
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Ingawa ilikuwa inanibana kidogo lakini iliweza kunisitiri mwili wangu.Akatoa tena na pesa zake kidogo za akiba na kunipa. Akanambia hiyo hali ambayo inanipitia hata yeye ilishawahi kumtokea kipindi hiko yupo Dar es salaam.Nilimwabia asante na akiulizwa nimeenda wapi awajibu hajui.
Dada huyo alinionea huruma sana akaendelea kuniuliza kuwa kwa hiyo naenda wapi.Bado sikuweza kumjibu kitu zaidi nilimwambai asante kwa msaada wake.Nilitoka nje na kiwizi wizi nikaanza safari ya kuelekea stend.Wazo ambalo lilinijia ni kwenda sehemu inayoitwa Ifakara.
Yule dada alikuwa amenipa kama elfu 20 hivyo niliona itaweza kunitosha kwa nauli.Nilivyofika stend nilikuta kuna fuso ndo inaondoka.Sikutaka kupoteza mda niliingia kwenye gar hiyo na safari ya kuelekea huko Ifakara ikaanza.
Usishangae ndugu msomaji kusikia upanda fuso badal aya basi.
Huko kipindi hicho usafitri ndo huo yaani hakan cha basi wala nini. Lilikuwepo moja tu liloitwa Moro best na lenyewe lilikuwa lifanya safari zake kwa machale sana. Niifika Ifakara salama na niliposhuka sasa nikatafuta mahali nikagiza chakula huku nikiendelea kutafakari kuwa nitaenda wapi sasa.
Nilifikiri sana kuhusu sehemu hiyo bado nikaona bado si salama sana kwa sababu nisehemu ambayo naweza kukutana nawatu ambao wanaweza kunijua. Nikapata wazo lingine kuwa niende sehemu ambayo sifahamiki kabisa na kutafuta mbinu yoyote ya kaunza maisha.
Wazo lilonijia kwa haraka ni kwenda Morogoro Mjini lakini sasa sikuwa na nauli ya kutosha kunifikisha hapo.Nikafikiria haraka haraka nikaona bora nipande gari na kwenda mpaka mikumi.Niliamini kuwa hapo naweza kukaa kwa mda na kufanya kazi yoyote.
Kipindi hicho nilikuwa namvuto sana na nimenona vya kutosha hivyo ukiniangalia kwa harakaharaka huezi kujua kuwa nilikuwa na mimba. Nilishuka mida ya jioni hivyo kwa kuwa nilikua mgeni nilianza kuzunguka huku na kule ili kuangalia ni kazi gani naweza kufanya ili kukabiliana na maisha hayo mapya.
Wazo nililolipata ni kuanza kupita kwenye sehemu za kuuzia chakula lengo ni kuomba kazi. Kila mahali inilipoingia nilikaribishwa vizuri wakajua kama ni mteja.Lakini nilipotaka kuongea na boss watu walishtuka na kuwa na mashaka na mimi.Na nilipoongea na boss naye hakuamimni kuwa msichana mzuri kama mimi eti nilikuwa natafua kazi yeyote ya kufanya.
Tatizo kumbwa ni kwamba ile nguo aliyonipa yule binti ilikuwa ni nzur na pia ilikuwa ikinibana sana na kuonesha mautamu yangu. Hivyo watu walihisi labda mimi ni tapeli.Nilizunguka sehemu kama tutu lakini zote walinikatalia. Sasa nilikuwa nadanganya na kusema kuwa mimi nilitokea Iringa kuna mtu alikuwa amenichukua na kuniambia kuwaa ananipeleka Morogoro mjini kufanya kazi lakini cha ajabu nilipofika hapo amenitelekeza.
Uwongo huo nao haukufua dafu maana watu wenye upeo mkumbwa wa kufikiri walisema kuwa niende polisi. Kusikia polisi hapo ndo sikutaka kabisa maana wangeweza kuujua ukweli na kunirudisha mahenge.Usiku uliingia na nilikuwa sina pa kwenda zaidi ya kushangashangaa mji mdogo wa mkumi. Usiku ulivyozidi kuwa mkumbwa kwanza nilikuwa nimechoka kuzunguka hivyo nilirudi pale pale stendi na kukaa.
Nilikaa hapo kama vil kuna mtu nilikuwa namsubiri.Nikawa nashanga tu magari ambayo yalikuwa yakitoka Iringa na kutamani hata kupanda limoja niende tu huko watu walipokuwa wakielekea.Hatimaye ilfika mida ya saa 4 na sasa sikuwa na uhakika wa kulala.Ile pesa niliyopewa ilibaki kidogo sana na nilichoamua ni kuimaliza kabisa kwa kwenda mahali kula kabisa chipsi kavu.
Nilipanga kuwa nitalala maeneo hayo hayo ya stend na itakapofika asubuhi basi nitaanza kuzungka kwenye bar zote kuomba hata kazi ya kuhudumia.Kamji kalikuwa hakajapooza sana maana kulikuwa na harakati za hapa na pale. Mda ulivyozidi kweda ndivyo hivyo watu walivyozidi kupungua na kimya kutawala.
Mmbu wasumbufu wakawa wananisumbua pale lakini niliamua kukomaa.Baadaye kabisa nilibaki mwenyewe na palikuwa pametulia sana.Kuna mlinzi ambaye alikuwa akilinda maduka upande wa pili aligundu uwepo wangu hapo hivyo aliamua kunifuaa na kuniuliza mbona nipo hapo usiku huo.
Niliamua kutumia mbinu za kike kidogo kumwelezea ili anieleze. Nilianza kueleza vitu ambavyo vingemfanya mwanaume yeyote anisikilize.Kwanza nilimwambia hasinione hivyo kwa nje ila moyoni nimebebe mzigo mzito ambao sijui pa kuutua.Nilimwambia umri wangu mdogo unashindwa kuhimili matatizo na mitihani ambayo mwenyezi Mungu ananipatia.
“Matatizo gani hayo mtoto mzuri ebu eleza mimi huenda nitakusaidia”,Mlinzi aliuliza kwa staili ya kuchombeza. “Matatizo makumbwa ambayo ni vigumu kuamini kama kwa jinsi nilivyo hivi dunia inanielemea.Moyo wangu umebeba kinyongo ambacho kinaweza nipa hata mauti kama tu sitopata wa kunisaidai.
Ndoto zangu nzuri za maisha zinakatshwa na mtu ambaye sikumtegemea”.Hapo sasa nikaanza kutumia mbinu za kike maana niliona mlinzi huyu ndiye pekee ambaye anaweza kunisaidia. Nilianza kumwaga chozi utazani nimepatwa na msiba mzito.Chozi likayafunika mashavu ya uso wangu huku kwikwi nazo zikianza kunitoka.
“Jamani mtoto mzuri usilie niambe ni nini kinakusibu naweza kukusaidaia”,Mlinzi aliongea kwa upole na sauti ya kubembeleza. “Kaka yangu kwa sasa ndo kwanza na umri wa mika 17 tu licha ya umbo kumbwa nililokuwa nalo.Umri huu mdogo tayari nina kiumbe nilichokibeba kwenye tumbo langu.
Hapa nilipo siijui kesho yangu ila naiona leo lenye huzuni na majonzi, kuacha jana iliyopita kwa kudra za mwenyezi Mungu. Mimi ni Yatima ambaye kwa sasa sistahili kudeka japo nashindwa kuyazuia machozi ya huzuni kunitoka.Simjui baba yangu, sijawahi kumwona na hata sitarajii kumwona,Mama yangu ambaye ndo alikuwa ngao yangu furaha na tulizo la nafsi yangu naye alifariki dunia.
Ameniacha mpweke kama kifaranga aliekosa mama.Nilihitaji sana malezi yake lakini ndo hivyo Mungu kamchukua.
Nilikia sio kwamba najiliza bali ni machungu yanayouchoma moyo wangu”. Baba huyu alikuwa kimywa sana huku akaitega sikio lake kwa huzuni kaujaribu kushiriki hisia nzito hasi nilizokuwa nikizihisi.
“Baada ya mama yangu kufariki nilichukuliwa na baba mmoja ambaye alijitolea kunilea.Baba huyu ambaye mwanzoni alionekana ni malaika aliyetumwa na Mungu kunisaidia ndiyo huyo kwa sasa amegeuka shetani na kuniangamiza. “Sijakuelewa hapo mdogo wangu naomba ufafafunue vizuri alidakia mlinzi huku akainisogelea karibu na kujaribu kufuta machozi yangu.
Ndio amekuwa wakala wa shetani kama so shetani kabisa. Baba huy amabye ndo amekuwa akinisomesha ndiyo huy ambaye amenibaka na kunisababishia ujauzito huu. Amekubaka? Lilikuwa ni swali la mshangao kutoka kwa mlinzi huyo.
Kimyoymoyo nilikuwa najisemeha tulai maana mchezo huo hautaji papara..Utulivu wake ndio nilihitaji kwa sasa ili aweze kunielewa na ikibidi kunisaidia. “Baada ya kukubaka mbona hukuenda polisi”. “Huyu ni kama baba yangu tena kwa umri wake napaswa kumwita babu.
Haya yalikuwa ni kama mambo ya kifamilia ambayo isingekuwa busara yangeweza kuharibu familia. Alinisihi kupotezea na akanisihi kutunza siri na akaniahidi kutoa mimba hiyo.Kwa kudra za Mungu zoezi hilo likashindikana na akakubali kuilea na tulimpakazia mwanaume mwingine ili mke wake hasijue”.
“Mbaya zaidi siku moja mkewe akiwa ametoka alainifuata tena chumbani kwangu nakutaka tufanaye tena ule mchezo mbaya.Nilishindwa kumkatalia kwa kigezo kuwa nikifanya hivyo huenda akanifukuza hapo nyumbanii.Siku hii sasa ndo ilikuwa ni siku ya 40 ya mzee huyo.
Sio arobaini ya mazishi bali ni arobaini ya kukamatwa ugoni.Hii sasa ndo siku mbaya kutokea kwenye maisha yangu kwa sababu licha ya kufumaniwa pia mkewe alidondoka na kuzimia.Mimi kwa kuwa nilijua mama huyo alikuwa na presha nikajua anaweza kufariki na kwa jinsi nilivyokuwa nampenda sikutaka hilo litokee mbele yangu.
Usiku huo huo niliondoka na kwenda kulala kwa majirani.Asubuhi palipokucha lawama zilikuwa nyingi kuwa mimi ni ni sawa na muaji kwa maana nataka kukatisha uhai wa mama huyo.Maneno hayo yalinichoma sana na kunikuta nikifanya maamuzi yaliyonifikisha huku.
Niliamua kutoroka kaka yangu na hapa sijui hata naenda wapi. Sitamani tena kuishi natamani hata kuyakatisha misha yangu lakini hiki kiumbe kilichotumboni mwangu ndicho nakiogopa. Naapa kuwa nitakuwa nimetenda dhambi mara mbili.Kufikia hapo nilikuwa nimechoka machozi yametoka mpaka yanataka kunikauka.
Sikuweza kuendelea kwa kweli nilibaki nikigugumia kwa kwikwi na huzuni ya hayo mazito ya moyo niliyoweza kuyatoa. Mlinzi huyu kwa kweli alikuwa ni mwema sana maana hakuonesha kuwa haamini kile nilichokuwa nakisema zaidi alianza kunifariji na kuniuliza maswali ya kiupelelezi.
Kwa hiyo kwa sasa unahitaji msaada wa namna gani ndilo swali la msingi aliniuliza.Nahitaji hifadhi kwa mda na pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ili tu niweze kuishi mimi na hiki kiumbe kiliyopo tmboni.Marehemu mama yangu alinisimulia kuwa aliwahi kupita mswahibuu kama haya hasa alipokuwa na ujauzito wangu lakini hakuitoa mimba hiyo.
Alinionya sana juu ya kutoa mimba hivyo hata mimi kwa kweli sifikiriii kutoa mimba kwa sasa. Ni kweli kutoa mimba ni dhambi kumbwa sana dhambi ya uaji na pia ni kinyume na maadili ya mwenyezi Mungu.Si hivyo tu pia ni kinyume na sheria za nchi.Kwa hiyo mdogo wangu nakupongeza kwa hatua hiyo nzuri ya uvumilivu.
Amini avumiliaye mpaka mwisho atavikwa taji la ushindi.Na pia usisahau apandaye kuwa huzuni atavuni kwa kelele za furaha. Uhai ni zaidi ya maisha, mapito ya maisha yasikusababishie ujifikirie kujiua. Labda nikuambie hayo unayoyapitia ni madogo sana wapo wenzio wanaopitia makubwa zaidi ya hayo.
Maneno haya yalikuwa ya faraja sana kwangu lakini bado nilisubiri tamko la mlinzi huyo kama yupo tayari kunisaidia. Mdogo wangu kuna wakati unawezafikiri dunia inakutenga lakini la dunia sio mbaya bali wakaawo ndio wabaya. Mimi nitakusaidia ingawa na mimi maisha yangu ni ya kuungaunga.
Hapo nilinyanyua masikio juu kama punda baada ya kusikia maneno ya faraja ambayo yaliambatana na ahadi ya msaada.Nimekusikiliza kwa ingawa huku mjini matapeli ni wengi sana lakini kama umenidangaya juu kamwe hutofanikiwa kwenye maisha yako.
Sijakudanganya kaka yangu naomba uniamini na unisaidie nilimwambia huku nikimkazia macho.Sawa nitakusaidia ila kwa leo utanibidi uvumilie usiku huu tutakuwa wote lindoni maana siwezi kukupeleka nyumbani nikakuacha hapa. Haina shida kaka yangu huku kimoyomoy nikimshukuru Mungu kwa kumtuma maaiaka huyu.
Kibaridi kilikuwa kikali na kwa mara ya kwanza nikajikuta nikinywa kahawa na mlinzi huyo.Alikuwa na birika lake ambalo ni maalumu kwa ajili ya kumpa sapoti ya kazi hiyo. Story za hapa na pale zikagona na nilishukuru usiku huo ulikuwa mfupi maana mlinzi alikuwa ni mcheshi sana.
Asubuhi ikafika na mlinzi mwingne akaja wakabidhiana na sasa tuliondoka na kwenda kwa huyo mlinzi.Mlinzi aliyekuja naye alikuwa na maneno maneno maana alimsifia sana kuwa eti ameng’oa kifaa.Mimi niliwasikiliza tu huku huyo aliyenipa msaada akisisitiza kuwa mimi ni dada yake.
Tuliondoka kwenda huko nyubani kwa mlinzi huyo.Haikuwa mbali sana hivyo tulitembea kwa mguu.Ilikuwa ni nyumba ya kupanga yenye wapangaji wa wstani na yeye alikuwa na chumba kimoja tu.Kweli nikakumbuka kauli yake kuwa atanisaidia japo na yeye maisha yake yanahitaji msaada.
Chumba chake kilikuwa kidogo alafu ni kimoja tu.Ndani ya chumba hicho kulikuwa na kitanda kama vile vya wanafunzi kameza cha kulia na vyombo kidogo vilivyoweka ndoo ya maji. Hapa nadhani unapata picha jinsi palivyokuwa kwenye nyumab hii.Sikujua kama kipato chake ndo kinasababisha hayo au kuna jambo lingine nyuma ya pazia.
Vitu vyote hazikunivutia isipokuwa kitu kimoja yaani picha ya mwanamke mrembo mwenye wowoo kumbwa kama mimi.
Yaani umbo la msichana huyo lilikuwa linafafanana kabisa na umbo langu. Juu ya picha hiyo kulikuwa na maneno ya kiingereza yaliyoandikwa kwa mchannganyo wa rangi “ BAMBUCHA, The girl of My dream” yaani msichana wa ndoto zangu.
Nilijiuliza maswali kadhaa juu ya ile picha lakini sikupata jibu kamili. Wakati huo nimekaa kwenye kistuli ambayo kilikuwa kinachezacheza kwa sababu ya uchakavu wake na uzito wangu pia ulichangia. Mlinzi huyo ambaye hata jina nilikuwa sijamjua alikuwa ametoka nje na kuniacha mimi nikitafakari juu ya nini itakuwa hatima ya msaada huo.
Alirudi huku akiwa amebeba vitu vilivyofungwa vizuri kwenye gazeti. Akawasha jiko lake la mchina na kubandika sufuria.Alipoweka majani ya chai ndo nikagundua kuwa alikuwa akipika chai.Kidogo nimkataze hasiweke majani maana kwa yule mzee aliyeniaharibia maisha huwa hatuweki tunaweka vungo vingine kwa madai kuwa majani ya chai yana madhara.
Nilizoeshwa hivyo na nina mda sana sijanywa chai yenye majani.Sijui ukweli wa jambo hilo mtawauliza madaktari jamani. Chai ikaiva na sasa ikawekwa mezani kwa jinsi nilivyokuwa na njaa na mwili ulivokakamaa kwa baridi ya usiku mzima sikutaka kujivunga. Lile gazeti likafunguliwa na nikakaribishwa na vitumbua vilivyonona vizuri.Tulikunywa chai huku akinikaribisha na kuniambia hapo ndo nyumbani.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA