NIFANYE NAMIMI KAKA (28) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 26 Machi 2021

NIFANYE NAMIMI KAKA (28)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Mick akakurupuka kutoka kwenye sofa alilokuwa amekaa na kuja upande niliyokuwepo huku akiwa ameishika simu yake, alikuwa akinionyesha mahojiano yaliyokuwa yakifanyika Live kupitia Application ya Hiza Tv, yalikuwa ni mahojiano kati ya mwanaume mmoja ambaye alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari.

SASA ENDELEA...
“Unamfahamu huyu mwanaume?” aliniuliza Mick.
“Hapana simfahamu,” nilimjibu.
“Aiisee wewe mwehu kweli inamaana hata kusoma huwezi,” aliniambia kisha nikayasoma yale maandishi ambayo yalikuwa yameandikwa kwa chini, yalikuwa ni maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa rangi nyeusi na yalikuwa yakisomeka,
“MUME WA MWANAMKE ALIYEJIUA KISA SKENDO CHAFU.” Maneno hayo yaliambatana na picha ya Precious.

Sikutaka kuamini kuwa Martine Deus jina ambalo liliandikwa pale ndiye alikuwa mume wa Precious. Moyo wangu ulizidi kuwa katika maumivu makali mno, kila nilipokuwa nikimuona Martine Deus nilihisi kuchanganyikiwa.
“Tunafanyaje?”nilimuuliza Mick.
“Hapa hakuna cha kufanya zaidi ya kutoroka, inabidi uende mbali sana ukajifiche maana inaonekana mpaka sasa unatafutwa,” aliniambia Mick kisha nikakubaliana na maneno yake. Niliamini kama ningeweza kuondoka na kwenda kujificha mbali nisingeweza kukamatwa.
“Sasa natakiwa kwenda wapi?”
“South Africa.”
“South Africa?”
“Ndiyo huko ndiyo kwenye usalama wako.”
“Naenda kufikia kwa nani?”
“Kuna ndugu yangu mmoja yuko huko nitafanya mazungumzo naye kwa njia ya Email halafu kila kitu kitakuwa sawa.”
“Una uhakika?”
“Niamini,” aliniambia Mick.
Siku iliyofuata Mick alianza kunihangaikia mipango ya kusafiri kwenda South Africa. Ilikuwa ni safari ya ghafla! na nilikuwa nikienda kwa kuzamia. Hakukuwa na njia nyingine niliyoiona kuwa na usalama kwangu zaidi ya kuondoka na kwenda huko mahali ambapo niliamini kulikuwa na usalama wa maisha yangu.

Hatimaye siku ya safari ikawadia, nikaenda Airport kwa kujifichaficha, Mick alikuwa akinisindikiza lakini kitu cha kushangaza tulipofika Airport tulikamatwa na watu waliyojitambulisha kuwa walikuwa ni polisi. Walikuwa na lengo la kunikamata na kunipeleka polisi, sikutaka kubisha wala kupingana na lolote lile kwa wakati huo, safari ya kwenda 

South Africa iliishia hapo na sasa nikakamatwa na wale watu waliojitambulisha kuwa walikuwa ni polisi, wakaniingiza katika gari lao kisha tukaondoka eneo lile. 

Mick tulimuacha Airport, sikutaka kujiuliza mara mbilimbili kwanini tulimuacha. Ajabu wale watu waliyojitambulisha kuwa ni polisi nilishangaa wakinipeleka sehemu nisiyoijua, ilikuwa ni sehemu tofauti na kituo cha polisi kama ambavyo waliniambia hapo awali. 

Tulitoka nje kidogo na jiji la Daresalaam, tuliingia katika moja ya pori ambalo kiukweli mpaka kufikia muda huo sikuwa najua lolote lililokuwa linakwenda kutokea.
“Shukaaaa,” aliniambia jamaa mmoja baada ya gari kusimama pembeni na pori lile.
“Kuna nini jamani?” niliwauliza.

“Wewe unajifanya kidume subiri sasa uoneshwe kuwa hapa mjini kutembea na mke wa mtu ni hatari,” alisema yule jamaa maneno ambayo yalinishtua sana, nilifahamu kuwa wale hawakuwa polisi kama walivyokuwa wamejitambulisha. 

Nilikuwa nimetekwa na wale watu nisiowafahamu kabisa, niliposhuka na wao wakashuka. Kuna muda nikatamani kukimbia eneo lile lakini nilishindwa. Wale watu walionekana kuwa katika miili iliyojengeka kimazoezi, walionekana kutisha mno kutazama na ni hapa ambapo niliamini ule ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yangu.

Baada ya dakika kadhaa mara likatokea gari aina ya Hummer, lilikuja na kupaki pembeni na pale ambapo nilikuwa nimesimama kisha akashuka mtu aliyevalia mavazi ya suti nyeusi, alionekana kuwa mtu nadhifu sana, nilipomtazama sura yake haikuwa ngeni, niliwahi kumuona sehemu. 

Alikuwa ni yule mume wa Precious. Alionekana kutawaliwa na hasira sana, uso wake ulihifadhi chuki, alionekana kunichukia sana aliponitazama.

“Ulidhani utanikimbia?” aliniuliza kisha akawa anajilazimisha kucheka kwa sauti kubwa sana huku akiwa ananipigia makofi ishara kama ya kunipongeza jambo fulani.

“Hongera sana Dick, hongera kwa kufanikiwa kummiliki mke wangu tena kwa kuuonyesha ukidume wako ukadiriki mpaka kuzaa naye,” aliniambia maneno ambayo yaliniumiza sana.

“Nadhani ulifikiri kwa mpango aliyokushauri rafiki yako ungeweza kuwa salama, ulipanga kuondoka sasa ona uko sasa hivi?” aliniuliza swali la kunikejeli kisha nikajaribu kuyalinganisha na maneno ya Mick. Kulikuwa na uhusiano, niliamini bila shaka Mick alikuwa ameniuza na kweli alifanikiwa katika hilo.

Yule mume wa Precious hakutaka kuwa muongeaji sana, alipanga kufanya vitendo kwa wakati ule. Kitu ambacho nakikumbuka aliniuliza swali moja tu, swali ambalo majibu yake yaliweza kunigharimu.

“Umetembea na mke wangu, amekuhonga nyumba, gari na kila kitu ulichokuwa unakihitaji. Hilo siwezi kukudai wala kuhusu nyumba na gari nimeamua vibaki kuwa kama zawadi yako lakini kwa muda huu nataka uchague kati ya vitu hivi vitatu ili uweze kuyaokoa maisha yako,” aliniambia.

“Vitu gani hivyo?” niliuliza huku nikionekana kuwa na hofu, wale watu waliyokuwa wamenikamata kwa wakati huo walikuwa wamenizunguka halafu mimi pamoja na mume wa Precious tulikuwa katikati.
“Chagua Kati ya kifo yani tukuue, tukuingilie kinyume na maumbile yako au tukuchome sindano ya kuua nguvu zako za kiume?” aliniuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa gumu.

Kwa muda ambao nilikuwa nikifikiria tayari Martine alikuwa ameitoa bastola na kuninyooshea, alikuwa amedhamiria kuniua.

“No! No! usiniue,” nilimwambia kwa sauti ya uwoga kisha nikanyamaza kidogo kiasi cha kumeza fundo la mate halafu nikaendelea kuzungumza.

“Ni bora unichome sindano tu, ndiyo nipo tayari,” nilimwambia kisha akaonekana akiwapa ishara wale watu waliyokuwa wamenizunguka. Haikupita sekunde wakanikamata na kunichoma sindano.

Kwa kweli niliyasikia maumivu makali mno, nilijitahidi kuvumilia lakini uvumilivu ulinishinda mwisho nikapitiwa na usingizi wa nusu kifo.

Niliamka na kujikuta nipo hospitalini, sikujua niliwezaje kufika eneo lile. Waandishi wa habari walikuwa wamenizunguka kila kona. Nilipopata fahamu kila mmoja alitaka kuzungumza na mimi.

Nilijaribu kuzungumza nao ukweli wa kila kitu, sikutaka kuficha lolote na kitu kikubwa ambacho nilikizungumza ni tuhuma za kutembea na mke wa mtu, hilo niliweza kukiri wala sikutaka kuficha lolote.

Majibu ya daktari aliyokuja kunipa yaliweza kunipa wakati mgumu sana hasa wa kuweza kuamini. Nilikuwa nimepoteza nguvu za kiume, mishipa yangu ya sehemu za siri ilionekana kudhurika kwa kiasi kikubwa sana hasa baada ya sindano ya sumu niliyochomwa, nilikuwa hanithi kwa maana nyingine.Dah!

Nayaandika haya huku machozi yakinilengalenga machoni. Najua sitakuwa na uwezo tena wa kupata mtoto hata yule ambaye nilibahatika kumpata kwa mke wa mtu hivi sasa ni marehemu yeye pamoja na mwanaye. Uhuni wa kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe umeweza kuniacha na funzo kubwa sana katika maisha yangu. 

Naweza kusema haikupangwa mimi kuchagua kifo, au kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume wenzangu kwa kosa la kutembea na mke wa mtu. Ilipangwa yote haya yanifike ili siku moja niwe shahidi ambaye nitakusimulia kitu kilichowahi kunitokea katika maisha yangu kisha na wewe kijana mwenzangu mwenye tabia kama zangu uweze kujifunza.

Leo mimi nimekuwa hanithi na hakuna kitu kilichoniweka katika hali hii kama sio wanawake, wanawake wamenipa funzo kubwa sana katika maisha yangu.

Nimeamua kuandika kitabu changu kilichobeba uhalisia wa maisha yangu, nimekipa jina la NIFANYE NA MIMI KAKA DICK, naomba vijana wakisome ili wajifunze kitu kupitia mimi. 

Najua sina muda mrefu wa kuishi tena hapa duniani ile sumu imeweza kuniathiri kwa kiasi kikubwa sana na mpaka hivi ninavyokuandikia nimekutwa na Kansa ya ini. Najua naenda kufa lakini nakufa huku nikiacha elimu tosha kwa vijana. Naomba nisiwe mfano bora wa kuigwa.

NB: Evadia aliweza kuolewa na mwanaume mwingine na baadae walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike.

Irine na yeye aliamua kurudiana na Juma Hiza na mapenzi yao yanaendelea mpaka leo.

Nashukuruni sana kwa kulifuatilia Chombezo hili. Mungu awabariki.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

MWISHO

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni