PENZI PENZINI (11)

Jpt
0
Mwandishi: Eliado Tarimo

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
“Hamna shida, hofu yako tu mpenzi” Alice alijaribu kumtetea dakatari. “Sema safari hii nilisikia sana uchungu tofauti na mara ya kwanza na hata mara baada ya kuamalizika kwa zoezi hilo nilihisi kuishiwa nguvu mpaka dakatari akanipa glukosi nilambe”alienedele akufafanua Alice. Walipga stori mbili tatu baadaye waliweka filamu ambayo ilitosha kuwapotezea mda.Wikiendi iliisha na Alice alirudi zake chuoni na Dullaha akarudi zake shule-

SASA ENDELEA...
Kwa upande wa Gaston maisha yaliendelea kama kawaida na alijitahidi sana kupunguza mazoea na Mwajabu kwa sababu alihisi kuwa kitendo cha kuendelea kuwa naye kinaweza kumsababishia kuyumbisha jahazi lake la mapenzi na Jesca mtu ambaye hakuwahi kufikiria kuaachananaye.Akaanzisha shera au utaratibu wake mpya kuwa msichana anayesoma naye darasa moja ni marufuku kabisa kuingia chumbani kwake. Alifanya kila hila na kufanikiwa kuachana na Mwajabu. Alimueleza binti huyu ambaye mahusiano yao yalianzishwa na fumanizi kuwa yeye ana wake na Mwajabu ana wake basi kila mtu abaki na wake.

Gaston kummaliza kabisa akachonga mpango na Alice kuwa Alice ajifanye kuwa yeye ndo demu wake mpya hivyo kumrusha roho mwajabu.Gaston alimuweka wazi shemeji yake huyo kuwa binti huyo anamtaka kimapenzi. Gastona alidai kuwa yeye hayupo tayari kumsaliti mpenzi wake Jesca hivyo hiyo ndo njia sahihi. Alice kwa kuwa alikuwa hajui ukweli wowote baina ya Gaston na Mwajabu hivyo alikubali kutumika kama chambo. Visa vilipozidi Mwajabu akakubali matokeo kuwa hawezi kulazimisha mapenzi. Binti huyu akaamua kuendelea na maisha yeka ambayo alikuwa akiishi kabla hajafumaniwa.Mwajabu aliumia sana maana alimpenda Gaston kutoka moyoni kuacha wale waume za watu ambao alikuwa nao kwa sababu za kimaslahi.

Baaada ya fumanizi alijiweka kwa Gaston akiamini kuwa atakuwa akimsaidia helaya kula maana alikuwa akifanya hivyo kabla hata ya kujuana kimwili kwa sababu walishakuwaga ni marafiki. Mwajabu ikumbukwe hakuwa na mkopo na alitokea familia masikini sana ambayo haikuweza kumudu gharama za chuo hivyo aliamua kufanya mambo yote hayo ilimaradi tua apate elimu ya chuo.Kwa hiyo kuachana kwa Gaston kulimaanisha kuwa hata helaya kula itakuwa ni tatizoo kwake.Kwa hiyo Mwajabu ilibidi amtafute baba Juma mume wa mtu ambaye ndo alikuwa msaada wake.

Baba Juma ambaye alipata msukosuko mingii sana baada ya lile fumanizi ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye banda la ngurume alikuwa amepata funzo la mwaka. Ilibidi amueleze ukweli Mwajabu kuwa sasa hivi hawezi kuwa na mchepuko wa aina yeyote.

Mwajabu alijaribu kumshawishi kwa njianyingi lakini ilishindikama kwa sababu mzee huyuo aliamua kutulia na mkewe akasema hawezi kurudia kosa lilomwaibisha hivyo kwa kumsaidia tu alimtumia shilingi elfu 50 akamwambia waachanae kwa amani tu. Mwajabu akaendelea kuishi maisha ya upweke lakini bado aliaamii siku moja ataweza kuwa na Gaston kwa sababu licha ya mambo mengine ya kimaisha ila yeye anahisi moyo wake ulimpenda kiukweli ukweli kijana huyo. 

Gaston alikuwa ni mwanume mkarimu sana kwa sababu alikuwabado akimsaidia kimasomo na siku zingine alikuwa akimpa helaya kula kwa asbabu alikuwa akijua maisha halisi ya bintii huyo. Siku zote Gaston alisisitiza kuwa atamsaidia kwa hali na mali lakini sio kuwa wapenzi. Ukarimu huo ndo ulikuwa ukimfanya Mwajabu aendelee kuamini one day Gaston atakuwa wake. Mwajabu kuonesha kuwa ni kweli anampenda Gaston kutoka moyoni alishafanya uchunguzi na kugundua Alice sio mpenzi wake na Gaston bali ni shemeji yake na pia Alice ana boyfriend wake amabye kila wikienda anakuwa naye tena nje ya maeneno ya chuo ambaye ni Dulah.

Siku zilizidi kwenda na hatimaye wakaingia mwaka mwingine wa kimasomo.Huu ulikuwa ni mwaka mgumu kwa kina Gaston kwa sbabu ndo ulikuwa ni mwaka wao wa mwisho. Gaston alijitahidi kusoma sana kwa bidii ili kuhakikisha wastani wake (GPA) inapanda. Akiwa katika harakati hizo siku moja Beatrice yule msichana wake wa kwanza alikuja Moshi maalumu kwa ajili ya Gaston na hiyo ni kutokana na ahadi yake aliyompa mara ya mwisho walipowasliana.Kama mnakumbuka Beatrice alimwambia Gaston katika maisha yake hajawahi kukutana na mwanaume anayejua mapenzi kama Gaston.Kwa mujibu wa Beatrice yaani pamoja na kwenda Uganda kimasomo lakini bado hakuna mwanaume aliyeweza kumpa furaha ya kweli kama Gaston alivyokuwa akimpa.

Ujio wa binti huyo Moshi ulimchanganya sana Gaston hasijue atafanya nini ili aweze kumkwepa. Akaona njia sahihi ni kumzimia simu siku anayosema anakuja. Lakini kuna wazo moja lilimjia eti kwa nini hasimuone hata jinsi alikvyokuwa je, amezidi kuwa zuri au amechuja?. Gaston kilichokuwa kinamsumbua ni kwamba katika mademu zake wote aliowahi kuwa nao hakuna hata mmoja aliyeweza kufiki uzuri wa Beatrice..Gaston aliamua kumueleza ukweli kuwa yeye ana mtu wake na wapo wote chuoni tena wanakaa chumba kimoja.

Beatrice alyakubali yote hayo lakini alisisitiza kuwa anaomba kuonana na Gaston.Akatoa wazo kuwa yeye atashukia Arusha ili waweze kuonana huko kukwepa usumbufu. Beatrice alisistiiza kuwa Gaston hasiwe na hofu kwa sababu gharama zote ni juu yake. Beatrice kumchnagnya kabisa aliamua kumtumia picha zake zile ambazo zitamtoa udenda Gaston na kuamua kuonana naye.Alimtumia picha za utamu utamu ambazo ni ngumu sana mwanamke kumtumia mwanaume kama hamuamini.Gaston alijikuta akikubali ofa hiyo kwa sharti moja yaani wasubiri wikiendi ifike ili waweze kulala wote na kula bata.Wakati Gastona akitaka kutimiza ule msemo wa awali ni awali hakuna awali mbovu mpenzi wake Jescanaye alipata safari ya kwenda Arusha ambapo alitumwa na baba yake.

Jesca aliamua kumfanyia suprise mpenzi wake Gaston kwa kutomwambia ujio wake ili aafanyie suprise ya kufika gheto kwake.Pia hakuona haja ya kumwambia rafiki yake kipenzi Alice juu ya ujio wake huo. Kwa bahati nzuri au mbaya safari au ujuo wa Jesca na wenyewe ulikuwa ni wikiendi kama ulivyokuwa kwa Beatrice.Basi ijumaa ilifika Gaston akawa anajiandaa vya kutosha kabla ya kwenda Arusha kuonana na Beatrice. Beatrce alimwambia Gaston kuwa apende usafiri mwingine na yeye kwa kuwa anatokea Dar basi wote wakifika Arusha watajua wakutane wapi.

Beatrice hakutaka tabu alipofika Arusha alichukua chumba kwenye moja ya hotel ya kifahari aambayo ilikuwa maeneno ya stendi. Na baada ya kupata room nzuri iliyoendana ana hadhi yake ya kuwa mtoto wa Waziri mstaafu alimwandikia Gaston meseji kumuelekeza mahali alipo.Mda ambao sms inatumwa ndo mda huo huo ambao Gaston alikuwa amefika stend na pia ndo mda huo huo Jesca naye alikuwa akifika stend ya Arusha. Gaston alishuka kwenye gari na kuulizia jengo hilo ambalo alielekezwa. Wakati akaielekezwa mpenzi wake Jesca ambaye alikuwa anashuka kwenye gari alifanikiwa kumouna kupitia dirishani.Jesca alinyanyua simu yake na kumpigia ili kuahkikisha kuwa ni yeye au la. 

Alifanikiwa kuona Gaston akipokea simu jambo lilomfanya Jesca akate na kuanza kushuka kwenye gari.Hata kabla hajasimama vizuri kuna sms ya Gaston iliingia kwenye simu yake. “Nipo darasani mpenzi nitakupigia baadaye. “Huyu mtu atakuwa si mwema kuna ualifu anaenda kufanya yaani mimi ndo huwa nadanganywa hivi yaani leo atanitambua aliwaza Jesca huku hasira zikizidi kumpanda”.Jesca akaamamua kumfuatilia hatua kwa hatua ili aone mwisho wake.Gastona akenda moja kwa moja kwenye hotel hiyo na alipita reception akauliza chumba namba 116 chumba ambacho alikuwepo Beatrice.

Muhudumu akapiga simu kwenye chumba hicho kuthibitisha kama ni kweli binti huyo alikuwa na mgeni wa kiume yaani Gaston. Beatrice alijibu ndio na aelekezwe aende. Jesca na yeye amabaye alikuwa nyuma nyuma baada ya Gaston kukwea lifti na yeye akasema anaenda chumba namba 116 na hapo muhudumu akashangaa ikabidi apige tena simu..****

Baada ya zoezi la kutoa mimba baina ya Alice na Dullah kukamilika kila mtu alirudi kambini kwake.Wikiendi iliyofuta Dullah alikuwa akikabiliwa na mitihani ya MOCK hivyo hakuweza kushuka mjini. Alice alitumia nafasi hiyo kuenjoy na marafiki zake. Alice alishuka gheto akiwa na marafiki zake wawili yaani Easther na Stela.

WikiendI ingine ilifika tena ambapo Dulla alikuwa yupo free baada ya kumaliza mitihani hivyo alikuwa na hamu sana ya kuwa na mpenzi wake Alice.Lakini Alice hakuwa tayari kuwa nae kwa sababu alitakaa mwezi mzima upite bila ya yeye kufanya mapenzi. Hivyo basi alijua kama akikutana naye lazima watachakachuana kwa hiyo alitumia kigezo kuwa na yeye alikuwa na test jumatatu kitu ambacho si kweli. Mbaya zaidi Dullah alikuwa akipata ratiba zote za Alice kuanzia ratiba ya kuingia darasani mpka test na mitihani.

Na alikuwa akipata ratiba hizo kutoka kwa marafiki zake na Alice ambao alijenga nao sana urafiki.Dulah kwa kuwa alikuwa amechoshwa sana na mitihani hakuona hajaya kubisha akaendelea na ratiba zake ikiwa ni pamoja na kuwatafuta marafiki zake ili waweze kubadilishana mawazo.Aliwasilisha hoja ya Alice ili kuomba ushauri kwa marafiki zake ambao aliwaamini sana. Aliwaeleza marafiki zake kuwa mpenzi wake Alice amebadilika sana na amekuwa muongo je afanyaje? “Ujue wasichana wana tabia ya kuchoka kufanya kitu fulani mara kwa mara hivyo cha msingi wewe mpe mda ajitafakari na kama wikiend ijayo hasipoonekana basi utakuwa na hojaya msingi” alifafanua Omary.

Kabla Dulah hajasema kitu Peter rafiki yake mwingine alidakia na kusema hapana “watoto wa kike sio hata wa kuwapa mda, wakishaanza upuuzi wao ni shida ukimpa nafasi tu atakutawala” Dullah akasema anamuunga mkono Peter kwa sababu mwanamke ukimwendeeza atakutawala.Ila kwa namna moja au nyigine hatuwezi kulea ujinga mimi naona tusubiri hiyo wikiendi ijayo hasipokuja ndo tumtafutie adhabu ya kumpa alisema Dulla. Wote kwa pamoja wakakubalina wasubiri wikiendi ijayo ili wajue nini kitaendelea.Waliendelea kupunguza stress za mtihani na baadaye waliamua kwenda club kwa sababu muziki ilikuwa ni moja ya starehe yao.

Kama kawaida waliingia club na kukaa kwenye viti virefu na kuanza kupiga vinywaji.Walikaa sehemuambayo wangeweza kuona kila mtu anayeingia.Watu walizidi kuongezeka kadiri mda ulivyokuwa unaenda. “Ebwana daaaah hao mabint watatu wanaoingia ni shida cheki walivyobomba”alisema Omary ili kuwashitua wenzake. “Wa mbele mbona kama ni shemeji yetu” alishituka Peter mara baada ya kumuona Alice akiwa amevaa kigauni kifupi ambacho kiliacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi hasa mapaja na mgongo.Akafuatiwa na Stela ambaye yeye alikuwa amevaa kibukta kifupi kilichombamba pamoja na Easther amabye na yeye alivaa skin mtepweto ambayo ni shida wenyewe waliziita soksi.

Dullah alitumbua mimacho mara baada ya kuwaona mabinti hao wamekwenda kukaa kaunta utazani makahaba wanaotafuta wateja. Omary alimzuia Dullah mara baada ya kuona anataka kunyanyua na kweenda kuwafuata. “Utaharibu movie broh waache kwanza ili tujue wapo wenyewe au la?” Alisema Peter Waliamua kuahama sehemu hiyo wakaamua kwenda sehemu amabyo ni giza zaidi ili wasionekane. Wlivyonyanyuka tu wale mabinti wakenda kukaa kwenye viti walivyoviacha.

Mziki uliendelea na Stella miongoni mwao ndiye aliyeonekana kuwa na mzuka sana wa kucheza muziki.Baadaye wote mizuka iliwapanda wakaingia stegini na kuanza kucheza.Baadaye waliongezeka wanaume watatu wanaosoma nao hivyo kila mmoja akachukua msichanawake na kuanza kucheza naye. Dullah akaenda chuoni ili ampigie shushushu wake ili kupata habari zaidi.Shushushu wake alimwambia kuwa hapo chuoni kulikuwa na shindano la Mr and Mrs University.Kwa hiyo kwa mda huo shindano lilishamalizika na mshindi alishapatikana na watu wakaenda club kumalizia siku.Dulah akaumuuliza kama anamjua mshindi.Shushushu akamjibu kuwa mshindi ni mmoja wa rafiki zake na Alice .

Hapo Dulah akawa amepata picha kamili kuwa mshindi atakuwa ni Easther maana ndo alikuwa na muonekano wa kimisss na pia alikuwa na kipaji cha kuimba. Hata kama ni hivyo kwa nini anidanaganye si angenambia tu ukweli tungekutanaClub aliwaza Dulah mara baada ya kukata simu. Akasema ataanzisha fujo na hawata amini kitakachotokea.Hakutaka kusubiri alienda moja kwa moja kwenye vile viti na kumshika bega Alice.Alice alipogeuka alikutana na sura ya mpenzzi wake Dulah.Alishituka sana na kujikaza kisha akamwambia “karibu mpenzi”. Dulah kwa hasira akamuuliza hapa ndo chuoni? Alice na yeye akajibu kwa dharau na wewe hapa ndo shuleni.

Kauli hiyo ilimkera sana Dulah akajikuta amemnasa kibao bila ya kutarajia.Alice ikabidi aangue kilio bila kutarajia.Kama hiyo haitoshi Dulah alimvuta nywele na kumpa vibao viwili vya nyongeza jambo lilomfanya Alice alie kwa sauti kubwa. Wale vijana waloikuwa kampani na Alice hawakutaka kusubiri walimvamia Dulah na kuanza kupigananaye. Dulah alikuwa ni mtu wa mazoezi sana si unajua tena ndo waziri wa ulinzi shuleni kwao.Peter na Omary nao hawakuwa mbali walikuja kumsaidi rafiki yao. Ilibidi Dj asimamishe mziki ishara kuwa kuna matatizo.Mabausa walikuja kuamua ugomvi huo kablaya kujua nini chanzo.Dulah alikuwa amevua mkanda wake wa kiunoni kwa hiyo yeyote aliyemsogelea alikuwa akimpatia dozi.

Katika purukushani hizo bausa mmoja alifanikiwa kuudaka ule mkanda hivyo Dulah akawa hana jinsi zaidi ya kukimbia.Alipotoka nje anataka kuvuka barabara maana wale mabausa walikuwa wanakuja kwa kasi akasikiamlio wa defender ya polisi akaona isiwe tabu akaingia chini ya gari moja ambayo lilikuwa karibu nalo. Ile defender ikapita kwa nguvu na ikafanikiwa kuwakamata wasichana wachache ambao walikuwa wakijiuza hapo nje.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)