PENZI PENZINI (17)

Jpt
0
Mwandishi: Eliado Tarimo

SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
“Ukiwa na mimi naomba usilitaje hilo jina tafadhali” alisema Beatrice kuonesha kuwa amekereka. Gaston ahakujibu kitu zaidi ya kuendelea kufakamia chakula amabcho kilikuwa mbele yake. “Asante kwa chakula alisema Gaston mara baada ya kumaliza kula. “Yaani wewe unanichekesha sana asante kwa chakula kwa ni mimi ndo nimepika?” aluliza Beatrice. Mama yangu alinifunza kushukuru kabla na baada ya kula na kama chakula hiki umelipia wewe basi inanipasa kushukuru alisema Gaston. “Dah inaelekea siku hizi una busara” sana alisema Beatrice mara baada ya kufurahiswa na maneno ya Gaston.

SASA ENDELEA...
Waliendelea kupiga stori za hapa na pale huku kila mmoja akimuuliza mwenzake maisha yaliendaje mara baada ya kuachana.Kila mtu alaieleza raha na karaha alizozipitia. Baadaye waliamua kuingia ndani mara baada ya kuona hali ya hewa imebadilika na kuwa ya baridi.Kibaridi cha Arusha kilianza kupuliza na kufanya sehemu hiyo ya juu kushindwa kukalika. Waliingia ndani na kulala. Usiku wa manane Beatrice aaimwamsha Gaston ambaye alikuwa akifurahia usingizi mwanana kwenye kitanda hicho chenye raha za ajabu.

Beatrice hakuona aibu ya kumuamsha kwa nguvu mara baada ya kuona juhudi zake za kumchezea na kumshikashika kunako haziizai matunda. Gaston kwa kuwa alikuwa na uchovu wa masomo alijigeuza na kumpa ishara kuwa Beatrice ajipakulie mwenyewe.Beatrice akapanda juu na kuanza kuongoza safari hiyo inayoaaminika kuwa na raha sana raha za huba. 

Beatrice akajipakulia saizi yake na alisahau tu kuweka matunda ambayo yangefanya umlo huo kuwa mlo kamili. Gaston kwa kuligundua hilo aliamua kumuwekea matunda kwenye sahani yake kwa kumsalidia kumpakulia vitu hadimu. Sio matunda tu bali alimwekea chachamdu kali ya mapenzi na kumfanya Beatrice kutoa machozi na kujuta kuomba kupakuliwa chakula hicho usiku huo.

Walimaliza na kupitiwa na usingizi.Alfajiri na mapema kibaridi kilizidi na kumfanya Gaston ashituke na kutaka kutafuta joto kwenye mwili wa Beatrice. Kwa kuwa Gaston ndo alikuwa dereva mzoefu basi hakutaka kumsubiri sana abiria wake yeye aliwasha gari na kupiga honi kuashiria safari inataka kuanza. Abiria Beatrice alikuwa anasuasua kuamka hivyo 

Gaston aliamua kuupanda mchuma hivyo hivyo. Beatrice kuja kushituka usingizini anakuta tayari ndege ishaanza safari ikabido na yeya afunge mikanda vizuri ili hasije kupatwa na majanga.Safari hii Beatrice alikuwa chini akizungusha zungusha ki kwetu kwetu kile kiuno laini alichojaliwa na Mungu. Alizungusha kisawasawa na ikumbukwe Beatrice alijua kutofautisha mauno ya sebene na mauno ya mahaba niue nilegeze na kunigaragaza kabisa.

Zoezi liliendelea mpaka wote wakafikia safari yao ya mda mrefu ambayo walikuwa wameianza tangia jana na kuweka vituo mbali mbali kwa ajili ya kupumzika.Walikaa hapo mpaka mida ya kurudisha chumba na kwa sababu Gaston alisisitiza kuwa anataka kurudi chuoni basi ziara yao iiishia hapo. Beatrice naye akasema anaenda Moshi kumsalimia bibi yake hivyo wote safari yao ikawa ya kuelekea Moshi. Walipofika stend ya Moshi Gaston ilibidi amsindikize Beatrice kwenye stend ndogo ambapo angepata magari ya kuelekea huko Marangu Mtoni.

Kumbe wakati huo na kina Jesca na Alice walikuwa stend.Jesca alikuwa akirudi zake Arusha kukamilisha kazi aliyotumwa na baba yake. Walifanikiwa kumuona Gaston akiwa na kimwana huyo ambaye pamoja na mambo mengine aliwafunika Jesca na Alice kwa uzuri. Mbaya zaidi Jesca alifanikiwa kumtambua Beatrice kwa sababu licha ya kusikia historia yake pia Gaston aliwahi kumuonesha picha zake na kumueleza kuwa huyo ndiye alikuwa girlfriend wa kwanza.

Roho ilimuuma sana Jesca na kuamua kumfuta Gaston na kabla hata Beatrice hajapanda gari alitokea mbele yao.Ilikuwa ni zaidi ya shoti ya umeme kwa Gaston kumwona Jesca akiwa mbele yake na sio Jesca tu bali na shemeji yake Alice. Jesca alimsogelea huku machozi yakimtoka na kumwambia “ Gaton asante kwa zawadi ya usalit lakini tambua ipo siku utanikumbuka na wewe utaonja machungu ya usaliti”. 

Beatrice naye kwa mbwembwe aliuliza huyu ndo nani babee? Gaston hakuwa na jibu la swali hilo zaidi ya kuendelea kukaa kimya na kutetemeka utazani kulikuwa na baridi kali ya kutisha.
Gari likuja na Beatrice akambusu Gaston akaanda gari na kuondoka zake. Jesca akazidi kupandwa na hasira na yeye akavuka barabara na kuondoka zake.Alice alishika kichwa kwa jinsi rafiki yake alivyovuka barabara kizemba bila kuangalia pembeni. Mlio wa honi ulipoigwa na gari ndo ndo ulimshitua kila mtu na kuthibitisha kuwa Jesca alikuwa amechanganyikiwa kwa kile alichokiona.

“Take care of her, we will talk later on”(muangalie tutaongea baadaye) alisema Gaston mara baada ya kuhisi kuwa Jesca hakuwa sawa na anaweza kupatwa na matatizo makubwa mda wowote. Alice naye alivuka barabara kumkimbilia rafiki yake.Gaston alifikiria haraharaka cha kufanya akaona bora awafuate kwa nyuma Aliwakuta ndo wanaagana hili Jescaa ingie kwenye gari tayari kwa kuondoka na kurudi zake Arusha. “Please baby, naomba tuongee” alisema Gaston kwa upole. “Sina mda wa kuongea na msaliti, nimekuona jana Arusha kwa macho yangu na leo pia”alisema Jesca kwa hasira. “Ndio lakini hujui yule ni nani yangu nahitaji kukuelewesha” alijaribu kujitetea Gaston.

“Usipoteze mda wako huo ndo mwisho wa mapenzi yetu wewe endelea tu na Beatrice wako sihitaji kuwa na wewe tena endelea na ex wakoo maana naona penzi limefufuka upya” ,alisema Jesca na kupanda gari.Wakati huo huo Dulaha naye alikuwa ghoofani hapo stend akiwaangalia watu hao waliokuwa chini.Ingawa alikuwa juu lakini aliweza kuliona tukio hilo na akajua kabisa kulikuwa na kutokuelewana. Alibahatika kumtambua Jesca na Alice lakini Gaston hakaumfahamu.Jesca alimtambua kwa sababu kipindi kile alipokuwa akimfuta Alice Dodoma huyo ndo alikuwa kampani kubwa ya mpenzi wake Alice.

Ili kujua nini kinaendelea alimwambia rafiki yake Peter aliyekuwa naye amfuatilie Alice na Gaston ajaue wanaenda wapi alafu yeye atamfuatilia Jesca kujua nini kimetokea mbona kama walikuwa hawaelewani.Kwa bahati mbaya Dulaha hakubahatika kumjua Gaston hivyo hakujua nini kilikuwa kinaendeea na alihisi labda ni mpenzi mpya wa Alice.Dulaha akaingia kwenye gari alilopanda Jesca na alimfuta. “Vipi shemu alimgusa begani mara baada ya kumuana Jesca akiwa amejiinamia kwenye siti ya gari.

Jesca alinyanyuka kwa nguvu akizani labda ni Gaston aliamua kumfuata tena huko ndani. Alivuta pumzi ndefu mara baada ya kugundua kuwa sura hiyo haikuwa ya Gaston bali shemeji yake Dulah.Jesca alikuwa akimkubali sana Dulaha na aliaamini kuwa ni miongoni mwa wanaume waliojua kupenda, kujali na kutunza msichana. “Mambo shem alisema Jesca mara baada ya kumwangalia Dulah machoni. “Salama tu shemu za kwako , alafu umekuja hata kunitafuta? Alilalamiaka Dulah. “Yaani wewe acha tu niipanga kukutafuta ila kwa majanga yaliyotokea nimechanganyikiwa mwenzio” alijibu Dulah.

“Yaani hapa na majeraha ya moyo sina hata chembe ya amani moyoni mwangu” alisema Jesca. Kwa bahati mbaya gari lilianza kuondoka hivyo ilimpasa Dulah kushuka ikabidi kondakta wa gari hilo kumuuliza vipi kamanda unaenda Arusha?.Hapana nashuka ila huyu ni abiria wangu msimtoze nauli aliwambia konda kisha na yeye akashuka. Jesca aliendelea kujiuliza maswali mengi sana kuhusu wanaume.

Hivi ni kweli huyu naye ni mkorofi au rafiki yangu Alice ndo mkorofi alijiuliza jesca mara baada ya Dulah kushuka kwenye gari. Jesca roho ilikuwa inamuuma sana kuona anampoteza Gaston mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana. Au sijui nimsamehe tu tuendeeee na mapenz yetu ila no, kuna makosa ya kusamehewa lakini sio usaliti aliendelea kujisemea Jesca. Aliendelea kuwaza kuhus mapenzi huku akilinganisha pia na mapenzi baina ya Alice na Dulaha ambao na wao walifikia mwisho.

Aliendele kumtafakari Gaston na kujikuta akijisema kweli awali ni awali na hakunaawali mbovu. Yaani Gaston na ujanja wale wote amekwama kwa Beatrice mtu aliyemwacha na kumtupa kama kifaranga cha kuku ndipo mimi nikamuokota?Kweli mapenzi yanarani dunia aliendela kujiuliza maswali mengi Jesca yasiyo na majibu.Dulha alishuka kwenye gari alimpigia simu rafiki yake Peter na kumuuliza yupo wapi. Peter yeye baada ya kupewa kazi ya kuwafuta Alice na Gaston aliwashuhudia wakienda stend ya KCMC.Hivyo kwa mantiki hiyo ni kwamba walikuwa wanaenda chuoni na wala Alice hakushitushwa na habari kuwa Dulha alikuwa amelazwa hospitalini.

Walifikiri cha kufanya haraka harakawasijue cha kufanya na kwa sababu Omary hakuwepo waliamua kuingia mahali wakaendelea kupata kinywaji huku wakimsubiri mwenzao Omary maarufu kama mzee wa plan B.Alice alifika chuoni na rafiki yake Stela na Easther walikuwa wakimsubiri tayari kwa ajili ya kwenda kukamilisha lile zoezi la kuchukua vitu kwenye gheto la Dulah. Waliingia kwenye Noah na kulikuwa pia na wanaume wawili ambao walikuwa wakiwamini kwa ajili ya usalama wao. Walifika sehemu ambayo gheto lilkuwepo wakafungua na kuingia ndani.Wakaanza kukomba vitu vyote vilivyokuwa vikibebeka.

Alice alikuwa akijiamini kwa sababu walikuwa na wanaume ambao waliaminika sana kwa mambo ya vurugu pale chuoni kwao.Baada ya kuhakisah kuwa wamebeba vitu vyote vya thamani isipokuwa kitanda na sofa waliingia kwenye Noah na safari ya kurudi chuoni ikaanza. Jirani ambaye alishuhudi vitu vikibebwa aliingia hofu kwa sababu Dulha alishamueleza kuwa walikuwa na ugomvi na Alice. Pia Dulah alishampa kazi mama huyo ambaye mda mwingi alikuwa akishinda nyumbani kuwa atakapo muona tu Alice ampe taarifa.

Hivyo alimpa taarifa na Dulaha na kikosi chake na wao wakawa wanakuja kwa kasi ili kuzuia uharamia huo uliokuwa ukitendwa na mabinti hao pamoja na wanaume wa kukodi. Yaani wanafika tu wanakutana na Noah ikitoka na kuondoka ikabidi wageuke na kuanza kuwafukuzia kwani na wao walikuwa kwenye gari ainaya spacio.

Ile Noah ilienda mpaka stend kisha Alice na mwanaume mmaja wakashuka wakawa wanaelekea kwenye jengo la ghorofa ambalo lipo hapo stendi. Dulah naye akashuka kwa kasi ya ajabu huku mkononi akiwa ameshika chupa kubwa ya konyagi wenyewe wanaita Mzinga bapa tayari kwa kwenda kufanya fujo. Omary ilimbidi apaki gari na kujaribu kumfuata Dulha kwa sababu alijua kabisa kwa jinsi Peter alivyokuwa na umbo dogo ni lazima atashindwa kummudu. Omary alimkimbilia Dulah na kujaribu kumsihi hasifanye tukio lolote baya ambalo litachafua jina lake na jina ya kampuni yao hapo stendi. “Nasema niacheni niipasue sura yake ambayo ndo anaringia alisema Duhal kwa ghadhabu. Peter yeye alimfuatilia Alice ili ajue alikuwa akielekea wapi.

Kumbe Alice alikuwa ameshatafuta mteja wa baadhi ya vitu ama flat screen na sabufa. Baada ya Peter kusikia watu hao wakipatana bei alishuka ngazi tayari kwa ajili ya kwenda kutoa taarifa. “Jamani tusifanye makosa hivi vitu vinataka kuuzwa”alisema Peter.Tufanyaje aliuliza Dulha huku akionesha kuwa ni mtu aliyechanganyikiwa kutokana na tukio hilo. “Sasa sikia hapa tutumie sheri na tuwakamate kama wezi” alipendekeza Omary huku akianza kutembea na kuelekea kituo cha polisi ambacho kipo hatua chache kutoka hapo stendi. Peter wewe baki hapo angalia wasije wakatoroka, lipendekza Dulah.

Wakati wanaelekea kituoni Dulah alimuona polisi anayemfahamu hivyo kamuuelezea suala lake haraka haraka sana. “Sasa siku hizi huwezi kumkamata mtu bila kuchukua RB kwa hiyo nendeni mkachukue Rb kwanza kisha ndo tumkamate alipendekeza afande huyo.Dulaha hakutaka kuongea mengi aliingiza mkono mfukoni akatoa noti ya shiling elfu 10 akamkabidhi kisha akamwambia “ naomba tusaidiane tumkamate kwanza then tutafuata hizo taratibu zingine” alisema Dulah. Yule polisi hakujivunga siunajua tena mambo ya mama bandika ugali mboga nitaleta.

Sasa kama mtu mwenyewe ni wa kike mimi siruhusiwi kumkamata njooni huku tuchukue askari wa kike alipendekeza huyo afande. Fasta fasta askari wa kike alipataikana na Alice alifuatwa na kuwekea chini ya ulizni. “Upo chini ya ulinzi kwa kosa la uwizi alisema askari huyo wa kike. “Naomba utii sheria bila shuruti twende kituoni na utaambiwa umeiba nini na nini alijibbiwa Alice mara baada ya kujitetea kuwa yeye sio mwizi. 

Alice hakuwa na ujanja zaidi ya kukubali kwenda polisi.Yule kaka aliyekuwa na Alice akawafuta wenzake kwenye gari na kuwaeleza kuwa mambo yameshaharibika dili limegeka dirisha. Alice alipelekwa rumande na kinyume na sheria RB ikakatwa baada ya yeye kukamatwa.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)