SEHEMU YA KUMI NA ANE
ILIPOISHIA...
Alice hakuwa na ujanja zaidi ya kukubali kwenda polisi.Yule kaka aliyekuwa na Alice akawafuta wenzake kwenye gari na kuwaeleza kuwa mambo yameshaharibika dili limegeka dirisha. Alice alipelekwa rumande na kinyume na sheria RB ikakatwa baada ya yeye kukamatwa.SASA ENDELEA...
Baadaye wote wawili yaani Dulah na Alice walitakiwa kuandika maelezo. Alice alisisitiza kuwa yeye hajamuibia bali alichukua vitu alivyonunua yeye. Kwa mujibu wa maelezo aliyayaandika Alice, ni kwamba katika chumba hicho kila mtu alikuwa na mchangoo wake.Kwa hiyo yeye alinunua vitu vya ndani na Dulah ndo alilipa kodi.
Maelezo ya Dulaha yalitofautiana maana yeye alisema binti huyo hakuwa na kitu hata kimoja na vyote alivinunua kwa pesa yake.Yaani kwa kifupi wote walikuwa wakiongopa na kudanaganya polisi. Ukweli ni kwamba Alice alikuwa na mchango kidogo katika kodi na vitu vyote alinunua Dulah.Ikabidi polisi waende mpaka gheto kuangalia chumba hicho na vitu vilivyochukuliwa.Wakakuta kweli chumba kimekombwa na cheupe peee kama mtu ndo alikuwa anaanza maisha. Polisi walienndelea kubaki dilema wasijue mkweli ni nani, ikabidii watumie diplomasia.
Waliwasii wapenzi hao wayamalize mambo hayo na warudiane na waendelee na maisha yao kama kawaida.Lakini Alice alikiri na kutamka mbele ya polisi na Dulaha kuwa hayupo tayari kurudiana na mwanaume huyo na wala hampendi hata kidogo.Kauli hiyo ilikuwa ni zaidi ya mkuki moyoni aua mwiba kidoleni kwa Dulah.
Dulah alikuwa yupo tayari wayamalize na waendeeaa na mapenzi yao lakini Alice alitamka kwa kinywa chake kuwa hampendi na anamchukia kuliko maelezo. Ikabidi Alice aendeeelee kukaa rumande na Dulaha alisistiza kuwa Alice afunguliwe kesi ya wizi. Dulaha alikuwa yupo tayari kutumia gaharamm yoyote ilimradi tu amshikishe Alice adabu.
Huko nje ya kituo chao polisi idadi ya wanachuo ilizidi kuongezeka na kila mmja alitaka kuonesha mchango wake wa kumtoa Alice kituoni. Juhudi zao zilikuwa zikigonga mwamba kwa sababu Dulah alikuwa ni mtu maarufu akitumia jina la baba yake na kuna baadhi ya polis alishawapa pesa ilimradi tu binti huyo alale polisi.
Baadaye taarifa zilimfikia Gastonn kuwa shemeji yake yupo kituoni hivyo na yeye akashawishika kwenda ili aone atamsaidiaje. Gaston alivyofika eneo hilo akakuta mambo ni magumu na wanachuo wenzake walishakata tamaa ya kumtoa Alice maana inaonesha dhairi sheria zilikuwa zinapindishwa mara baada ya nguvu ya pesa kutumika.
Gaston akafikiria haraka haraka akaona njia sahihi ni kutafuta msaada wa kisheria kutoka kwa mtu aliye na uelewa mkubwa wa sheria. Wazo lake likadondokea kwa binamu yake ambaye alikuwa ni wakili wa kampuni moja hapo mjni Moshi.Alimpigia na kumuelezea kwa kifupi kilichotokea.Mwanasheria huyo akamwambia hakuna sababu yoyote itakayomnyima Alice dhamana na kumfanya alale rumande zaidi ya kumsumbua tu.
Kosa kama hilo ni dhairi kuwa anatakiwa apewe dhamana na kisha kama kuna ushadi wa kueleweka kesi ipelekwe mahakamani na huyo mwanaume anatakiwa atambue kama aliishi na huyo binti zaidi ya miezi sita kama mke na mume basi hivyo vitu watagawana aljaribu kufafanua mwanasheria huyo mara baada ya kupigiwa simu. Basi Gaston alimuomba mwanasheria huyo aje polisi kuwasaidia kumtoa huyo binti maana wao wamegonga ukuta. Basi wakili huyo akakubali na wakakutana polisi.
Mda ulikuwa umeenda sana na kina Dulah walikuwa wameshaondoka huku wakiwa na imani kuwa binti huyo atalala rumande kutokana na hongo waliyokuwa wametoa. Alice naye alishakata tamaa kwa sababu watu wote walishaondoka akawa amebaki mwenyewe huko ndani ya kituo.
Hakuona msaada wa kina Deo, Easther , Stela na wapambe wengine waliomshauri kufanya upuuzi huo wa kuchukua vitu vyote vya Dulah. Alice hakuamini kuwa kosa hilo ambalo llikuwa halina kichwa wala miguu ni kweli llikuwa likimfanya alale polisi.Roho ilimuuma sana na kuamini kuwa Dulaha alikuwa ni mwanaume mwenye roho mbaya pengine kulo wanaume wote huku duniani.
Mida kama ya saa sita usiku Alice alishangaa kuitwa na polisi kaunta na alishangaa kuona anatolewa sehemu hiyo iliyokuwa na sifa mbaya. Alikabiziwa vitu vyake na kuambiwa kuwa ahakikishe kuwa kesho saa mbili anafika kituoni hapo. Gaston alimtambulisha Alice kwa mwanasheria huyo na baada ya utambulisho walikuwa wapo huru kuondoka zao. Alice hakuaamini kuwa eti Gaston ndo alikuja kumpa msaada mara baada ya rafiki zake wote kushindwa kumsaidia.
Hakujua ni zawadi gani Gaston anastaili kwa mchango wake huo wa kuepusha historia mbaya ambayo ilikuwa itokee historia ya kualala polisi.Kwa sababu wakili huyo alikuw ana gari na yeye alikuwa akikaa Soweto na mda ulikuwa umeenda sana aliamua kuwalipia tax iwapleke huko maeneo ya chuoni na yeye kuwahi nyumbani kwa sababu hata hivyoo kwenye gari alikwa na mkwe amabaye alikataaa kuachwa mwenyewe nyumbani usiku huo.
Kwa hiyo wakaachiana hapo kituo cha polisi. Gaston na Alice wakaingia kwenye gari(tax) tayari kwa kuelekea maeneo ya chuoni. Wakafika kwenye geti la chuo ambapo Alice alitakiwa kushuka kwa sababu alikuwa anakaa hostel za ndani ili amuache Gaston aendelee na safari mpka ghetoni kwake mita chache kutoka hapo getini.
Mlizi wa kwenye geti la chuo alimtaka Alice aoneshe kitambulisho kuthibitisha kuwa yeye ni mwanachuo. Kwa bahati mbaya Alice siku hiyo hakutembea na kitambulisho.Mlizi akaweka ngumu kuwa hawezi kuingia bila kitambulisho.
Alice akabidi amuulize Gaston kuwa wafanyaje? Gaston akajibu hakuna jinsi ingine usiku huyo waende tu gheto kwake yeye atalala hata kwa jirani. Mmmmh haugopi? aliuliza Alice.Niogpe nini sasa kwani wewe ni si ni shemeji yangu aliibu Gaton.Shemeji yako kwa nani sasa wakati rafiki yangu Jesca ushamzingua aliseme Alice huku akipanda gari. “Yaani huwezi amini kilichotokea sio hata usaliti bali tu rafiki yako sio muelewa ila nitakueleza kila kitu hope utaelewa alijaribu kujitetea Gaston.
Walifika gheto kwa Dulah wakaingia ndani na Gaston alitoka ili aweze kwenda kumgongea rafiki yake ili aone kama wanaweza kulala wote usiku huo.Jirani yake huyo ambaye pia ni mwanachuo alifungua na kuuliza kulioni usiku huo. “Daaah kuna majanga yametokea vipi naweza kulala hapo kwako nina mgeni alafu wa kike nataka nimpishe”. Jamaa akacheka kidogo na kusema sasa kama ni wa kike si alale naye tu au ni nani yake?.Gaston akajibu kuwa alikuwa ni shemji yake.
Jirani yake huyo akaendelea kucheka na kumwambia leo nina kicheche au mchepuko kwa jina rahisi hivyo haitowezekana kukupa hifadhi. “Wewe lala naye tu jiarani tena ikiwezekana kula mzigo kabisa shemeji kitu gani kwani alifikaje machinjioni usiku huu” alishauri jirani huyo wa Gaston amabaye pia alisifika kwa sifa mbaya wa kuwa na mademu wengi.Yaani alikuwa akibadilisha mademu kama nguo.
Wakati Gaston anatoka na kuenda kuomba sehemu ya kulala,
Alice alijisogeza mlangoni na alikuwa akifuatilia maongezi yao.Alirudi kwa kunyata na kukaa kwenye sofa mara baada ya kuona Gaston anarudi. “Sasa shemu leo tutashea umasiki wewe utalala kitandani , mimi nitalala kwenye sofa ila usiwe na wasiwasi kuwa huru alisema Gaston mara baada ya kuingia ndani.Alice alitabasamu akasema usiwe na hofu mimi nitalala kwenye sofa na wewe ulale kitandani..
“Hapana shemu naomba ulale kitandani najua leo umechoka sana kimwili na kiakili”. Basi tutalala wote ila mzungu wa nne alipendekeza Alice. Vipi nikuekee maji ya moto au utaoga ya baridi Gaston alimuuliza Alice mara baada ya kuhisi kuwa atakuwa na uchovu.
Naomba nipashie tu shemu wangu alijibu Alice. Gaston akaweka maji kwenye jiko la gasi huku akimlalamikia mzee mwenye nyumba kuwa amempa taarifa kuwa heater ya bafuni kwake imeharibika na hajatuma fundi mpaka wakati huo.Gaston baada ya kubandika maji alifungulia radio yake na kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana aliweka ile miziki laini ya kuchombeza na kubembeleza.
Maji yalichemka kisha Alice aliingia bafuni na kuoga. Wakati Alice ameingia bafuni kuoga Gaston alianza kuwaza ujinga. “Hivi patakucha kweli au ndio kama siku ile mambo ya Mwajabu. Alafu mimi ninakuwaga na bahati ya mtende yaaini mipira ya kona nishindwe tu kumalizia alijisemea Gaston huku akoiongeza maji jikoni ili na yeye akaoge pindi tu Alice atakapotoka bafuni.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA