UZOEFU (2) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 31 Machi 2021

UZOEFU (2)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
Hadi majira ya saa kumi na mbili unusu za jioni, tayari basi lilikuwa limeshatia nanga ndani ya stendi ya Tabora.
"Alhamdulilah tumefika salama!" Niliongea huku nikijishosha kivivu.
SASA ENDELEA...
"Mbona hushuki sasa!?" Bite aliniuliza huku na yeye akiwa bado amekaa.

"Nasubiri wenye haraka zao washuke kwanza afu mimi ntashuka taraaatibu kwa raha zangu nna haraka gani bwana tumeshafika!" Nilimjibu Bite kwa maneno mengi na muda wote alikuwa akinitazama kwa jicho lenye alama ya ulizo lakini mimi sikutaka kufungulia mazungumzo yoyote kwa wakati huo.

"Tom?" Bite aliniita baada ya kuniona nipo kimya.
"Nambie!" Niliitika huku nikimtizama usoni.
"Unakaa mtaa gani!"

"Yaani mimi ndio nimeshafika tayari nakaa mtaa huu huu!" Kwa kuwa alishazoea kutaniwa alijua hata hili namtania lakini nilijaribu kumuhakikishia.

"Ok! Can i get your number!(Naweza kupata namba yako)" Aliniuliza tena Bite lakini hapa nilitaka kumruka, nilijua nikiendeleza mawasiliano na yeye huenda urafiki wetu ungevuka mipaka jambo ambalo sikupenda litokee ndani ya mji huu.

"Oh am sorry!(oh samahani) zijazishika kwa kichwa afu simu yangu imezima chaji!" Nilimdanganya huku nikiwa napapasa mifuko yangu kana kwamba naitafuta simu.

"Ah jamani sasa itakuwaje?" Bite akawa mpole ghafla huku akionyesha kuamini nilichomwambia.
"Wee ntajie tu zako mi ntazishika!" Nilimpa moyo baada ya kuona amezama kwenye dimbwi la mawazo ili kuipotezea mada hiyo lakini akaonekana kunishtukia.

"Come on Tom! Za kwako tu hujazishika zangu ndo utaweza!" Point yake hiyo ingekuwa na mashiko iwapo kweli ya kwangu ningekuwa sijaishika lakini usilolijua ni sawa na kiza kinene laiti angejua hakuna mtu mwenye kichwa chepesi kwenye kushika namba kama mimi wala asingesema.lakini alikuwa sawa kwa asilimia mia kwani alifwata nilichomwambia.

"Ok let me do something!"(sawa acha nifanye jambo fulani) Aliiongea kwa furaha na kufungua mkoba wake kisha akachana kikaratasi kidogo kwenye notebook yake na kuandika namba zake.

"Make sure (fanya hima) unanitafuta Tom!" Alinisisitiza alipokuwa ananikabidhi kile kikaratasi.

Nilimjibu asijali huku kimoyo moyo nikimsifu kwa kuweza kutembea na vitu muhimu kwenye mkoba wake,ni rahisi sana kukuta lipstick kwenye mkoba wa msichana kama yeye lakini si kalamu pia ni rahisi kukuta make up lakini si notebook alionyesha kidogo alikuwa ni mtu makini.

"Byee Tom! Tutaonana siku ingine" Aliniaga Bite baada ya kushuka kwenye basi na kupanda gari la ndugu zake waliokuwa wamekuja kumpokea stendi hapo,nami sikuongea kitu ila kumpungia mkono tu kisha baada ya kumsindikiza kwa macho hadi kuhakikisha amezamia niliitoa simu yangu mfukoni na kuiwasha ili na mimi nimtafute mwenyeji wangu

"Ama kweli dunia haina usawa yani wee ukiwa unalia njaa kali mwenzako anatafuta kiwanja ajenge ghorofa!" Nilijikuta najiwazia peke yangu wakati natafuta namba ya bamdogo wangu kwenye simu ili aje anichukue hapo stendi.Japo nilikuwa nimeishi mjini hapo kwa miaka chungu tele,

Kitendo cha kuondoka miaka minne tu kilitosha kabisa kubadisha manthari na mfumo wa maisha katika mji wa Tabora.Kulikuwa na majengo mengi mapya pamoja na maduka makubwa yaliyonichanganya kiasi cha kupoteza kumbu kumbu kabisa.Si mashariki tu na magharibi hata kusini na kaskazini sikujua ziko upande gani..

Si mazingira pekee yaliyokuwa yamebadilika bali hata watu wengi niliowaona walikuwa ni wageni machoni mwangu.Licha ya kutaka kufika nyumbani kwa mtindo wa kuwashangaza (kuwasuprize) nilishindwa kutokana na mabadiliko niliyokutananayo.

"oh karibu mwanangu!!...umekuwa mrefuu!" Hiyo ilikuwa ni sauti ya bamdogo akinishangaa kwa muda kitambo kabla ya kunikumbatia kwa furaha.
"Enhee! habari za Dar es salaam?"

"Nzuri tu baba tunamshukuru Mungu!" Tulizungumza mawili matatu na bamdogo huku tukitembea kuelekea nyumbani safari ambayo ilituchukua dakika tatu kabla ya kufika.

Tulipofika nyumbani mamdogo pia alifurahi sana kuniona na watoto wao wawili wadogo walikuwa wakinirukia rukia muda wote sijui ni kwajili ya kunipenda kaka yao,ama zawadi nilizowapa.

Baada ya kusalimiana na familia hii ya baba mdogo nilionyeshwa chumba cha kulala kisha nikaandaliwa maji ya kuoga,na kama ingekuwa ni hiyari yangu basi ningechagua nisioge hasa kutokana na hali ya hewa ya baridi niliyoikuta mji huu tofauti kabisa na ya Dar ninapotokea ila kwa kuwa ni mgeni sikuwa na budi kuwaridhisha wenyeji wangu hata kama mimi moyoni sijaridhia.

Ukiwa mgeni bhana huna tofauti na mtumwa, nilijiwazia nilipokuwa najifunga taulo kwenda bafuni.

Baada ya kumaliza kuoga na kupumzika kidogo.Saa iliyo kuwepo ukutani ilitoa mlio mara tatu na nilipoitazama ilisema ni saa tatu za usiku.

Naam ilikuwa ni muda muafaka kabisa wa mamdogo kuandaa chakula.

Kuku ni mtamu lakini ladha yake inazidi mara dufu unapoambiwa umechinjiwa wewe.Jogoo nililochinjiwa pamoja na ubwabwa wenye kutiwa nazi vilinifanya niufurahie usiku ule.

Japo Bamdogo na mkewe walifurahia uwepo wangu ndani ya mji wao,mimi nilifurahi mara mia zaidi hasa ukizingatia shughuli iliyonileta mjini hapo.

nkooh! nkoooh! nkoooh!

Ilikuwa ni sauti ya mlango wa chumba nilicholala ukilalamika baada ya kugongwa konzi kadhaa,,na lawama zake zikafika hadi kwenye ngoma za masikio yangu na kuniamsha katika usingizi mzito niliokuwa nimelala,nilijaribu kufumbua macho lakini nikayafumba haraka kutokana na kumulikwa na nuru ya mwangaza wa jua iliyosheheni chumbani hapo.

"Hee! pamekucha mara hii!" nilijikuta nikishangaa mwenyewe baada ya kufumbua macho kwa mara ya pili na kuangalia saa iliyokuwepo kwenye simu yangu,saa iliyoniambia imetimu saa nne asabuhi.Siku hiyo nilikuwa nimelala sana,sijui ni kwajili ya uchovu wa safari ama utamu wa godoro la kitanda kipya nilichokilalia.

"Tom!?...Tom?" yule aliyekuwa akigonga mlango sasa alikuwa hagongi tena ila alikuwa anaita na sauti yake niliweza kuitambua mara moja alikuwa ni bamdogo.Haraka nikanyanyuka toka kitandani na kuanza kutafuta pensi ya kuvaa kwani huwa nna utamaduni wa kulala na boxer pekee,huwa sipendi bughuza ya kubanwa banwa na nguo nikiwa usingizini.

"Haya mi natoka!..nilikuwa nataka tu kujua kama umeamka salama!" Aliongea bamdogo baada ya kuona naitika tu bila kufungua mlango na mimi ikanibidi nikubaliane nae kwani hadi muda huo sikuwa nimeipata pensi na nisingeweza kufungua mlango hali nikiwa na boxer pekee.

Nilisikia vishindo vya bamdogo akiondoka lakini pia nilisikia mtetemo (vibration) ya simu yangu ikiingiza jumbe fupi mfulululizo,nikaamua kuachana na kibarua changu cha kutafuta pensi na kuhamia kwenye simu.

"Aarrrrgh!"nilighazibika mwenyewe mara baada ya kukuta ni jumbe (messages) za 'kufowadiwa' nikaitupa simu kitandani na kwenda kuendelea na shughuli yangu ya awali,sinaga muda wa kusoma jumbe za kufowadiwa kabisa.

Baada ya kuipata pensi yangu nilitoka nnje kusafisha kinywa (kupiga mswaki)
Nikiwa katika kusafisha kinywa mbele ya macho yangu niliiona nyumba ya kina Lisa.Nyumba iliyokuwepo baada ya kupita nyumba moja kisha kuvuka barabara ndogo.

Nilisitisha kibarua cha kusafisha kinywa na akili yangu ikanirejesha miaka kadhaa nyuma.Kipindi hicho mimi nikiwa nasoma darasa la tano kwenye shule ya msingi Isike huku Lisa akiwa anasoma darasa la nne katika shule ya Westland zote zikiwa mkoani Tabora ila zikitofautishwa na hadhi.Isike ikiwa ni saint Kayumba na Westland ikiwa ni English Medium ni katika kipindi hicho ndipo tulipohamia 

Kwenye nyumba yetu mtaa wa Mwinyi.Na bahati pekee kwangu katika mtaa huu ilikuwa ni kuishi karibu na nyumba ya kina Lisa na nyumba zetu zilikuwa zikitenganishwa na nyumba moja tu iliyokuwa katikati lakini ujirani wetu ukabaki pale pale.Mwanzo nilikuwa na marafiki wengi katika mtaa huu,lakini kadrii Urafiki wangu na Lisa ulivyozidi kukua na kukomaa ndivyo nilivyopoteza marafiki wengine.

Wengi walikuwa wakimshutumu Lisa kuwa anadharau na anajidai labda kwa kuwa alikuwa akisoma international school.Lakini sababu hizo kwangu hazikuwa na mantiki yoyote kwani tangu nimemjua Lisa hakuwahi kunidharau wala kujidai mbele yangu.

Hivyo niliona kuwa sababu zao hazina maana kitu kilichosababisha wanitenge na mimi,sijui ni kwa kuona wivu ama chuki binafsi kutokana na upendo wetu mimi na Lisa.Hayo yote mimi sikujali nilijali jambo moja tu,kuwa na lisa.

Tabia hujenga mazoea,mimi na Lisa tulijenga tabia ya kuwa pamoja kila uchwao kiasi kwamba ilifikia mahali Lisa aliposhushwa na basi lao la shule alipitia kwetu kwanza na baada ya kuniona alienda kwao tu mara moja kwajili ya kubadilisha nguo za shule kisha akarudi tena tukacheza na kushinda pamoja hadi nuru ilipolikaribisha giza na usiku kututenganisha,tuliagana kishingo upande huku kila mmoja akitamani pawahi kukucha ili kesho tuonane tena.

Upendo wetu ulishamiri kiasi cha kuwa gumzo mtaani.Wengi waliamini hakuna kilichobaki kati yetu ambacho hatujafanya na wengine wakatuchukulia kama watoto tu.

Urafiki wangu na Lisa ulikula ukashiba hivyo kuzifanya hata familia zetu kuwa rafiki pia.Mimi nilishinda na hata kula kwa kina Lisa na wazazi wangu hawakuwa na shida halikadhalika Lisa alifanya vivyo hivyo kwetu na wazazi wake hawakuwa na tabu.

Ilifikia hatua hata nikae chumbani na Lisa hakuna aliyekuwa na shaka yoyote na hata nimpakatie Lisa kwenye bembea hakuna aliyehoji.Pamoja na michezo mimi na Lisa tulikuwa tukishirikiana hadi kwenye masomo.Mimi nilimfundisha hesabu na yeye akanifundisha kuumba sentensi kwa kiingereza.

Hakika mimi na Lisa tulipenda sana lakini hakuna aliyewahi kumwambia mwenzake kuwa anampenda ila nafsi na vitendo vilithibitisha hilo.Ilikuwa ni rahisi sana Lisa kununa iwapo ataniona na msichana mwingine halikadhalika na mimi sikujisikia vyema nilipoona kaambatana na mvulana mwingine.

Hakuna kitu kinachofanywa na wapenzi ambacho mimi na Lisa hatukuwahi fanya na ingawa tulishafanyiana hadi massage tukiwa nusu uchi hatukuwahi kudiriki kufanya ngono.Naam,hayo ndiyo yalikuwa maisha yetu ya kila siku mimi na Lisa kabla ya siku moja mimi kupokea habari mbaya.

Nakumbuka vizuri ilikuwa ni siku moja jioni,nikiwa bado nasubiri matokeo yangu ya mtihani wa darasa la saba ndipo siku hiyo jioni baba aliponiita na kuniambia kuwa amepata uhamisho (transfer) ya kikazi hivyo mapema siku inayofuata tungekuwa safarini kuelekea Dar es salaam.

Ingawa habari hiyo kwangu aliileta kwa kila namna ya bakshaksha na furaha lakini kwangu ilikuwa ni sawa na kumwagiwa spirit kwenye kidonda kibichi.nilihisi uchungu usioelezeka moyoni mwangu.

"Wewe si ndio kila likizo unaliliaga kwenda Dar mbona uko hivyo sasa!" Baba aliniuliza baada ya kuniona nimepoa kama nimemwagiwa maji ya baridi.Hakujua akili yangu yote kwa muda huo ilikuwa kwa Lisa.Wapi ningempata kama Lisa.Msichana aliyetokea kuuteka moyo wangu.

Ingawa nilikuwa simlaumu baba kwa kuhamishwa kwake kikazi lakini nilimlaumu kwa kuchelewa kunipa taarifa hiyo hadi dakika za majeruhi,Sijui alinichukulia mimi ni mtoto sipaswi kujua ama aliwaza nini.

Nikataka kumkoromea juu ya hilo lakini isingesaidia kitu hasa ukizingatia sikio halizidi kichwa,Nilielekea chumbani kwangu muda huo huku machozi yakinilenga,sikumbuki kama kabla ya siku hiyo nilishawahi kupokea habari mbaya namna hiyo.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni