UZOEFU (22) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 10 Aprili 2021

UZOEFU (22)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Nilimnon'goneza kiutani dada tulipokuwa tunapanda daladala lakini kiukweli nilikuwa namaanisha nilichokisema kwani tulipopanda tu nilikaa na Caro huku dada akikaa upande wapili.
" Tom!?" Baada ya gari kutembea umbali mrefu huku tukiwa kimya Caro aliniita.
SASA ENDELEA...
" Yes dear!" Niliitka na kumtazama Caro.

" Sorry kwa hichi ntakachokwambia!" Caro aliongea kwa sauti iliyopoa sana ingawa alinitisha, nilijikaza kisabuni.
" Don't care Caro just tell me!" ( usijali Caro we niambie tu. Nilijibu kwa sauti ya kawaida huku hofu ikisalia moyoni, mara nyingi inapotangulizwa Sorry huwa kinachfwata si chema.

"Tom nilikudanganya jina me naitwa Sunshine sio Caro kama nilivyokwambia!" Aliongea Sunshine huku akiona haya kiasi.
" Ha ha ha!! unajua siku hiyo nilihisi kitu ka hiyo coz ( sababu ) ulifikiria sana kabla ya kuniambia unaitwa nani!" Niliongea kwa furaha baada ya kufahamu Sunshine ambaye nilimtambua awali kwa jina la Caroline alitaka kusema nini.
" So please forgive me (Kwaiyo tafadhali nisamehe) nilijuta sana badae" Sunshine alitaka kuhakiki kama nimemsamehe.
" Usijali my Sunshine! Sichukii sababu ulinidanganya jina ila nafurai kwa kuwa nimelijua jina lako..S.u.n.s.h.i.n.eeee ...you got da cute name!" Niliongea kwa mikogo huku nikiwa nimeanza matumizi ya jina jipya la Sunshine.
" Vipi mbona unaniangalia hivyo!?" Nilimuhoji Sun baada ya kumuona ananiangalia sana.
" Your so awesome Tom sijawahi kukutana na mtu kama wewe!" Alinifagilia Sun huku akisafisha kucha zake ambazo hazikuwa chafu.
"Thanks Sun pia nafurahi kukutana na wewe!" Nilimjibu huku nikiona noma (aibu) kiasi kutokana na kufagiliwa.

"Afu umefanana na dadaako!" Aliendelea kuchombeza Sun.
" Wee unaona hii!?" Nilimwambia Sun huku nikimuonyesha ngumi niliyoikunja baraabara bila shaka alielewa ni utani.
" Nini kwani uongo!?" Alichombeza tena Sun kuonyesha kuwa hajaogopa mkwara mbuzi wangu.
" Mimi sifanani na dadaangu ila yeye ndo anafanana na mimi!"
" khaa! sasa tofauti ipo wapi hapo swala ni lile lile mmefanana!"
"Ukisema me nimefanana na yeye inamaana me nna sura ya kike lakini yeye ndio kafanana na mimi kwaiyo ana sura ya kiume!"
" mmmh! Mwanaume unajua kujitetea wewe!"

Tukiwa katika mabishano hayo kondakta alikuja kuchukua nauli na kutuanzishia mabishano mapya ya kulipa nauli, mara zote tukiwa pamoja, Mimi na Sunshine kila mtu hutaka kulipa yeye hali inayochukiwa na makondakta kwasababu inawachelewesha kwenda kudai kwa abiria wengine.

Baada ya safari kudumu kwa muda wa lisaa limoja na ushee hatimaye tulifika nyumbani huku tukimuacha Sun kituo cha kwao.

Baada ya kupata mlo wa usiku nilimfwata dada chumbani kwake kwa nia ya kujadiliana naye mawili matatu kuhusiana na siku hiyo.

" Vipi leo umeenjoy!?" Nilimuuliza dada nilipoingia chumbani kwake huku nikitafuta mwanya wa kuchomekea mada yangu.

" Yeah saana tu!...na yule ndo wifi nini maana wee naye!?" Aliongea dada kimikogo huku akinitangulia kwa kile nilichotaka kumwambia, nilifurahi kwa kuwa mwanzo ni mgumu na yeye alikwishanirahisishia.

" Aah ni rafiki tu kama nilivyokutambulisha mchana, ila wewe ni dadaangu sitokuficha kitu ukweli ni kwamba Sunshine ananipenda sana japo bado ni marafiki wa kawaida tu!" Nilimmegea dada kipande kidogo katika donge kubwa.

" Sunshine ama Caroline mbona sielewi!?"
" Aargh! Yote ni majina yake yani kama Pesa na hela!"

"Ok ngoja nikwambie kitu mdogo wangu! Uyo sijui ndo Caro sijui Sunshine hakufai hata kidogo amekomaa sura kama mbuzi wa shughuli so kama una mpango naye mie hata sikushauri.

!" Aliongea dada akiwa kabetua midomo yake.

" Lakini nimekwambia sisi ni marafiki tu sio wapenzi!" Nilijitetea.

" Aya ndo muendelee kuwa marafiki hivyo hivyo ila ukitaka dame mzuri hata mimi ntakutafutia!" Alimaliza dada na mie sikuongeza la kheri wala la shari zaidi ya kumtakia usiku mwema na kwenda kulala.

Tom ndo huyoo ushauri ameupata!, Je ataufanyia kazi ama atautupa kapuni???

Akili ya kuambiwa jumlisha na ya kwako unafanya maamuzi kamili. Ingawa nilitegemea ushauri wa namna hiyo toka kwa dada angu lakini sikutegemea kama angeuleta kwa namna hiyo.Aliyosema ni kweli ndio sababu hata mimi awali 

Nilihisi hivyo na ndio sababu ya kuomba ushauri lakini mwanaume rijali kama mimi nawezaje kumuacha kirahisi rahisi namna hiyo mlimbwende kama Sun hasa ukizingatia nimeshamgeuzia kibra?. Usiku huo hadi usingizi kunipitia niliwaza mengi na mwisho nilikubaliana na kamati yangu ya ubongo kuwa sitamtongoza Sun lakini pia sitamuacha hivi hivi.

Baada ya siku chungu tele kukatiza huku nikiwa sina mawasiliano yeyote na Malha.Ni siku nyingine tena majira ya usiku nikiwa sebuleni naangalia luninga, simu yangu iliita. Zilikuwa ni namba tu tena nisizozifahamu, mara nyingi huwa sipokei namba ngeni kwa kuhofia kuwa ni wrong number na tunaweza kusumbuana ama kuulizana wee nani!.

Sababu hiyo ilinifanya kuipuuzia simu hiyo lakini niliipokea mara moja baada ya kukumbuka kuwa tangu nimeanza kazi Numerator's Entertainment mara nyingi nimekuwa nikipata deal za kwenda kufanya u mc kwenye shughuli mbalimbali.

" Hello!?" Niliita baada ya kupokea simu kwa ki besi ( sauti ya nne)
" Hello Tom mamboo!" Ilikuwa ni sauti maridhawa ya kike.
" Poa tu!...sijui naongea na nani!" Niliongea huku nikinyanyuka kwenda nnje maana mzee ambaye nilikuwa naye alishanigeuza luninga.
" unaongea na shem wako!" Sauti hiyo ilijibu kwa uzuri ule ule.
" Sijui shem nani maana nna kaka wengi kweli yani!" Nilijibu kisiasa kumkwepa yeye kuwa shemeji yangu ila kumfanya mimi ndo niwe shemeji yake.
" Ok unaongea na Salha!"
" wow Salha! Mambo vipi!?" Nilifurahi baada ya kumjua
" Mabayaa..Umetususa!" Alilaumu Salha.
" Sijawasusa jamani mambo tu ndo mengi!" Tayari sauti yangu ilishalegea toka ile ya nne niliyopokelea simu hadi ya kwanza. Kweli wasichana nouma saana.
"Shem!?" Salha aliita kuonyesha kuwa ana jambo anataka kusema.
"Yap!" Niliitika kifupi
" Sijui hapo ulipo uko free ( huru ) kuongea coz ( sababu) nna mazungumzo marefu kidogo!" Kauli yake ilinitisha kiasi cha kutaka kukata simu lakini nikajikaza kiume.
" Yeah we sema tu niko poa!" Nilijibu huku nikimeza funda la mate lililopita kooni kwa tabu kwani bado nilikuwa na hofu juu ya mazungumzo yake marefu anayotaka kusema.
" But am sorry kama ntakukwaza shem!" Salha alizidi kunipa hofu.
" Usijali Salha wee niambie tu!" Nilijibu kishupavu.
" Hivi kwanini uliachana na dadaangu shem!?" Hatimaye Salha alifungua mazungumzo na swali ambalo kwangu ilikuwa ni kama ngumi ya kushtukiza, lazima inipepese!
"Kwani Malha yuko wapi!" Badala ya kujibu swali na mimi niliuliza swali ili kujiweka sawa.
" Yupo Tanga saivi!"
" Kwanini umeniuliza hilo swali Salha!?" Niliendea na maswali huku nikijipanga kujibu yake.
" Tom wee nijibu tu alafu utajua kwanini!" Salha alikwepa swali langu lakini tayari nilishajipanga kumlipua.
"Salha nikikwambia sababu ya kuachana na dadaako hutaniamini milele!" Taratibu nilianza kutega mabomu yangu.
" kwanini nisiamini!?" Salha aliuliza akiwa na walakini ndani yake.
" Sababu chanzo ni wewe Salha!" Hatimaye nilimpasulia jipu.
"Khaa!.. kivipi!" Salha alishikwa na butwaa na kuhoji kwa hamaki.

"Ndomana nilikwambia huwezi kuamini Salha ila ukweli ni kwamba tangu nilipokuona mara ya kwanza siku ile usiku ulitokea kuuteka sana moyo wangu, kiasi cha kunifanya hata nijute kwanini nilikutana dada yako kwanza.Hata dada yako alipokuwa anakupa simu usiku nikiongea naye unisalimie, hakika nililala usingizi mororo, nimekuwa nikijaribu kuzificha hisia zangu kwako ili nisije kukugombanisha na dadaako lakini kiukwei nilikuwa nashindwa hivyo njia pekee niliyoona inafaa ni kuachana na dada yako ili niwe mbali na wewe kwani isingeleta picha nzuri kukutongoza wewe akati nimeshakuwa na dada yako na wewe usingenielewa hata kidogo!" 

Nilitoa maelezo marefu bila kupumzika, niliongea taratibu lakini kwa uhakika na sumu niliyokuwa nikimtemea Salha ilionekana imeshaanza kumuathiri kisaikolojia kwani alibaki akijiuma uma asipate la kusema.

"Salha!?" Nilimuita baada ya kuona yupo kimya.

" bee!" Aliitika kwa sauti ya uvunguni akionyesha yupo kwenye fikara nzito.

"Nimejikuta nashindwa kubishana na moyo, Nakupenda sana Salha na wewe kama unanipenda kama nnavyokupenda mimi, tafadhali niambie lakini isiwe leo, nakupa muda wa kufikiri juu ya hilo pia kama hunipendi uwe huru kwani mapenzi ni hisia, mwisho kabisa napenda kukwambia kuwa haya yote niliyokwambia leo ni siri niliyoitunza kifuani kwangu muda mrefu sana, nakuomba uitunze pia!..usimwambie mtu yeyote yule sawaa enh!?"

" Sawa Tom nimekuelewa!" Alijibu kwa upole Salha huku akionyesha nguvu zimemuisha kabisa hata kubonyeza kitufe cha kukatia simu inaweza ikawa ni tabu.

" Aya uwe na usiku mwema!"

" Na wewe pia!"

Hivyo ndivyo nilivyomalizana na shemeji yangu Salha aliyenitafuta mwenyewe.

Kiukweli sikuwahi kumpenda Salha hata kumtamani, Na sikuwahi kufikiria kama itatokea siku moja hapa duniani nikaja kumtongoza ila siku hiyo nilithubutu kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili.

Kwanza kabisa sikutaka kuamini hata kidogo kuwa Salha alitaka kunisuluhisha mie na dada yake kwa akili zake mwenyewe kile niliamini lilikuwa ni shinikizo toka kwa dada yake kwa asilimia mia, Kitu kingine sikuamini hata kwa mbali kuwa Malha kweli alienda Tanga ila kile akili yangu ilinituma ni kuwa wapo pamoja muda huo na si ajabu waliniweka loud speaker.

Na mara nyingine Salha alipokuwa akikaa kimya nilipokuwa naongea naye sikutaka kuamini ni kwajili ya maneno yangu matamu hata kidogo ila nilichowaza ni kuwa alikuwa akitazamana na dada yake na huenda walijadiliana ajibu nini.

Kitendo cha mimi kumtongoza Salha ilikuwa ni sawa na kukata mzizi wa fitina kati yangu na dada yake Malha.Sikutaka Malha aendelee kuwa na hisia zozote za mapenzi juu yangu hivyo kitendo hicho cha kumtongozea mdogo wake kama kweli alikuwa naye muda huo kilitosha kabisa kulisambaratisha tumaini lake lililobakia.

Kwa upande mwingine nilichowaza kama Salha hakuwa na dada yake muda huo ni wazi kwamba asingenipigia simu tena maana kama kweli anampenda dada yake asingekubali kutumwa tena sehemu ambayo inaweza kumsababishia matatizo na kama 

Angerogwa na kulikubali ombi langu la kutaka niwe mpenzi wake basi nilikuwa nimemuandalizia zawadi nzuriii ambayo kama ningemkabidhi angenichukia hadi kufa kwake, naam! Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Salha hakurudi tena na mimi sikushughulika na yeye wala dada yake abadani.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni