UZOEFU (15) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 7 Aprili 2021

UZOEFU (15)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
Tuliongea mengi siku hiyo na Amani na uhakika wa kufanya kazi ukawa umetiki kwa asilimia mia, mjini Network (mtandao) bhana. Bila mtandao utaishia kuwa mtu wa mipango isiyotekelezeka.
SASA ENDELEA...
Ni Jumapili ya kwanza kabisa Tom nikiwa juu ya jukwaa kubwa linalotazamwa na macho ya wengi ni hapa nikiwa nimesimama kama Mc (msema chochote) wa shughuli hiyo ya burudani kwa siku hiyo hii ni baada ya kuunganisha mitambo inayofanya kazi uwanjani hapo. Ingawa sikuwahi kusomea sound engeenering, Amani alishangaa jinsi nilivyoifanya kazi hiyo ya kuuda sound system kwa muda mfupi. 

Zawadi moja niliyopewa na Mungu akati nakuja duniani ni kujua kufanya mambo mengi. Hata wazazi wangu walilijua hilo hadi fundi aje nyumbani basi kuna tatizo lililokwenda shule ( kubwa sana). Hii yote nilitaka kufanya kazi kama mtumwa ili niishi kama Mfalme na kubwa ambalo lingenipa raha katika ufalme wangu ni kumuona Malkia wangu Lisa akiwa na furaha.

Hadi mwisho wa shughuli hiyo siku hiyo kila kitu kikawa kimeenda sawa.Boss mkubwa wa kampuni alinisifu kwa kuwa na sauti yenye punch kama B 12, Ingawa mwanzo nilianza kwa kutetemeka kutokana na kutozoea kusimama mbele ya kundi kundi kubwa la watu tena nyomi (wengi) lakini mwisho wa siku Boss mwenyewe alikiri kwamba naweza. Na huo ndio ukawa mwanzo mzuri wa deal yangu kati ya mimi na Numerator's Entertainment.

Utamu wa kazi Pesa. Kiasi cha shilingi elfu sitini nilizozipata siku hiyo kwangu ilikuwa ni kama milioni mia moja sabini elfu. Ni muda mrefu sasa sikuwa nimeshika pesa nyingi za kwangu mwenyewe tangu nilipoacha kazi yangu ya umeneja wa mgahawa wa Bamdogo mkoani Tabora. Nilifurahi sana kwa kuwa pesa zilianza kuninukia tena. 

Katika elfu sitini niliyopata nikaweka elfu thelathini tigo pesa na pesa hiyo nikaiita kofliny (dawa ya kikohozi) yaani Lisa akikohoa tu nampa. Kisha elfu sita ikawa fungu la kumi ( sadaka ) na iliyobaki ingenisaidia mimi kurudi tena kazini mwisho wa wiki mwingine. Ratiba yangu ya maisha ikawa imekamilika.Siku tano za week enda, shule, siku mbili za weekend, moja kanisani moja kazini, wiki imejaa, maisha yanaendelea.

Huo ndio ukawa mfumo mpya wa maisha yangu. Majira yakasonga na kampuni yetu ikaendelea kukua na kutanuka. Sasa siku ya maonyesho ( show) haikuwa tu mwisho wa wiki, Kampuni ikaiteua siku ya Alhamisi na yenyewe kuwa siku ya show (maonyesho). Hivyo siku za show zitakuwa ni mbili kwa wiki japo hii ilikuwa ni habari njema kwa upande wa mapato lakini kwa upande wa shule haikupendeza kusikiliza. 

Pesa nazitamani, Elimu naipenda, kwani kuua siku moja ya vipindi vinne shuleni kisha nikaingiza kiasi fulani cha pesa kuna hasara gani? Nilijiuliza na kichwa kikadakia upesi upesi kuwa hakuna shida moyo nao ukaridhia.Hivyo ndivyo siku ya Alhamisi ilivyogeuka kutoka kuwa siku ya shule na kuwa siku ya kazi.

Siku hii begi likawa halibebi madaftari tena bali lina beba nguo za shughuli. Nikawa naondoka nyumbani kwa tiketi ile ile ya nguo za shule na nauli ya mia mbili mia mbili juu. Lakini nikitoka hapo naua root ya shule, nabadilisha nguo nakwenda mzigoni ( kazini ) kama kawaida.

Haikuwa tabu kufanya hivyo na nilipoenda shule siku ya Ijumaa nili cover wenzangu walivyojifunza Alhamisi. Kazi ikazidi kunogeshwa na donge la pesa lililokuwa linaongezeka kila uchwao. Na pesa kama kweli ni chachu ya mapenzi basi iligandisha donge zima la mapenzi. Kwani kutamani kutoa wakati huna ndipo tatizo linapokuja lakini kutoa kama kipo ni kama ilivyo sawa bin sawia. Sasa nilikuwa na amani na mpenzi wangu.

