UZOEFU (10) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 4 Aprili 2021

UZOEFU (10)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
"Ila Tom sema kweli,Lisa ni dame wako ama sio!?" Dora aliniuliza swali ambalo sikutaka kulijibu maana kama ningejibu ndio ningekuwa nimempa mada mpya ya kunitania na kama ningejibu hapana ningevunja kiapo cha Lisa kuwa sitakaa nimkane maishani mwangu.Sasa iweje nimkane mbele ya Dora hali yakuwa na mimi niliapa mwenyewe.
SASA ENDELEA...
"Kwanini unauliza hivyo!?" Badala ya kujibu swali na mimi nikauliza swali.
"Nilitaka kujua tu sababu nawaonaga wote alafu simpendi yule mtoto yaani simpendi kweli!"
"Khaah!..sa kwanini unamchukia!?"

"Sio kama namchukia lakini simpendi tu ana pozi nyingi,dharau kama ameshuka toka juu bhana!" Dora alianza kunieleza sababu kwanini anamchukia Lisa.

"Sema kwa kuwa hamjazoeana tu lakini Lisa ni mtu poa sana!" Nilijikuta nashindwa kuvumilia tuhuma hizo juu ya mpenzi wangu na nilianza kumtetea lakini nilipokumbuka kuwa naongea na mtu wa aina gani nilisitisha zoezi hilo la kumsafisha Lisa.

"Vipi kitabu lakini mambo yanakwendaje!" Nilichomekea mada nyingine ambayo Dora hakupenda kuijadili zaidi, mara nyingi nnapokutana na huyu binam yangu huwa anapenda kuongelea hadithi za mapenzi.

"Sasa tuhamie ndani basi hapa nimeshamaliza!" Dora aliongea huku akibeba beseni la vyombo.Hiyo ni mara baada tu ya kulijibu kwa kifupi swali langu lililohusu habari za shule.

"Sisi hatuna dijitali bhana njoo chagua cd hapa ya kuangalia!" Dora aliniambia huku akiwasha video ( luninga).

"Weka cd yeyote ya music yenye nyimbo kali lakini!" Nilimuamuru Dora naye akafanya hivyo.

" Sasa nakuja dakika mbili basi!...hata huu wimbo hauishi!" Aliniaga Dora mara baada ya kuweka cd hiyo na mimi nikamkubalia kwa kutikisa kichwa.

Zile dakika mbili zikawa kumi na ule wimbo mmoja zikawa nyimbo tatu yaani ina maana ya kuwa Dora alichelewa kurudi.

"Haaah una tabia mbaya wewe! Kumbe ulienda kuoga!?" Nilimwambia Dora mara baada ya kurudi akiwa na muonekano mpya kabisa.Kwanza uso wake ulionekana laini kabisa kwa poda aliyopaka na midomo yake ilinona kwa lipstick aliyopaka pia kimini cheusi na kiblauzi cheupe alivyovaa vilimpendeza sana.

"Mtu mwenyewe wee sharo ningekuja kukaa karibu yako mchafu siungenikimbia wewe!" Dora alijibu mashambulizi huku akija kuketi karibu na mie na pua yangu ikatabasam kwa harufu nzuri ya unyunyu aliokuwa kajipulizia.

"Umependezaa!" Nilimpa pongezi zake Dora kwa kung'ara.

"Chantee lakini sikushindi wewe!" Alijibu Dora kwa sauti ya kitoto alipokuwa anajiweka sawa sofani.

" sasa Tom nna tatizo moja!....sijui utaweza kunisaidia!?" Aliongea Dora kwa sauti iliyotulia sana huku akionekana kutafakari kwa kina.

"Tatizo gani?.....wee sema tu!!" Niliongea kwa kujiamini kwani vijisenti nilivyokuwa navyo vilikuwa vinanipa kiburi na nisingeshindwa kumtatulia tatizo lake kama lingekuwa ni la kipesa.

"Yaani hata sijui nianzie wapi!" Dora aliongea kwa sauti ya chini kama vile anajiuliza mwenyewe.

"Wee sema tu!" Mie nilimsisitiza huku bado nikiwa sina hofu.

"Yaani kiuno kinaniuma kweli hata sijui ni kwanini!" Hatimaye Dora aliyaweka wazi yaliyokuwa moyoni mwake.Kauli yake hiyo ilinishtua kwa kiasi kikubwa.Kauli hiyo ambayo nilizoea kuisikia toka kwa mpenzi wangu wa zamani kipindi tukiwa shule,mara zote aliitumia kauli hiyo kumaanisha alinihitaji kimwili sasa Iweje kauli hiyo niisikie kwa ndugu yangu wa damu,mtoto wa shangazi yangu,mdogo wake tumbo moja na babaangu.Kwa kweli ilikuwa ni haki yangu kushtuka tena sana.

"Mbona upo kimya sasa!" Dora aliniuliza kwa upole.Ingawa nilikuwa shapu kumjibu swali hilo ex (mpenzi wa zamani) wangu lakini kwa Dora ulimi ulikuwa mzito kila neno nililotaka kujibu moyo ulisita.

"Hamna sipo kimya nafikiria ni dawa gani itakufaa......vipi ulishajaribu kutumia Volin!?" Nilijitetea kisha nikamuuliza Dora swali lilionekana kumkera.

"Jamani mi naumwa kiuno Volin hiyo si dawa ya misuli!?" Alijibu kwa sauti ya kukereka huku akionekana kupanic.

"Sasa inabidi umwambie Judy basi aje akukande!" Nilitoa ushauri huku nikipendekeza jina lingine la ndugu yetu wa kike asaidie kazi hiyo.

" We mpumbavu nini!?...hivi unazani akati nakwambia wewe hivyo sikujua kama kuna Judy?"

Dora alining'akia na kutusi juu.Na hapo ndipo niliamini kuwa yupo serious (anamaanisha) na hicho anachokisema.Nikiwa bado siamini amini yanayoendelea kati ya mimi na binamu yangu Dora niliongezewa shambulizi lingine la kupigwa na mto kichwani kisha 

Dora akainuka kwa hasira na kuanza kuondoka huku akizitikisa vilivyo wezere zake.Akiwa katika mwendo kasi wa kuelekea chumbani.Nnje ilisikika sauti ya Shangazi akimuita kwa nguvu.

"Doraaa?......Doraaaah!.....weeh...Doraa!??"

Baada ya sauti hiyo ya shangazi kusikika nilimshuhudia Dora akitupa tupa mikono yake mithili ya mtu aliyedhira,nadhani hakufurahia kabisa ujio wa mama yake muda huo.Kwa hasira alibadilisha muelekeo wake wa kwenda chumbani na kuelekea sauti ilipotokea.

Baada ya muda alirudi ndani tena akiwa na mifuko miwili myeusi,bila shaka alimpokea Shangazi.Dora hakuwa tena na uchangamfu kama ule aliokuwa nao awali nilipofika,Na kila aliponiangalia jicho lake lilitangaza chuki juu yangu.Niliendelea kusikia sauti ya Shangazi nnje akizungumza na mtu mwingine na baada ya muda aliingia ndani.Shangazi alifurahi sana kuniona nimewatembelea siku hiyo.

Tulizungumza mawili matatu kuhusiana na ukoo wetu huku nyingi zikiwa ni story ( hadithi) za mababu.Babu yako alikuwa mtanashati kama wewe.Ooh wewe una busara kama bibi yako ili mradi tu furaha wanandugu tumeonana.Sikupenda kukaa sana kwa Shangazi kutokana na mawili matatu yaliyotokea dakika chache zilizopita kati ya mimi na binamu yangu,hivyo nilipopata mwanya tu niliaga na kuondoka.

"Tomm!...Tommm.....Tommm!?" Nikiwa njiani narudi nyumbani mdogo mdogo ( pole pole) huku nachezea simu yangu kwa nyuma nilisikia sauti ya mtu ikiniita kwa juhudi,Sikuwa na haraka hivyo nikamsubiri anayeniita anifikie.

"Mambo vipi mwanangu!" Huyu alikuwa ni Mudi moja kati ya wapambe nuksi wa Robby.

"Vipi tena kuna dame wenu mwingine nimechukua!?" Sikujibu salamu yake na matokeo yake nikamuuliza swali lililokuwa na nusu shari ndani yake kwani nawajua hawa watu vizuri,Hawanaga jipya.

"Acha izoo mwanangu!...unajua mi nakukubali sana!" Mudi alianza kujikosha mbele yangu.
"Unanikubali nini sasa!?" Nilihoji kwa dharau sababu sikutaka unafki.

"Yaani mi nakukubali kishenzi yani,machizi wote kitaani wamemfukuzia Lisa sana yani,hawajampata hata kidogo lakini wewe mzee mwenyewe umekuja juzi kati tu!..mtoto kakolea mwenyewe!!"

"Nyie si mlisema ni dame wenu sasa mbona unasema hamjampata hata kidogo!?"

"Unajua nini?....Robby anajipendekeza tu kwa Lisa,ashapewa makavu yake mara kibao tu lakini hasikii.Mtoto anamwambia mi nampenda Tom yani mshikaji anamind wewe!" 

Ingawa Mudi alikuwa na habari kebekebe zilizoyavutia masikio yangu lakini sikutaka kuendelea kumsikiliza kwani naitambua vizuri kanuni ya wanafiki,hawaleti neno pasipo kuondoka na neno.Hivyo nikaongeza mwendo kumkwepa mtu huyo.

Kama ilivyo desturi yangu,usiku huwa silali kabla ya ku review (kupitia) mambo mawili matatu yaliyojiri mchana na mara nyingi usingizi hunipitia nikiwa katika hali hiyo.

Nikiwa nawaza machache ya mchana huo neno Mpumbavu lilinirejea kichwani.Lakini kwanini haswa binamu yangu aliruhusu kinywa chake kunitusi hivyo?.Ni kwa sababu na sababu pekee ni kumpa ushauri juu ya kiuno chake.Si kama sikumuelewa binamu yangu Dora alimaanisha nini,La hasha!.Nilimuelewa vizuri sana lakini kwenye utekelezaji ndipo mbinde ilikuwepo.Si kwamba sikuliona umbo lake zuri lililojazika barabara kila kona,Si kuwa sikuwa na ugwadu wa tendo hilo muda huo.

Ugwadu nilikuwa nao tena saana tu.Lakini nawezaje kushiriki ngono na ndugu yangu wa damu moja?.Hapo ndipo upumbavu wangu ulipoonekana.Ni bora kuitwa mpumbavu kuliko kufanya jambo ambalo likijulikana aibu yake haitafutika maisha yangu yote.Nilijiwazia hayo kabla ya kufikia maamuzi ya kuwa mpumbavu mbele za Dora na nikauahidi moyo wangu kuwa sitokwenda kumtembelea tena Shangazi hadi naondoka Tabora ili nisionane na Dora tena.

Siku moja majira ya alasiri nikiwa sebuleni naangalia filamu,simu yangu iliita,na nilipoangalia kioo ilikuwa ni namba ngeni.

"Hallo!" Niliipokea huku nikiisikiliza sauti ya upande wa pili kwa umakini kama naweza kumtambua mzungumzaji.

"Hello Tom mzima wewe!" Sauti nzuri ya kike iliongea upande wa pili.

"Me mzima sijui naongea na nani!" Nilijibu nakuuliza upesi upesi kwa kuhofia kuwa anaweza akawa ni Bite.

"Unaweza kuotea ni nani!?" Sauti hiyo ya kike ilioongea kwa kujigonga ili kuumba uzuri ambao kwangu ulikuwa ni kama kero.

"Eeh bhana eenh! Niambie we ni nani na kama husemi nakata simu sasa hivi!" Nilichimba mkwara na kama angepuuzia ningekata kweli.Niliona kama nacheleweshwa kuangalia filamu yangu.

"Aaanh hutaniwi?....haya unaongea na Dora hapaa!" Hatimaye mtu huyo alijitambulisha na ni mara mia angekuwa Bite kuliko huyo Dora nnayemjua mimi.Nikatamani kukata simu lakini sikuwa na sababu ya kufanya hivyo nikabaki kusikiliza ana lipi jipya la kuniambia.

"Vipi Aunt anaendeleaje!?"

"Anaendelea vizuri lakini bado hajaruhusiwa kutoka hospitali!"

"Ila nini kinachomsumbua zaidi!?"

"Ni malaria!"

"Mmmh!..malaria au mimba!?"

"Malaria!"

Huyo alikuwa ni Dora akiulizia taarifa za mama yangu mdogo ambaye yeye ni shangazi na mazungumzo yake yalienda mbali zaidi.

"Ah jamani sasa kwahiyo nyumbani uko na nani!?"

"Niko na movie tu!"

"Ha ha ha! Tom bwana!...sasa nani anawapikia!?"

"Ha ha ha!...umesahau kama kuna mgahawa hapa nyumbani!"

"Duh kweli kichwa changu kipo mbali ata sijui nawaza nini!"

" Kusahau kupoo"

"Sasa Tom naomba nikuombe kitu!" Dora aliirudia kauli ile ile iyotukosanisha siku kadhaa zilizopita hivyo nikawa mzito kukubali kulisikia ombi lake lakini aliendelea.

"Naomba unisamehe kwa yaliyotokea last time ( muda uliopita) sikukusudia kukukwaza so am sory!"
"Usijali mbona mie nilishakusamehe!"

'Kweli umenisamehe Tom!" Dora aliuliza kama vile haamini.

"Ndio tena kwa roho nyeupe kabisa!" Nilisisitiza.

"Ok! Kama kweli umenisamehe naomba nikuletee zawadi yangu sahivi!"

"Zawadi ya nini Dora we jua nimekusamehe tu!"

"Tom kama hautakubali nikuletee zawadi yangu basi haujanisamehe!"


Wakati bado najiuma uma nimjibu nini binamu yangu,simu ilikatatika.Je Dora amenikatia ama simu imeishiwa vocha hilo sikutaka kujua ila nilimshukuru Mungu kwa kuniondoa salama mahali hapo na hata kama ningekuwa na muda wa maongezi wa laki moja nisingethubutu kumpigia Dora.

Nikatupa simu pembeni, nikaendelea na kuangalia filamu,na kila ilipoisha niliweka nyingine kali zaidi.

Baada ya Muda mrefu kupita,nilisikia vishindo vya mtu akitembea na kisha mlango ukagongwa.

"Pita ndani tu pako wazi!" Nilimuitikia mtu huyo aliyekuwa akibisha hodi huku nikiamini kuwa ni dada wa mgahawani maana ndiye akikaa mda mfupi bila kuniona hapati raha.Lakini kinyume na matarajio yangu nilishangaa kuona Dora ndiye anayeingia.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni