UZOEFU (1) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 31 Machi 2021

UZOEFU (1)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA KWANZA
'Grrrrrrriii! grrrrrrriiii!' Huo ulikuwa ni mlio wa simu yangu ikitimiza wajibu wake wa kuniamsha saa kumi unusu za usiku.Kabla ya kulala ilinibidi nitegeshe vyema alarm ya simu yangu kukwepa usumbufu wa kulala kisungura,kungojea muda wa kuamka.
Siku hii ilibidi niamke mapema kabisa tofauti na siku nyingine,hii ni kutokana na umuhimu wa ratiba yavsiku hiyo.
Haraka haraka nilijiandaa na takribani dakika zisizopungua ishirini nilikuwa tayari kwa kuianza safari yangu.

"Mamaa....mamaa.....!?" Nilitaka kuondoka lakini ghafla nikakumbuka kuwa sikuaga,nikaelekea kwenye mlango wa chumba cha wazazi ,nikaanza kuita.
Haraka haraka haina baraka,nilijiwazia mwenyewe hasa baada ya kukumbuka umuhimu wa baraka za wazazi hasa katika safari kama hii nnayohitaji kufika salaama.

"Mbona umeamka usiku saana!?" Mama alilalama kwa sauti ya uchovu alipokuwa anakuja kufungua mlango.
"Mama wee mwenyewe si unapajua Ubungo palivyo mbali!sikawii kuachwa na basi!" Nilijitetea na kueleweka.
"Haya nenda salaama mwanangu mi hata sikutoi narudi zangu kulala" Aliongea mama huku akipiga miayo na kuniongezea kiasi kidogo cha fedha.

"Hii utakunywa soda njiani na hii utawachukulia wadogo zako zawadi!" Aliongea huku akinipa pesa hizo kwa mafungu.
"Ahsante mama,mbaki salaama!" Niliaga haraka haraka na kuanza kuondoka.
"Wewe!..umekumbuka kusali!?" Mama aliniuliza huku akinifwata nyuma nilipokuwa nataka kutoka mlango wa nnje.
"Ndiooo ndiooo niliomba!" Nilijibu haraka haraka huku nikiendeleaaa kufungua mlangoo.Lakini ukweli ni kwamba sikukumbuka kufanya hivyo lakini sikutaka kumpa nafasi hiyo mama kwani nilifahamu fika ni mtu wa sala ndefu lakini nikala kiapo cha moyoni kuwa sitaianza safari bila kusali mwenyewe.

Hadi inatimu majira ya saa kumi na mbili kamili za alfajiri, tayari nilikuwa nimeshawasili Ubungo na tayari nilikuwa ndani ya basi la NBS.Basi mahususi kabisa kwa safari za Dar es salaam,Tabora.Kama kawaida nilikuwa kwenye seat ya dirishani.Nipo tayari kughairi safari kuliko kuikosa seat hiyo,Kwani mbali na kufika nnapokwenda huwa napenda sana kuangalia manthari ya nnje, huwa navutiwa sana kuona jinsi nchi hii ilivyobarikiwa achilia mbali miti kurudi nyuma.

Baba na mama hawakuweza kutambua ni kwa nini haswa niliishupalia na kuibebea bango safari hiyo ya Tabora.Mji tulioishi miaka minne iliyopita kabla ya baba kuhamishiwa kikazi jijini Dar es salaam.Tangu ni hitimu kidato cha nne sikuwa ni wimbo mwingine zaidi ya 'nataka kwenda Tabora'.Ingawa Shule nilihitimu mkoani Kilimanjaro.Wazazi wangu walijua ningekuwa na hamu ya kukaa na kutulia Dar kipindi hicho cha kusubiria matokeo yangu ya Kidato cha nne lakini kinyume na matarajio yao walishangazwa sana na nia yangu ya kutaka kwenda Tabora.

"Inamaana umewakumbuka sana ndugu zako wa Tabora kuliko sisi wazazi wako?"Ilifikia kipindi mama aliniuliza maswali ya namna hiyo lakini sikuwa na majibu ya msingi zaidi ya kuendelea kuwasisitiza kuwa nataka kwenda Tabora.
Kama ilivyo ada mtoto haombi mkate akapewa jiwe.Wazazi wangu hawakuwa na kingine cha kunipa nifurahi kwa wakati huo zaidi ya nauli ya kwenda Tabora na ndivyo walivyofanya.
Furaha ilioje kwangu.

Hadi kufikia majira ya saa mbili asubuhi,basi lilikuwa limeshakolea mwendo na hadi kufikia muda huo tulikuwa tumeshapita mji wa Morogoro na dereva alinifurahisha sana kwa mwendo wake kwani ulikuwa na nia ya kutufikisha mapema.Mimi binafsi huwa sipendi sana kufika ugenini usiku!.

Baada ya basi kwenda mwendo mrefu,earphone zilizokuwa zinapiga mziki zilikuwa zimeshayachosha masikio yangu.Muda huu nilihitaji kitu tofauti.Nikawaza kuanzisha mazungumzo na abiria mwenzangu tuliyeketi seat moja lakini roho ikasita nilipokumbuka kuwa hatukusalimiana alivyokuja.Hivi nani anatakiwa kuanza kumsalimia mwenzake,yule aliyekutwa ama yule aliyemkuta? Nilijiuliza swali hilo na jibu nililolipata kwa haraka ni yule aliyekukuta.Sasa kwanini huyu binti alipokuja hakunisalimia? Hilo ni swali lingine lililonigonga kichwa na kukosa majibu! Baada ya kufikiri hayo punde nilikumbuka kuwa mbali na mp 3 niliyobeba pia nilibeba na vitabu viwili vya hadithi.

Huwa napenda sana kusoma vitabu mbali na kusikiliza mziki. Kumbu kumbu hiyo ikawa furaha katika kichwa changu na kujenga tabasam katika kinywa changu.Kitendo bila kuchelewa nikasimama na kuchomoa vitabu hivyo vilivyokuwa kwenye begi langu dogo nililolitoa kwenye carrier ya basi,Baada ya kukaa na vitabu hivyo kwenye seat yangu nikaviangalia punde kabla ya kuchagua kipi cha kuanzakusoma.kimoja kilikuwa ni Riwaya ya ORODHA YA SHETANI na kingine kilikuwa ni Tamthilia ya WAHUNI WA KITAA.vyote vimeandikwa na Mtunzi mahiri katika fani hiyo,Elisha Msafiri.Baada ya kuviangalia kwa muda nikaamua nianze na Orodha ya Shetani ambayo nilikuwa nimebakiza kurasa chache kabla ya kumaliza.

"Excuse me!" Ilikuwa ni sauti nyororo ya yule binti kigoli niliyeketi naye seat moja na nilipogeuka kumtazama alikishika kitabu cha Wahuni wa kitaa akiwa na maana anakihitaji akione.
"Nawewe ni mpenzi wa vitabu eeenh!?" Nilimuuliza huku nikiwa nimemuachia akivute kitabu hicho toka juu ya mapaja yangu kilipokuwa.
"Yeah napenda sana kusoma!" Alinijibu kwa sauti tamu huku akiangalia kwa umakini picha ya juu ya kitabu hicho na huo ndio ukawa mwanzo wa mazungumzo yetu.

Tulizungumza machache tu kuhusiana na uzoefu ws safari kisha kila mmoja akaendelea na yake.
Nilipokuwa nikiendelea kusoma nilikumbuka mfukoni nna chew gum (big g )nzuri aina ya P.K.
"Hey karibu P.K!" Nilimwambia abiria mwenzangu tuliyeketi naye seat moja,baada ya mimi kuchukua vipande viwili na yeye nilimpa viwili vilivyobaki.
"Wow! I like this..thanks!!"(wow! Nazipenda hizi ..ahsante!) Alinishukuru baada ya kupokea kipaketi kidogo cha P.K nilichomkabidhi.

"Mi nazipenda sana hizu huwezi kunikosa nazo mfukoni!"
"I think me more (nafikiri mi zaidi)aisee hunishindi kwa hilo!' Aliongea binti huyo huku akipendelea zaidi kuziunda sentensi zake kiswanglishi (Nusu kiingereza nusu kiswahili)
"You know what!?(Unajua nini?)" Nilimuuliza binti yule swali lililovuta umakini wake.
"What!?"(nini!?) Naye alijibu kwa haraka kuonyesha kuwa ana hamu ya kutaka kusikia kutoka kwangu na ingawa alinikazia jicho kiasi cha mimi kuona haya sikusita kuendelea na nilichokusudia.

"Unajua sijapenda kabisa nilivyokuita hey! Yaani sijapenda kiukweli!" Nilimpa maelezo hayo makusudi kwa nia ya kutaka kujua jina lake nami nashukuru akawa muelewa katika hilo.
"Ooooh my God(Ooooh Mungu wangu) mi naitwa Beatrice au kifupi you can call me (Unaweza kuniita) Bite!" Aliongea binti yule kwa mtindo ule ule wa kiswanglish kitu kilichonifanya nifikiri atakuwa kasomea shule za English medium ama atakuwa mpenzi wa kuangalia Tamthilia.

"Love bite sio!?" Nilimtania naye akaangua kicheko.
"Acha utani bwana!"
"Nimefurahi kukufahamu Bite!"
"Nice to meet you too but you did'nt tel me your name(Nimefurahi pia kukutana na wewe lakini hujaniambia jina lako)"

"Ha ha ha! Nilijua hutaniita ndomana!" Nilicheka kicheko cha kutengeneza alafu nikamtania tena!.
"Ooh! Come on!...you can't stop joking (Ah jamani huwezi kuacha utani?)"
"Ok mi naitwa Tom!"
"Thomas?" Aliniuliza akizani ndo kirefu cha jina langu.
"Nop! Only Tom!" Nilimjibu kwa kiingereza cha mbwe mbwe kwasababu ndio lugha aliyeonekana kuipenda japo sikuongea kama mzungu lakini somo hilo shuleni sikuwahi kupata f.
"Jina lako fupi nimelipenda!"
"Ahsante!"

Baada ya kuzungumza hayo nilibobea tena katika kitabu changu na nilipomaliza zile kurasa chache zilizokuwa zimesalia nilimuangalia tena Bite kwa jicho la wizi na nilipoona na yeye yupo bize katika kusoma kile nilichompa sikutaka kumsemesha neno nikaamua zangu kulala.

"Tom...Tom......wee Tommmm!?" Nikiwa katika usingizi mzito nilihisi bega langu kutikiswa na kwa mbali nilisikia sauti ya kumtoa nyoka pangoni ikiniita.
"Asee unalala bwana yani ningeamua kukuuza hata hizo hela ningekuwa nimeshatumia zimeisha!" Bite alinitania mara tu baada ya kufumbua macho.
"Yaani ungejua nilikuwa naota nini hata usingeniamsha!" Nilichimba mkwara kupotezea mada ya mimi kulala fofofo maana usingizi ulinikamata kweli si mchezo.
"Kwani umeota nini!?" Aliniuliza kwa hofu Bite kuonyesha kuwa ameogopa mkwara mbuzi niliomchimba.

"Mwenzako nimeota shafika Tabora tena nilikua nasalimiana na mtu muhimu kweli!" Nilimwambia hivyo makusudi ili kumpima kama ana wivu na mimi na kweli alikuwa nao.
"Ulikuwa unasalimiana na nani huyo!"Aliniuliza kwa upole na mimi nikajua tayari ameshafikiria kingine.
"Sii mkuu wa mkoa!" Nilimtania tena naye hakujibu kitu zaidi ya kunipiga kikofi cha upole begani mwangu.
"Kwani hapa ni wapi?"Nilimuuliza huku nikichungulia dirishani kana kwamba naweza kupajua.
"Nimesikia wanasema ni Gairo,tushuke bwana tutachelewa!"
"Sasa sikia mi siwezagi kula njiani, naomba ukishuka uniletee azam mango kubwa pamoja na...."Niliongea huku nikitoa pesa kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yangu lakini kabla sijamaliza akanikata kauli.

"Ah jamani mie mwenyewe naona uvivu ndomana nimekuamsha ili twende wote!" Alilalama Bite kwa sauti iliyobanwa na pua zake kisha akanishika mkono tushuke,nikajikuta nalegeza msimamo wangu wa kutokushuka.
Baada ya kula na kuchimba dawa,tulirejea tena kwenye gari,Ndani ya muda mfupi mimi na Bite tulikuwa tumeshajenga na kuukuza urafiki wetu kiasi cha kumfanya abiria yeyote humo ndani ya basi kuzani kuwa safari yetu ilikuwa ni moja.lakini ukweli ukabaki mioyoni mwetu.

Ingawa karibu kila mtaa wa Tabora nilikuwa na ndugu lakini nilichagua kufikia mtaa wa Mwinyi,Mtaa niliokuwa naishi na wazazi wangu kabla ya kuhamia Dar,Mtaa ambao ndio haswaa umeibeba stendi ya mji wa Tabora,Mtaa ambao wenyeji wa hapo wanapaita mjini lakini sikuamua kufikia mtaa huu tu kwajili ya umaarufu ama umashuhuri wake,Naam,ndani ya mtaa huo kulikuwa na kitu cha ziada nilichokifuata,Kitu kilichoutesa moyo wangu kwa muda wa miaka minne,Kitu ambacho niliamini ni sehemu ya maisha yangu,kitu ambacho sikuwa na uhakika kama ntakikuta ama la!,lakini hilo halikuwa neno kwangu cha msingi ilikuwa ni mimi kufika kwanza.

Hadi majira ya saa kumi na mbili unusu za jioni, tayari basi lilikuwa limeshatia nanga ndani ya stendi ya Tabora.
"Alhamdulilah tumefika salama!" Niliongea huku nikijishosha kivivu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni