongeza mwendo wa kumfwatilia nikashangaa akielekea kweny vyumba vya chini akiacha kupanda vya ghorofani.

Akaingia kwenye moja ya chumba na mimi nikaingia pasipo kubisha hodi, gafla macho yangu yakakutana na Regina akiwa mtupu kama alivyo zaliwa huku mwili wake ukiwa umejaa maji, akionekana kutoka kuoga, 

Nikatazama kila kona ya chumba na sikumuona binti ambaye nilikuwa ninamfatilia, Regina hakuonekana kushangaa wala hukuficha sehemu zake za siri, zaidi akabaki akiwa ametabamu na kuanza kupiga hatua za kunifwata, gafla nikastukia mlango ukifunguliwa nyuma yangu na nilipo geuka nikakutana na Rahma akiwa anatushangaa
*Eddy ndio unafanya nini hapo?”

Rahma alizungumza huku akinitazama kwa hasira,
“Kwani wifi wewe, unatuona tunafanya nini?”
Regna alimuuliza swali Rahma, ambalo likazidi kumkasirisha Rahma
“Koma wewe, sijazungumza na wewe, nimemuuliza mume wangu”
“Ndio unijibu sasa, umetukuta tumesimama unababaika, ungenikuta nimemuweka kifuani mwangu si ndio un-gekufa”

Regna alizungumza kwa dharau wala sikujua ujasiri kama huu ameutolea wapi, Rahma akanipiga kikumbo, ni-kastukia akimvaa Regna na kumuangusha chini, na kuanza kupigana, nikabaki nikiwa ninashangaa, sikujua hata nifanye kitu gani, Regna akamgeuza Rahma na kumkalia tumboni mwake, na kuanza kumtandika vibao vya ma-shavu, 

Rahma naye hakubaki nyuma, akajikakamua hadi akafanikiwa kumuweka Regna chini ambaye yupo uchi, na kuanza kunzaba makofi ya hasira.Nikamkimbilia Rahma na kumuwahi mikono yake, na kumchomoa mikono-ni mwa Regna
“Rahma, tulia mke wangu, mbona unataka kuleta aibu kwa wageni waliofika hapa”
Nilizungumza huku nikiendelea kumshikilia Rahma kwa nguvu
“Niache nimkomeshe huyo malaya wako”

Rahma alizungumza huku akijikakamua kutoka mikononi mwangu
“Malaya mwenyewe, hivi unadhani utaweza kuwa peke yako, na ninakuambia ni lazima nimchukue huyo mume wako, kwanza mwanamke mwenyewe huna kizazi, unadhani mume wako ataendelea kukaa na mwanamke tasa kama wewe? Uyooooo”

Maneno ya Regna yalizidi kunishangaza kwa maana si kawaida ya mtu anaye jitambua kuzungumza mambo ka-ma hayo
“Eddy niachie, nimfundishe adabu huyu malaya, hawezi kunvunjia adabu ndani ya nyumba yangu”
“Rahma tulia, ninakuomba utulie mke wangu”
“Unamtetea huyo malaya wako eheee, niache sasa”

Nikastukia Rahma akinipiga kisukusuku cha tumbo na kujikuta nikimuachia, akamvamia Regna na kumuangu-sha chini, kwa haraka nikafunga mlango, kuepuka watu wa nje kusikia kitu kinacho endelea ndani ya chum-ba.Rahma akazishika nywele nyingi za Regna na kuanza kukibamiza kichwe chake kwenye kwenye sakavu yetu ya kisasa, 

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kumuona damu zikiwa zinasambaa chini, zikitoea kwenye kichwa cha Regna.Kwa haraka nikavuta Rahma kwa nguvu zangu zote na kumzuia kuendelea kumpigiza Regna kichwa chake chini

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)