UZOEFU (21) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 10 Aprili 2021

UZOEFU (21)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Pili na ya tatu alikuwa akijaribu kuuliza ni kwanini sipokei simu na ya nne ilikuwa ni ya lawama nayo ilisomeka hivi ' Tom hivi dada yako akikukosea si unamwambia tu anajirekebisha kuliko kumnyamazia kama hivi!!...Tom naomba unisamehe kama nimekukosea ila tafadhali usinifanyie hivi!"
SASA ENDELEA...
Kadrii Caro aliyoendelea kunitumia meseji na kuongeza missed call ndivyo aliendelea kujichumia marks (alama ) za juu katika jaribio langu na kwa upande mwingine nilihofu asije akapata A+ na kuuteka moyo wangu moja kwa moja. Majira ya saa tisa tena za alasiri nilipokea ujumbe mwingine toka kwa Caro ' Tom nimeshindwa kula toka asubuhi kwajili ako naomba upokee simu yangu niweze kunywa japo maji' akati bado nasoma ujumbe huo 

Caro alipiga simu kwa mara nyingine, sikuweza kuipokea ingawa nilikuwa nalifanya jaribio hilo kama mzaha lakini sasa mambo yalikuwa yameanza kuwa serious, tayari nilishaanza kumuonea huruma dada yangu wa hiyari ( Caro ) Japo awali nilizifurahia meseji zake za kulalamika kwa kuamini ananipenda na kunijali lakini muda ulivyoenda meseji hizo zikaanza kunigusa ( kuni touch) ghafla uzalendo ukaanza kunishinda. 

Japo nilipanga nisiwasiliane nae kutwa nzima hadi siku inayofuata lakini nilijikuta me mwenyewe nimenyanyua simu na kumpigia, Simu ilipoanza kuita moyo ulinidunda sana, sikuwa nimejipanga niseme nini na sikujua niseme nini.

" Hallo!" Nikiwa katika tafakuri zangu za niseme nini, simu ikapokelewa na nikashtuliwa na sauti ya Caro .
" Hallo Caro!" Nilijibu huku nikiigiza sauti ya ugonjwa ambayo pia ilionekana kunishinda.
"Tom una nini kwanini unifanyie hivi lakini!" Caro aliongea kwa sauti iliyokwama kwama na niliamini alikuwa akilengwa lengwa na machozi muda huo.
" Caro yaliyonikuta leo si madogo naomba badae tuonane nkusimulie!" Mambo hayakuwa marahisi kama nilivyozani, sauti ya Caro iliyogubikwa na majonzi ilitosha kabisa kuikombereza furaha yangu na kujikuta nashindwa kuongea.
" Badae tutaonana wapi?" Caro alihoji kama vile hana imani na mimi.
" Jioni ntakuja mtaani kwenu!"
" ok fine!"
" take care my dada!"
" you too!!"
Baada ya kupatana naye nikakata simu huku nikiwaza jioni nitamkabili vipi.
' uhuuuh! walau nna nafuu kidogo!" Caro alinitumia ujumbe mfupi baada ya muda kidogo kupita.
' usijali dada nipo kwajili ako' nilimpoza kwa ujumbe huo.

Majira ya saa moja unusu za usiku tayari nilishakanyaga kwenye viunga vya mtaa anaoishi Caro. Nia na madhumuni hasa yakiwa ni kutoa maelezo ya kina juu ya swala la kutotaka mawasiliano naye siku hiyo, Ingawa sikuwa nimeandaa neno lolote la kusema niliamini kuwa sitakosa jema la kumueleza Caro akanielewa.

" Hallo dada me nishafika hapa!.. njoo basi!" Niliongea kwa madaha baada ya Caro kupokea simu yangu.

" Poa ...dakika sifuri basi ntakuwa shafika!!" Alinijibu kihuni Caro na mie nikatafuta sehemu nzuri ya kumsubiri.

Naifahamu fika njia ambayo atakuja nayo hivyo nikakaa pembeni kwenye kigiza kidogo ili niweze kumuona pindi atakapotokea. Baada ya muda mfupi kweli nilimuona Caro akija ingawa haikuwa dakika sifuri lakini hazikuzidi dakika nyingi. 

Nilipokuwa mimi niliweza kumuona vizuri japo yeye hakuniona hata kidogo, nilimshuhudia akitoa simu yake nakuibonya kabla ya kuiweka sikioni, bila shaka alikuwa akinipigia mimi. nikamnyatia taratibu kisha nikaikamata simu yake iliyokuwa sikioni kana kwamba nikibaka anayetaka kumpora, Caro alishtuka sana na kugeuka kwa hofu huku akiwa anajiandaa kupiga kelele za mwizi.

" Achia simu...achia simu....!!" Niliongea kwa kuiga besi naye baada ya kujua ni mimi akanipiga kikofi cha mzaha kama vile anaua mmbu mwilini mwangu.

"Ohhhuuuu!!......Tom umenishtua!" Aliongea kwa sauti ndogo Caro huku akishika mkono wangu wa kuume na kuweka kwenye titi lake la kushoto, nadhani ili nisikie mapigo ya moyo wake yanavyokwenda kasi.

"Aah jamani sikukusudia ushtuke ivyo!...pole eenh!" Niliongea huku nikiutoa mkono wangu kwenye titi lake haraka kwani tofauti na mapigo ya moyo kuna hisia zingine nilishaanza kuzipata.titi lake la mviringo lililosimama sawia sanjari nakijoto cha huba lililokuwa nalo tayari lilishaanza kuubusti mwili wangu.

" Naona leo umekusudia kuniua kabisaa!" Alilalama kiutani Caro.

"Ahh jamani nikikuuwa wewe nitampata wapi dada mwingine mzuri namna hii??....Sasa tukae wapi kuzungumza hapo au kule!" Nilimuhoji Caro huku nikimuonyesha Caro Restaurent moja iliyokuwa karibu nasi na nyingine ikiwa upande wa pili wa barabara.

" Sitaki kukaa sehemu yenye watu...twende tutembee ili nikuchambe vizuri!" Alichimba mkwara Caro.

" Ayaaa mtoto sijui una nini wewe yani kukuona tu nimesahau kama nilikubebea zawadi!" Niliongea huku nikijisachi mifukoni mwangu kwa kasi kuitafuta zawadi hiyo. Si kwamba nilikuwa nimesahau kama nna zawadi yake, la hasha! Nia na madhumuni ya kufanya hivyo kwa wakati huo ilikuwa ni kuipotezea mada yake ya kunichamba, ingawa sikuamini kama angefanya hivyo ila nilihofu kama atafanya hivyo.

" Hii huondoa hasira za haraka haraka, hali ya kutaka kuchamba wengine na ladha yake huufanya ubongo kusahau kero zote za mchana." Niliongea huku nikimfungulia Caro Chocolate aina ya Franklyn na baada ya kumpatia niliyaanzisha mazungumzo yangu rasmi na muda wote Caro alikuwa akitabasam sijui ni kwajili ya maneno yangu matamu ama ladha nzuri ya chocolate aliyokuwa akiimumunya muda huo.

"Caroline tumekuwa friends ( marafiki ) kwa muda mrefu na ili ujue kuwa darasani somo linaeleweka ni lazima utoe mtihani. I am sorry ( samahani ) kwa kukutest ( kukujaribu ) lakini baada ya jaribio hili napenda kukwambia kuwa nimegundua kuwa wewe ni rafiki mzuri, mwenye real love ( penzi la dhati ) mwenye ku care ( kujali ) na unayetambua value ( thamani ) ya urafiki hivyo am proud of you ( najivunia kuwa nawe ) na nna amini kuwa urafiki wetu utadumu kwa miaka mingi sana, napenda kukupromise ( kukuahidi ) sitakufanyia jaribio lolote lingine na tafadhali sana, nakuomba usije kujaribu kufanya nilichokufanyia wewe kwasababu ukijaribu kufanya hivyo utaniua kabisa na utakuwa umepoteza kaka yako wa pekee anayekupenda sana" Nilimaliza kuongea maneno ambayo sikujua yametokea wapi na nilipomuangalia Caro machozi yalikuwa yakimlenga lenga na yeye baada ya kumuona akanikumbatia.

" Tom kwanini kila siku unakuwa mpya kwangu!?" Caro alinihoji kwa kunong'ona tulipokuwa tumekumbatiana na mimi sikuwa na jibu lingine zaidi ya kumuomba iwe hivyo milele.

Siku hiyo ikawa imeisha kinamna hiyo na bila shaka urafiki wetu baada ya siku hiyo ukawa umepanda ngazi kadhaa juu.

Nilimuahidi Caro kuwa sitampa jaribio lingine lakini pia niliuahidi moyo wangu kuwa iwapo angefaulu jaribio hilo basi ningeenda hatua inayofuata, ni kweli Caro alifaulu vizuri, sasa ilikuwa ni wakati wangu tena kufanya yangu.

Moja kati ya watu nnaoweza kuwaamini hapa duniani ni yule aliyesema mapenzi upofu.Ingawa moyo wangu tayari ulishaanguka juu ya huba la Caro lakini bado nilikuwa nikisita kumtongoza si kwakuwa nilikuwa na hofu ya kupigwa cha mbavu ( kutoswa ). Niliamini kuwa kama ningemwambia Caro nahitaji awe mpenzi wangu basi asingesita kuwa hata kidogo kwani mapenzi siku zote ni kikohozi na nilishaliona hilo.

Sababu moja tu iliyonifanya nisite kutangaza nia ni juu ya umri wa Caro. Mimi nikiwa bado kidato cha sita mwenzangu alishafanya bachelor ( degree ya kwanza ) na kuanza kazi.Ingawa sikuwahi kumuhoji juu ya umri wake , sababu hiyo ilitosha kabisa kuamini kuwa Caro amenifunika ( kanipita ) katika sekta hiyo.Muonekano wake wa kama mtoto wa juzi ( mdogo ) ndio haswaa ulinifanya nitake kuwa nae. 

Hali ya kutojiamini ndio haswaa ilinifanya nitake kupata ushauri wa kimapenzi kwa mara ya kwanza. Sikuwahi kuomba ushauri wa kimapenzi na huwa siombi ushauri wa kimapenzi hata siku moja kwa kuamini kuwa Mapenzi hayana mjuzi hata proffesor (muhadhiri) mtu mwenye elimu kubwa kuliko mwingine kwenye Mapenzi anasanda ( Anachemka ) na analizwa kama kawaida.

Sababu ya kutojiamini kama ntakuwa sahihi au la! Kumtongoza Caro ndio ilinifanya nimshirikishe dada yangu kipenzi.

Sikutaka kumwambia dada jambo lolote kabla ya kumkutanisha na Caro na Sikutaka kumwambia Caro kuwa nitamkutanisha na dada angu nilifanya hivyo makusudi ili mmojawapo asije akapiga chenga pia nilitaka kuwasurprise ( kuwashangaza ). 

Baada ya kumpanga vizuri Caro kuwa nataka kumtoa weekend hii kwa upande wa dada haikuwa tabu nilifahamu fika kuwa dada angu ni mpenzi wa pizza na nikatumia Pizza kufanya mualiko naye.

Kama ilivyo desturi yangu nikilenga sikosi.Ni siku ya Jumamosi tulivu ndiyo niliamua kuifanya special ( maalum) kwajili ya kazi yangu hiyo.

Mimi na dada tukiwa tumetokelezea ( tumependeza ) tayari tulikuwa ndani ya mgahawa Maridadi wa Bongo Flava pande za Masaki, mgahawa unaosifika kwa kuuza harmbugger zenye ladha za kimataifa. Kama kawaida yake dada aliagiza Pizza na mimi niliagiza fanta Orange.

Dada hakuweza kutambua mara moja kwanini sikutaka kula kwanza na kunywa tu fanta pekee lakini ukweli ni kwamba nilikuwa nikimsubiri Caro ambaye hadi muda huo alishakaribia sana kufika, Sikupenda mrembo wangu huyo akifika ale peke yake.

Baada ya dakika chache kupita Caro aliwasili tulipokuwa.Alipendeza hadi nikamsahau.Moyoni nikamsifu saana kwa kupendeza kwake." Ulijuaje kama unakuja kukutana na wifi yako!?" Nilijisemea kimoyo moyo nilipokuwa namvutia kiti ili aketi.

"Mamboo!" Alimsalimu dada angu baada ya kuketi na baada ya Muhudumu kuchukua oda nilitumia nafasi hiyo kutoa utambulisho.

"Caroline she's my sister jina lake atakwambia mwenyewe" Nilimwambia Caro huku nikimshika dada bega.

" Sister she's my best friend jina lake atakwambia mwenyewe!" Pia nilitoa utambulisho kwa dada nikiwa nimemshika Caro bega.

" Iloooh!!... si ushamtaja tayari anaitwa Caroline!" Dada alinipeza bila kunichelewesha maana hata yeye kwa mzaha tu hajambo.

Baada ya utambulisho huo nilihisi Caro amekuwa mpole ghafla sijui ni kwajili ya kutambua uwepo wa wifi yake mahali hapo ama nini ila kwa upande wa dada nilishuhudia akimtazama Caro kwa jicho la udadisi mara kwa mara kama vile anamthaminisha.

Baada ya misosi kuletwa, tulikula huku tukiendelea na porojo za hapa na pale hadi tulipomaliza na kuondoka.

" Saa ya kuja tulikaa wote saivi nakaa na rafiki yangu!" Nilimnon'goneza kiutani dada tulipokuwa tunapanda daladala lakini kiukweli nilikuwa namaanisha nilichokisema kwani tulipopanda tu nilikaa na Caro huku dada akikaa upande wapili.

" Tom!?" Baada ya gari kutembea umbali mrefu huku tukiwa kimya Caro aliniita.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni