SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Akaeleza kwa kuwa yeye mara nyingi anakuwa shift ya usiku basi mimi nitakuwa nalala ila wiki ambayo hatoingia usiku basi tutafanya utaraibu mwingine. Hiyo sehemu anayolinda ni hizi sehemu ambazo zinajihusisha kutoa mikopo.Hivyo kwa mantiki hiyo walikwa na shift yaani wiki hii anaingia usiku inayofuata anaingia mchana.
Sikuweza kupinga wazo lake nilimshukuru kwa wema wake huo na kumwambia kama anaeza anitafutie kazi yeyote hata ya kuuza bar.Alinangalia kisha akacheka na kuniuliza eti mtoto mzuri kama mimi nataka kuuza bar sinitagombaniwa kama mpira wa kona.
Nilimwambia hasijali sana kuhusu mimi na kamwe sitoweza kukaa kusubiri eti yeye aniletee chakula. Wakati tunaendelea kunywa chai huku macho yangu yakiganda kwenye hile picha na kutamani kuuliza kuhusu hiyo picha kuna sauti ya kike ilisikika ikigonga huko nje.
Karibu mama alijibu huku akinyanyuka hapo alipokaa na kutaka kwenda kumsikiliza. Kabla hata hajafika mlangoni mama huyo alishaingia ndani. “Hivi wewe Chacha unajifanya mkorofi sana si tulishakubaliana nyumba yangu kamwe haingii mwanamke?.” “Hii ni kwa ajili ya mabachela tu sasa kwa nini unanifanyia utemi?”.
Alifoka mama huyo na hapo sikuhitaji kuuliza kuwa mama huyo ni nani.Moja kwa moja niligundua kuwa alikuwa ni mama mwenye nyumba. Nilijikuta nikiwa mpole ghafla na kujuta tena kuja hapo. Nilimwangalia mwanamke mwenyewe nilitamani kucheka maana kwanza alikuwa ni kimbaumbau amenyooka kama msumali hata hakufanania kuwa mama mwenye nyumba.
Pili rangi yake ya usoni haikufanana na rangi yake ya mikononi na miguuni.Ni wazi kuwa alijichubua kupita kiasi hivyo madhara ya mkorogo yalionekana dhairi bila kificho. “Hapana mama lazima uniulize tena kistarabu kwa nini nimefanya hivyo sio kukurupuka na kufoka mbele ya mgeni. Huyu binti ana matatizo sana hivyo niliamua kumsaidia na nilimleta huku ili nimkutanishe na wewe ili kama ataweza basi umpe kazi ya kufanya”.
“Hayo ndo maneno sasa sio eti uniambie kuwa nimekurupuka hii ni nyumba yangu na nipo kibiashara. Basi akiwa tayari utamleta ili aje tumpe majukumu ya kazi itakayompa pesa”. Alisema mama huyo huku akiniangalia.Binti usiwe na hofu hapa ndo umefika kwa mama la mama kumbwa la maadui, kimbilio la mabinti waliokata tamaa na maisha”.
Ilibidi nitabasamu maana hizo tambo zilikuwa ni kiboko.Hiyo inaitwa gusa unatae, ikisimama panda, ikiwaka mulika na ikizimika papasa. “Alafu binti unalipa sana naamini kwa umbo lako lilojazia na kujichora kama soda ya Bambucha lazima tu utapata pesa ni aibu kwa wewe kufa na njaa”.
Kweli nimepatikana niliwaza mara baada ya mama huyo kunipa sifa na kutoweka chumbani hapo.Sasa nikawa najua kabisa kuwa safari ya maisha niliyoamua ni ngumu sana. “Dada samahani ndio nyumba zetu za kupanga zilivyo hivo kuwa na amani”. “Huyo ndio mama mwenye nyumba?”, niliuliza ili kupata tu uhakika.
Ndio huyo ndo mama mwenye nyumba alijibu kwa unyonge baba huyu. “Sasa ni kazi gani ambayo yeye anauhusika nazo?”. “Kazi anazohusika nazo kwa kweli si nzuri sana”. “Wewe nambaie tu usiwe na wasiwasi”. “ Huyu mama ujue hataki wanawake kwenye nyumba hii kwa sababu tayari yeye anacho chumba kwa ajili ya wasichana tu.
Huyu mama anafanya biashara haramu ya ngono. Yaani hataki wasichana wapange hapa kwa sababu kufanya hivyo ni kuharibu biashara yake na kupugngza wateja”. “Kwa hiyo nyie ndo wateja wake nilimuuliza”. “Ndio dada sisi ni wateja wake na kuachilia sisi pia kuna wanaume wengi ambao wanakuja hapa kupata huduma”.
Pia ana bar hivyo watu wakishalewa inakuwa rahisi sana kuwaleta huku ili kufanya bishara hiyo”. “Kwa nini uliamua kukaa hapa na si nyumba ingine”. Maisha, maisha pamoja na umri wangu huu mkumbwa lakini maisha yananifanya niishi bila matuamaini. Pamoja na mambo mengine huyu dada ameshanisaidia sana na ndio ameniwezesha mimi kupata kazi pale ninapolinda”.
“Ulivyonambia unashida niliumia sana kwa sababu najua jinsi maisha yanavyobadilika”.Zamani mimi sikuwa hivi mimi nilikuwa somebody katika nchi. Mimi nilishawahi kuwa polisi nikaja nikafukuzwa paia nilishawahi kufanya bishara nyingi nikafanikiwa sana nan do nilipojuana na huyu dada.
Lakini baadaye ndo kama hivi nilifilisika na kurudia ufukara.Huyu dada kwa sababu alikuwa ni rafiki wa karibu sana na msichana niliyewahi kumpenda sana basi aliamua kunisaidia. Aliongea baba huyu wa makamo nikajikuta namuonea huruma sana. “Kwa hiyo huyu mwanamke mna uhusiano?”,niliuliza swali hilo.
“Ndio huyu mwanamke tuna uhusiano naye na nimezaa naye mtoto wa kiume mkumbwa tu nadhani atakuwa size ya rika lako au kukuzidi kidogo.Sasa hivi yopu huko Dar es Salaam anafanya biashara zake.Naye ni shida alikaa taa shule yopo tu ni mfanyabiashara sasa hivi”.
Mzee huyu akawa amenipa mwanga kidogo wa kujua kuwa maisha yanachoma kama pasi.Sasa swali ambalo nilijiuliza mwenyewe ni kuhusu kuwa nitaweza kufanya kazi ya kujiuza.Ikabidi nimuulze huyu mzee kuwa hamna kazi ingine tofauti ya hiyo ya kujiuza.Lilikuwa ni swali la msingi na sio la nyongeza.
“Hilo siwezi kukujibu kwa haraka sana lakini cha msingi utaongea na huyo mama na pia husimfiche kuwa wewe ni mjamzito.Anaweza kukusaidia kwa sababu ana umaarufu fulani katika mji huu. “Hata mimi sipendi uingie kwenye biashara ya kuuza mwili ila mimi nimgeni kwenye mji huu nilikuja kama wewe ulivyokuja hata huyu mwanamke sikujua kama nitamkuta huku.
Yaani sipendi kabisa ufanye hizi kazi lakini msikilize na mimi nitajaribu kuongea naye ili aweze kukusaidia. “Sawa asante pia kwa msaada wako inaonekana una roho nzuri sana ingawa pia hali yako ya kimaisha sio nzuri”. Ilibidi nimpongeze kwa sababu watu kama hawa ambao hawana uwezo lakini wapo tayari kusaidia ni wachache sana.
Kimya kidogo kilitawala sana kabla ya mimi kumuulza kuhusu ile picha kumbwa ambayo ilikuwa ukutani na yenye maneno “Bambucha the girl of my dream”. Alitabasamu na kuniambia kuwa yeye pamoja na mambo yote lakini ni mzima sana katika kuchora. Huyo aliyemchora hapo ni mwanamke ambaye alimpenda sana na waliachana kwa mipango ya shetani na kila siku anatamani kama angeweza kuonana naye. Duuh kweli mapenzi kiboko.
Nilipoajaribu kuhoji sana kuhusu hiyo picha maana ilinivutia na ilikuwa ikifanana na umbo langu.Alinikatisha kwa kuniambia kuwa niende kuongea na huyo mama ngoja yeye alale kidogo hiyo story atanambia siku ingine akiwa kwenye mood nzuri.Hapa napo nikapata swali lingine kama hawa watu ni wa penzi mbona kila mtu analala chumba chake.
Nikaona nitajipasua kichwa bure ngoja niende kwa huyo mama.Nikatoka na akanambia iende kugonga chumba cha pili.Nilienda kugonga maana mlango ulikuwa umefungwa. Mlango haukufunguliwa lakini kuna sauti nilizisikia ambazo sikuzielewa.Ni kama watu walikuwa wakifanya mapenzi ndani ya chumba hicho.
Ilibidi niwe mpole na kusogea kwa pembeni na kuanza kuangalia mazingira ya nyumba hiyo.Hapo macho yakaangukia kwenye kamba ambayo ilikuwa imejaa vifuniko vya asali. Swali lingine likaja kwenye ubongo wangu nimeembiwa nyumba hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu sasa hizo nguo za ndani za wanawake zilizojaa kamba zimetoka wapi.
Mara “dada habari yako, nimemkuta mama la mama”.Lilikuwa ni swali kutoka kwa mwanaume ambaye aliingia kwenye uwa wa nyumba hiyo. Kabla sijajibu “Jamani dada wewe mgeni eeeeh, naona hayo mabambucha si ya mji huu”. “Kweli na bahati yaani leo nitakuwa wa kwanza kukukaribisha”, aliendelea kuchombeza kaka huyo huku amenitumbulia macho unadhani labda mwewe kaona kifaranga cha kuku.
“Wewe kijana wewe acha fujo huyu ni mwanangu ebu tulia kwanza”, ilikuwa ni sauti ya mama yule mwenye nyumba.Kumbe alikuwa ametoka maana zile sauti za kwenye kile chumba zilishanishtua na kuhisi labda ni yeye ambaye alikuwa anakamuliwa. “Kwa hiyo mama naniii huyu mwanao nikilipa ghali hunipi?”.
Yule kijanja aliendelea kuwa king’ang’anizi kuonesha kuwa alidata na umbo langu.Yaani niliatamani hata kuondoka niende huko nje kutafuta kazi ingine.Lakini nilisita kidogo nikaona sio mbaya kama nitamsikiliza mama huyo. “Huyu mwanangu haiwezekani labda nikupe mwingine ailyekuja juzi huyo bado kabisa yupo vizuri” alisema mama huyo.
“Sawa sawa natanglia kule V.I.P mwambei aje huko”, alisema kijana huyo na kwenda kwenye chumba ambacho kilikuwa kimejitenga pembeni. “Usishangae ana mtoto mzuri nisiburi hapo hapo nichukue kwanza pesa yangu.Mama aliongea huku akielekea kwenye chumba hicho.
Baada ya dakika mbili alitoka na kwenda chumba kingine ambapo kwa pamoja alitoka msichana mwingine mdogo mdogo na mshamba mshamba akampeleka kwenye kile chumba kinachodaiwa ni V.I.P.Baada ya hapo alinambia animfuate.Jamani mama alikuwa anapaiga hatua za haraka haraka kama mwanaume vile.Yaani mimi na kitumbo changu mbona nilikoma. Hatua kwa hatua nashangaa kuona hata hatufiki huko tulipokuwa tunaenda.
Tuliiingia kwenye bar moja na tuilpokaa tu muhuumu alikuja. “Mimi nipe kile kinywaji changu msikilize na mwanangu”. “Mimi nipe soda Fanta”, nilijibu na kumfanya muhudumu atabasamu. Sijui alitarajia niagize bia maana kinywaji cha huyo mama kilichokuja ni bia tena zile zenye kilevi kikumbwa.“Karibu sana mimi naitwa mama la mama, unaweza kujitambulisha na ukanambia kwa kifupi kuhusu wewe”.
Sikutaka kuzunguka mibuyu nilienda moja kwa moja kwenye pointi zangu za msingi ili niweze kusaidiwa.Nilimweleza kuwa mimi ni yatima na pia nilimweleza kwa kifupi majanga yaliyonikuta.Alikuwa makini sana kuniuliza lakini niligundua kuwa mama huyu alitokea kunipenda na kunikubali maana hata zile nyodo zake ziliisha na akaonesha hali ya kuhuzunika kila neno nilolokuwa nikiliongea.
Siku hiyo nilikuwa nikiongea kwa hisia sana. Baada ya mimi kumwaga sera zangu zikionesha kuwa kuna kila sababu na mimi kupewa msaaada mama huyo akaanza na yeye kuongea. “Mwanangu usikonde moyo kwani maisha ni safari, tena safari yenye milima na mabonde.Kuna kupanda na kushuka, kuchanua na kunyauka.Yaani nimekufananisha sana na rafiki yangu ambaye naye tuliishi vizuri sana ila tulikuja kupotezana kisa tu mwanaume”.
“Mwanaume aliwafanyaje?, Nilimuuliza. “Wacha tu mwanangu mwanaume huyo alikuwa akituchanga hivyo kwa kuwa alikuwa na pesa tukajikuta tunagombana na kila mmoja akafauata maisha yake.Sasa mwanangu mimi nipo tayari kukusaidia ingawa kazi zangu zote ni kinyume na sheria na ni hatari kwa haki za binamu na kiafya pia.
“Kazi gani hizo mama?”, ilibidi nimuulizze ingawa tayari nilishapata picha ya vitu anavyofanya. “Kazi ya kwanza mimi namiliki wasicha wengi ambao huwa nawahifadhi na kuwafanyisha biashara ya ngono. Mwisho wa mwezi nawalipa mshaara.Naendesha biashara hiyo kwa siri sana na pia nimeunda urafki na watu wanahusika kusimamia sheria.Biashara hii inanilipa sana na imenifanya nijuane na watu wengi.
Lakini pia nafanya kazi ya kuuza pombe haramu na pia nauza bangi na madawa mengine ya kulevya ambavyo nayapata kutoka huko mijini kwa watu wazito. Kwa hiyo nafikiria kukutafutia kazi kupitia watu lakini mwanangu kazi ni ngumu itachukua mda.Hapo ikabidi nimkumbushe kuwa mimi ni mjamzito hivyo naoagopa kufanya kazi za ngono.
Akacheka kidogo na kuniambia kwa kuwa ujauzito sio ugonjwa hivyo naweza kufanya mpaka miezi ya kukaribia kujifungua. Wakati tukiendelea na mazungumzo hayo kuna baba mmoja aliingia na moja kwa moja alikuja kutusalimia.Ilionekana walikuwa wakifahamiana.
Huyo baba akakanza kumwambia kuwa amtafute mtu kwa sababu kuna msichana ameondoka jana. “Hawa wasichana wamekuwa wasumbufu sana yaani wanakuja hapa washambashamba sasa wakishakutana na wanaume wanatoroshwa”. Mama akasema ni kawaida hata pale kwake kuna watu wa namna hiyo wakishapata pesa kidgo wanasepa. “Kwa hiyo unataka binti?”, mama huy aliuliza tena.
“Ndio nataka kwa haraka ila awe mwaminifu sana”. “Sawa binti ushapata tena nitakupa mwanangu kabisa huyu hapa ila sitaki mumuuze kwa wanaume”. “Huyu ni mwanao?”, aliuliza mzee huyo. “Ndio huyu ni mwanangu mtoto wa kaka yangu mimi ni shangazzi yake hivyo ataanza kesho wakati anasubiria mambo mengine yakae sawa.
“Acha utani bwana mtoto mzuri kama huyu hawezi kuuza bar”. “Sio utani huyu kwanza ni mzoefu sana baba yake ana bar kumbwa huko mjni hivo itabidi umpe kaunta kabisa sitaki ashikwe shikwe matako hapa. Kaunta nitampa lakini ili wenzake wasijisikie vibaya ni lazima aanze huku pembeni na akijituma vizuri ndo nampandisha cheo”.
“Wewe haupo seriazi yaaani mwanangu jinsi alivyokuwa mzuri na mabambucha yake yalivyojazia hivyo uumpe kazi hiyo. Mabishano yao alinifarji sana na kuona sasa naweza kupata kazi ambayo kidogo itakuwa na nafuu kuliko zile za yule mama”. Basi mama akamwambia ngoja aongee na mimi aone kama nipo tayari kufanya kazi hiyo.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
