TANGA RAHA (52)

Zephiline F Ezekiel
0
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Nilizungumza kwa sauti nzito na kumfanya daktari kuanza kutetemeka, mwili mzima, hata miwani aliyo ivaa ikaanguka chini.
SASA ENDELEA...
“Tumeshiindwa kuuuu…okoa maisha ya mke hadi ametutoka duniani”

Taarifa ya daktari ikanistua sana na kujikuta nikumuachia, mwili mzima ukahisi umepatwa na mstuko kama nilio upata siku ya kifo cha wazazi wangu walipo kufa shambani, machozi yakazidi kunitiririka mfululizo na kujikuta nikiwa nimekaa kwenye benchi lililopo pembeni ya mlango wa kuingilia kwenye ofisi ya daktari.
“Eddy tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuyaokoa maisha ya mke wako ila tukashindwa”
“Pia mke wako alituomba sana tukutafute, azungumze maneno ya mwisho na wewe ila hatukuona, na hatukujua ni wapi alipo”

Maneno ya daktari wala sikuyatilia msisitizo zaidi ya kuyatazama machozi yangu yanayo mwagika chini, kwenye sakafu.
“Mwili wake upo wapi?”
“Tuliupeleka mochwari”
“Twende ukanionyeshe”
“Labda asubuhi, kwa sasa ni ngumu kwenda mochari”
“Twende ukanionyeshe sawa”

Nilizungumza kwa msisitizo, hadi daktari akanijibu kwa kutingisha kichwa chake, akiashiria kukubaliana na mimi kwa kitu ambacho nimekizungumza.Nikanyanyuka kwenye benchi na kumshika mkono daktari na kumtanguliza mbele, akatoa si-mu yake mfukoni na kupiga sikujua anazungumza na nani
“Wee Merry maiti ya mgonjwa mumeiweka wapi?”
“Sanduku namba”
“Ahaa sawa, tangulia mochwar sisi tunakuja”

Akakata simu na kuidumbukiza kwenye mfuko wake wa koti alilo livaa, tukazidi kupigahatua za haraka hadi kwenye jengo la kuhifadhia maiti, nililo toka muda mchache ulio pita.

Nikakuta nesi wawili wakiwa wamesimama nje ya mlango wa chumba cha maiti pamoja na mzee mmoja aliye valia mavazi meusi mkononi mwake akiwa ameshika jitochi kubwa
“Mbona kunagiza?”
“Daktari aliuliza?”
“Umeme umekatika, kuna shoti imetokea muda mchache ulio pita”

Mzee alijubu
“Ila maiti ya yule msichana muliiweka?”
“Ndio, tuliiweka”

Nesi mmoja alijibu, macho yangu yakatazama pande zote za eneo la jumba la kuhufadhia maiti, nilipo ridhika kwamba kina Regina hawapo, nikaanza kutangulia kuingia ndani
“Ahaaa wewe kaka subiri mlizi atangulie na tochi”

Nesi mmoja alizungumza huku akiniwahi kunishika mkono
“Giza halina maana mbele ya mke wangu”

Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikiutoa mkono wa nesi ulio nishika, mlinzi ambaye ndio yule mzee aliye valia nguo nyeusi, akafwatia kwa nyuma huku akimulika mulika kwenye madroo ya sehemu zilipo hifadhiwa maiti.
“Muliseme droo namba ngapi?”
Daktari aliuliza
“D-210 ipo kule mwisho”

Tukaelekea sehemu zilip droo, aliyo zungumza nesi, katika sehemu ambayo muda mchache nilikuwa na kina Regina haina uchafu wa aina yoyote na haionyeshi kama kuna tukio lolote lilifanyika siku hiyo.Mlizi akavuta droo alilo alekezwa na ma-nesi hawa, ambao ninashangaa wana ujasiri mkubwa kama wanaume.Macho yetu tote yakatua kwenye sura ya binti mmo-ja ambaye sote hatukumtambua
“Mmmm”

Nilisikia mguno mmoja ukitoka kwa nesi aliye alekeza sehemu alipo tuagiza tufungue droo
“Nini?”
Doktar aliuliza kwa mashangao
“Mbona siye?”
“Muna uhakika mumemuweka humu?”
“Dokta sisi tunauhakika tumemuweka humu, si yule dada wa kiharabu?”
“Ndio, au mumekosea?”
“Dokta hatujakosea, mimi ndio nilikuwa mtu wa mwisho kulisukuma hili droo, au mlinzi ninakosea”
“Kweli hata mimi mwenye ninashangaa”
“Sikieni nyinyi musiniletee ujinga mke wangu, yupo wapi?”
“Kweli kaka yangu mkeo tulimuweka huku”

Gafla tukasikia mtikisiko wa kabati moja lililopo upande wa pili, sote tukakaa kimya, mtikisiko huo upo kama kuna mtu aliye zinduka kutoka katika usingizi mzito na kujikuta yupo ndani ya eneo hilo.
“Shiii”

Niliwaonya wasizungumze chochote, nikaanza kupig ahatua za kuelekea lilipo sanduku alinali kurupuka, nikawatazama daktari na wezake kila mmoja akaonekana kuwa katika hali ya mshangao, huku mlizi mikono yake ikitetemea hadi tochi aliyo ishika mwanga wake ukaanza kucheza cheza.Nikafika kwenye droo, kabla sikaulifungua moshi ukaanza kutoka kwenye droo hilo, huku likizidi kutetemeka.

Kwa ujasiri mkubwa nikaupeleka mkono wangu hadi kilipo kishikizo cha kisanduku, na kulivuta taratibu, kabla sijamalizia kulifungua, nikastukia kitu kikianguka nyuma, ilanilazimu kugeuka haraka na kukuta tochi ya mlinzi ikiwa imeanguka na kusababisha mwanga wake kupiga katika sehemu nilipo simama huku ukitokea chini.Macho ya daktari na manesi yakaanza kushangaa sana
“Nini mbona munashangaa?”

Niliwauliza baada ya kuona mshangao wao unazidi, kidole kimoja cha nesi mmoja kikaniashiria nigeuke nyuma yangu kuangalia kitu kinacho toka kwenye droo nililo lifungua.Nikageuka kwa haraka, sikuamini macho yangu, hii ni baada ya kukutana na 

Mtu niliye fanana naye kuanzia juu hadi chini, isitoshe nguo zake na zangu zimefanana sana, jambo lililo nistua kupita maelezo.Akaanza kupiga chafya nyingi, nikastukia kishindo nyuma yangu, nikageuka na kumkuta nesi mmoja akiwa ameanguka na kupoteza fahamu huku mlinzi naye akifwatiakuanguka na kukaa kimya
“Mambo Eddy”

Jamaa alinisalimia, na sauti yangu inafanana sana na sauti yangu, nikabaki mdomo wazi nisijue nini nimjibu

Jamaa akatoka kwenye droo ya kuhifadhia maiti na kusimama karibu yangu, mwili mzimwa ukaanza kunitetemeka kwa maana katika maisha yangu sijawahi kukutana na vihoja kama hivi japo kuna matukio mengi ya kutisha yalisha wahi kupita kipindi cha nyuma ila la mtu anaye fanana na mimi kwangu limekuwa ni laajabu sana
“Usishangae sana”

Alizungumza huku akielekea walipo simama dokakta na nesi, akawatazama mlinzi na nesi ambao wamepoteza fahamu ki-sha akaachia tabasamu pana kidogo
“Hawa nao kilicho waangusha ni nini?”

Swali lake hapakuwa na mtu aliye lijibu zaidi ya sisi sote kubaki kimya tukimtazama, akachuchumaa na kumshika mlizi kichwani, gafla mlinzi akaanza kutoa chafya zilizo pelekea akazinduka na kukaa kitako na macho ya mlinzi yakabaki kuwa na mshanga kati yangu na 

Eddy mwenzangu.Macho yangu yakatua kwenye suruali ya dokta na kukuta ikiwa imelowa maeneo ya mbele, ikiashiria ameshindwa kuibana haja yake ndogo kutokana na woga wa kukutanan na jamaa.Akamshika nesi kama alivyo fanya kwa mlinzi na neshi fahamu zikamrejea na kuzinduka.
“Ninaamini nyinyi nyote mutakuwa munashangaa kwa nini mimi nipo hivi, jina langu ninaitwa Eddy ni pacha wa Eddy yule pale”

Eddy alizungumza huku akiwatazama manesi, akangeukia kisha akamshika bega dokata ambaye hadi sasa hivi mwili wake wote namtetemeka mithili ya mtu aliye pigwa shoti
“Mzee usiogope sana, mimi sio mtu mbaya, ila kazi yangu ni moja tu.Nimekuja kumsaidia Eddy katika swala zima la ku-mrudisha mke wake ambaye hajafa kama munafyo fikiria nyinyi, ndio maana kwenye droo muliyo muweka hamjamkuta”
“Amekwenda wapi?”

Nilimuuliza kwa kujiamini
“Eddy hilo swali nitakujibu baadaye na si mbele ya hawa watu”
“Jamani enendeni kwa amani ya bwana, ila hakikisheni hamuitoi siri hii ya kwamba kuna Eddy wawili.Yoyote atakaye toa siri hii basi atadili na mimi na sio Eddy yule sawa”

Jamaa alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo, na kuwafanya dokta na watu wake kutingisha vichwa kwamba wameelewa, akawaruhusu watoke ndani ya jengo la kuhifadhia maiti, wote wakatoka wakiwa wanakimbia kila mmoja akijaribu kuwahi kufika mlangoni na asiwe wa mwisho.Baada ya dokata na watu wake kutoka, Eddy akanifwata sehemu nilipo simama na kunishika bega
“Niambie ndugu yangu”
“Safi” nilijibu hiyo basi ila kwa mbali woga umenitawala
“Pole sana na matatizo”
“Nimeshapowa ndugu yangu”

Tulizungumza huku tukielekea nje, tayari kulisha anza kupambazuka, tukaanza safari ya kuelekea kwangu huku tukitem-bea kwa miguu cha ajabu njiani watu hawatushangai na mara nyingine baadhi ya watu walinisalimia mimi mwenyewe
“Mbona wewe hawakusalimii?”
“Mimi hawanioni, wakiniona watajikojolea kama yule dokta”
“Umefanya fanyaje hadi hawakuoni?”
“Ni mimi mwenye ndio najua jinsi nilivyo fanya, ila usiwe na shaka utajua tu”

Kwa njia za mkato, tukafika kwangu na moja kwa moja tukaingia ndani, tukakuta baadhi ya watu walio hudhuria kwenye sherehe wakiwa wamejilaza sebleni, wakisubiria kupambazuke waende makwao, wengine wakiwa na shahuku ya kutaka kujua hali ya mke wangu inaendeleeja
“Kaka Eddy shem anaendeleaje?” Jamaa mmoja aliniuliza baada tu ya kukaa kwenye sofa
“Muambie anaendelea vizuri”
“Anaendelea vizuri”
“Pole sana kaka”
“Asante”

Baadhi ya watu wakaanza kunihoji hiji maswali kadha na kila aliye niuliza swali, alijibiwa na Eddy mwenzangu huku wote wakiamini kwamba mimi ndio ninao wajibu maswali yao.Waalikwa wote wakondoka mida ya saa nne asubuhi na tukabaki mimi na Eddy
“Ngoja nifanye usafi wa nyumba”

Eddy alizungumza na kuanza kufanya usafi wa nyumba nzima, kitu kingine kilicho niacha hoi ni jinsi kasi aliyo itumia kui-safisha nyumba yangu, hapo ndipo nikaamini kwamba jamaa sio mtu wa kawaida
“Unashangaa nini?”
“Nashangaa jinsi ulivyo safisha jumba lote hili ndani ya muda mchache!!”
“Usishangae sana”
“Wewe ni nani haswa kwa maana sijakuelewa hadi sasa hivi japo unafanana na mimi?”

Eddy akaanza kucheka kicheko kikali kilicho anza kuyaumiza masikio yangu, alipo gundua ananiumiza masiko yangu akajifumba mdomo na kuandelea kucheka ndani kwa ndani
“Mimi ni Eddy, ila nimetoka sayari nyingine na sio duniani”
“Sayari gani?”
Marsi, hii ni sayari ambayo inasadikika kwamba watu wanaweza kushi si ndivyo?”
“Sina uhakika”
“Una uhakika gani, wewe si ulikuwa mwalimu wa Sayansi au umesha jisahau?”
“Yaa nilikuwa ni mwalimu ila sio kama nilikuwa ninafwatilia maswala hayo”
“Basi ukweli ni kwamba sayari ya Marsi watu wanaweza kuishi, ila si watu kama nyinyi”

Eddy alizungumza huku akijirusha kwenye sofa na kupandisha miguu yake yenye viatu juu ya meza ya kioo
“Watu wote wanao ishi kule wanauwezo wa ziada, na kama maishani mwako ulishawahi kusikia viumbe vyenye uwezo mkubwa wa akili kupita binadamu wanaitwaje?”
Ellians
“Ndio, mimi ni miongoni mwao.Kipindi nipo kwenye matembezi yangu ya kuizunguka dunia kwa bahati nzuri nikakuona wewe, ukiwa unafanana na mimi, isitoshe hadi jina tukawa tunaonana.Usiku nilikuona jinsi unavyo muhangaikia mke wa-ko, ulivyo pambana na wale mabinti ila wale ndio walio muiba mke wako kipenzi”
“Tutampata vipi mke wangu?”
“Mke wako yupo mbali sana na hapa, hayupo chini wala hayupo juu”
“Sijuakuelewa vizuri, hayupo chini wala juu kivipi?”
“Kwa sasa huwezi kunielewa, ila kikubwa ambacho ninataka kukifanya kwako ni kuitoa hiyo pumzi uliyo pandikizwa”
“Ukiitoa si nitakufa?”
“Ndio utakufa, kwani unaogopa kufa”

Sikumuelewa Eddy ana maana gani na kila nilivyo mtazama mwenzangu hakuwa na wasiwasi hata kidogo, gafla akasima-ma na kuanza kunifwata katika sehemu ambayo nimesimama, nikajaribu kurudi nyuma ila akaniwahi kuukamata mkono wangu, gafla nikastukia nikirushushwa na kujibamiza kwenye ngazi na giza kubwa likatawala kwenye macho yangu, na kukaa kimya

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)