TANGA RAHA (53)

0
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Sikumuelewa Eddy ana maana gani na kila nilivyo mtazama mwenzangu hakuwa na wasiwasi hata kidogo, gafla akasima-ma na kuanza kunifwata katika sehemu ambayo nimesimama, nikajaribu kurudi nyuma ila akaniwahi kuukamata mkono wangu, gafla nikastukia nikirushushwa na kujibamiza kwenye ngazi na giza kubwa likatawala kwenye macho yangu, na kukaa kimya
SASA ENDELEA...
Mwanga mkali ukaanz akupiga kwenye macho yangu, nikayafumbua macho yangu na kukutaa na sura ya Eddy akinitazama
“Karibu tena kwenye uhai, Eddy”

Nikajaribu kuinuka ila nikashindwa, nikajitazama pembeni na kukuta nikiwa nimefungwa kwenye kitanda, na mikanda migumu sana ambayo sio rahisi kwangu kunyanyuka, akaisogeza taa ambayo inanimulika usoni
“Unajisikiaje?”
“Vizuri”

Nikatizma pembeni na kukuta watu sita wali valia mavazi meupe wakiwa wamesimama, sura zao tofauti kidogo na bina-damu wa kawaida kwani vichwa vyao ni vikubwa kiasi na wanamacho makubwa, ila pia zao ni zakawaida na hata midomo yao ni yakawaida
“Eddy hao ni kina nani?”
“Hao ni madaktari ambao wamekufanyia, huduma ya kukutoa pumzi ya kinyoka na kukuwekea pumzi ya binadamu wa kawaida”

Madaktari hao wakatabasamu, na mimi nikaonyesha tabasamu, Eddy akazungumza nao kwa lugha ambayo sijawahi kuisi-kia hata siku moja kwenye maisha yangu.Wakanisogelea na kuifungua mikanda walio nifunga, Eddy akanipa mkono na ku-nyanyuka na kukaa kitako kitandani
“Pole Eddy”
“Asante”

Nilimjibu kwa sauti iliyo jaa furaha kwani, hali ninayo jihisi ni tofauti na pale nilivyo kuwa awali, macho yangu yakazungu-ka kwenye chumba kizima, ambacho kimejaa mitambo ya ajabu ajabu nisiyo wahi kuiona
“Eddy usishanga sana, hapa upo kwenye jengo la hospitali yetu sisi”
“Ni duniani kweli huku?”
“Hapana ila nitakurudisha duniani, huku ndipo ulipo mji wetu sisi ma elians”

Eddy akaanza kunitembeza kwenye maeneo ya jengo hili la hospitali lililo jengwa kwa vyuma vitupu, watu wake ni waaja-bu sana, kiasi kwamba muda mwengine nilijikuta nikiogopa
“Eddyunatambua kwamba imetuchukua muda wa mwaka mzima hadi wewe kurudi katika hali ya kibinadamu”
“Weee!!”
“Ndio, na haikuwa kazi ndogo kuifanya”
“Eddy asante sana”
“Usijali, ila kuna watu wezangu unatakiwa kwenda kuwapa shukrani”
“Kina nani hao”
“Utawaona”

Tukaingia kwenye moja ya jengo lenye mnara mrefu, tukaingia kwenye moja ya chumba na kukuta suti nyingi nzuri, Eddy akaniomba nichague suti nitakayo ipenda, nikachagua suti nzuri nyeusi, iliyo nipendeza sana.Tukatoka kwenye chumba na kuelekea kwenye majo ya lango kubwa lililopo humu ndani ya hili jengo na kuingia ndani 

Nikashangaa kukutana majitu makubwa yenye misuli iliyo kaza vizuri, japo sura zao ni zakutisha ila inanibidi kuwazoea tuu, tukapita katikati yao na kwenda kusimama mbele ya mtu mmoja aliye kaa kwenye kiti kikubwa cha dhahabu tupu
“Huyu ni mkuu wa jeshi la Ellians wote ulimwenguni na nibaba yangu mzazi”

Eddy alizungumza huku akiinama kwa kusujudia, ikanibidi na mimi kufanya hivyo, mkuu huyo akasimama na kutuamuru sisi kusimama.Akatusogelea na kunipa mkono mimi huku akitabasamu, nikampa mkono wangu na akaanza kuutingisha huku akitabasamu
“Karibu sana bwana Eddy”
“Asante”
“Kuna zawadi yako tumepanga kukupatia”
“Zawadi?”
“Ndio”

Akaniachia mkono wangu, akapiga kofi moja na watu wate wakapiga goti moja na kusujudia, tukabaki tukiwa tumesimama sisi watatu, mlango mmoja mkubwa ulio tengenezwa kwa dhahabu ukafunguliwa, kundi kubwa la wasichana walio valia mavazi 

Meupe wakatoka, na kuanza kutembea mwendo wa taratibu.Wakasimama mbele yangu na wote wakaipiga goti moja chini na akabaki mmoja wao akiwa amesimama na amevalia shele kubwa huku sura yake ikiwa imefunikwa
“Nenda kamfunue”

Eddy alizungumza, nikamtazam Eddy usoni, akaachia tabasamu pana.Nikapita katikati ya wasichana walio inama chi-ni.Nikasimama mbele ya msichana, taratibu nikamfunua kitambaa kilicho ziba sura yake, sikuamini macho yangu baada ya kukuta ni Rahma akiwa amepabwa vizuri sara yake
“Rahma!!”
“Eddy!!”

Tukakumbatiana kwa furaha huku machozi ya furaha yakianza kutumwagika kwenye sura zetu, hatukuona aibu yoyote taratibu tukaanza kunyonyana midomo yetu,
“Mmmm”

Mguno wa baba yake Eddy ukatufanya tuachiane huku sote tukiwa na furaha sana.
“Eddy mke wako tulimuokoa kutoka mikononi mwa mabinti walio kuwa wamemteka, na tulifanikiwa kuwaangamiza ma-binti wote na kwasasa mutaishi kwa amani na furaha kwenye maisha yenu”
“Asante sana baba”

Nilizungumza huku machozi ya furaha yakinimwagika usoni mwangu.Akatuomba tumsogelee sehemu alipo simama, akai-shika mkino yetu kwa pamoja kisha akamnyooshea Eddy mkono, Eddy akatoa visanduku viwili vidogo mfukoni mwake na kumkabithi baba yake, akatupa kila mmoja kisanduku chake na kutuomba tuvifungue.Macho yetu yakakutana na pete za dhahabu ambazo zinag’aa sana
“Munaweza kuvishana pete hizo”

Alizungumza, nikachukua pete iliyopo kwenye kisanduku changu na kumvisha Rahma, kisha Rahma naye akanivisha pete, shangwe na kelele za watu waliopo kwenye ukumbi huu zikatustua sote mimi na Rahma, maua mengi kutoka juu ya dari la jengo hili yakaanza kumwagika katika eneo zima la ukumbi.Machozi ya furaha yakaendelea kumwagika katika nyuso zetu zilizo jaa furaha.
“Nawatangaza rasmi kwamba mumekuwa mke na mume”

Baba Eddy alizungumza na shangwe zikaendelea.Eddy akatuchukua hadi kwenye moja ya kifaa cha kushangaza na kutom-ba tuingine sote wawili
“Jamani, ninawarudisha duniani”

Eddy alizungumza huku akikiwasha kifaa hicho, safari ya kwenda duniani haikuchukua muda sana kutokanana kifaa tuli-cho kipanda kwenda kwa mwendo mkali sana.Akatufikisha hadi kwenye eneo la jumba letu, tukashuka sote watatu na ku-kuta nyumba za taa zikiwa zimewashwa kutokana ni usiku
“Karibuni ndani”

Eddy alitukaribisha ndani, tukaingia hatukuamini kukuta nyumba yetu ikiwa imepabwa vizuri na kuwekwa vitu ambavyo kusema ukweli vimezidi kuipendezesha nyumba yetu
“Eddy na Rahma nninawatakia maisha mema”

Eddy alizungumza huku akiwa ametushika mikono yetu
“Muishi kwa amani na upendo, na watoto mutakao wapata siku moja moja nitakuwa ninakuja kuwatembelea”
“Hata wewe ninashukuru kwa msaada wako wote ulio tupatia”

Eddy akatukumbatia, akatuachia na kutoka nje, akaingia kwenye kifaa chake ambacho si kikubwa sana, na hakina mlio, akatupungia mkono wa kutuaga na kuondoka zake, nikambebe Rahma hadi gorofani kwenye chumba chetu, sote tukabaki 

Tukishangaa baada ya kukuta chumba kikiwa na kitanda kikubwa kilicho tengenezwa kwa madini ya dhahabu huku kwenye ukuta kukiwa na picha yetu kubwa iliyokuwa ikituonyesha jinsi tulivyokuwa tunavishana pete, sakau nzima im-ejaa noti nyingi za dola mimi za kimarekani
“Eddy hii picha imefikaje hapa?”
“Hata mimi sijui”
“Na hizi el..”

Sikumpa ruhusa Rahma kuzungumza chohota, nikawahi kuinyonya midomo yake na sote tukaangukia kitandani na kuanza kuchojoana nguo moja baada ya nyingine, kama kawaida yetu tukaanza kupeana ile kitu roho inapenda huku kila mmoja akiwa na furaha ya utamu wa mwenzake
“Eddy”
“Mmmmm”
“Unajua kuwa mimi ndio nimekufundisha mambo haya”
“Nenda zako huko”
“Kweli”

Rahma alizungumza kwa utani huku akinikalia kiunoni mwangu na kuendelea na kupeana raha zetu.
Bada ya mwezi mmoja Rahma akaanza kuona dalili za ujauzito jambo liliozidi kujenga furaha ya upendo kati yetu, kazi yangu kubwa 

Ikawa ni kumpeleka mke wangu cliniki kila kipindi cha yeye kwenda cliniki kilipo fika.Kipindi cha miezi ya Rahma kujifungua nikawadia, nikamkimbiza hospitalini kujifungua.Madaktari wakaniomba nisubiri nje ya chumba cha ku-jifungulia baada ya muda mlango ukafunguliwa
“Bwana Eddy, hongera sana”

Dokta zalizungumza huku akivua gloves zake mikononi na kujikuta nikiwa ninashauiku ya kutaka kujua ni nini dokta ana-taka kuzungumza
“Mke wako amejifungua salama, na amejifungua watoto mapacha wa kike, wanaafya nzuri na kilo za kutosha tu”
“Kweli dokta”
“Ndio, na mke wako amevunja rekodi ya hospiali yetu kwani haijawahi kutokea mwanake kuzaa watoto mapacha wenye kilo zaidi ya nne”
“Weeee!!! Naweza kumuona mke wangu na wanangu?”
“Ndio unaweza”

Dokta akaniruhusu kuingia ndani ya chumba ambapo nikamkuta Rahma akiwa amewabeba watoto wetu, Rahma alipo nio-na akaachia tabasamu pana huku akitabasamu, akanikabidhi watoto niwabebe, watoto watu wamechukua kila kitu kwetu, nywele zipo kama za mama yao ambaye ni muarabu, huku nyusi na macho yao yakiwa kama yangu.

Mke wangu akakaa hospitali kwa kipindi cha wiki mbili tukaruhusiwa kurudi nyumbani, ambapo Rahma akwasiliana na wazazi wake wakaja kutoka Dubai, kila mmoja akafurahia kuona watoto watu ambao kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi walivyo zidi kuwa wazuri na afya nzuri
“Eddy unapendekeza waitwe majina gani?”

Rahma aliniuliza siku kadhaa kabla ya kwenda kuwabatiza
“Kurwa aitwe Xaviela na doto aitwe Xaviena”
“Sawa mume wangu”

Siku ya kuwabatiza watoto wetu ikawadia, sikuamini kuona watu wengi wakiwemo waandishi wa habari wakijumuika nani katika sherehe ya kuwabatiza watoto watu ambao kila mtu, anahamu ya kuwaona wengine wakitamani hata kuwashika jambo lililozidi kuifanya familia yangu kuwa maarufu katika jiji zima la Tanga na Tanzania kwa ujumla
“Mume wangu kweli TANGA RAHA”

Rahma alizungumza huku akiwa amembeba Xaviena
“Kwa nini?’
“Tazama watu walivyo kusanyika kwa kutuunga mkono sisi”
“Yaa wanupendo na sisi na watoto wetu”

Nilizungumza kwa furaha huku nikimrusha rusha Xaviela ambaye muda wote anatabasamua usoni mwake
“Nakupenda sana baba Xavina”
“Hata mimi pia ninakupenda sana mama Xaviela”

Nikampiga busu la mdomoni mke wangu kama ishara ya upendo kati yetu, jambo lilio fanya watu wengi kupiga makofi hu-ku wakishangilia kwa furaha.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

MWISHO

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)