Kuachana na pesa sasa nilihisi kuna tatizo jipya limeingia kwenye penzi letu. Nilihisi upendo wa Lisa umepoa kwa kiasi kikubwa. Sikutaka kukurupuka juu ya hilo nikaanza uchunguzi wangu yakinifu taratibu. nikagundua kwamba kama nisipoanza mimi kumtafuta Lisa basi nayeye atakaa kimya hadi nitakapomuanza. Nikajaribu kukaa kimya siku mbili.Lisa naye akakaa kimya siku mbili hadi nilipoanza kumchatisha tena.

' hellow hun! ' nilimtumia Lisa ujumbe mfupi baada ya siku mbili za ukimya.
'Hellow swt!' Naye akajibu ivyo.
' ur so quet nw dyz wat da prbm? ' (upo kimya sana siku hizi nini tatizo)
' natin wrong hun! ( hakuna tatizo mpenzi)' alijibu Lisa nami sikutaka maelezo marefu nikaachana naye.
" ok enjoy ur tym hun'(sawa furahia mda wako mpenzi)
' tanx bby bt sory nna shida ya ela!'
' lyk how much?' Kama shilingi ngapi vile.

' 15 bby' alinijibu kifupi Lisa. Japo ningeweza kumtumia elfu moja mia tano kutokana na alivyoiandika sikuwa na hiyana nikamtumia shilingi elfu kumi na tano pamoja na ya kutolea.

Lakini cha ajabu alikaa kimya, sawa nilimwambia hana haja ya kunishukuru nikimpa hela kwa kuwa mie na yeye ni kitu kimoja lakini sikumbuki kama nilishawahi kumwambia kuwa hata hela ikifika akae kimya, nikalazimika kumtumia ujumbe mfupi.

' vipi umeipata ' akajibu 'yap' . Hali hiyo iliuchoma moyo mithili ya msumari wa moto kwa kidonda japo nilivumilia lakini chembe chembe fulani za kutomjali Lisa zilishaanza kuijenga roho yangu.

Maisha ya kero ndo hivyo yakawa kiongozi wa penzi letu.Kimya kwa kimya, ujumbe mfupi kwa ujumbe ujumbe mfupi na swali kwa jibu.

Katika vitu viwili vinavyonishindaga maishani ingawa huwa navijaribu mara kwa mara cha kwanza ni kusubiri na cha pili ni kubembeleza.Kuna Vitu nilianza kuhisi vimeshaanza kunishinda kwa Lisa. Kila mara kumuuliza mtu anatatizo gani na anajibu hana, Ilikuwa ni kibarua kinachokera kuliko kuzibua chemba za maji machafu.

Mimi si abiria mjinga kupanda basi linalokwenda nisipopajua, gari lenye shehena ya mapenzi ya Lisa tayari lilishapoteza dira nami nikashuka kimya kimya bila kutoa taarifa. Japo sikumwambia Lisa neno lolote tayari nilishambwaga kimya kimya, Nikawa sihangaiki naye tena kwa ujumbe mfupi wala kwa simu.

Siku moja bila kutarajia Lisa alinitumia ujumbe mrefu kwenye simu uliojaa malalamiko kuwa nimempotezea siku hizi, niliusoma lakini sikuhangaika naye kumjibu. Hakuridhika na kimya changu baada ya muda mfupi akanipigia simu, Sikufanya kiburi nikaipokea simu yake, Leo ilikuwa ni zamu yake kulalamika na kunibembeleza.

" Tom nini tatizo lakini mpenzi wangu, mbona umekuwa hivyo!?! Hii ni kauli laini ya Lisa iliyopenya masikioni mwangu na kuamsha vilivyolala. Nadhani alitarajia ntamwambia hakuna tatizo sababu ya tabia yangu ya upole siku zote kwake lakini leo hii sikubakiza la moyoni ' nilifunguka kiroho safi' yote yanayonisibu.Ingawa yeye ndiye aliyepiga simu hakuwa na la kusema zaidi ya kuwa msikilizaji, na hapo yakazihirika ya wahenga kuwa ukimuamsha aliyelala utalala wewe. Hadi mwisho wa mazungumzo yetu 

Lisa hakuyakubali makosa yake wala hakuyakataa, akawa amenichezea mchezo wa siasa, mchezo ambao naumudu vyema sana, nikajiapia kuwa ntaenda naye sawa. Mara tu baada ya simu kukata Lisa akatuma ujumbe mfupi kuomba radhi ya makosa aliyoyakataa na kwenye ujumbe wake aliweka neno ' kama kweli nimefanya ivyo" neno lililonifanya niamini kuwa hatojirekebisha na kwa kuwa siasa naimudu vyema, ujumbe wake sikuujibu ili ashindwe kuelewa kuwa umefika, nimeusoma, nimemsamehe au la! 

Huenda akapata nafasi ya kujifikiria tena.Na kweli ikawa hivyo kwani baada ya muda mfupi akatuma tena ujumbe mwingine kusisitiza msamaha ' bby m sorry ma luv najua nimekuuzi!'
"Itz ok no prblm' ( ni sawa hakuna tatizo) kwakuwa hakutaka kukiri makosa namie kwenye ujumbe wangu sikuainisha kuwa nimemsamehe au la!.
'Bt bby m sorry i have a prblm' (Lakini mpenzi samahani nna tatizo) ujumbe huo ukaanza kunichefua kwani nilijua huyu mtoto kilichomleta kwangu ni pesa nikajipanga kumchinjia baharini ( kumnyima)
'Which prblm?'
' ur kiss hun! If i wl ev it m gonna b fine' ( busu lako mpenzi kama ntalipata ntakuwa sawa) Lisa kama alijua vile, aliwasha endcater za kulia na kukata kushoto, nikajiona mimi ndo nawaza pesa, nikajisikia vibaya.
'Mmwaah!' Nikamchumu.
'Hun hujanambia wapi!"
' kwenye shavu bby!'
' ctaki shavu hun nata kwenye lipz!'
'Mmwaaaaaah! Kwa lipz!'
'Ooh thnx ma luv nw m gud!'

Hivyo ndivyo tulivyoagana usiku huo. Nikahisi huba la Lisa kuchomoza tena mithili ya jua la asubuhi, nikalala usingizi mororo usiku huo.

Asubuhi na mapema mara tu baada ya kuamka nilikuta ujumbe mzuri kwenye simu yangu toka kwa Lisa. Alikuwa amenitakia siku njema sanjari na maneno mazurii ya kimahaba, nilipoujibu tu ujumbe huo nilitandikwa kirungu papo hapo (niliombwa pesa).

'Bby nna shida ya shilingi elfu 50 plz help me ma luv if u can' Huo ndio ujumbe nilioweza kuusoma, niliitupa simu pembeni na kushika kichwa!!
"Ooh my God yaani salaam tu shilingi elfu hamsini" niliongea mwenyewe kama kichaa kwa sauti ya chini sana na baada ya kuachia kichwa changu niliujibu ujumbe wa Lisa.
'I cant babie sory'( siwezi baby samagani) naye akanijibu ile herufi yake moja ' K '.
Ingawa nilishatoa jibu la kukataa lakini bado kichwa kiliendelea kulifikiria ombi hilo.

Namkumbuka Rafiki yangu Ayatola mara tu baada ya kurudi hosteli kuishi nyumbani na mimi kuamua kumuuliza kwanini kafanya hivyo, alinipa jibu moja tu "asee kama una mpenzi wako anayeishi hostel akikuomba pesa hata kama huna, kakope uumpe!"

Hiyo ni kauli ya Ayatola iliyojirudia kichwani mwangu baada ya kupita siku nyingi.Sikumuuliza Ayatola kamaanisha nini kwani hata mimi nilishapitia maisha ya boarding (kulala shuleni) kwaiyo najua mtu akifulia (akikosa hela) huwa inakuwaje.

Sikumnyima Lisa pesa kwa kuwa sikuwa nazo la hasha! Nini elfu hamsini hata laki moja ningemtumia ila kilichonikera mimi ni yeye kunigeuza mimi A T M yaani ananitafuta akiwa na shida ya hela tu. pamoja na yote hayo niliichukua simu yangu na kumtumia kiasi cha pesa alichohitaji kwa hasira naye akajibu 'enx hun!' Tukawa tumemalizana kwa siku hiyo huku moyoni mwangu nikijua kuwa atanitafuta tena pesa hiyo itakapokuwa imekwisha.

" Hellow Lisa mzima wewe!" Baada ya siku nyingi kupita huku kimya kikiwa kimetawala kati yetu niliamua kumpigia simu Lisa na baada ya simu kuita mda mrefu hatimaye ilipokelewa.
" Mie mzima sijui wewe!!" Sikutaka kuirefusha salaam hiyo moja kwa moja nikaelekea kwenye dhumuni langu la kupiga simu.
"Hivi Lisa maisha gani haya tunayoishi, kama tumelazimishwa bwana!....sasa nataka kujua kitu kimoja unanipenda au hunipendi!?"
"Tom kiukweli naona siku hizi hisia zangu zimeisha kwako yaani sijui najisikiaje...!" 

Lisa alijibu huku akijiuma uma sikuweza kuvumilia kuendelea kumsikiliza nikakata simu huku akiwa bado hajamaliza kuongea sikutaka kujua kuwa alikuwa anatania au anamaanisha anachokisema. Baada ya kukata simu hiyo nilianza kutetemeka kwa hasira hasa baada ya kujizuia nisibamize chini simu yangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni