PENZI PENZINI (10)

Jpt
0
Mwandishi: Eliado Tarimo

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Aliendelea hivyo mpka wote wakamaliza.Hapo ikawa ngoma drooo hakuna mshindi wala mshindwa.Kwa jinsi walivyochoka hawakuweza hata kuingia bafuni kuoga zaidi ya kila mtu kulala kwa staili ambayo aliijua mwenyewe.Mwingine alikatisha kitanda na mwingine alijikunja kama vile alikuwa akisikia baridi. Kila mtu akapitiwa na usingizi mpaka asubuhi.Asubuhi waliendlea kulala usingizi ule wa kiboss mpaka saa 5 asubuhi.Alice akaamka akandaa chai ya nguvu.Alikaanga mayai na karanga kisha akapaka mayai kwenye karanga kisha akapka asali kwenye silezi za mkate tayari kwa kufungua kinywa.

SASA ENDELEA...
Alitoka nje akaaenda dukani kununua maziwa na kutengeneza chai ya kusukumia hivyo vikorombwezo..Baadaye rafiki yake na Dulah bwana OMARY alikuja wakaenda mjini kuchukua flat screen na king’amuzi na kuzidi kulifanya gheto liwe na mvuto sana.Alice alikumbuka kuwa siku hiyo ndo ilikuwa siku ya welcome freshers hivyo alimuomba 

Dulah ruhusa lakini Dulah alikataa akamwambia haina maana cha msingi wabaki wote waendelee kufurahia wikiendi.Roho ilimuuama sana kulikosa tukio hilo na hasingeweza kulazimisha kuondoka na kumkera mpenzi wake huyo wenye hasira na wivu uliopitiliza.Dulah alimtoa tena mpenzi wake huyo na kumpeleka sehemu ingine tofauti na ya jana.Waliendelea kufurahia wikiendi wote huku Alice akipigiwa simu nyingi sana na marafiki zake kitendo ambacho kilikuwa kinamkerasana Dulah.Alice kuepusha hayo aliamua kuizima simu yake.

Wikiendi ilisha kila mtu akarusi shuleni kwao.Marafiki zake na Alice walimlaumu sana binti huyo kwa kulikosa tukio la jumamosi.Pia walimponda sana kusikia eti boyfriend wake ndo alimzuia. Walimuuliza kwani Dulah amemeoa mpaka akuchunge na kumpangia ratiba na masharti yasiyokuwa na maana. Aliwasikliza tu na kujisemea moyoni hawa hawajui tu jinsi Dullah alivokuwa mkorofi. Kama siku hiyo tu akipanda chuoni waligombana kutokana na nguo alizovaa kuonesha sehemu kubwa ya mgongo. Yaaani Dulaha alikuwa akimpangia binti huyu mpaka mavazi ya kuvaa na yale ambayo yalikaa kimtego mtego na kuwavutia sana wanaume aliyakataa kabisa.

Alice wakati mwingine hakufurahishwa na tabiaa hiyo ya mapenzi wake kumnyima nyima uhuru lakini aliamua kuvumilia kwa sababu alikuwa akimpenda sana mwanume huyo ambaye alikuwa na wivu uliopitiliza.Alice alimpenda sana Dulah na aliamua kumvumilia kwa sababu pia alikuwa akitimiziwa mahitaji yake yote ya muhimu.Yaani Alice aliishi kama malkia na alikuwa na uwezo wa kuja mjini na kufanya shoping yoyote anayoitaka na Dulah akalipia bila kinyongo chochote.Pamoja na mambo mengine yote mazuri Dulah alikuwa akijulikana mpaka kwenye famili yao, hapa namaanisha ndugu jamaa na marafiki wa Alice waliokuwa wakiishi Moshi naArusha.

Na sio hiyo tu Dulah alionesha roho nzuri na alikuwa akiwasaidi mpaka na wadogo zake Alice. Dada zake na mama zake wakubwa na Alicee walimpenda sana kijana huyo wakiaamini kuwa alikuwa chaguo sahihi kwa ndugu yao japo dini ndo ilikuwa ni kikwazo kikubwa sana.Alice alijulikana sana mjini kupitia wanaume huyo na alikuwa akiheshimika sana. Wakati wa likizo Dulla alikuwa akifanya juu chini mpaka kumfuata huko kwao Dodoma ili mradi tu wawe wote.Ilikuwa ni swala gumu sana kwa Dulaha kukaa mbali na Alice kwa zaidi ya wiki mbili. Kwa hiyo Dulah alikuwa akitumia gharama yeyote kuhakisha hawi mbali sana na Alice.

Maisha yaliendelea na marafiki wa karibu wa Alice ambao kila siku walikuwa wakimjaza maneno binti huyo walipelekwa mahali ambapo alikuwa akiishi Alice na Dulah.Kutona na sehemu nzuri na uzuri wa chumba hicho rafiki zake Alice walikuwa wakitamani maisha ya raha kama hayo na pengine walikuwa wakimuonea wivu sana na kumuona ni mwenye bahati ya kupendwa na kijana aliyetokea kwenye famili ya kitajiri.Wapo baadhi ya marafiki ambao walikuwa hawajatulia walidiriki kumtaka Dulah kimapenzi.Dullah akatumia nafasi hiyo kujenga ukaribu nao ilimradi tu awe anapata taarifa za Alice.Kwa hiyo kila Alice alichokuwa akikifanya chuoni yeye alikuwa akikjua.

Alice alitambua kuwa analindwa sana na kufuatiliwa kwa ukaribi hivyo alipunguza idadi kubwa ya marafiki hasa wa kiume na mtu pekee aliyekuwa na mazoea naye ni shemeji yake Gaston.Ilibidi amzoe sana Gaston kwa sababu ndiye aliyekuwa akimsaidia mambo mengi sana ya darasani. Alice hakutaka kabisa rafiki zake wamzoee Gaston sababu rafiki zake pia walikuwa wakimtakahasa Stella. Kwa hiyo Alice hakupenda kuona rafiki yake Jesca ambaye yupo mbai anasalitiwa na yeye akiwa ni sababu ya usaliti huo wakati alipewa jukumu la kumlinda.Ingawa hata yeye alikuwa akivutiwa sana na Gaston lakini mda mwingi alijitahidi kuzuia hisia zake maana aliamini akiziruhusu mda wowote zinaweza kuleta maafa.

Siku zilizidi kuyoyoma na baada ya mwezi tangia siku ile wafanye mapenzi bila kutumia kinga, Alice akaanza kuhisi huenda mambo yameshaharibika kwa sababu hakuweza kuona siku zake.Akaamua kupuuzia akiaamini huenda zimechelewa maana ilikuwa ni kawaida yake wakati mwingine kuchelewa hata wiki moja. Hivyo kutokana na sayansi yake ndogo aliyoisoma akiwa sekondari aliamini yeye ni baadhi ya wanawake ambao walikuwa wakienda mzunguko mrefu wa hedhi.Kuacha ule wa kawaida wa simu 28 yeye aliamini kuwa mzunguko wake ni wa siku 35.

Lakini baada ya miezi miwili ilimbidi amshirikishe Dullah swala hilo na uamuzi uliofikiwa ni kwamba wasubiri wikiendi ifike waende hospitali kupima ujauzito.Kweli wikiendi ilifika wakenda kupima na wakakuta ni kweli Alice alikuwa na mimba. Hapo sasa ikabidi wafanye vikao kujadili swala hilo. Kwa upende wa Alice hakuwa tayari kupata mtoto wakati huo na aliaamini kuwa ilikuwa bado ni mapema sana kwa yeye kuitwa mama.Sio kwake tu hata kwa upnde wa Dullah ilikuwa hivyo hivyo kwa sababu yeye ndo kwanza alikuwa bado yupo form six. Swala la Alice kushika mimba halikuwa la mara ya kwanza bali hiyo lilikuwa la mara ya pili.

Kwa hiyo mara ya kwanza walishafanya machezo huo wa kutoa na sasa walitaka kurudia tena. Wakamtafuta yule daktari wa mara ya kwanza kwa sababu walikuwa na namba zake za simu lakini kwa bahati mbaya alikuwa nje ya nchikikazi.Akawasaidia namba za daktari mwingine amabye angeweza kuwasaidia jambo hilo haramu kinyume na sheriaza nchi na amri za mungu.Walimpata dakatari huyo na aliwaambia atawasaidia ila kama tu watakuwa tayari kulipa kiwango anachotaka kwa sbabu shughuli hiyo kwanza ni dhmbi na pia ni kinyume na sheria.

Aliwaambia ili kuponesha sehemu hizo kwa haraka ni lazima waandae hela ya vidonge ambavyo atavitumia.Hawakuwa na jinsi libidi watoe helahiyo ambayo waliambiwa.Alice aliingia kwenye chumba maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo..Daktari huyo kwa mbwembwe alimuonesha vifaa ambavyo alitakiwa kuvitumia na kumwambia “si unaona hivi ni vipya kabisa na vinatakiwa vitumike kwa mtu mmoja kwa sababu ya afya na tatizo huko mtaani wanatumia zaidi ya mtu mmoja ambayo ni hatari kwa afaya”.Dokta huyo aliendelea kusisitiza kuwa thamani ya mikasi hiyo ni sawa na bei wanaoambiwaga ya kutoa mimba huko mtaani.

Daktari huyo kabla ya kufanya zoezi hilo alimpa somo kidogo Alice kuhusu njia za kuzuia mimba. Alimwambia kuwa yeye sasa hivi ni binti mkubwa mwanachuo kwa hiyo ni aibu sana kushindwa kuzuia mimba. Alice alijitetea eti njia za kuzuia mimba zina madhara lakini Dokta alisisiiza kuwa madhara yake ni mdogo ukilinganisha na madhara ya kutoa mimba mara kwa mara.

Dakatari alimueleza madhara ya kisaikolojia na kiafya ya utoaji wa Mimba.Maneno yale yalimuumiza sana Alice lakini akawa anajisemea “huyu naye si afanye kazi yake mbona nishamlipa ghali”. Daktarri alivaa gloves na kuanza kazi yake. “Panua vizuri miguu tusije tukagusa kizazi” alisema daktari huyo.Alice alishangaa kuona daktari huyo akimpapasa papasa sehemu hizo mpaka akawa anapata stimu za ajabu ajabu za ufanya mapenzi. “Samahani dokta naomba uifanye kazi yako kwa uadilifu maana huko unapogusa gusa ni kutakana ubaya” alisema Alice. Usinifundshe kazi wewe binti hivi unafikiri nisipozilainisha sehemu hizo si utapata maumivu makali? aliuliza Dokta.

Alice ikabidi awe tu mpole na kumuacha daktrai afanye anavyotaka. Baadaye daktari aliingiza vile vifaa nakukamilisha zoezi hilo haramu. Safari hii Alice alisikia maumivu sana tofauti na mara ya kwanza.Daktari akamwandikia dawa na kumuelekeza sehemu ambayo ataweza kuzipata.Yaani Alice hakuweza hata kutembea hivyo ikabidi apumzike kidogo na baadaye alimpigia Dullah na kumwambia asogeze gari karibu.Dullah na yeye aliingiwa na hofu kwa sababu zoezi hilo lilichukua mda mrefu tofauti na alivyzoea.Akaanza kuhisi au daktari pengine ameingiwa na tamaa akajikuta akianza kula kwanza tunda lake. “mbona umechukua mda mrefu sana?” hilo likikuwa swali la kwanza aliloulizwa Alice mara baaada ya kuingia kwenye gari. 

Alice hakujibu swali hilo zaidi ya kumwambia aendeshe gari harakaharaka kwani anajisikia vibaya. Dullah ilibidi afuate tu maelekezo aliyopewa. “Wait , wait, naomba unichukulie dawa kwenye hilo duka hapo mbele alisema Alice mara baada ya Dullah kuenesha gari kwa kasi. Dullah akashuka akanunua hizo dawa na safari ya kuelekea gheto ikaanza. Kwenye gari kimya kilitawala na kila mtu alikuwa bubu. Raha imegeuka karaha. Walifika gheto kwao wakaingia ndani na Alice alikunywa zile dawa na kujilaza.Dullah hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kukaa hapo kwenye sofa kama msafiri aliyekuwa akisubiri gari.

Baadaye mda ulienda na Dullah akawa anataka kwenda mjini kufuatilia mipango ya pesa kwa sababu hakuwa na hela kabisa.Aliamua kutoka na kwenda kununua chipsi kuku sodan na kuweka hapo mezani na yeye akatoka akaingia kwenye gari na kueleka mjini. “Wakati mwingine lazima uwe na roho ngumu sana maana watoto wakike kwa kudeka hawajambo” alijisemea Dullah wakati anaingia kwenye gari. Maadamu simu ipo kukiwa na shida atanipigia alizidi kuwaza Dullah kabla ya kujirizisha kuwa alichokuwa anataka kukifanya ni sahihi.Dullaha ilimbidi avae ujasiri huo kwa sababu hakuwa na hela kabisa na pesa zote za akiba ziliisha kwenye zoezi hilo la utoji mimba.

Alice aliendelea kujilaza pale na baadaye aliamka.Harufu ya zile chipsi zilimshawishi binti huyu kusikia njaa na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa hajala tangia asubuhi. Alianza kufungua soda kisha kuchuku simu na kumigia Dullaha na kumuuliza yupo wapi? Dullaha alimwambia kuna gari la kampuni liliharibika na kaka yake hayupo hivyo imembidi aende ili wakanunue spea kwa sababu wakiwaachia mafundi wenyewe wanachakachua na kuiibia kampuni. Alice hakujibiu kitu zaidi ya kukata simu na kuanza kukata takeaway iliyotumika kufungia zile chipsi. “Daah chipsi za namna hii sijala siku nyingi sijui hata amezinunulia wapi” alijisemea Alice.

Akazifakamia zile chipsi huku akikumbuka jinsi yule dakatari alivykuwa akimchezea sehemu zake za siri kabla ya zoezi lile la kutoa mimba. “Yaani pale nisingemuonya angeweza hata kuniingilia mpuuzi yule asiyejua maadili ya kazi yake” alijisemea Alice. “ Inaeleleka atakuwa ndo tabia yake ya kuwala watu kwa kuwapandisha nyege” aliendelea kujisemea Alice. Hapa inaelekea ule mpapaso wa dakatari ulimsisimua sana Alice sema ndo hivyo haikuwa sehemu sahihi na mtu sahihi wa kufanya naye kale kamchezo. Alice baada ya kula aliendelea kutafakari maishayake ikiwa ni pamoja na raha na karaha za mapenzi alizowahi kuzipitia.

Hapo akakumbuka tukio la yeye kutaka kujinyonga kisa penzi la Dullah.Anakumbuka kipindi hicho ndo alikuwa form five ambapo penzi lao ndo alilikuwa limekoleakupita maelezo.Siku hiyo walitoroka shule yeye na marafiki zake wakaenda mahali kula bata na marafiki zao wa kiume. Sasa walikuwa pair pair ingawa hawakuwa wapenzi lakini kwa mtu hasiyejua angeweza kuzani labda walikuwa ni wapenzi. Wakaenda sehemu moja ambapo pia kuna sehemu ya kuogelea.Huko wakawa wanajiachia kupia maelezo kwa kuwa siku hiyo ilikuwa ni birthday ya mmoja wa rafiki yao.Na kwa kuwa alijiweza kifedha aliandaa kitafrija cha kizungu. Yaani watu sita tu wale, wanywe wacheze na kila kitu ambacho kingewapa furaha.

Kwa bahati mbaya sehemu waliyoenda kulikuwa kuna mtu anayemjua na alipomuona tu alifikisha umbea kwa Dullah.Dullaha akaenda hewani na Alice alipopokea simu swali la kwanza aliloulizwa ni yuppo wapi? Alice kwa kijiamini alimjibu kuwa yupo shulleni. 

Basi Dullah alikata simu na kuamua kwenda sehemu hiyo waliokuwepo kina Alice na marafiki zake wakila bata. Ingawa na yeye Dullah alikuwa shuleni lakini na yeye alitoroka ilimradi afike tu eneo hilo kwa gharama yoyote.Na kweli alifanikiwa kufika na akakuta watu ndo wamekumbatiana wakicheza miziki ya taratibu. Kila mtu alishangaa ujio wa mtu huyo na hawakujua kwa nini mtu huyo aliruhusiwa kuingia sehemu hiyo wakati wenyew waliikodisha kwa matumizi binafsi.

Lakini ukweli ulikuwa ni kwamba hiyo hotel hiyo ilikuwa ni ya baba yake Dullah.Alice siku hiyo ilibidi apagawe maana sehemu yenyewe ilikuwa ni pembeni ya swiming pool na Dullah alimwangalia tu na kuondoka zake kabla ya baadaye kutuma sms ya kuachana naye.

Tukio hilo ni miongoni mwa maatukio yanayomkumbusha Alice juu ya misukosuko aliyopitia mpaka akataka kujiua maana Dullaha alikuwa hamuelewi kabisa.Lakini baadaye Dullah alimsamehe na wakarudiana.Alikula chipsi akamaliza na kurudi zake kitandani na kujilaza. Dullaha aliporudii alikuta Alice ameshakula zile chipsi na amejilaza hapo kitandani huku akichezeea chezea simu yake.

Dullah alaifurahi kuomuona mpenzi wake akiwa ameshakula maana ilikuwa ni ishara nzuri kuwa anaendelea vizuri. “Vipi dear unaendeleaje? Ndo lilikuwa swali la kwanza la Dullah “Naendelea vizuri dearest usijli” alijibu Alice.“Kwani ilikukwaje maana hujanambia kilichotokea zaidi ya kukaa kimya au dakari alianza mambo yake ya kupima maji maana nasikia anatamaasanaa yule hasa akiona vitu vizuri” alihoji Dullah. 

“Hamna shida, hofu yako tu mpenzi” Alice alijaribu kumtetea dakatari. “Sema safari hii nilisikia sana uchungu tofauti na mara ya kwanza na hata mara baada ya kuamalizika kwa zoezi hilo nilihisi kuishiwa nguvu mpaka dakatari akanipa glukosi nilambe”alienedele akufafanua Alice. Walipga stori mbili tatu baadaye waliweka filamu ambayo ilitosha kuwapotezea mda.Wikiendi iliisha na Alice alirudi zake chuoni na Dullaha akarudi zake shule-

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)