NIFANYE NAMIMI KAKA (27) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 26 Machi 2021

NIFANYE NAMIMI KAKA (27)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Baada ya kupita dakika kadhaa Mick aliweza kufika nyumbani kwangu, nilimkaribisha kwa kumpa juice hapa ni baada ya kudai kuwa alikuwa ameshiba chakula kisha sikutaka kupoteza muda nikaanza kumwambia kile nilichokuwa nimemuitia.

SASA ENDELEA...
“Nimekuita hapa ndugu yangu nina tatizo.”
“Tatizo gani tena au kuna demu wa kishua umempata nini?”
“Acha masihara ndugu yangu ina maana unataka kuniambia hujasoma magazeti leo?”
“Hapana ujue mimi sio mpenzi sana na hayo magazeti hasa ya udaku nikisoma labda nimekosa kazi ya kufanya. Vipi kwani kuna nini?”
“Aisee ndugu yangu mambo yameharibika.”
“Mambo yameharibika! Mambo gani tena.”
“Waandishi wahabari tayari wameshaufahamu ukweli wangu.”
“Ukweli wako upi tena?”
“Wameniandika kuwa nimezaa na Precious yule mke wa mtu.”
“Duh! Sasa ni nani ambaye ameenda kuwaeleza waandishi wa habari.”
“Yani mimi mwenyewe sielewi hapa nimechanganyikiwa.”
“Na Irine naye imekuwaje?”
“Irine amekataa kabisa kunielewa baada ya kuziona habari hizi yani hapa ninavyokwambia hataki kabisa kuniona.”
“Umejaribu kuongea naye vizuri?”
“Yani nimeongea naye kila aina ya lugha lakini hataki kabisa kunisikia wala kuniona.”
“Duh! Sasa itakuwaje?”
“Sielewi Mick yani akili yangu imechoka.”
“Lakini rafiki yangu mimi nilikwambia huo mchezo wako unaoufanya kuna siku utakugharimu sasa umeona jinsi unavyotaabika wakati kazi ilikuwa ni ndogo tu!”
“Kazi gani?”
“Kazi ilikuwa ni kutulia na demu mmoja tena Evadia yote haya yasingekukuta.”
“Mick nimekuita hapa kwa ajili ya ushauri na si unikumbushie kuhusu huyo Malaya Evadia.”
“Evadia ndiyo Malaya au wewe mbona sijakuelewa hapo.”
“Mick embu tuachane na hiyo mada, tuongelee haya ambayo yanatuhusu.”
“Mimi kwa ushauri wangu hapo itabidi umtafute huyo mwandishi aliyeandika hiyo habari kisha fanya kuzungumza naye kirefu nadhani anaweza akakueleza ukweli kuhusu mtu au lengo la yeye kuiandika habari hiyo.”
“Tayari nimeshafanya mawasiliano naye.”
“Anasemaje?”
“Bado sijazungumza naye ila tumepanga kukutana sehemu kwa ajili ya mazungumzo.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo.”
“Mnaenda kukutana wapi?”
“Sunrise.”
“Mimi naamini endapo ukikutana na huyo mwandishi wa habari kila kitu kitaenda sawa hivyo jiamini.”
“Imani imepotea Mick yani nimekuwa mpole nauona mwisho wangu kwa kweli.”
“Nadhani katika hili kwako litakuwa ni funzo na tena utajifunza haswaa!” aliniambia Mick maneno yaliyopenya vyema na kuniingia akilini.

Nilimuamini sana Mick na kila ambacho alichokuwa akiniambia nilikishikilia kama ngao ambayo nilihakikisha inanikinga na kila baya ambalo lilikuwa linakwenda kunitokea. Maneno yake machache yaliyojawa na ukarimu yaliniongoza vyema japo kuna kipindi nilikuwa mkaidi nikaona ufahari kwa kubadilisha wanawake kama nguo lakini hakuacha kunisihi kuacha tabia niliyokuwa nayo.

Nilifanya yale kwa sababu ya umaarufu wangu, tangu nilipokuwa maarufu Facebook na Instagram kupitia Machombezo yangu na hatimaye nilikuwa maarufu katika kiwanda cha filamu na kuwa kama mwandishi bora wa filamu niliyekuwa napendwa zaidi.

Siku iliyofuata nilikwenda kukutana na Isack Mwakyonya mwandishi wa habari tuliyeahidiana kukutana Sunrise, nilipofika nilimtafuta na kumjulisha kuwa tayari nilikuwa nimeshafika lakini ajabu simu yangu hakuwa akipokea hata pale nilipomtumia ujumbe mfupi wa kumtaarifu kuwa nilikuwa nimeshafika hakuweza kunijibu lolote. Hilo lilizidi kunishangaza, nikaangalia vyema kama pale nilikuwa Sunrise kweli au la. 

Naam! Nilikuwa ndani ya Sunrise lakini mtu ambaye niliahidiana kukutana naye pale hakuweza kunipa ushirikiano wowote, sijui niseme katika lugha ipi ili muweze kunielewa vyema labda niseme alinidanganya au aliniuza kwa maana nyingine. Nilimsubiri eneo lile huku nikitegemea wenda angeweza kunijibu lakini haikuwa hivyo. Ukweli ni kwamba alinidanganya na baada ya kukaa masaa kadhaa bila mafanikio yoyote niliamua kuondoka.

Barabarani nilionekana kukasirishwa sana na tukio lile, sijui ni nini ila nilihisi kudharauliwa mno. Ni bora angenieleza ukweli kuliko kunidanganya. Hilo lilizidi kuniweka katika wakati wa mawazo na lawama nilizokuwa nikizitoa kama mwendawazimu.

Nakumbuka nilipofika kivuko cha Kigamboni Ferry, nilipokea ujumbe kutoka kwenye namba nisiyoifahamu, iliniandikia hivi,
“PRECIOUS AMEJIUA YEYE PAMOJA NA MTOTO WAKE.”
Nilipousoma ujumbe huo uliweza kunitatanisha, ghafla! mwili ukaanza kunyong’onyea nikaishiwa nguvu.

Kwa kweli nilikuwa nimeshaanza kuchanganyikiwa, akili yangu haikuwa sawa kabisa. Nilichoamua kukifanya ni kutafuta mahali ambapo niliweza kuegesha gari halafu nikautumia muda huo katika kuwaza kile nilichokuwa nimetumiwa katika ujumbe mfupi. Kuna muda nilijaribu kuyafumba macho yangu na kuhisi wenda nengeweza kuamka katika usingizi wa ndoto lakini haikuwa hivyo, nilikuwa katika maisha halisi, maisha ambayo tayari nilikuwa nimeanza kuyaona machungu.

“Amejiua?” nilijikuta nikijiuliza swali ambalo sikujua hata nilitakiwa kujijibuje, ni hapa ambapo nilihisi kuchanganyikiwa kabisa. Nikaichukua simu yangu kisha nikaifungua na kuingia katika kitabu cha kuhifadhi majina. 

Nilianza kupitia jina moja baada ya lingine, kwa wakati huo sikuwa najua hata nilikuwa natafuta nini. Nilikuwa nimeshapagawa ndugu msomaji. Niliwaza mambo mengi sana kila nililokuwa nikiliwaza sikulipatia ufumbuzi mwisho nilizidi kujiumiza kichwa.

Ghafla! Mick akawa ananipigia simu, haraka nikapokea kisha nikanyamaza kimya kumsikiliza kwa umakini.
“Dick ndugu yangu umeona sasa maisha yako ulivyoyaharibu, Aagghh! Ona sasa nimesikia yule mke wa mtu uliyezaa naye amejiua halafu sijui nani Precious kitu kama hicho yani Dar imechafuka kila kona ni habari kuhusu wewe,” aliniambia Mick maneno yaliyonifanya niingiwe na uwoga wa hali ya juu.
“Sasa ndugu yangu hapo tunafanyaje, eeehh! Utanisaidiaje ndugu yako niondokane na janga hili?” nilimuuliza Mick, yani hata sikuwa najua ni nini nilichokuwa nakizungumza. Akili yangu haikuwa kabisa pale.
“Yani hata sijui nitakusaidiaje,” aliniambia kisha akanyamaza kidogo halafu akaendelea kuzungumza.
“Kwani uko wapi sasa hivi?” aliniuliza.
“Nipo huku Ferry Kivukoni,” nilimjibu.
“Vipi yule mwandishi tayari umeshakutana naye na anasemaje?”aliniuliza.
“Hakuna nilichoambulia, ameniuza nimekuja mpaka huku nampigia simu ajabu hapokei wala hataki kujibu meseji zangu,” nilimwambia Mick kwa sauti ya kipole iliyoambatana na uwoga ndani yake.
“Dah! aisee pole sana ndugu yangu,” aliniambia Mick.
“Asante kwahiyo tunafanyaje?” nilimuuliza.
“Wewe si unarudi huku?”
“Ndiyo kaka.”
“Fanya tuonane ili tuzungumze kitu.”
“Mick nimekwama ndugu yangu sijui kama utaweza kunisaidia ili niweze kuondokana na fedhea hii iliyonikuta.”
“Kila kitu kitawezekana ila fanya tukutane pale Bamaga.”
“Bamaga?”
“Ndiyo.”
“Hapana Mick unajua wazi kabisa sasa hivi habari zangu zimesambaa kila kona sasa tukikutana hapo bamaga huoni itakuwa kama najiuzisha vile na waandishi wa habari wananitafuta kila kona.”
“Sasa wewe unataka tukutane wapi?”
“Mimi nafikiri tungekutana nyumbani kwangu tu.”
“Kweli basi tufanye hivyo,” aliniambia Mick.

Nilianza kuhisi Mick ndiye alikuwa mtu wa pekee ambaye angeweza kunisaidia kuondokana na janga hili ambalo lilikuwa limenipata, hofu yangu bado ilikuwa katika habari ambayo niliipata kuhusu kifo cha Precious, niliamini kwa asilimia kubwa kulikuwa kuna tukio lililokuwa linafuata baada ya hapo. Nikaanza kumfikiria mume wa Precious, sikujua kuwa alikuwa katika hali gani. 

Nilijaribu kuyapima yale maumivu ambayo angeweza kuyapata kipindi ambacho angeweza kusikia kuwa nilikuwa nikitembea na mke wake ambaye nilizaa naye mtoto aliyekuwa akimlea huku akiamini kuwa alikuwa ni mtoto wake wa damu, sikuacha pia kupima yale maumivu ya kufiwa na mke ambaye tena aliamua kujiua kwa kukiikimbia fedheha. Kwa kweli nilizidi kuziona siku za uhai wa maisha yangu zikupungua taratibu, nilikuwa nikikiona kifo changu mbele ya macho yangu.

Nilipofika nyumbani kwangu nilimkuta Mick akiwa tayari ameshafika, alionekana kunisubiria muda mrefu sana bila kuchoka. Niliposhuka kwenye gari mlinzi aliweza kunifuata na kuniletea habari nyingine ngeni kabisa. Aliniambia kulikuwa na watu watatu ambao walikuja kuniulizia, kati yao alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa amembeba mtoto, mwanaume pamoja na mama mtu mzima.

Aliponiambia hivyo nikakumbuka kama kulikuwa na watu ambao nilipanga kukutana nao kwa siku hiyo, hakukuwa na mtu ambaye nilipanga kukutana naye, nikazidi kuchanganyikiwa aliponiambia kuwa kati ya hao watu pia alikuwepo mwanamke ambaye alikuwa amembeba mtoto. Kwa kweli nikazidi kuchanganyikiwa sana, sikujua ni nini kilichokuwa kikiendelea. Akili yangu ilikuwa imechoka, nikaamua kuingia ndani na Mick.
“ Vipi ndugu yangu,” aliniambia Mick.
“Dah! we acha ndugu yangu nahisi kufakufa,” nilimwambia Mick kisha akawa anacheka kwa sauti.
“Na utakufa kweli kwa huu mchezo unaoendelea aisee usipokuwa makini tunakwenda kukusahau,” aliniambia.
“Mchezo…Mchezo kivipi na kwanini useme nitakwenda kusahaulika?”
“Usijifanye huelewi kitu Dick, usijitioe ufahamu.”
“Sielewi kitu ndugu yangu ndiyo maana nauliza, sipo sawa kabisa.”
“Sasa ukisikia ukubwa au yale maneno sijui kuwa uyaone ndiyo haya, wanawake wanakwenda kukutoa roho.”
“Dah! yani nimekoma ndugu nimekomaa.”
“Huwezi kukoma bila funzo inabidi kwanza upate funzo halafu ndiyo ukome.”
“Unamaanisha nini unaposema hivyo.”
“Muda mfupi kabla hujaingia niikuwa nafuatilia habari katika website fulani hivi…nimekuta wameandika kuwa unahusikakwa namna moja ama nyingine na kifo cha Precious ambacho kimewaacha watanzania kinywa wazi….kila mtu haamini kwa kilichotokea, sijui hata utasema nini hapo.”
“Lakini..”
“Hakuna cha lakini hapo inabidi ukubaliane na kila kitu kilichotokea.”
“Siwezi, siwezi Mick lazima nipambane katika hili.”
“Huwezi nini sasa na utapambanaje kwa kitu ambacho ni kweli kinakuhusu….ukweli ni kwamba wewe ni Malaya na umalaya wako leo unakwenda kukugharimu maisha.”
“Mick.”
“Niambie Dick Mapenzi.”
“Mi naona kama hunishauri kitu hapo na lengo la mazungumzo haya ni unishauri nini nifanye ili niondokane na fedheha hii.”
“Cha kukushauri nini ufanye kwa kweli nitakudanganya labda nikwambie kitu kimoja.”
“Kitu gani?”
“Subiri dunia ikufunze kwanza maana umeshachelewa.”
“Mick unajua sikuelewi kabisa.”
“Huwezi kunielewa kwasababu akili yako haipo hapa..inawaza mambo mengi kwa wakati mmoja, sasa utawezaje kunielewa hapo,” aliniambia Mick.

Maneno ya Mick yalizidi kunifanya niiingiwe na hasira hasa baada ya kuwa nilikuwa nikimtazama wakati alipokuwa akizungumza, kuna muda nilitamani hasira zangu zote nizimalizie kwake kwa kumpiga lakini nilihisi kukosea kufanya hivyo. Nikabaki kuwa mpole nikiendelea kumsikiliza.
Sijui ni nini kilitokea ila nilishangaa 

Mick akakurupuka kutoka kwenye sofa alilokuwa amekaa na kuja upande niliyokuwepo huku akiwa ameishika simu yake, alikuwa akinionyesha mahojiano yaliyokuwa yakifanyika Live kupitia Application ya Hiza Tv, yalikuwa ni mahojiano kati ya mwanaume mmoja ambaye alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni