SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
Kwa kweli nilijiona kuwa kidume tena kidume haswaa! Ufahari wangu ilikuwa ni kuona msichana anakuja kwangu kwa lengo la kusifia chombezo langu kisha nakuwa na mahusiano naye ya kimapenzi. Haikuwa kazi ngumu sana, nilikuwa nikikitumia kipaji changu kuwa kama muhimili katika kunirahisishia hilo.SASA ENDELEA...
“Dick mpenzi nimeshafika muda mrefu home.” alinitumia ujumbe mfupi Evadia kunijulisha kuwa alikuwa ameshafika nyumbani kwao.
“Pole sana malkia wangu.” nilimjibu na huo ndiyo ulikua muendelezo wa chatting zetu.
“Asante honey unafanyaje?”
“Nimekaa tu kitandani akili yangu inakuwaza wewe muda wote.”
“Unaniwazia nini jomoni.”
“Mambo mengi sana.”
“Kama yapi?”
“Kwanza unafanyaje?”
“Nipo kitandani tu nimejilaza kwani vipi?” aliniuliza swali ambalo sikutaka kuhangaika nalo kumjibu. Nililipotezea.
“Umelala na nani?”
“Peke yangu.”
“Haya tuendelee.”
“Mmh! Ndiyo wivu au?”
“Sasa ulitaka wivu wangu nikaupeleke wapi?”
“Hahaha! Baby.”
“Naam.”
“Nakupenda sana.”
“Nakupenda pia.”
“Kuna kitu nataka nikuombe.”
“Kitu gani?”
“Nataka ulitumie jina langu katika moja ya chombezo lako zuriii.”
“Wala usijali mpenzi ondoa shaka katika hilo.”
“Nitafurahi.”
“Kwahiyo kesho inakuaje?”
“Kuhusu nini?”
“Ina maana umesahau?”
“Nikumbushe baby.”
“Kuhusu kwenda Loliondo.”
“Hahahaha!”
“Unacheka nini?”
“Nimekumbuka.”
“Umekumbuka nini?”
“Kuhusu Party?”
“Ndiyo.”
“Jamani ndiyo useme kwenda Loliondo?”
“Ndiyo uniambie sasa inafanyika muda gani na sehemu gani?”
“Itafanyika usiku pale Club Africado Mwananyamala.”
“Sawa”
“Ila baby nataka kesho niitumie pia kukutambulisha kwa marafiki zangu of course nimeshawaeleza kuhusu wewe na wanatamani wakuone.”
“Umewaeleza nini kuhusu mimi?”
“Jinsi ninavyokupenda,” alinijibu Evadia kisha ghafla simu yangu ikawa inaita, ilikuwa ni namba ngeni iliyokuwa ikinipigia kwa wakati huo.
“Hallo,” nilisema mara baada ya kupokea, ajabu upande wa pili sikuweza kupokea jibu lolote, ilikuwa ni kama nilikuwa nikijiongelea peke yangu kwani hakukuwa na sauti ya mtu ambaye aliweza kunijibu lolote kwa wakati ule.
Ghafla! mpigaji wa simu alikata, kitendo ambacho kilinifanya niingiwe na hasira sana. Nilihisi kama aliyenipigia simu alikuwa amenitukana matusi ya nguoni, nilichoamua ni kuangalia salio langu na kuangalia kama nilikuwa nimebakiza dakika za kuweza mpigia lakini nilishindwa, sikuwa na salio kwa wakati ule, hilo lilizidi kuniweka katika wakati wa maswali nisijue ni nani ambaye alikuwa amenipigia simu hasa katika usiku kama ule.
Niliendelea kuchat na Evadia mpaka pale ambapo ile namba iliweza kunipigia tena. Safari hii sikutaka kupokea kabisa niliiacha ikaita mpaka ikakata, lakini mpigaji wa simu ile alionekana kutokata tama, aliendelea kupiga tena zaidi na zaidi mpaka pale nilipoamua kupokea, hapa ilikuwa ni baada ya kupigiwa mara nne bila kupokea.
“Hallo,” nilisema kwa sauti ya ghadhabu huku nikionekana kukasirishwa mno.
“Samahani nazungumza na Dick?” ilisikika sauti ya kike ikiniuliza simuni, ilikuwa ni sauti nyororo ambayo iligubikwa na kila aina ya nakshinakshi za kuyateka masikio ya mwanaume rijali. Sauti ile ilipenya masikioni mwangu vyema na kuzitetemesha ngoma za masikio yangu lengwa na ghafla! ile hasira niliyokuwa nayo nilishangaa ikitoweka na kutokomea kusikojulikana. Nilikuwa mpya kabisa utadhani si yule ambaye nilikuwa nimechukia dakika mbili zilizokuwa zimepita.
“Yes, ndiyo mimi sijui nazungumza na nani mwenzangu?” nilisema kwa sauti ya upole, kuna muda nilikuwa nikiigiza kuwa ya kibusara yote haya yalitokea baada ya kuisikia sauti ya mtoto wa kike aliyekuwa amenipigia, moyoni mwangu nilikuwa na shahuku ya kutaka kusikia walau neno lolote kuhusu nia na madhumuni ya simu yake, nilikuwa kama zezeta yani pindi niisikiapo sauti ya mwanamke huwa kuna vitu nahisi vinaongezeka mwilini mwangu.
“Oooh, mimi naitwa Latifa ni shabiki yako nimeona nikupigie simu maana nimeshindwa kabisa kuvumilia,” aliniambia Latifa baada ya kujitambulisha.
“Umeshindwa kuvumilia nini jamani?” nilimuuliza swali la kinafki, akilini nilikwisha fahamu kwanini alikuwa ameniambia hivyo lakini niliamua kumuuliza ili kuzidi kuleta msongamano wa mazungumzo.
“Unaandika machombezo mazuri sana,” aliniambia.
“Asante sana Latifa.”
“Ok.”
“Hivi unaishi wapi vile?”
“Mimi niko Tabora.”
“Tabora?”
“Ndiyo.”
“Sawa.”
“Karibu kwetu.”
“Asante,” nilimjibu na huo ndiyo ukawa mwisho wa mazungumzo yetu.
Ngoja nikwambie kitu ndugu yangu, katika maisha yangu nilikuwa na wasichana wengi sana, orodha yao ilikuwa ikijipanga kila siku, wala siwezi kukataa hili nina sababu za msingi za kukueleza haya, wapo baadhi ya wasichana waliyokuwa wakinifuata inbox na kuomba kuanzisha mahusiano ya kimapenzi, kwa kweli kama ilivyokuwa kawaida yangu wote niliweza kuwakubalia na nilikuwa makini katika kuwapanga ili siku moja nisiweze kuumbuka.
Kati ya hao wasichana ambao walikuwa wakinifuata kwa lengo la urafiki na mwisho wa siku tukawa wapenzi, wapo ambao walikuwa ni wa mikoani, ilikuwa ni kazi kubwa mno kuweza kuonana, mapenzi yetu yaliishia mitandaoni tu, nilikuwa
Nikiutumia muda wangu mwingi katika kuwasiliana nao humo kupitia mtandao wa Facebook, WhatsApp pamoja na Instagram hata pale lilipofikia suala la kufanya mapenzi niliamua kufanya nao mapenzi kwa njia ya simu, mapenzi ambayo naweza kujitapa kuwa nilikuwa kinara katika kuyafanya na wasichana wote ambao niliwahi kufanya nao hawakuweza kuamini kama kweli nilikuwa hodari katika hilo.
Ningeweza kusimulia japo kwa ufupi njia ambazo nilikuwa nikizitumia katika kufanya mapenzi kwa njia ya simu lakini nasikitika kuwa sitaweza kuzielezea mahali hapa kwa kuhofia usalama wa watoto wetu, naamini chombezo langu hili litasomwa na watu wengi sana, wakubwa na hata kwa wadogo pia, nisingependa kuwa sababu ya kushawishi jamii kuyafanya yale machafu ambayo nimewahi kuyafanya japo najua wengi mnanishutumu
Kuwa mimi ni muhuni niliyekithiri lakini nataka mfahamu kuwa ipo sababu ya msingi ya mimi kuwasimulia haya yaliyotokea katika maisha yangu, maisha ya ujana ambayo kila hatua niliyokuwa nikiipiga kwangu ilikuwa ni kama moja ya somo kubwa ambalo naamini ndiyo matokeo ya kazi hii unayoisoma kwa wakati huu.
Hata hivyo naomba nisiwe muongeaji sana wa mambo yaliyoweza kupita, ngoja tuendelee na mkasa wa chombezo hili uliyoweza kunikuta mimi Dick Mapenzi kama wengi wanavyonifahamu……
Baada ya kumaliza kuwasiliana na Latifa kwanza nilitabasamu, nilitabasamu kwa sababu niliamini hakukuwa na tukio lingine ambalo lingeweza kutokea zaidi ya uhusiano. Uhusiano wa kimapenzi ndiyo ambao ungeweza kutokea kati yetu.
Sikutaka kuendelea kuwasiliana naye, niliamua kuachana naye kwanza kitendo cha yeye kuweza kuniambia kuwa alikuwa akiishi Tabora kiliweza kunifanya nipoteza hata ile hamu ya kuendelea kuzungumza naye, nilihisi kutokuwa na mada ya kuzungumza na yeye zaidi ya kuzipokea sifa alizokuwa akinimwagia na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu.
“Tulale Dick wangu kesho Mungu akipenda ulale salama, nakupenda sana,” niliusoma ujumbe mfupi aliyokuwa amenitumia Evadia kisha nikamjibu jibu ambalo nililisindikiza na maneno ya kimapenzi na sikutaka kuendelea kujishughulisha chochote tena, nilianza kuutafuta usingizi.
SIKU ILIYOFUATA.
Mahali:Mwananyamala, Daresalaam.
Eneo:Club Africado.
Tukio:Siku ya kuzaliwa IRINE KISOKA.
Muda:Saa 1 usiku.
Ilikuwepo meza kubwa ambayo ilikuwa imetumika kuwekewa keki maalumu kwa mlengwa, keki ilikuwa imeandikwa “HAPPY BIRTH DAY QUEEN” maneneo ambayo sikuwa nimewahi kufahamu yalikwa yakimaanisha nini zaidi ya kuyatafsiri kama ilivyokuwa maana yake. Vinywaji vilikuwa vimechukua sehemu kubwa sana siku hiyo. Urembo nao haukuwa mbali, ulikuwa umechukua nafasi kubwa sana katika kupambia eneo lile ambalo lilikuwa likionekana kuwa la kipekee sana.
Kila mtu alionekana kupendeza machoni mwangu, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa katika mavazi ya ovyoovyo siku hiyo pale Club Africado Mwananyamala. Macho yangu kila yalipokuwa yakitazama wale wasichana waliyokuwa wametawala latika tafrija ile hakika hayakuacha kukiri na kukubali kila kitu kilichokuwa
Kikishuhudia, pua zangu nazo hazikuacha kuvuta harufu ya manukato mazuri waliyokuwa wakinukia kiasi kwamba nikazidi kuwa kama niliyekuwa katika bumbuazi fulani, nilionekana kushangaa kila kitu kilichokuwa kikendelea kwa wakati ule hasa
Katika majira yale ambayo kila niliyekuwa nikimuona alikuwa katika muonekano nadhifu si kwa wasichana wala wavulana waliyoungana kwa pamoja katika siku ile ya kuzaliwa rafiki yake na Evadia ambaye mpaka kufikia wakati huo sikuwa namfahamu kwa jina lake.
Nilikuwa mwenye shahuku ya kutaka kumfahamu kila msichana ambaye nilikuwa nikimuona pale, nilijifanya kama kipofu kutowatazama wale wavulana wenzangu ambao walionekana kuwa watanashati kama mimi nilivyokuwa, wakati huo
Evadia alikuwa ubavuni mwangu huku mikononi kila mmoja wetu akiwa ameishikilia glass iliyokuwa na kinywaji laini kisichokuwa na kilevi ambacho kilikwenda kulisafisha koo langu vyema lililokuwa limeanza kunikauka kwa
Uzembe wa kuacha kinywa wazi kwa tamaa za kushangaa wale wasichana warembo. Wakati hayo yote yakiendelea mbele yetu katika jukwaa dogo walikuwa wamesimama wanamuziki kutoka katika moja ya bendi maarufu sana hapa nchini ambayo haikuwa mbali katika kutusindikiza na mziki wao wa ‘live’ usiku huo.
“Jamani mabibi na mabwana ambao mmekubali kuziacha shughuli zenu na kuamua kuudhuria katika sherehe hii fupi ya kuzaliwa dada yetu Irine Kasoka tunaomba tuianze shughuli yetu rasmi naona mwenyewe ameshafika eneo la tukio,”
Ilisikika sauti ya mshereheshaji ikisema kupitia kipaza sauti maneno ambayo yaliniacha katika wakati wa maswali mengi, nilianza kujiuliza kimoyomoyo kuwa huyo Irine Kisoka alikuwa ni yupi.
Kwa mawazo ya harakaharaka nilianza kuijenga taswira ya yule muigizaji wa filamu za kibongo ambaye alikuwa akifanya vizuri sana hasa katika filamu zake za mapenzi alizokuwa akiigiza. Macho yangu yalikuwa makini kutaka kumuona huyo Irine Kisoka ambaye alikuwa ameshawasili eneo lile, kila mtu alikuwa akishangilia kwa wakati huo huku wakilitaja jina la Irine Kisoka msichana ambaye nilikuwa na hamu ya kutaka kumuona.
“Huyo Irine ni nani?” hili lilikuwa ni swali lililozidi kutawala kichwani mwangu.Nilizidi kutazama kwa umakini katika lango lile kuu huku nikiyapa wasaa macho yangu yapate kumshuhudia huyo Irine ambaye alikuwa akiingia kwa wakati huo.Dah! Sikutaka kuamini macho yangu.
Nilihisi kama mapigo ya moyo wangu yakienda ndivyo sivyo kwa wakati ule, nilikuwa nikimshuhudia Irine Kisoka akiingia eneo lile huku akiwa amezungukwa na wapambe waliyozidi kuweka mlolongo mrefu hata katika utembeaji wake. Sauti zilizogubikwa na wimbi la furaha zilizosindikizwa na nyimbo mbalimbali za ‘Happy Birth Day’ , ‘Happy Birth Day’ hazikuacha kumkumbusha kila mmoja wetu kuwa alikuwepo mahali pale kwa lengo gani hasa.
Hata kama ungekuwa hujawahi kupata bahati ya kutazama kwa macho hata mara moja katika maisha yako lakini kwa kupitia sauti pamoja na zile nyimbo zilizokuwa zimetawala pale hakika usingekuwa mgumu wa kutaka kuelewa kuwa kulikuwa na kitu gani cha zaidi kilichokuwa kikiendelea.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA