SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
DEO wakati yeye fikra zake zilimtuma kuwa aacahane nao wote na kubaki single.Alice alitaka kabisa kuachana na kitu kinachoitwa mapenzi na badala yake aliweka dhamira ya kusoma kwa bidiii na kufanya mambo yaliyompeleka chuo. Alirudi shuleni na kuendelea na mambo yake.SASA ENDELEA...
Jesca baada ya kumfuatilia mpenzi wake Gastoni mpaka kwenye ile hotel akitaka kujua nini Gaston anakwenda kufanya humo aliwekewa kizuizi mlangoni.Aliulizwa uunakwenda chumba namba ngapi akasema 166 namba aliyoisiki Gaston akiitaja.Muhudumu alimzuia kwa sababu chumba hicho tayari kilikuwa na watu wawili yaani Gaston na Beatrice.
Na kwa sheria za hapo hotelini idadi ya wanaotakiwa kulala kwenye chumba kimoja wanatakiwa wasizidi wawili.Jesca wa watu mpenzi wa Gaston ujanja ukawa umemuishia akatamani na yeye achukue chumba sehemu hiyo lakini gharama yake ilikuwa ni kubwa sana.
Akaondoka zake na kuamua kurudi stendi.Alichukua simu yake na kumuandikia sms Gaston iliyosema “najua haupo darasani,upo Arusha kwenye hotel fulani. Gaston mpenzi wangu unavyonifanyia ni usaliti mkubwa ila poa tambua kuna matunda ya Usaliti mara baada ya penzi penzini”. Meseji hiyo ya malalamiko haikuweza kusomewa na Gaston kwa sababu simu yake aliwek asilence mara baada ya kuingia kwenye chumba alicokuwepo Beatrice. Jesca alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hasaamini kilichotokea.Au nimemfafanisha alijiuiza Jesca lakini hapana sijamfananisha kwa sababu pale stend nilipopiga simu aliitoa na kunitumia sms eti yupo darasani.
Jesca akaamua kumpiga rafiki yake Alice simu kumpa habari hizo. Waliongea mengi na alimueleza kuwa yupo Arusha aliapewa majukumu na baba yake.Alice alimuuliza mbona amekuja kimya kimya bila taarifa.Jesca akamjibu kuwa alitaka kumfanyia suprise Gaston hivyo anakuja Moshi.
Jesca akamuuliza Alice kuwa si anajua chumba anachokaa shemeji yake Gastoni na Alice akamjibu ndio.Badi nakuja ili tuje tumfanyie suprise ya nguvu.Yaani mpka hapo alikuwa hajamwambia ukweli kuwa amemeuona Gaston Arusha alitaka kufika Moshi kwanza ili akakikisha macho yake hasije kuwa anamfananisha.Jesca aliamua kupanda magari ya Dar yanayorudi Moshi kuanzia safari zake hapo.Mida ya saa 3 kasoro alikuwa tayari ameingia mji wa Mmoshi na moja kwa moja alienda mpka chuoni wa kina Alice. Alienda mpaka hostel wanayokaa na alipokelewa vizuri sana.
Baadaye alimueleaza ukweli rafiki yake kuwaa pamoja kuwa amekuja na alitaka amfanyie Gaston suprise lakini mwaanume huyo yupo Arusha na kimwana mwingine. “Gaston huyo shemeji yangu ninayemjua mimi? aliuliza Alice kwa mshangao.
Ndio huyo huyo shosti, wakati nashuka stend ya Arusha nilimuon kwa macho yangu mawili nikamigia simu akatoa kisha akakata na kunitumia sms kuwa yupo darasani alizidi kufafanua Jesca. “Wewe utakuwa na wenge la macho, ebu kwanza twende gheto kwake tukamwangalie maana hanaga mambo hayo kabisa na mda mwingi anakuwa gheto kwake akiangalia movie” alisema Alice. Wakaanza safari kuelea kwa kwa Gastoni.
Kwa sababu ilikuwa bado ni mapema waliamua kutembea kwa miguu na walipofika walikaribishwa na kufuli kubwa liloandikwa Top security. “Si nilikwambia ebu jaribu kumpigia simu wewe alipendekeza Jesca mara baada ya kuona kufuli hilo.Alice akachukua simu na kumpigia Gaston.Simu iliita lakini haikupokelewa.Akamtumia sms na kumuuliza “shemu uko wapi mini nipo hapa kwako lakini bado haikujibiwa. Huenda maneno uyasemayo yakawa kweli kwa sababu simu yangu na mimi hapokei alisema Alice mara baada ya kupiga zaidi ya mara moja.
Wakati akisema hayo simu yake iiliita na alikuwa ni Deo akipiga simu.Alice aliiangalia ile simu lakini alishindwa kuipokea. Jesca akamwambia kama ni Gaston anapiga pokea simu tu. “Hapana bora ata angekuwa Gastonn huyu anayepiga simu ni zaidi ya majanga alisema Alice. Baada ya simu kupigwa pigwa mara nyingi ilibidi Alice haipokee na swali la kwanza aliloulizwa ni upo wapi akajibu hostel. “Mbona sikuoni na mimi nimekuja hapa alhoji Deo. “Nipo na rafiki yangu nimemsindikiza kwa boyfriend wake” alijibu Alice.
“Nimekuja kuchukua simu yangu kwa sababu nimechoka kutishiwa maiasha na kutukanwa na bwana wako Dulah. Alice akajibu kwa kifupi kuwa “ataipata kesho kwa leo haiwezekani” kisha akakata simu.
Akavuta pumzi ndefu kisha akaiiachia na kusema “yaani wanaume si jui wapoje wote ni wale wale siku zote”. “Vipi best nani tena anakuvuruga?” ilibidi aulize Jesca. “Wacha tu shosti yale majanga ya Dulaha niliyokwambia yanazidi kuwa makubwa hapa sijui hata nifanyaje maaan huyu aliyenipigia sa hivi alinionga simu yake na huyu ni yule mwanaume aliyekuwa akinisumbua sana sasa mara baada ya kugombana na Dulaha nikajikuta namkubalia yaaani najuta najuta kuwafahamu wanaume” alilalamika Alice huku akipga piga miguu.
“Pole sana rafiki yangu sasa si umrudishie tu simu yake maana huyo hana mapenzi ya kweli” alipendekeza Jesca. “Ujue juzi Dulha alinipigia simu na kunimba tuyamalize tukaenda mimi na rafiki yangu na yeye akawa na rafiki yake, tukafanya kikao na kumaliza na tukaenda kulala gheto. Usiku kumbe mwenzangu akaamkana kuanza kupekua pochi yangu ndo akaikuta hiyo simu ya huyo Deo. Sijui hata aliyejuaje password akaifungua na kukutana na sms za mahaba ambazo nilikuwa nachati na huyo mwanaume” alijaribu kufafanua Alice.
“Sasa sijui kwa nini Dulaha ameshindwa kunielewa maana huyu Deo mimi sijawahi kumvulia chupi zaidi ya kuchati naye utumbo tu.Ebu nishauri nifanyaje maana nimechanganyikiwa mwenzio” alisema Alice. “Sio nikushauri bali tushauriane maana hata mimi sipo sawa” alisema Jesca.
Ikabidi waanze safari ya kurudi hostel kwa kina Alice. “Ujue shosti wewe umefanya makosa kwa sababu ni mda mchache sana ukaruhusu moyo wako kumpenda mtu mwingine ambaye pengine hata hakupendi kiukweli alikutamani tu na kutaka kupita nawe.Maana ni kawaida ya wanaume kupenda ngono hata kama ameoa na ana watoto “alifafanua Jesca.
Alice akamjibu kwa kumwambia “hayo yote unayoyasema ni kweli lakini maji yakishamwagika hayazoleki na kwa jinsi Dulah alivyonipiga na kunigeuza gunia la mazoezi siwezi kurudi tena nyuma nitaaishii mwenyewe” alisistiza Alice.Jesca akamwambia “mapenzi ni upofu usiseme hivyo kwa sababu mbele huoni”. Waliendelea kuongea mpaka wakafika hostel ambapo walimkuta Stella na Easther.
“Yaanii bora umekuja matusi ninayotukwanwa kwa ajili yako ni makubwa” Stella alimkaribisha Alice kwa staili hiyo. “Nani amekutukana best?” aliuliza Alice kwa upole. “Yaani Deo amekuja hapa kama mbogo amesema eti siku ile tulivyoenda mjini alikuwa anakufuatilia mpaka tulipokuwa pale Uhuru Park na anajua kila kitu kinachoennndelea na bwana wako amempigia simu na kumtishia maisha kama eti ataendelea kukushika masikio” alisema Stela akinukuuu maneno ya Deo.
“Wote ni wapuuuzi tu wasitake kunichanganya” alisema Alice kwa hasira. “Sio wapuuuzi wewe umeshindwa kuzichanga karata zako vizuri huna msimamo hujui ushike wapi na uache wapi” alidakia Easther. “We naye usitake kunivuruga niache kila mtu afuate mambo yake alimjibu” Alice kwa hasira. Alice akamwambia Jesca waondoke eneo hilo wakatafute chakula. Wakenda kuchukua chipsi take away huku Alice akionekana kuchanganyikiwa kabisa. Wakiwa njiani Alice alikuwa akilalamika juu ya Easther “Yaani huyu Easther kushindwa miss university anajiona yeye ndo kila kitu anaweza kuniendesha atakavyo wewe muache tu aaendelee nitamvuruga hasiamini”.
“Achana naye bwana wala usipaniki mambo ya kawaida sana alisema Jesca. Wakachukua chakula na kurudi hostel wakaanza kula huku Alice akiendelea kuzama kwenye dimbwi la mawazo mazito sana hasijue nini cha kufanya. Hapa cha msingi ni kumpigiaa simu Dulah na kumwambia mwenyewe anataka simu yake aliwaza Alice.
Alice akanyanyua simu na kumpigia Dulaha ambaye wakati huo alikuwa bar akinywa pombe kama mtu aliyechanganyikiwa. Dulah hakuweza kufanya jambo lolote zaidi ya kumwaaza Alice huku akijiuliza maswali mengi ambayo yalikosa majibu. Aliingalia ile simu ya Alice akaaiacha ikaaita mpaka ikakata kisha akapiga yeye a baada ya salamu Alice alimwambia mwenyewe anataka simu yake.
Dulah kwa akili za pombe akacheka sana na kumwambia “mimi nikajua unaniletea funguo ila kama ni ishu ya simu sahau mimi siwezi kulea ujinga nishaivunjilia mbali”. Alice kwa hasira akakata simu na kusema “huyu hanijui mimi ngoja kukuche nitamuaoneshea”.Akamwangalia rafiki yake Easther aliyekuwepo pembeni na kumwambia haya toa ushauri ila sio lawama.
“Mimi naona hapo kwa kuwa una ufunguo kesho tufike eneo la tukio tuchukue kila kitu kinachobebeka alafu tuone nani atakuwa amefaidi kati yako na yeye” alipendekeza Easther. Kwanza vile vitu si mlinunua wote? aliuliza Easther ambaye alionekana ni mjanja kuliko wote kwenye grup lao. Alice akasema “vitu vyote ni vyake sema kwenye hela ya kodi nilimsaidia”.
“Hata kama kwani si alikuwa anaishi na wewe kama amekuoa vile sasa mbona sheria ipo wazi wewe kubali tu ushauri wangu niandae kikosi kazi” alisema Easther. Kila mtu alibaki akimuangalia mwenzake wasijue ujasiri huo mtoto wa kike Easther anaupata wapi. “Mnachoshangaa nini na kunitumbulia mimacho hivi umesahau ile simu ya Deo ni iphone latest thamani yake ni zaidi ya laki tano sasa unafikiri hiyo hela utaipata wapi kama simu imeshavunjwa vunjwa” alihoji Easther.
Wakati wakiendelea na mashauriano juu ya ukatili wanaotaka kufanya simu ya Alice iliita na kuangalia alikuwa ni Omary rafiki yake na Dulah. “Niambie shemu” alisema Alice mara baada ya kupokea simu. “Naomba unisaidie kitu kimoja” alisema Omary.Kitu gani aliuliza Alice? Ni kuhusu hizo funguo maana mule ndani pia kuna vitu vyangu alisema Omary .
“Utanisamehe shemu wangu fanya mambo yako hayo mengine tuachie mimi na Dulah” alisema Alice na kukuta simu. Baada ya kukata simu akamwambia Easther sasa unaweza kuandaa kikosi cha kazi akikisha hicho kikosi kuna wanaume wa nguvu maana kishanuka hapa ni kuwindana na kulipa visasi maana huyo aliyepiga simu ndo mbaya zaidi anaweza kumpa ushauri Dulah ukawa na madhara makubwa sana kwetu.
“Sasa hayo ndo maamuzi ya kiume alisema easther huku akinyanua simu na kuwapigia simu wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao aliwaamini kuhusu mambo ya fujo. Akaja kijana mmoja na kuanza kupanga mikakati ya kwenda kukomba vitu vyote kwenye gheto la Dulah.
“Kama ni hivyo tutaingia na Noah tutasomba kila kitu isipokuwa soffa na kitanda yaani mpaka godoro tutabeba” alisema kijana huyo huku akitafuna mirungi ambayo ilikuwa imejaa mdomoni mwake.
Kwa upande wa Dulah na Omary mara baada ya kupewa majibu hayo mabaya na wao walishauriana juu ya nini kifanyike.Omary alisema huyu mwanamke sio mzuri tukiendelea kumchekea atakuja kubeba vile vitu pale chumbani.Cha msingi ni kuongea na mwenye nyumba tuvunje mlango tubadilishe na kuweka kitasa kingine.
Dulah alicheka mno na kumwambia rafiki yake huyo aache mawazo ya uwoga maana Alice hana ujasiri huo kwa sababu vitu vytoe pale ndani ni vya kwake na Alice alichangaia kodi tu. Usijiaminishe ndugu na cha msingi ni bora tukachukua angaliazo aliendelea kusistiza bwana Omary.Na siku zote “usimwamini mbwa anayechechemea au mwanamke anayelia”.
Pia ni vigumu sana kwa sheteani kuwa malaika ila ni rahisi sana kwa malaika kuwa shetani. Wewe unafikiri kwa nini aondoke na funguo zote mbili kama sio ana lake la moyoni alihoji bwana Omary. “Aaaaaahhha hacha uwoga mtoto wa kiume yule demu ni malaya tu hana lolote na hii simu ndo inamchanganya na kwa ushenzi si mrudishii ili nione atafanyaje” alisema Duulha huku akipiga pafu la pombe. Yaani alikuwa ameleewa chakari na Omary alikuwa anaogopa hata kumuacha mwenyewe maaana mda wowote angeweza kufanya kitu kibaya.*
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA