UZOEFU (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 4 Aprili 2021

UZOEFU (9)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
"Nani huyo!?" Niliuliza nikiwa nimemkazia jicho.
"Robby!" Lisa alijibu kwa upole kana kwamba si yeye aliyekuwa akibwata sekunde chache zilizopita,Sikuwa na swali la ziada kwake,tukakaa kimya tukimsubiri Auntie!.
SASA ENDELEA...
Auntie alirudi akiwa na visahani viwili vidogo vilivyokuwa na karanga zilizokangwa kwa kuchanganywa na mayai,tulikula pamoja huku tukiendelea na hadithi mbalimbali hadi ilipofika jioni tulipoaga na kuondoka tukawa tumeiita Jumamosi hiyo siku nzuri (Quality day).

Mapenzi yangu na Lisa yaliendelea kung'ara kila uchwao hadi sasa Bamdogo alijua nini kilikuwa kikiendelea kati yetu kwani mara kadhaa alishanibamba na Lisa tukiwa katika pozi (mikao) tofauti tofauti za kimahaba.Ila hakuwahi kunikoromea juu ya hilo nadhani hata yeye alikuwa ananisifu kimoyo moyo kuwa nimepata chuma cha nguvu ( msichana mzuri).

Siku zikapita kama upepo na hatimaye ikafikia sehemu ya kutengana.

Ilikuwa siku moja majira ya jioni tukiwa katika viwanja vya Orion,viwanja ambamo panauzwa makulaji ya aina mbali mbali majira ya jioni kama ingekuwa ni Zanzibar basi hapa pangeitwa Forodhani.Ni kawaida yetu kuwasili maeneo haya mara kwa mara kwajili ya kupata juice ya ukwaju pamoja na korosho.

Siku hiyo mara baada ya kununua tu vitu hivyo na kwenda kuketi mahala ambapo tumepazoea ndipo Lisa alipoanza kuniaga rasmi kuwa muda wake wa likizo umekaribia kwisha na siku si nyingi angerejea tena mkoani Kilimanjaro kwaajili ya masomo.Ingawa habari hii ilikuwa nzuri kimasomo lakini haikupendeza katika mapenzi yetu tayari nilishaanza kujisikia upweke kama vile Lisa ameshaondoka tayari,Hata saa ya kurudi nyumbani njia nzima nilikuwa kimya nikiliwazia jambo hilo.Kuishi mbali na mpenzi umpendaye sana ni moja kati ya mitihani mikubwa ya kimapenzi.

Usiku wa siku hiyo niliwaza mengi mno na wazo la mwisho nililolipata usiku huo ni kuondoka pamoja na Lisa.

Nilikuja Mkoani Tabora kwajili yake,nimefanikisha zoezi kubwa la kumrudisha tena kwenye himaya yangu.Sasa baada ya hayo yote nibaki Tabora kufanya nini tena?.Swali hilo ndilo lililonifanya nifikie maamuzi ya kuondoka na Lisa.

Nikavuta picha jinsi nitakavyosafiri na Lisa,jinsi tutakavyokaa seat moja huku tukishangaa pamoja miti inavyorudi nyuma basi likisonga mbele,Hakika ingekuwa ni furaha ya pekee sana kati yetu zaidi ya yote nilipanga kabla ya kufika Moshi tukae Kwanza Arusha siku mbili ndipo Lisa aende shuleni na mimi nirudi nyumbani Dar es salaam.Nikavuta picha pia tukiwa mimi na Lisa tu ndani ya chumba kimoja juu ya kitanda kimoja pia ndani ya blanketi moja,jumlisha na kile kibariidi cha 

Arusha,nikajikuta mwili mzima unanisisimka kwa raha za fikara hizo.Katika kipindi chote nilichoishi mkoani Tabora nikiwa na Lisa kama mpenzi wangu,hatukuwahi kushiriki ngono kabisa,sikuwa na haraka na jambo hilo hata kidogo.Niliamini Lisa ndio mke wangu wa maisha yote sasa kwanini niharakishe mambo kiasi hicho,kwa kuwa njiwa alikuwa ni wangu mwenyewe sikuona sababu yeyote ya kumshikia manati.Siku zote mvumilivu hula mbivu na mbivu zangu nadhani zilipangwa nikazilie Mkoani Arusha.

Siku iliyofuata niliona nimshirikishe Lisa katika kile nilichokiwaza usiku uliopita na Lisa akaonekana kulifurahia pia jambo hilo.

"Kwa hiyo baby ndo hivyo,ujipange tuondokee mapemaa yani sipati hata picha ndani ya hizo siku mbili jinsi ntakavyokuwa bonge kwa raha!" Nilimwambia Lisa baada ya kuukubali ushawishi wangu juu ya kukaa Arusha siku mbili kabla hajaenda shule.

"Mie hata sifurahii sahivi labda hadi tupande basi!" Lisa aliongea kwa upole kuonyesha wasi wasi wake.

"Kwani mpenzi huniamini ama nini!?"
"Nakuamini sana tu my sweetheart na nnaombea iwe hivyo!".

Baada ya kumuweka Lisa sawa katika swala hilo sasa nilibakiza mtu mmoja tu anipe go ahead (niendelee) naye alikuwa ni baba Mdogo,nikimuaga huyo tu kuwa naondoka naye akaniruhusu swala la kula kuku kwa mrija juice kwa uma lilikuwa liko wazi kabisa,Kuhusu swala la kipesa nilikuwa sina wasi kabisa kwani akiba niliyokuwa nimejiwekea ingetosha kukaa hata siku kumi na Lisa kwenye Hoteli nzuri tukila na kunywa bila hofu yeyote.

Sasa nilianza kumvutia Bamdogo kasi ili niweze kumueleza swala la mimi kuondoka kwa namna nzuri ambayo asingeweza kunipinga juu ya hilo.

Baada ya kuzipanga hoja zangu baraabara ndipo siku moja jioni nilimkabili Bamdogo kwajili ya kumueleza jambo hilo.

"Sasa Bamdogo matokeo yamekaribia kutoka kwahiyo naomba nirudi nyumbani kwaajili ya kuanza kujiandaa!" Hivyo ndivyo nilivyofungua mazungumzo yetu lakini bamdogo alionyesha moyo mgumu sana mbele yangu.

Japo mimi niliandaa sababu mia za kutaka kuondoka nadhani yeye alikuwa na sababu elfu moja za mimi kubaki.Bamdogo alionyesha utayari wa hata kunigharamikia kila kitu kuhusu masomo alimradi tu nisiondoke Tabora.

Hizi ndio hasara za kutenda mema sana wakati mwingine,nilijiwazia mwenyewe baada ya bamdogo kushinda katika kinyang'anyiro hicho cha mimi kubaki.Japo nilionyesha tabasam la kinafki mdomoni lakini moyoni nilibubujikwa na machozi,nilikosa raha kuliko kawaida.

Nilijua lisingekuwa jambo rahisi Bamdogo kuniachia kirahisi kwa sababu tangu nimekuja nimeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi katika familia yake.Hata mimi ningekuwa ni yeye nisingekubali kijana kama mimi kuondoka hivi hivi tu.

"Kwa hiyo wewe mwangu wee tulia tu hapa hapa kwa babaako matokeo yakitoka tutajua tunafanya nini na ukiwa na tatizo lolote lile usisite kuniambia!" Hivyo ndivyo tulivyomalizana na bamdogo,yeye akaondoka akiwa ameridhika huku mimi nikikereketwa na donge la uchungu kooni.

Habari hiyo sikutaka kumcheleweshea sana Lisa ili asije akaishi katika fikra zilizokwisha haribika.Fikra kuwa tutakuwa pamoja katika safari ya kwenda Moshi.

Hivyo nilivyojiona nimetulia kidogo tu niliamua kumpigia Lisa simu kumjulisha na yeye.

"Yaas! Darling yaani nashindwa hata nianze wapi kukwambia!" Nilimwambia Lisa mara baada ya kupokea simu na kuitikia kwa furaha.

"Nambie bhana...mbona unapenda kuniweka roho juu hivyo!?" Lisa alilalama kwa sauti ya deko.

"Honie Bamdogo kanichomolea (kanikatalia) kuondoka yaani hapa nimeconfuse (nimechanganyikiwa) kweli yani!!" Hatimaye nikalitumbua jipu.

"Hiyo nilijua tu yaani,yaani nilijua!" Lisa alilalama kwa hasira kiasi kuonyeshwa kukerwa na taarifa hiyo muhimu.

"Usiseme hivyo baby.....inakuwa kama mimi ndio nimesababisha iwe hivyo!"

"Ok fine badae basi!" Lisa aliaga haraka haraka na kukata simu,Nilijua hayuko sawa hivyo sikumpigia tena.

Siku iliyofuata nilielekea mjini kumfanyia Lisa shoping (manunuzi) ya vitu ambavyo vingemfaa katika safari yake ya shule,Kwa njia hiyo nilijua ningeweza kupunguza machungu yake ya kunikosa katika safari yake japo kidogo.

Siku zilipita na hatimaye ikafika ile siku ya Lisa kuondoka.Siku hiyo niliamka mapema sana na kumsindikiza kituo cha basi.Nilikaa naye kwa muda mrefu kabla ya basi hilo kuondoka.

Katika muda huo tuliutumia vizuri kupeana nasaha mbalimbali huku kila mmoja akimsisitiza mwenzake kuwa anampenda sana.Sanjari na mazungumzo hayo pia nilitumia nafasi hiyo kumkabidhi Lisa zawadi nilizomnunulia siku moja nyuma.Alifurahi sana,

"Ndani ya bahasha hii nimekuandikia barua nzurii,tafadhali uwe unaisoma mara kwa mara!" Nilimwambia Lisa na kumkabidhi bahasha hiyo iliyokuwa imepambwa kwa maua.Shuleni kwao hawaruhusiwi kutumia simu hivyo nilijua barua hiyo ingemfaa sana kuamsha hisia zake za kimapenzi juu yangu kama angenikumbuka.

Hadi muda wa basi kuondoka ulipofika nilimuacha Lisa huku nikiwa bado namuhitaji.Kilichonipa raha asubuhi hiyo ni Lisa alivyounyonya ulimi wangu kwa muda mrefu tena mbele ya abiria wenzake.Nilifurahi kwa sababu penzi letu lilikuwa na hatua mpya kila uchwao.Tukawa tumeagana huku nikimuombea kwa Mungu amfikishe salama na amlinde hadi tutakapoonana tena.

Tangu Lisa alipoondoka kuna jambo likaanza kunisumbua.Nilishazoea tukishinda pamoja huwa tunafanya michezo mbali mbali ya kimapenzi ( romance) kwa minajili hiyo labda ndio maana sikuwa kabisa na hamu ya kushiriki ngono.

Lakini siku chache kupita tu mara baada ya Lisa kuondoka nikapata ashki kubwa ya kushiriki tendo hilo.Sijui yale mawazo ya Arusha nayo yalichangia kunisisimua ama vipi!.Sasa kushinda mgahawani kuanzia asubuhi hadi usiku ikaanza kunichosha.

Mawazo ya ugwadu ugwadu yalikuwa yakinitawala kila nilipokaa peke yangu.Ili kuiepuka hali hiyo siku moja majira ya jioni niliamua kwenda kumtembelea Shangazi yangu mwingine aliyekuwa akiishi mtaa wa Chemchem.Huu ni mtaa wa pili toka mtaa wa Mwinyi ambapo ilipo nyumba ya bamdogo.

"Annh!! Karibu karibu!.....sharo letu hilooo!" Nilipofika kwa shangazi nilipokelewa na Dora mtoto wake wa pekee ambaye ni mchangamfu mno.Hata aliponitania mi ni sharo sikujibu neno lolote lile,nilitabasamu tu hali nikijua yakuwa kama ningejibu neno hilo huenda lingezaa mengine saba mia elfu.

"Karibu ukae namalizia hapa sasa hivi twende ndani!" Aliongea Dora aliyekuwa akiosha vyombo huku akinikabidhii kigoda chake nikae.

"Aargh! Dora!...mi si mgeni hapa wee kaa tu umalizie!" Niliongea kwa msisitizo huku nikirudisha kigoda chake alichonipa.

"Ah Sharooo huyooo!....mee sikai kwenye kigodaa utanichafua maan!" Alinitania Dora kwa mara nyingine huku akiigia sauti ya Sharo milionea.R.I.P Sharo milionea.

"Acha hizo basii....vipi Shangazi yuko wapi kwanza!?" Nilizizima tani zake nakumtupia swali.

"Aunt yako yupo kazini bado hadi badae badae saana ndio utamuona hapa!"

"Duh siku hizi kazini wanatightiwa (wanabanwa) eenh!?" Nilimuuliza Dora kujua hali ya shangazi kazini lakini swali langu hilo likazua mengine.

"Mbona wee unatightiwa sie hatusemi!" Alichombeza Dora kiutani.

"Nataitiwa na nini tena jamani!" Nilihoji huku nikiwa sijajua bado ipi dhamira yake ya msingi.

"Si wifi huyoo yaani kakubana kweli kweli hupumuiii!" Alijibu Dora huku akiwa katizama vyombo nisiyaone macho yake.

"Wifi gani tena huyo!" Nilihoji huku nikijitia sielewi somo wala darasa.

"Ha ha ha!....punguza kaka yani wako wengi hadi hujui ni yupi!?" Badala ya kunijibu Dora aliangua cheko la kinafki na kunitwanga swali ambalo lilinifanya nijute kuuliza swali langu.

"Afu unapenda masihara wewe!" Nilijitahidi kuua hiyo mada lakini wapi!

"Niambie basii wifi langu leo liko wapi!..toto la kinyamwezi!..yani limekuachia uje hadi huku peke yako!?" Dora aliendelea kuchombeza maneno kebe kebe na sasa walau niliweza kutambua kuwa aliyekuwa akizungumziwa hapo ni Lisa.Nilistajabu kuwa Dora kamjua vipi.

"Ah wapi!....hakuna lolotee hizo hisia zako tu!" Nilimwambia Dora ili kumpoteza katika fikra zake.

"Ila Tom sema kweli,Lisa ni dame wako ama sio!?" Dora aliniuliza swali ambalo sikutaka kulijibu maana kama ningejibu ndio ningekuwa nimempa mada mpya ya kunitania na kama ningejibu hapana ningevunja kiapo cha Lisa kuwa sitakaa nimkane maishani mwangu.Sasa iweje nimkane mbele ya Dora hali yakuwa na mimi niliapa mwenyewe.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni