SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Akachukua namba za Deo akazisevu kwenye simu yake pia akachukua za marafiki zake wa karibu na Alice pia akazisevu. Kisha aakaamua kutuma sms kwa Deo iliyosema “vipi mpenzi, natamani tungekuwa tumelala wote” meseji ikajibiwa mda huo huo “Kwa hiyo ukiwa kwa dada yako ndo unazima simu mpenzi ?. “Hapana simu iliisha chaji alafu umeme ulikatika” alijibu Dulah akijifannya yeye ndo Alice. Deo akaamua kupiga simu mara baada ya kuona sms zake hazijibiwi tena.SASA ENDELEA...
“Usipige simu mpenzi usiku huu si unajua nimelala na dada yangu” .Mara baada ya Dulaha kujibu sms hiyo hasira zilimpanda sana hasijue nini cha kufanya.Wanasemaga kuwa kuna zawadi ya uvimilivu na ushindi lakini hii itaukwa ni zawadi ya usaliti.Anasatahiili avune alichokipanda this is too much anda i cant tolerent anya more.
Wakati Dulah akaiendelea kuwa kwenye mawazo mazito na kuonja machungu ya mapenzi usiku huo.Alice alishituka kutoka usingizni na akajikuta yupo mwenyewe kitandani.Akajifunga khanga yake na kutoka nje ambapo alimkuta Dullah akilia kilio ambacho hakikuwa na sauti.Kilio kilichoonesha kuwa alikuwa na uchungu sana ndani ya nafsi yake.
Alice alisogea karibu yake na kuanza kumuuliza “mbona unalia kwani kuna tatizo gani babee.?”.Hapo ndo akawa amemzidishia machungu na kufanya Dulah azidi kulia kama mtoto mdogo.
“Mbona sijakuelewa mpenzi wangu tatizo nini?” alihojii Alice kwa upole.Dullah hakutaka kuongea kwa meneno tu bali vitendo, alimpa ile simu ambayo ndo ilikuwa na ushaidi wote. Alice alianza kutetemeka hasijue nini cha kufanya.
Mbona niiificha mbali sana na na ninii kilimfanya apekeue simu yangu aliwaza Alce huku akiendelea kutetemeka?. “Mbona hujibu kitu” aliuliza tena Dulah akwa hasira. “Babee hiyo simu ni ya rafiki yangu alinipa nimsaidie niipeleke kwa fundi alijibu Alice. “Kwa hiyo rafiki yako anaitwa Alice siyo aliuliza tena Dulah kwa ghadhabu. .”Ndio babeee huyo ni wajina wangu aliendelea kudanganya Alice.
“Kwa hiyo wewe unanifanya mimi ni mtoto mdogo sio aliuliza Dulaha na kunyanyua na kuiingia chumbani”. Alice alimfuata huku akimsihi apunguze jazba kwa sababu mambo kama hayo yanazungumzika. “Nilishakwambia nifanyie vitu vyote ila sio usaliti” alisema Dulalah. “Unastahili matunda ya usaliti na leo nitakuonesha” alisema Dulah huku ailifunga mlango na kuongeza sauti yaradio. “Babee punguza sauti ya radio utawaamsha majirani usiku huu” Alice lijaribu kumuelewesha Dulah mara baada ya kuona hiyo sauti ilikuwa ni kubwa sana na ukizingatia ilikuwa ni usiku sana.
Hapo Dulaha hakumjibu kitu zaidi ya kuanza kumshushuia kipondo utazani alikua akipiga mwizi.Alizivuta nywele, akampiga makofi, akachukua mkanda na kuanza kumchpa mapajani. Alimpiga sana mpaka Alice ilimbidi aombe masamaaha kwa kusemaa “babee utaniua niache tu nikuambie ukweli”. “Niaache niachee nitasema ukweli” alilalamika Alice mara baada ya kuona kipigo kimekuwa kikali sana. Alice alilia sana na kujuta kukubali kurudiana na Dulaha ambeye ni mkatili hasiyejua njia sahihi za kujua ukweli kutoka kwa mwanamke. “Haya sema huo ukweli kabla sijakuulia huku ndani” alisema Dulah.
“Kwa kifupi Deoo ni mwanaume aliyekuwa akinisumbua tangia niingie chuoni lakini sikuweza kuwa nae. Siku ile tulipogombana pale club na nikaona umekaa kimya mimi nikajua basi huo ndo mwishoo wa mapenzi yetu, nikaamuaa kumkubalia” alisema Alice huku akijifuta machozi.
Hapo Dulaha akashuka kidogo na kuwa mpole na kuuliza “Kwa hiyo ndani ya wikiendi 2 tu ushapata mtu mpya na amekuonga mpaka simu”?. “Babee nisameehe nilifanya maamuizi ya kukurupuka na hata hivyo simpendi ilikuwa ni stresss” tu aliendelea kujitetea Alice. “Kwa hiyo kama humpendi kwa nini ulikubali kuongwa simu tena sim uyagharama kama hii” aliuliza Dulaha kwa hasira.
“Hivi ungenambia kama unataka simu ya kuuzia sura si ningekununulia tu kuliko hivyo unavyofanya kutuchanganya” aliuliza kwa mtindo wa kulalamika kijana Dulah.Waliongea mpka pakakucha lakini hawakufikia muhafaka. Kwa sababu Alice alikaomaa na msimamo kuwa atajua jinsi ya kumalizana na Deo na kwamba ataenda chuo na kumueleza ukweli kuwa amerudiana na mpenzi wake.
Dulaha yeye alikomaaa na msimamo kuwa kama kweli anataka kuendelea na yeye ahakikishe kuwa wanampigia simu Deo aje mjini akutane na kuongea ana kwa ana wote watatu. Alice alisema anawajua wanaume wa darasani kwao sio waungwana ni wapenda shari hivyo wakifanya hivyo watamjengea bifu na watu wengi na pia Deo anaweza kumchafuadarasani.
Msimamo wa Alice ndo ulikuwa ni huo hawezi mpigia simu Deo, wala hawezi kumwambia kuwa aende mjini. Muafaka ukashindwa kupatikana ikabidi Omary mzee wa usuluhishi mwenye busara nyingi japo ni kijana mdogo apigiwe simu. Alice alichukua simu yake na kumpigia omary. Omary alipopokea akakutana na sauti ya kike na mara baada ya salamu fupi akamuuliza kulikoni asubuhi yote hiyo?. “Shem naomba uje mara mojakuna tatizo limetokea” chukua bodaboda mimi nitalipi alisema Alice na kukakata simu. Omary hakurizika na maelezo hayo ya Alice akaamua kupiga simu kwa Dullah lakini bado ilipokelewa na Alice an akuulizwa vipi tayari umefika. Hapo ikabdi Dulah awe mpole na kumwabia ndo kwanza yupo njiani anaenda.
Omary akachukua bodaboda na kuelekae eneo a tukio haraka haraka maana alihisi labda Dullah amepatwa na tatizo kubwa na ndio maana hata simu yake ilikuwa ikipokelewa na Alice. Omary alibisha hodi na alipokaribishwa aliingia na kuwakuta wapendanao hao wakiwa wamekaa kihuzuni kama vile kulikuwa na msiba. Alipomwangalia Dullah aligundua kuwa alikuwa na macho mekendu na alipomwangia Alice aligundua kuwa alikuwa amevimba usoni. Dulah aalimpa ishara kuwa aketi sofani.
“Shem basi tumekuita hapa kuna tatizo limetokea usiku” alifungua mazunguzmo Alice kwa staili hiyo. “Baada ya kile kikao kama ulivyoshauri sisi tulikuja hapa huku tukiwa wenye furaha. Ila usiku furaha iliingia doa kwani rafiki yako aliamka na kupekeua pochi yangu na kakuta kuna simu aliyoifungua na kukuta sms za mapeni ambazo nilikuwa nikichati na Deo.Sasa ndo najaribu kumuelewesha Dulaha haelewi na amenipiga sana usiku wa leo” aliongea Alive bla kuweka nukta.
Omrry akauliza “huyo Deo ni nani wako mpaka mnachati sms za ampenzi?”. “Ujue shemu siku ile club Dullaha aliniuzi sana na siku zilizofuata hakunitafuta na uyu Deo mimi alikuwa akinisumbua sana kwa mda mrefu akinitaka kimapenzi ikabidi nimkubalie tu kwani niliamini Dulaha hawezi kuwa na mimi tena” alifafanua Alice.Kauli hiyo ilimchanganya
Omary kwa sababu haingii akilini unagombana na mpenzi wako leo alafu kesho yake unakuwa tayari umemkubali mwingine. Alice anasisitiza kuwa alifanya maamuzi akiwa na stress ila bado hajafanya lolote na mwanaume huyo hapa alimaanaisha kufanya mapenzi.
Kauli hiyo ilimfanya Dulah hashindwe kuendelea kukaa kimya na kusema “Haingii akilini kwa sababu mimi na wewe hakuna aliyemtamkia mwenzeke kuwa mapenzi yameisha na na ndani ya wiki hiyo hiyo umemkubalia mwanaume mwingine na amekuonga mpaka simu. Mimi naomba utamke mbel aya Omary kuwa upo tayari kuendelea na mimi au Huyo Deo wako”.
“Mimi nipo tayari kuendelea na wewe na ndio maana nimempigia Omary aje tuyamalize.
Omary akasema sasa kama ni hivyo mimi naona swala hapo ni dogo sana mpigie huyo Deo mwambie aje mjini mkutane alafu sisi tutajua cha kufanya. Tutakuja sehemu hiyo na kufanya ambushi ya kumuonya aache kutembea na wake za watu.Nazani hiyo ndo itakuwa njia sahihi ya kumfanya akate tamaa na wewe na kukuogoa alisema Omary . “Exacly yaani kama ulikuwa kichwani mwangu alipigilia msumari bwana Dullaha.
“Sio sawa shemu mimi nilikuwa naomba mnipe mda mimi nitamalizana na huyu mtu kwa njia zangu mwenyewe ambazo hazitanichafulia jina hapo chuoni” alisema Alice. “Shem kama kweli umeniita hapa kwa ajili ya usuluhishi basi naomba umpigie simu au niwaache mimi niendelee na shughuli zangu maana tunachojadili hapa ni upuuzi alisema
Omary huku akinyanyuka ishara kuwa alikuwa akitaka kuondoka. Alice kuona hivyo akasema “Shemu kaa chini nampgia sasa hivi.Alice akachukua simu lakini hakupiga zaidi ya kubofya bofya kama mtualiyekuwa akichati.Omary akampa ishara Dullah kuwa aikwapue simu.Dullah akafanya kama alivyoambiwa kwa ishara ya kichwa na mikono kisha akafungua mlango na kuondoka zake na kuwaaacha Alice na Omary ndani.
Kitendo cha Dulaha kumpokonywa simu Alice kilimkera sana binti huyo kwa sababu alikuwa kwenye mchakato wa kumtuma sms ya uwongo Deo.Kwa kifupi Alice alikuwa hataki kuachna na Deo kwa ghafla na wakati huo huo alikuwa yupo tayari aendelee na Dulah.Dulah yeye mara baada ya kuipokonya ile simu alitoka nje na kufunga mlango kisha kuondoka na ufunguo.Kwa mantiki hiyo ndani alibaki Omary na shemeji yake.
Alice kwa hasira alianza kupaki nguo zake kwenye mabegi. Dulaha alivyofika getini akamtumia sms Omary kuwa wafanyaje?Omary akamwambia “njoo tufungulie mlango kisha wewe uondoke na hiyo simu mimi nitamalizana naye taratibu kisha nitamwomba tukutane mjini tuyamalize”.
Kwa hiyo Dulah alirudi akafungua mlango kisha akondoka zake kama alivyopewa maagizo na mzee wa usuluhishi wa mgogoo wa mapenzi. Omary alifanikiwa kumbembeleza Alice mpaka akakubali kuacha kupanga nguo na kwenda mjini kuongea na Dullah. Basi waliondoka pamoja na wakiwa wanaenda stend ya hice Alice alibadili mawazo na kumwambia Omary “ Shemu mimi sipo sawa hivyo sitaki tena mazungumzo ngoja niende tu kwa mama yangu mkubwa.”
Omary kwa kuwa na yeye alikuwa amechoka kumbembeleza Alice alimkubalia na kumwambia vyovyote atakavyoona yeye ni sawa. Alice akamwambia basi anaomba funguo akachukue pochi yake maana ndo ilikuwa na hela. Ilibidi Omary ampigie simu kwanza Dulah na kumwambia kuwa Alice hataki tena mazungumzo na je ampe funguao maana anadai anataka kwenda kuchukua pochi yake anayodai ina hela.Dulah akajibu kwa kifupi mpe tu hizo funguo. Ingawa Omary alisita kumpa funguo ila kwa sababu mwenye nyumba alisema apewe alimpa.
Alice akaita bodaboda na kuondoka zake. “Huyu mwanamke atakuwa na matatizo mengi sana” alisema Omary mara baada ya Alice kuondoka.
Omary akampigia simu rafiki yake Dulah na alimwelekeza sehemu aliyopo.Omary alifika sehemu aliyoelekezwa na alishangaa kumkuta Dulah akiwa anakunywa pombe asubuhi hiyo. “Stress is fertilizer of creativity” Dulah alaimkaribisha kwa kauli hiyo.
Ingawa Omary aligundua kuwa rafiki yake anautumia msemo huo vibaya na yeye badala ya kuagiza pombe yeye aliagiza supu. “Kwa hiyo amesema hataki tena aliuliza Dulah wakati Omary akiendelea kusubiri oda yake. Omary alicheka kidogo na kumwambia “ If cant and imposible no way out leave them baried”. “Haina haja ya kung’anga’nia huenda sio fungu lako” aliongeza bwana Omary.Kweli kabisa alidakia Dulaha na kuongeza kuwa yeye anaamini bahati ya mtu ipo mbele kwa mbele.
Waliendela kupiga stori na Dulah alikuwa tayari ameshampigia simu Deo na kumueleza kuwa Alice ni mke wa mtu hivyo awe makini kwa sababu mke wa mtu ni sumu hisiyotibiwa kwa maziwa. “Huyu mwanaume anaoekana kuwa na kiburi sana lakini mimi nitamuonesha mimi ni nani?” aliendelea kusema Dulah.
Huu mji ni wa kwetu tumezaliwa humu tumekulia humu hivyo nitatumia gharama zangu zote kuwashikisha adabu aliongeza Dulah. Omary alimwambia haina haja ya kupoteza mda kuaangaika na wajinga kwa sababu kufanya hivyo ni kuwapa changamoto na misukosuko itakayosababisha wao kupendana.
Omary aliendelea kumsihi bwana Dulah hasiangaike na watu hao kwa sababu kufanya hivyo ni swa na kulazimisha mapenzi.
Dulaha alimwambia Omary anamuelewa sana kwa falsafa zake nzuri ila sasa revange is a reason he should get up each day(kisasi ndo sababu inayomfanya amke kila siku). “Ndo maana nakwambia njia hizo hazitakusaidia labda ungebadilisha mikakati kutoka kwenye kisasi mpaka kwenye “Forgiveness is the greatest revange”(msamaha ni kisasi tosha).Kwa upande wa Alice yeye alirudi gheto akapanga vitu vyake kisha akaita tax na kundoka zake. Alichukua vtu vilivyoweza kubebeka na muhimu kwake. Aliwaza kuhusu simu ya Deo aliyoongwa lakini bado hakupata jibu.
Kwa kuwa Dulah alimpokonya simu na kuondoka kibabe na yeye aliamua kuondoka kibabe kwa kundoka na funguo. Aliamini kitendo chake cha kuondoka na funguo kitamfanya Dulah aamtafute na hiyo ndo itakuwa njia rahisi ya yeye kupata simu ya watu aliyoongwa. Aliamini pia bila kurudisha simu hiyo itamlazimu yeye kuendelea na mapenzi na
DEO wakati yeye fikra zake zilimtuma kuwa aacahane nao wote na kubaki single.Alice alitaka kabisa kuachana na kitu kinachoitwa mapenzi na badala yake aliweka dhamira ya kusoma kwa bidiii na kufanya mambo yaliyompeleka chuo. Alirudi shuleni na kuendelea na mambo yake.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA