SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Nilianza kuisahau ile ndoto ya kutaka kuuliwa na sasa nikaanza kuifikiria hiyo jioni itakuwaje, kuna muda nilihisi kama masaa yalikuwa yamesimama kwani ndiyo kwanza yalikuwa ni majira ya saa mbili za asubuhi. Niliamua kumtumia ujumbe mfupi Helena kama salamu hapo nakumbuka tayari nilikuwa nimemtumia Precious ujumbe wa asubuhi njema na aliweza kunijibu.SASA ENDELEA...
“Poa mzima uko wapi?”aliniuliza Helena kupitia ujumbe mfupi aliyokuwa amenitumia.
“Niko geto hapa.”
“Hutoki?”
“Hapana leo nipo tu nitaandika Chombezo ila jioni ndiyo nitatoka.”
“Utaenda wapi?”
“Kwa marafiki zangu.”
“Anha!”
“Njoo basi.”
“Nije nifanyaje?”
“Unisaidie kufua nguo.”
“Kwanini usimpe mpenzi wako akufulie?”
“Nimpe mpenzi wangu yupi wakati mimi niko na wewe.”
“Mmmh! Wewe muongo unanidanganya.”
“Nakudanganya na nini?”
“Yani ulivyo na mashabiki wengi hivyo katika Machombezo yako ukose mpenzi kweli?”
“Kwahiyo huniamini?”
“Nakuamini Baby.”
“Ila.”
“Hamna.”
“Njoo sasa unisaidie kufua.”
“Basi nakuja si hapo kwa Tumbo?”
“Ndiyo.”
“Haya ngoja basi nimalizie kufanya usafi halafu nije mpenzi.
“Haina shida.”
Kitu cha kushangaza sikuwahi kumtongoza kabisa lakini tayari alikuwa akiniita majina ya kimapenzi, ni wazi kuwa alikuwa akinipenda sana , nililifahamu hilo na sikutaka nililazie damu, nilichoamua kukifanya ni kumuita na siku hiyohiyo nilipanga kusafiri naye kwenda katika mji wa mahaba nigaragaze.
Nilianza kuisahau ile ndoto ya kutaka kuuliwa na sasa nikaanza kuifikiria hiyo jioni itakuwaje, kuna muda nilihisi kama masaa yalikuwa yamesimama kwani ndiyo kwanza yalikuwa ni majira ya saa mbili za asubuhi. Niliamua kumtumia ujumbe mfupi Helena kama salamu hapo nakumbuka tayari nilikuwa nimemtumia Precious ujumbe wa asubuhi njema na aliweza kunijibu.
“Poa mzima uko wapi?”aliniuliza Helena kupitia ujumbe mfupi aliyokuwa amenitumia.
“Niko geto hapa.”
“Hutoki?”
“Hapana leo nipo tu nitaandika Chombezo ila jioni ndiyo nitatoka.”
“Utaenda wapi?”
“Kwa marafiki zangu.”
“Anha!”
“Njoo basi.”
“Nije nifanyaje?”
“Unisaidie kufua nguo.”
“Kwanini usimpe mpenzi wako akufulie?”
“Nimpe mpenzi wangu yupi wakati mimi niko na wewe.”
“Mmmh! Wewe muongo unanidanganya.”
“Nakudanganya na nini?”
“Yani ulivyo na mashabiki wengi hivyo katika Machombezo yako ukose mpenzi kweli?”
“Kwahiyo huniamini?”
“Nakuamini Baby.”
“Ila.”
“Hamna.”
“Njoo sasa unisaidie kufua.”
“Basi nakuja si hapo kwa Tumbo?”
“Ndiyo.”
“Haya ngoja basi nimalizie kufanya usafi halafu nije mpenzi.
“Haina shida.”
Kitu cha kushangaza sikuwahi kumtongoza kabisa lakini tayari alikuwa akiniita majina ya kimapenzi, ni wazi kuwa alikuwa akinipenda sana , nililifahamu hilo na sikutaka nililazie damu, nilichoamua kukifanya ni kumuita na siku hiyohiyo nilipanga kusafiri naye kwenda katika mji wa mahaba nigaragaze.
Nilichokuwa natamani kwa muda huo ni kuona masaa yakikimbia kwa kasi ili niweze kuonana na Helena. Nilikuwa tayari nimeanza kupandwa na mizuka isiyojulikana. Nilikuwa nikianza kuhisi joto mara baridi kwa wakati mmoja hali iliyonifanya nizidi kumuhitaji kupita kawaida.
Sikumbuki kama kuna siku niliwahi kutumia zana katika kipindi chote kile ambacho nilikuwa nikilala na wanawake tofautitofauti ila nilijikuta tu nafsi yangu ikinishinikiza niende kwa mangi kununua zana. Nilifanya kama nafsi yangu ilivyokuwa imenituma na niliporudi niliamua kumtumia ujumbe mfupi Helena kumuuliza kuwa alikuwa anakuja muda gani?
“Niko njiani nimekaribia kufika,” alinijibu.
Moyo wangu uliingiwa na furaha ya ajabu mno, sikutaka kuipoteza bahati ile ya mtende iweze kuondoka hivihivi, nilipanga kumchombeza mpaka akubali kuingia mchezoni kwani ligi tayari nilikuwa nimeshaiandaa. Nilikumbuka kuweka zana zangu mfukoni hii ikiwa ni sehemu moja wapo ya kujihami.Baada ya dakika kadhaa Helena aliweza kunipigia simu.
“Dick nimeshafika,” aliniambia mara baada ya kupokea.
“Umefika wapi?” nilimuuliza.
“Hapa kwa tumbo.”
“Ok nisubiri dakika moja nakuja kukuchukua,” nilimwambia kisha nikatoka nje kuelekea kituoni, nilikuwa nimejipanga kisawasawa.
Nilipofika nilimkuta akinisubiria kituoni, alikuwa amevalia katika moja ya vazi ambalo nilikuwa nikilipenda sana hasa kumuona mwanamke mzuri aliyejaaliwa viungo pamoja na nyama za mwili wake kuvaa. Lilikuwa ni vazi ambalo nilikuwa nikilipenda sana na kama ikitokea muda huu ukaniuliza kwanini nalipenda vazi hilo kwa kweli sitakuwa na jibu sahihi la kukujibu isipokuwa nielewe tu kuwa nalipenda sana ten asana tu!.
Macho yangu yalimuona Helena akiwa amevaa Dera ambalo lilikuwa limembana kidogo kiasi cha kuyaonyesha baadhi ya maumbile yale yalivyo. Alikuwa amejaaliwa umbo matata ambalo kiukweli lilizidi kunipa uchu wa kutamani vya ndani. Macho yangu kila yalipokuwa yakimtazama yalizidi kuniambia nisichelewe kwani muda ulikuwa haunisubiri.
Nilipomfikia miili yetu ilishindwa kuvumilia, tukakumbatiana kumbato ambalo lilizidi kunipa wakati mgumu sana, askari wangu hakuchelewa kusimama kwa kiherehere cha kutaka kuangalia kilichokuwa kikiendelea.
“Nafurahi kukuona Dick yani kukutana na wewe nahisi kama bahati vile,” aliniambia kipindi tulipokuwa tumekumbatiana.
“Hata mimi pia niseme nafurahi sana kukuona japo usiku wa jana nimetoka kukuota,” nilimwambia katika namna fulani ya kumuweka katika wakati wa shahuku, nilifahamu fika kuwa alikuwa akiyapenda sana machombezo yangu, alikuwa akinipenda sana japo kuna wakati alikuwa haniamini hivyo niliamua kumwambia vile ili nizidi kumtengenezea mazingira ya kutaka kufahamu ni ndoto ya aina gani nilikuwa nimemuota.
“Umeniotaje?” aliniuliza swali ambalo sikulishangaa sana kuniuliza kwa wakati ule.
“Ah! No hapa si mahala pake subiri tukifika kwangu nitakusimulia,” nilimwambia kisha nikajitoa katika lile kumbato lake, muda huo alikuwa akitabasamu tu! kila alipokuwa akinitazama alizidi kujawa na tabasamu.
Ukweli ni kwamba Helena hakuwa miongoni mwa wale wasichana warembo kiasi kwamba kama ukamtazama ati! ujikute unamtamani tu sura yake au kutokana na urembo aliyokuwa amebarikiwa lahasha! Helena alikuwa ni miongoni mwa wasichana ambao hawakuwa wazuri wa sura ila walikuwa wamebarikiwa maumbo matata, nyuma walikuwa wamefungasha mizigo mikubwa, wapitapo nyuma wanaacha lawama.
Nilipokuwa nikimtazama nilihisi nafsi yangu ikiniambia kisirisiri “Dick unachelewa nini sasa mpeleke ndani.”
Hatimaye tuliondoka pale na sasa tukawa tunaelekea katika chumba changu, ulikuwa ni mtaa mmoja uleule na sehemu kituo kilipo hivyo hakukuwa na umbali hata kidogo.
Baadhi ya majirani zangu walikuwa wakinitazama kwa macho ya umbeya, kila siku walikuwa wakiniona nikileta mali mpya, nilifahamu walikuwa wakinisema kichinichini lakini sikutaka kujali sana, nilichokuwa nakiangalia kwa wakati ule ni kumuingiza Helena ndani na mambo mengine yaendelee.
“Kumbe hukai mbali sana?” aliniuliza Helena tulipokuwa tumefika na kuingia ndani.
“Hapana mbona umesimama wima kaa hapo,” nilimwambia wakati huo nilikuwa nikiufunga mlango. Nilikuwa nimepanga kucheza na akili yake mpaka akubali kula tunda na mimi.
Nilipomaliza kuufunga mlango nilienda kukaa moja kwa moja kitandani. Wakati huo nilijifanya kuwa bize na simu yangu huku kichwani nikipanga mbinu za kumshinda kwani tayari alikuwa ameniletea mpira golini.
“Karibu sana Helena jisikie uko nyumbani ila umekuja muda ambao hata bado sijaandaa chai,” nilimwambia huku nikimtazama. Alikuwa akizing’ata kucha zake.
“Asante wala usijali,” alinijibu kwa sauti iliyochanganyika na aibu.
Muda huo nilipokuwa bize kwenye simu yangu, nilikuwa nikichat na Precious alikuwa akiniambia kuwa mume wake alikuwa akiwasili siku hiyo hivyo kwa wakati huo alikuwa yupo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius kwa lengo la kumpokea.
Nilipomaliza kuchat naye nilimgeukia Helena ambaye alikuwa akijichekesha kama mwendawazimu.
“Mbona unacheka?”nilimuuliza.
“Nimefurahitu!”
“Umefurahi nini?”
“Kukuona,” aliniambia kisha akanyamaza kwa muda halafu akaendelea kuzungumza.
“Enheee! Nimekumbuka halafu,” aliniambia.
“Umekumbuka nini?” nilimuuliza huku nikionekana kushangaa.
“Kuhusu hiyo ndoto uliyoiota kuhusu mimi,” aliniambia kisha nikakumbuka tukio la ndoto la kweli niliyoiota usiku wa kuamkia siku hiyo.
Ilikuwa ni ndoto ya kunusurika kifo baada ya kutekwa na wanaume watatu ambao walikuwa wamedhamiria kuniua baada ya kunishutumu kuwa nilikuwa nikitembea na mke wa mtu mzito ambaye hata sikuwa namfahamu, ndoto ile nakumbuka iliishia kipindi walipokuwa wakitaka kunipiga risasi na ndipo hapo ambapo niliweza kushtuka.
Kwa kweli nilipoikumbuka hiyo ndoto nilijikuta nikicheka peke yangu, nilikuwa nikicheka kwa uongo ambao niliutumia kuibadilisha hiyo ndoto. Ndoto ya kunusurika kuuliwa na wale wanaume nisiyowafahamu sasa nilikuwa nikiigeuza na kuwa ndoto ya msichana Helena ambaye nilikuwa nimemuota.
“Mbona unacheka tena?” aliniuliza.
“Hapana unajua nilishasahau kabisa kuhusu hiyoo ndoto kumbe na wewe husahau kitu,” nilimwambia maneno yaliyomfanya akatokwa na kicheko, alikuwa akicheka kutokana na lafudhi ya kichaga niliyokuwa nimeitumia kumwambia kwa wakati huo.
“Kumbe wewe ni mchaga?” aliniuliza huku akijaribu kujizuia kucheka, mwisho uvumilivu ukamshida akabakia akicheka mfululizo.
“Hapana mimi sio mchaga.”
“Sasa mbona umeongea kichaga?”
“Najaribu kuwaiga tu.”
“Hahahaha! umenichekesha wewe.”
“Pole.”
“Pole ya nini kwanza niambie kuhusu hiyo ndoto.”
“Ndoto ndoto ndoto,” nilimwambia huku nikijaribu kuiita hiyo ndoto, alizidi kucheka tu.
“Sasa mbona unacheka?”
“Dick bhanaa embu niambie huko acha kufanya masihara.”
“Sasa nitakuambiaje ukiwa huko mbali sogea hapa karibu nikunong’oneze wasisikie wapambe huko nje,” nilimwambia kisha akainuka pale kwenye kochi na taratibu alikuwa akizihesabu hatua zake kunifuata kitandani nilipokuwa nimekaa.
Aliponifikia alikaa karibu na mimi, alikuwa akinitazama kwa wakati huo. Nilipomtazama usoni sikuwa nikiuona uzuri wowote aliyokuwa nao zaidi ya yote nilikuwa nikijiambia kitu kilichokuwa kinafuata ni kufanya naye mapenzi halafu huo ndiyo unakuwa mwisho wetu kwanza sikumbuki kama niliwahi kumtongoza.
“Haya niambie sasa,” aliniambia huku macho yake akiyaelekezea kwangu, sijui alikuwa akitazama kitu gani maana alibaki kunitazama tu.
“Mbpto una moto hivyo poa kwanza,” nilimwambia kisha nikaurudia ule mchezo wangu wa kuchukua simu na kujifanya kuwa bize kidogo.
“Sasa mbona huniambii unachezea simu?” aliniuliza huku akionekana kuchukizwa na kitendo kile nilichokuwa nimekifanya cha kuwa bize na simu yangu.
“Helena,” nilimuita huku macho yangu yakiitazama simu yangu ambapo hakukuwa na kitu cha maana nilichokuwa nakitazama, nilikuwa nikizuga tu.
“Abee,” aliniitikia kwa sauti ya shahuku ya kutaka kuisikia hiyo ndoto ambayo nilikuwa nimeiota kuhusu yeye.
“Ila nahisi kama nikikuambia nitakuudhi maana ndoto yenyewe,” nilimwambia kisha nikasita kuzungumza.
“Niambie bhanaa wala usijali kwani ulimeotaje?” aliniuliza kwa sauti iliyoniambia niseme kila kitu nisifiche kwani alikuwa akitamani sana kusikia kila tukio lililokuwa limetokea ndotoni kuhusu yeye.
“Ndoto ya ajabu kweli.”
“Ndoto gani?”
“Nimeota tupo ufukweni mwa bahari lakini tukiwa katika mavazi ya harusi ni wazi kuwa tulikuwa tumefunga ndoa. Wakati huo tulikuwa tukitembea na kwa mbele yetu tuliwaona watoto wawili, mmoja wakike na mwingine wakiume wakiwa wanatukimbilia huku wakituita majina baba na mama, walipotufikia ghafla! nikashtuka,”
Nilimwambia maneno ambayo hayakuwa na ukweli hata kidogo, nilikuwa nikimdanganya na kweli aliwezakudanganyika.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA