SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
Nilikumbuka asubuhi sikuwa nimekunywa chai wala kula kitu chochote kile, nguvu zilikuwa zimeanza kuniishia mwilini, kila nilipokuwa nataka kuamka nilishindwa, nilikuwa nikitetemeka, nilihisi kufa kwa wakati huoSASA ENDELEA...
Ama kweli mapenzi ni mchezo hatari sana, yanaweza kukutoa uhai usipokuwa makini. Nilikuwa hoi nisijue ni nini nifanye kwa wakati ule. Nilikuwa nimelala huku akili yangu yote ikifiria chakula, sikuwa nimekula chochote tangu nilipokuwa nimeamka asubuhi na kibaya zaidi nilikuwa nimefanya mapenzi. Kuna muda nilikuwa nikimlaumu
Helena kuwa ni kwanini alikubali kuja na kosa kubwa alilolifanya ni kunikubalia kufanya naye mapenzi lakini lawama zangu hazikuweza kubadili chochote kwani ndiyo kwanza njaa ilizidi kuniuma, nilikuwa nikihisi kama vitu vipititavita tumboni na kunikwarua, hakika nilikuwa nimepatikana.
Nilitamani kuutafuta usingizi huku nikiamini wenda nitakapolala nikiamka sitahisi njaa tena lakini nilikuwa nikijidanganya. Kila nilipokuwa nikijaribu kufanya hivyo ndiyo kwanza macho yangu yalibaki yakitalii sehemu mbalimbali ya chumba changu. Nilizidi kuhisi kuchoka kusikomithilika.
“Dah!” nilijikuta nikisema neno hili kwa sauti ya kulalamika, wakati huo nilikuwa nikigaragara pale kitandani kama mtu ambaye alikuwa anakaribia kukata roho.
Kuendelea kulalamika pale kitandani huku nikizidi kukilalamikia chakula ambacho ilikuwa ni vigumu kuweza kuletewa nilihisi kama nilikuwa nikiufanya ujinga ambao ungeweza kunigharimu baadae, nilijikaza kiume, nikaamka, nikavaa nguo kisha nikatoka na kwenda kutafuta chakula kwa mamantilie ambaye hakuwa mbali na pale nilipokuwa nikiishi. Nilipomaliza kula niliweza kurudi katika chumba changu huku nikiwa nina nguvu mpya. Niliutumia muda huo kwa ajili ya kupumzika huku nikiisubiria jioni ambayo nilipanga kutoka na Evadia.
Moyo wangu ulikuwa unashahuku ya kutaka kumuona msichana huyo ambaye mpaka kufikia muda huo sikuwa nafahamu ni nini ambacho alikuwa amedhamiria, kuendelea kusubiri kukutana naye kulizidi kuniweka katika wakati wa furaha muda wote. Sikumbuki ni nini kilitokea ila nilijikuta nikiamka na kukutana na simu ya Evadia, haraka niliweza kupokea.
“Uko wapi?” aliniuliza simuni.
“Nyumbani,” nilimjibu.
“Umeshajiandaa maana ndiyo nakaribia hivyo.”
“Umefika wapi?”
“Nipo kona hapa.”
“Sawa ukifika utakuta nipo tayari nakusubiria.”
“Haya,” alinijibu kisha akakata simu.
Niliutumia muda huo kwa ajili ya kujiandaa, sikumbuki vizuri kama nilioga ama lah! ila ninachokikumbuka ni kuwa baada ya dakika kama kumi nilikuwa tayari nimejiandaa kwa kila kitu, nilienda kituoni kwa lengo la kumsubiria na haikuchukua dakika nyingi Evadia aliweza kuwasili, nilipanda kisha safari ikaanzia hapo ya kuelekea Mlimani City.
Niliendelea kujiuliza kuwa huko Mlimani City tulikuwa tukienda kufanya mazugumzo gani ambayo alikuwa ameniambia, sikuweza kupata jibu lolote lile niliamua kumuuliza, nilipomtazama alikuwa akitabasamu.
“Kwani huku Mlimani tunaenda kufanya nini?” nilimuuliza.
“Kuna sehemu nataka twende wote halafu pia nataka tutafute mahali tuongee au umeshasahau?” alinijibu kwa kuniuliza swali lililonifanya nitabasamu.
“Mbona unacheka?” aliniuliza.
“Hapana nakumbuka,” nilimjibu kisha ukimya wa muda ukatutawala.
Tukizidi kuvipita vituo mbalimbali na sasa tulikuwa tumeshafika Mlimani City.
“Vipi?” aliniuliza mara baada ya kuegesha gari na wote tukashuka.
“Poa,” nilimjibu huku nikimtazama kwa macho ya kumuuliza kuwa huku tumekuja kuzungumza nini?
Sikutaka kujifanya mjuaji sana wala mpangaji wa mambo mengi kwa wakati ule, niliamua kubaki kimya huku nikimsikiliza na kumfuata popote pale alipokuwa anataka kwenda.
Macho yangu hayakukoma kumkagua nywele zake alizokuwa amesuka, zilikuwa ni za gharama kubwa sana, T-shirt fupi iliyokuwa imepanda kwa juu upande wa nyuma pamoja ile suruali ya blue crazy aliyokuwa ameivaa, iliyokuwa imembana vyema huku mapaja yake yakibaki kuwa wazi, bila shaka yalikuwa yakitafuta hewa kwani yakikwisha choshwa na kubanwa na suruali ile.
Kila hatua aliyokuwa akiipiga na mimi nilikuwa nyuma yake, tuliingia ndani, tukawa tunazunguka sehemu mbalimbali huku safari ile nikizidi kuiona kuwa haikuwa na umaana hata kidogo. Kuna muda nilikuwa nikitamani kumtukana
Evadia hapa ni pale ambapo tulikuwa tumeingia Super Markert kisha akawa kama anayechagua kitu kwa lengo la kununua lakini aliweza kuacha. Kitendo cha kumfuata nyuma nyuma kama mkia wa ng’ombe kisha kuingia mara Mr. Price, Shopping Mall, Game, Nakumati halafu mara tunatoka bila kutoka na chochote hakika kilizidi kunikera mno wala siwezi kuficha kwa hilo.
“Ina maana tumekuja kuzunguka huku kama wendawazimu au tumekuja kwa ajili ya mazungumzo?” niliamua kumuuliza kwa ghadhabu baada ya kuzunguka kila kona bila kuona faida yoyote ile.
“Kuna zawadi namtafutia rafiki yangu ila sijui hata nimnunulie nini jamani yani mpaka napagawa mimi,” alinijibu huku akijichekesha, wakati huo nilikuwa nimeuweka ukauzu fulani hivi, kwa kweli nilikuwa nimeshaanza kuchoka.
“Zawadi ya nini?” nilimuuliza.
“Zawadi tu.”
“Kwani anaolewa?”
“Hapana ni zawadi ya Birth day yake.”
“Kwahiyo umenileta huku ili nikubebee hiyo zawadi au tuzungumze mbona unanichanganya sasa?”
“Hahaha! Dick na wewe umeshaanza vituko vyako.”
“Sio nimeshaanza sasa wewe tangu tumefika hapa unanizungusha tu! kama vile mwendawazimu.”
“Basi tutafute sehemu tukae ili tuongee.”
“Wapi sasa?”
“Huku,” alinijibu kisha tukaongozana mpaka Samaki Samaki, tulipofika tuliweza kukaa, tukaagiza chakula na kuanza kula. Nilikuwa nikimtazama tu muda wote.
“Dick nikuambie kitu?” aliniuliza huku akiendelea kula.
“Niambie,” nilimjibu.
“Kwanza naomba usahau yale yote yaliyotokea siku ile ni hasira tu zilinipelekea mpaka mimi nikawa vile,” aliniambia kwa sauti iliyokuwa ikimaanisha kile alichokuwa akikizungumza kwa wakati ule.
“Kweli?” nilimuuliza.
“Ndiyo Dick yani sijui hata nikuambie nini?”
“Niambie tu wala usijali lolote.”
“Kwa kifupi sikutegemea kama ningeweza kufanya mapenzi na wewe yani ulinishtukiza kwa kweli,” aliniambia huku akiyaelekeza macho yake chini kwa aibu.
“Nafahamu hilo Evadia na ndiyo maana nilikuomba msamaha au bado haujanisamehe?” nilimuuliza huku nikikisitisha kijiko kwenda mdomoni mwangu, nilikirudisha kwenye sahani.
“Usijali Dick yameshaisha hayo ila kuna kitu kinanisumbua moyoni.”
“Kitu gani?”
“Nakupenda.”
“Nakupenda pia.”
“Kweli Dick.”
“Nashindwa kujua nifanye nini ili uamini ila we niamini hivyohivyo hata kwa kuigiza.”
“Hahaha! Sawa ila siku ile mmmh!”
“Nini?”
“Amna,” alisema kisha wote tukajikuta tukicheka bila kutarajia. Nakumbuka sikuacha kumsifia, nilimsifia juu ya kupendeza kwake na uzuri wake pia hata hivyo sikuacha kumchombeza kama ilivyokuwa kawaida yangu.
“Nikuombe kitu mpenzi?” aliniuliza wakati ambao tulikuwa tunatoka pale Samaki Samaki tukielekea sehemu gari alipokuwa ameliegesha. Giza lilikuwa tayari limeshaingia kwa wakati huo.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Utakubali?” aliniuliza tena.
“Ndiyo nitakubali sasa kwanini nikatae wakati umeshakuwa Malkia Wangu,” nilimjibu huku mkono wangu wa kushoto ukiwa umekishikilia kiuno chake.
“Naomba kesho unisindikize kwenye Birth Day ya rafiki yangu.”
“Sawa haina tatizo,” nilimjibu jibu ambalo lilimfanya afurahi kupita kawaida, alinikumbatia kumbato alilolisindikiza na busu zito katika shingo yangu.
Tulipanda kwenye gari na breki ya kwanza ilikuwa ni kunirudisha nyumbani kwangu halafu ndipo hapo ambapo aliianza safari yake ya kurudi nyumbani kwao Tabata alipokuwa akiishi yeye pamoja na wazazi wake.
Labda nikuambie kitu ni katika hiyo sherehe ya siku ya kuzaliwa rafiki yake ambayo Evadia aliweza kuniomba nimsindikize, nilikutana na Irine Kisoka msichana ambaye alitokea kunipa umaarufu nisioutegemea katika maisha yangu. Ulikuwa ni zaidi ya huu umaarufu wangu niliyokuwa nao wa kuandika machombezo mitandaoni.
Nilikuwa nikikitumia kipaji changu vibaya, nilikuwa nikiutumia umaarufu wangu katika kuwateka wanawake ambao walikuwa wakijirahisisha kutokana na sifa walizokuwa wakinimwagia katika umahiri wangu wa kuandika machombezo mitandaoni.
Kila siku orodha ya wanawake ilizidi kuongezeka, hakukuwa na msichana ambaye alinifuata kisha nikamuacha salama, wote nilitembea nao. Nakumbuka niliwahi kukutana na wanawake wengi sana, kati yao walikuwepo wale wagumu ambao walinisumbua sana lakini pia walikuwepo wale wasichana waliyojirahisisha na mwisho wa siku niliweza kufanya nao mapenzi.
Kwa macho ya harakaharaka kama ungepata bahati ya kuniona najua usingeamini kama kweli mimi ndiye yule ambaye nilikuwa nikiwabadilisha wanawake kama nguo, usingeamini kama mimi ndiye yule ambaye nilikuwa nikitembea na wake za watu, niliyekuwa nikiwalaghai wasichana waliyokuwa wakionyesha ugumu na mwisho wa siku walijikuta wakiingia mikononi mwangu na kufanya nao mapenzi.
Hakukuwa na utofauti kati ya maisha ya machombezo niliyokuwa nikiyaandika na maisha yangu halisi. Naweza kusema nilikuwa nikiishi katika maisha hayo ya chombezo ambayo yalitawaliwa na mapenzi kwa kiasi kikubwa.
“Hivi utapunguza lini huo uhuni wako?” aliniuliza Mick simuni nilipompigia na kumsimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea usiku ule kuhusu mimi na Evadia.
“Nipunguze nini sasa,” nilimjibu kisha nikacheka sana.
“Wewe cheka ila siku yako moja,” aliniambia Mick.
“Siku yangu ipi sasa?”
“Wewe unaona ufahari kubadilisha wanawake kama nguo ila kuna siku moja itafika utajuta kuzaliwa mwanaume.”
“Hahaha! Aisee Mick sijui kama kuna siku itafika nitapunguza uhuni yani kila siku watoto wazuri wanazidi kuzaliwa na mimi ndo kwanza nazidi kupata hisia za kuandika machombezo mazuri ili yawateke.”
“Unaona ufahari,” aliniambia Mick.
Kwa kweli nilizidi kujiona hodari katika mchezo huu wa kuwabadili wasichana kila kukicha. Mtaani pale Tandale nilipokuwa nikiishi nilikwishaibua zogo kila kona walikuwa wakinizungumzia mimi.Kitendo nilichokuwa nikikifanya cha kuwabadili wasichana kiliwakera mno hasa baadhi ya akina mama waliyokuwa wakiishi mtaa ule, waliona kama nilikuwa nikiwadhalilisha.
Hilo halikuweza kuniumiza kichwa hata kidogo sikujali lawama na maneno waliyokuwa wakiniambia kuhusu tabia yangu. Akili yangu yote niliamua kuiwekeza katika kuandika Machombezo na kuwasiliana na wanawake waliyokuwa wakijipendekeza, niliamini kipaji ndicho ambacho kilikuwa kikiniweka mjini, sikuwa na kazi nyingine zaidi ya kuandika machombezo ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa yakinilipa. Kwanini sasa nisiwekeze akili yangu huko?
Hilo ndilo lilikuwa swali langu kubwa nililokuwa nikiliuliza kila ambapo nilikuwa nikifuatwa na kuulizwa juu ya mambo niliyokuwa nikiyafanya.
Nilipomaliza kuwailiana na Mick niliamua kumtafuta Precious, Helena pamoja na wanawake wengine na wote niliweza kuwasiliana nao kwa lengo la kuwajulia hali tu!.
Kwa kweli nilijiona kuwa kidume tena kidume haswaa! Ufahari wangu ilikuwa ni kuona msichana anakuja kwangu kwa lengo la kusifia chombezo langu kisha nakuwa na mahusiano naye ya kimapenzi. Haikuwa kazi ngumu sana, nilikuwa nikikitumia kipaji changu kuwa kama muhimili katika kunirahisishia hilo.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA