SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Ni katika zoezi hili fupi ambapo niliweza kukutana na jina la Mick. Mick alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana, alikuwa ni mtu ambaye niliweza kusaidiana naye mambo mengi sana, ulipokuwa unauzungumzia urafiki wa kweli wa kufa na kuzikana basi usingeacha kuuzungumzia urafiki wangu na MickSASA ENDELEA...
Tulifanana mambo mengi sana ila tofauti yetu ilikuwa ni moja tu. Mimi nilikuwa ni mwandishi wa Machombezo lakini yeye hakuwa mwandishi wa kitu chochote. Nakumbuka nilikuwa nikimsaidia mambo mengi sana, hasa lilipokuwa linakuja suala la wanawake waliokuwa wakimtesa niliweza kulichukua tatizo lake na kumsaidia.
Nilipoliona jina lake kwa wakati ule nilishtuka sana kwani zilikuwa zimepita siku nyingi bila kuzungumza naye lolote. Sikutaka kupoteza muda, niliamua kumpigia simu kwa wakati ule, simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Safari hii nikaamua kumtumia ujumbe mfupi lakini haikuchukua dakika aliweza kunijibu.
“Mambo vipi?”
“Poa mshikaji wangu niambie.”
“Aisee mbona umekausha hivyo?”
“Mambo mengi ndugu yangu.”
“Nakupigia simu hupokei au uko na shemeji nini?”
“Hahahaha nilijua tu utasema hivyo.”
“Ulijua nini?”
“Niko peke yangu bhana.”
“Ok uko wapi sasa hivi?”
“Nyumbani.”
“Wapi?”
“Kwani wewe unajua nakaa wapi?”
“Tegeta.”
“Ndiyo.”
“Hivi wewe utakuwa lini?”
“Hahaha! Kwanini?”
“Yani umri huo uliyokuwa nao bado tu unaendelea kula ugali wa baba yako.”
“Hahaha nini wewe maisha kujipanga.”
“Ohoo shauri yako.”
“Niambie.”
“Dah! Ndugu yangu kuna mtoto ananichanganya sana akili yangu.”
“Yupi tena huyo maana wewe kila siku huishiwi na vioja.”
“Hahahaha! Mtoto mmoja wa kishua yani anapenda kusoma chombezo zangu lakini kila nikitupia ndoano anachomoa.”
“Hahaha! Sasa utafanyaje?”
“Lakini lazima nimpate tu!.”
“Sawa nakuaminia.”
“Poa.”
Nilichokuwa nimepanga kumfanyia Evadia kwa wakati ule ni kuhack akaunti yake ya WhatsApp pamoja na Facebook. Niliamua kumfanyia mchezo huo kwa makusudi kabisa kwani niliamini udhaifu wake ulikuwa katika mitandao. Alikuwa akipenda sana kuchat, kusoma hadithi pamoja na kuperuzi mambo mbalimbali katika mitandao hii.
Sikuacha kuchat naye kupitia ile namba yangu ambayo alikuwa akinifahamu kwa jina la Majaliwa Majuni, niliendelea kumtumia ujumbe mfupi wa kumchombeza huku kila siku akionekana kunipuuzia. Kuna muda alikuwa akinitukana na kuniambia kuwa alikuwa haitaji usumbufu kabisa.
Hilo halikunifanya niache kumsumbua, nilizidi kumtumia ujumbe mfupi mpaka pale siku nilipoamua kuzihack akaunti zake na kila kitu alichokuwa anakifanya nilikuwa nikikiona, kuna kipindi nilikuwa nikibadilisha ‘Profile’ yake WhatsApp na kuweka picha ya bibi kizee bila ya yeye kufahamu lolote.
“Mambo mrembo?” nilimtumia ujumbe mfupi siku moja majira ya asubuhi kwa namba yangu ambayo alikuwa akiifahamu, hapa ilikuwa ni baada ya kuzihack akaunti zake.
“Poa Dick niambie.”
“Niko poa sema umenichunia sana.”
“Hamna bhana ubize tu ndugu yangu.”
“Sawa ila vipi lakini uko fresh?”
“Niko poa ila sio sana.”
“Vipi unaumwa?”
“Hapana?”
“Nini tatizo.”
“Kuna mtu amezihack akaunti zangu yani ananifanya mpaka nakosa furaha kabisa.”
“Sasa hilo ndilo linalokuumiza.”
“Ndiyo.”
“Mbona ni tatizo dogo sana.”
“Unaweza kulitatua?”
“Ndiyo kwani wewe uko wapi?”
“Niko hapa dukani.”
“Njoo basi nyumbani kama utaweza maana hapa kuna kazi nazifanya.”
“Hivi ulisema ni wapi tena?”
“Tandale kwa Tumbo.”
“Mmh! Kwahiyo nije?”
“Ndiyo mbona unaguna sasa.”
“Hamna! Kwahiyo nikifika hapo Tandale kwa Tumbo nikwambie.”
“Ndiyo ukifika niambie nitakufuata.”
“Sawa nakuja,”alinijibu kisha nikaanza kuandaa mazingira ya chumba changu vyema kwa ajili ya mapambano, sikutaka siku ile ipite hivihivi bila kuufahamu utamu wake.
Nilichokuwa nakifikiria katika akili yangu kwa wakati huo nimapenzi tu, nilikuwa nikitamani dakika zijongee haraka ili niweze kukutana na Evadia ambaye tayari alikuwa ameshaingia katika mtego wangu.
Kitendo cha kukubali kuja katika chumba changu hakika nilikifananisha na kitendo cha swala kuingia katika njia anayopita simba kwani isingekuwa rahisi kuachwa salama. Nilimaliza kukiandaa chumba changu na sasa nilichokuwa nasubiri ni ujuio wa Evadia.
Nilijihisi damu yangu ikinichemka kwa kulitamani penzi la Evadia, wakati wote askari wangu alikuwa amesimama.
“Mbona hafiki sasa?” nilijiuliza kisha nikacheka, nilikuwa nina haraka kwelikweli. Nilipoitazama saa yangu ya mkononi ilikuwa ikisoma saa tano za asubuhi.
Wakati nikiendelea kujiuliza maswali yangu yasiyokuwa na kichwa wala miguu huku nikiitazama saa kila mara ghafla! ukaingia ujumbe mfupi katika simu yangu. Ulikuwa ni ujumbe wa Evadia, haraka nilimjibu.
“Dick.”
“Niambie Mrembo.”
“Nimeshafika hapa kwa Tumbo.”
“Umefika?”
“Ndiyo nipo hapa kituoni.”
“Umekuja na gari?”
“Ndiyo.”
“Sawa ngoja nikufuate.”
“Sawa.”
Nilichoamua kukifanya kwa wakati ule ni kutoka na kumfuata kituoni, hakukuwa na umbali mrefu sana kutoka chumba nilichokuwa naishi mpaka kituoni. Nilipofika nilimkuta Evadia akiwa ameliegesha gari lake aina ya Harier pembezoni mwa barabara, wakati huo alikuwa ndani ya gari, alikuwa ameshusha vioo. Nilitabasamu baada ya kumuona akinipungia mkono, hapa ni baada ya kuniona.
Nilipofika niliingia ndani ya gari kisha nikamuonyesha sehemu sahihi ya kuliegesha gari lake na kitu kilichofuata ni kuanza kwenda katika chumba changu. Tulitumia dakika chache hatimaye tukaweza kufika. Evadia alionekana kushangaa kila kitu. Si kwa aina ya watu aliyokuwa akipishana nao, mitaa pamoja na nyumba zilivyokuwa zimesongamana katika mpangilio mbovu.
Harufu mbaya aliyokuwa akikumbana nayo ilimfanya mpaka azizibe pua zake kwa kutumia viganja vyake. Nilifahamu yale hayakuwa maisha yake kwani hakuwa amewahi kuyaona au kuishi hivyo kila kitu alichokuwa akikishuhudia kilikuwa ni kigeni kwake.
“Mbona ulikuwa unashangaa sana?” nilimuuliza, wakati huo tulikuwa tumeshafika katika chumba changu.
“Mazingira ya huku ni machafu jamani,” alisema huku akiwa ameziba pua.
“Hahaha! karibu hii ndiyo Tandale yetu,” nilimwambia huku nikiufungua mlango wa chumba changu.
“Asante ila huku sirudi tena yani kulivyo kuchafu hivi.”
“Hahahaha.”
“We cheka tu.”
“Usiogope na huku siku moja kutakuwa kama ulaya.”
“Nani kasema.”
“Mimi ndiyo nakwambia.”
“Mh! Labda mwisho wa dunia.”
“Hahahaha.”
“Karibu sana hapa ndipo ninapoishi,” nilimkaribisha huku nikijichekesha kicheko kilichokuwa kinamaanisha umeingia mtegoni lazima unase.
“Asante sana,” alijibu huku macho yake yakiangaza sehemu mbalimbali ya chumba changu, nilifahamu alikuwa akikithaminisha kutokana na samani zilizokuwemo mule ndani.
“Karibu uketi hapo,” nilimwambia kwa kumuelekeza akae kwenye kochi.
“Asante Dick,” alisema kisha akakaa.
Alionekana kuwa na wasiwasi, hakuwa akijiamini hata kidogo kila muda alikuwa akijihisihi kutokuwa sawa. Sikutaka kuendelea kumtazama tu! kama sanamu niliamua kumuuliza.
“Mbona una wasiwasi sana?” nilimuuliza.
“Hapana sina wasiwasi.”
“Unauhakika?”
“Ndiyo.”
“Ok unatumia kinywaji gani?”
“Chochote tu!”
“Mbona hakuna kinywaji hicho.”
“Hahahaha! Bhana umeshaanza vituko vyako we niletee chochote mi natumia isipokuwa chenye kilevi situmii.”
“Sawa,” nilimjibu kisha nikalielekea jokofu dogo na kulifungua, niliitoa juice halafu nikachukua glass mbili nikamimina tayari kwa kunywewa.
“Karibu,” nilimwambia huku nikimkabidhi ile glass ya juice kwa wakati huo.
“Asante,” alijibu huku akiwa ameyalegeza macho yake madogo.
“Usijali,” nilimjibu kisha nikaichukua ile glass yangu na kwenda kukaa katika kitanda kwa wakati ule. Nilikuwa nikimtazama Evadia msichana ambaye alikuwa ameumbwa ameumbika, nilipokuwa nikimtazama nilijikuta kimoyomoyo nikijiambia kuwa duniani kuna watoto wazuri jamani.
Alikuwa amevalia suruali nyeusi iliyokuwa imembana sana, ilikuwa imemchora kila kitu katika mwili wake na kwa juu alikuwa amevaa T-shirt ambayo sikutaka kujali kuifahamu ilikuwa ni aina gani bali nilichokuwa nakitazama kwa wakati huo ni kifua kichobarikiwa maziwa yaliyojaa na kuzidi kukifanya kipendeze.
Macho yangu hayakuacha kutalii sehemu mbalimbali za mwili wake. Kuna muda nilikuwa nikizitazama zile nywele zake alizokuwa amezibana kwa nyuma, mara nikawa namtazama sura yake, rangi yake nyeupe iliyozidi kuniteka vilivyo.
“Mbona kimya?” aliniuliza huku akiendelea kunywa ile juice katika utaratibu niliyokuwa nikiupenda sana. Alikuwa akinywa kwa mapozi kama mtu ambaye alikuwa hataki kumbe alikuwa anataka tena kwa haraka iwezekanavyo.
“Nasubiria umalize kabisa,” nilimwambia huku nikimtazama.
“Nimalize nini?”
“Kunywa.”
“Mmh! We tuongee bhana siunajua nimeacha kazi kule halafu yule msichana hawezi kufanya kila kitu kuna baadhi ya vitu natakiwa nikamsaidie.”
“Haina tatizo.”
“Haina tatizo?”
“Ndiyo yani usijali.”
“Hahaha! Haya bhana.”
“Hivi ulisema kuna mtu amezihack akaunti zako?”
“Ndiyo.”
“Sasa mbona tatizo ni dogo sana.”
“Mimi sijui sasa.”
“Hujui nini?”
“Kama ni dogo au kubwa ndiyo maana nikakufata.”
“Sawa usijali kila kitu kitakuwa sawa.”
“Sawa,” alijibu kisha nikaendelea na mchezo wangu wa kumtazama mpaka pale alipoanza kunionea aibu.
“Bhanaa usinitazame hivyo mi naona aibuu,” aliniambia kwa kuigiza sauti ya kitoto huku akijiziba uso wake kwa kutumia viganja vyake nilivyoviona kuwa laini sana.
“Basi sikutazami tena,” nilimwambia kisha nikamalizia kunywa ile juice wakati huo yeye ndiyo kwanza alikuwa nusu glass.
“Unakunywa kwa mapozi,” nilimwambia kwa kumchombeza.
“Ndiyo sasa unataka ninywe kama ninakimbizwa?” aliniuliza kisha akacheka kicheko kilichoniambia nipunguze ukali wa maneno, nilielewa na haraka niliendelea kumchombeza katika mtindo wa maneno ambayo ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuelewa nilikuwa nikimaanisha nini.
“Sasa si unakunywa hata kwa haraka jamani je, kama unaachwa na gari?”
“Umeshasema gari.”
“Kwahiyo huwezi kunywa harakaharaka.”
“Siwezi kabisa.”
“Kweli wahenga hawakukosea kusema.”
“Kusema nini?”
“Maneno yao.”
“Maneno gani?”
“Vitu vizuri kuliwa havitaki haraka sana sharti ule taratibu ili ufaidi kila kitu.”
“Hahahaha.”
“Unacheka tena.”
“Sasa kwani nimekatazwa kucheka?”
“Hahahaha.”
“Unapenda kula vitu vitamu?”
“Sana tu!”
“Wewe ni mzoefu na kula vitu vitamu?”
“Ndiyo.”
“Nitajie vitu vitamu ambavyo umewahi kula.”
“Vipo vingi mbona.”
“Kama…”
“Vingi sana.”
“Nitajie sasa.”
“Hee! kwani mpaka uvijue?”
“Ndiyo kwani kuna ubaya?”
“Hapana.”
“Hapana nini?”
“Hamna!”
“Umewahi kula asali?”
“Mara nyingi tu!”
“Umeionaje?”
“Tamu.”
“Utamu wake unakujaje?”
“Sijakuelewa.”
“Kila mtu ana aina yake ya ulaji wa asali. Mwingine akichanganya na chai ndiyo anahisi utamu, mwingine akipaka kwenye mkate ndiyo anahisi utamu, mwingine akiilamba yenyewe ndiyo anahisi utamu sasa wewe upo kundi lipi hapo?”
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA