SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Ukiwa mzuri raha sana yaani mtu hakuchoki kabisa anatamani tu kuwa na weee mda wote.Sabrina naye alikuwa ni kwikwi japo yeye ni mwembamba lakni ni mzuri sana. Aliwakilisha vyema maumbo hayo. Najua wanaume wengi wanadata sana na wasichana wa aina ya Sabrina yaani wembamba lakini sura kama mdoli kiuno kama dondola.
Bataa likaendelea tukajiachia huko ufukweni na kwa kweli nikajikuta naipenda Dar kwa haraka japo nilikuwa ni mgeni. Hatukukaa sana huko ile jiono jioni waliturudisha nyumbani sehemu ambayo Sabrina alikuw akaikaa. Tuliingia hapo na yule kaka aliniachia pesa nyngi kama laki mja huku akisisitiza kuwa tuwasiliane.
Sabrina kumbe alikuwa haishi tena nyumbani kwao yaani kwa wazazi wake.Alikuwa na chumba amepanga mahali pengine. Chumba selfu na sebule.Na alinieleza kinagaubaga kuwa yeye anakaa hapo na haishi tena na wazazi na kwa sasa anajitegemea. Nikaanza kumuuliza sasa najitegea kwa kazi gani.
Akanambia mjini hapo na kama kawaida yeye anatumia akaili kuishi mjini na sio nguvu. Pia alinisifia kuwa animezidi kuwa mzuri na akasema kama isingekuwa hiyo mimba angeningiza kwenye mtandaoo. Hapo sasa sikumwelewa ikabidi nimuulize mtandao gani.
Akanambia kama nilivyoona jana hizo ndo dili zake kutembea na vigogo au watoto wa vigogo. Akasisitiza kuwa wale vijana ni watoto wa mawaziri na wapo Uganda kimasomo lakini huwa wanakuja kula bata Dar na hata wazazi wao kujua. Akanambia kwa jinsi eti nilivyo mzuri naweza kuwa tajiri kwamda mfupi na wala sistahili kabisa kufanya kazi za ndani.
Wakati akiniambia vitu hivyo mara simu yake ikaita. Alionekana kufurahishwa na simu hiyo na aliongea kwa pozi na kutoa ile sauti yake ya kuwaibia wanaume. “Dili lingine shoga yaaani hiyo mimba sijui tukaitoke tu”, aliongea binti huyu bila aibu.
Kauli hiyo ilinishangaza sana yaani mimba ishakuwa kumbwa hivyo anawaza kuitoa.Kwanza angejua jinsi hii minba ilivyoleta majanga basi kamwe hasingewezza kusema upuuzi huo.
“Shoga huyu niliyeongea naye ni pedeshee mmoja mjini ana pesa sana sasa tufanyaje na amenambia leo anataka kuwa na mimi”. Mmmh shoga yaani jana umetoka kulala na mwanaume na leo tena” ilibidi nimuulize. “Ndio kwangu mimi hakuna kinachoshindikana kwanza mimi nikilala na mwanaume huwa nambania sana kama huyu mzee anayekuja hana shoda akipiga kimoja tu chali”.
Nilitamani kucheka maana mtu aliyekuwa akisema hivyo alionekana mdogo kama katoto.Lakini sawa maana waswahii walisema wembembe wa reli treni inapita. “Kwa hiyo shost kama una mishe si ni bora unipeleke tu huko kwa shangazi yako”. “Tatatzo sio kukupeleka kule tatizo utalipwa elfu 50 mwezi mzima na utafanya kazi zote za ndani.
Kwani yule mwanaueme uliyeala naye jana mekupa shilling ngapi alinuliza swali la kizushi”.Nikajibu laki moja.Akatabasamu na kuniambai sasa wewe huoni hiyo tofauati umepewe laki moja kwa usiku mmoja alafu pia umekula bata na kufuraisha nafsi yako. Haya ndo maisha mimi ninayoyapaenda mtu unakula kwa sababu ya uzuri wako”.
“Huku ni mjni dada hakuna shamba wala hakuna kulima lakini twala”. “Sasa wewe shosti wangu mimi na tumbo langu hili nitafanyaje”.Labda kama na mpango mwingne ambao utatuwezesha kupata pesa. Mimi nipo tayari sana kufanya hayo unayoyataka lakini sio kwa hali hii .
Nitafanya hayo yote pindi tu nitakapojifungua.Hivyo hii mimba kuitoa ni uongo nishajaribu zaidi ya mara moja ikashindikana. Tena hii wewe acha tu mpaka marehemu mama yangu alinitokea na kunionya kamwe nisithubutu kabisa huo mchezo. Hapo Sabrina alivuta pumzi akafikiria kidogo akanambia “ok nimepata jibu wewe leo baki hapa ngoja mimi nikaonane na huyu mzee”.
“Mara ya mwisho alikuwa akitaka kunifungulia biashara lakini mimi nilikuwa sitaki kukaa sehemu moja. Na pia alainipa mtihani kuwa kama nataka anifungulie biashara basi nitafute kama milioni mbili yeye ataniongezea tatu ili nianze na mtaji wa kama milioni tano”.
“Lakini shosti tukubaliane kuwa utakubali kukaa mahali usimamie biashara kwa maana mimi kukaa sehemu moja siwezi”. “Kwa hilo usijali shoga yangu tena utakuwa umenisaidia sana na naamini kwa mda mfupi tunaweza kuwa matajiri”. “Siunajua mimi yatima na yatima siku zote hadeki”.
“Sawa nimekuelewa kwa kuwa mtoko ni jioni sa hivi ngoja tupumzike”.
Basi kwei tulingia chumbani na yeye akatandia zulia na kulala hapo chini. Akanambia nisijali mimi nilale tu kitandani kwa maana yeye mgongo unamuuma.
Nilijitupa hapo kweye kitanda huku nikifurahiswa na jinsi kilivyotengenezwa. Yaani kiukweli huyu binti alijapanga na kama ni kweli uchi wake ndo uliompataia yote hayo basi acha tu kiuongo hicho kilaaniwe kama sio kubarikiwa. Sasa sio wewe msomaji wa kike ukaiga,iga ufe, gusa unate maana siku hizi maradhi yamejaa kila kona.
Na baishara hiyo inahitaji akili la sivyo utakufa kwa ukimwi kama sio kuisha kuchezewa na kukongoroka. Huyo binti alikuwa ni mdogo sana lakini mambo yake kwa kweli yalikuwa ni makumbwa sana mpaka aliniogopesha.Basi akanambia kwa kuwa tulikuwa tumechoka ngoja tu tupumzike na yeye alichukuza zulia na kutandika chini na kudai kuwa alikuwa akiumwa na mgongo.
Mimi nilijibwaga hapo kitandani huku nikikagua uzuri wa kitanda hicho.Kitanda kilikuwa kizuri unalala mapka unajihsi upo Ulaya. Kweli hakakuchuku adkaika nyingi nikapitiw an ausngiz mzito usngizi war aha usingzi ulionifanya nisahau shida zote na kuona labafda huo ndo utakuw amwanzo mzur wa maisha bora huko mjini.
Nilikuja kustuhswa na aharufu ya chps ya ambayo ilikuwa iknukia kupiata kaisai. Hapo usngizi uisa na nilipaongalia pemben sikuona shostit huyo. Ikabaidi niamk emaana na kanja akalikuwa kakiniuama. Nilienda sebuleni na kumkuata mtoto huy akaitetea afya yake.
“Eeeh una machale kweli maana ilikuwa nikimaliza hizi niahamie na za kwako” alisema kwa utani na kunionesha mzigo wangu uliokuwa ukinisubiri.Hapo sikutaka kufanya makosa nilirudi kwanza chumbani ambapo nilenda bafuni nikafungulia bomba la mvua na kuoga.
Kama kawaida yangu nilikisafisha vizuri kabisa na sikuangaika hata na kajipaka mafuta nilirudi pale sebuleni.Sinilishakwambia kwenye ishu za kula mimi sifanyagi masihara.Nilizipiga zile chipsi kama sina akili nzuri huku nikishushia na juisi ambayo ilikwua ikinisubiria.
“Ninachokupendea wewe best yangu kwenye kula tu huwa huna masihara”, ilibidi Sabrina anipongeze kwa hilo. Nilicheka tu na kumwambia asante kwa msosi huo.Hapo akawasha flat screen ambayo ilikuwa hapo sebuleni.Kininga kininga kweli mpaka utafikiri labda ni watoto wa kishua.
Kama alijua napenda movie akaniwekea movie ya “The last Kiss”.Tukaendelea kuangalia huku tukikumbushia na maisha ya shule na jinsi yalivyokuwa magumu.Sabrina alitumia tena mda huo kunipigisha story za marafiki zake.Pia akanikumbusha jinsi alivyokuwa akiwachanganya wanaume walimu kwa wanafunzi.
“Yaani shoga hizi harakati mimi nimezianza mda kweli, hapa yenyewe sijui hata kama ni mzma au la.Kuna mwanaume mmoja juzi alikuwa ananing’ang’anaiza eti tukapime mbona kesho yake nilimtafutia sababu mpaka tumeachana. Yaani mimi najihisi ni mgonjwa ninayetembea maana nishatembea na wanaume wengi sana aliendea kusimulia Sabrina”.
Mda ulienda mpaka kagiza kakaingia na Sabria aliniacha mimi nikiendelea kuangalia movie na yeye akaingia bafuni kuoga na kukipara tayari kwa mtoko.Akanambia nisiwe na wsiwasi hapo nikiskia njaa nitoke njee kuna vibanda vya chipsi naweza kuagiza tu.Au kama nitachoka niende kwa mbele kidogo nitapata chakula.
Basi akaondoka na kuanicha mimi hapo.Sikuwa na la kufanya zaidi ya kuangilia TV.Niliangalia Movie mpaka mda ukawa umeenda sana na hapo niliamua kutoka ili niende kutafuta chakula.Nilitoka mpaka sehemu hiyo ambayo huwa wanatengeneza chakula.
Nilipita kwenye chipsi lakini wakati naangaza kibanda gani hakuna watu wengi kuna mtu nilimuona.Si mwingine bali ni Athumani yule mwanaume mtoto wa yule mzee ambaye alinisababishia majannga ya mimba hiyo.Kwa kweli ilinibidi nirudi nyuma na kujibanza sehemu ya kigiza ili niweze kumwaangali vizuri. Nilimwangalai kwa umakaini sana nikagundua kuwa ni yeye.
Sasa nikawa najiuliza je niende kumsalimia au niache.Je vipi kama mama yake hakupona mimi nilivyoondoka kule Mahenge? vipi kama anakinyongo na mimi si anaweza kunitafuta au hata kunisababishia matatzo. Roho ya upendo bado ilikuwa ikinisukuma kwenda kumsalimia kijana huyu lakini bado miguu ilikataa kupiga hatua.
Kijana huyu nilimpenda sana lakni hii mimba ya baba yake ndo ilikuwa ni chanzo cha yeye kutoroka nyumbani na kujaribu kuanza maisha yake.Wakati najishauri nilimuona akiwa amefunga chipsi zake akija njia ile ile ambayo mimi nilikuwa nimejibanza kwenye uchochoro.
Hapo miguu ilijikuta ikipiga hatua yenyewe na kurudi nilipotoka.Nilitembea haraka haraka na kurudi kule nilipofikia.Niliingia ndani nikajibwaga kitandani na kumshukuru Mungu kwa kuwa hakuniona. Kiherehere cha njaa kiliisha na nilijikuta nikipanda kitandani na kulala.
Lakini baadaye niliona ngoja nilidanganye tumbo kwa kunywa juisi.Niliwaza itakuwa vipi kama kijana huyu atakuwa anaishi mtaa huo.Sikutaka kujiumiza kwa mawazo nikanywa juisi na kupanda kitandani na kulala.Kesho yake mida ya saa nee Sabrina alirudi na kama alijua nitakuwa na njaa alikuja na poti ambalo kulikuwa na supu na chapati.Nilikunywa na siku ikawa imeanza hivyo.****
Ni mwezi wa tatu sasa nipo jijini Dar es Salama kitumbo kimekuwa kikumbwa sana na sasa mimba yangu sio kificho ni dhairi kuwa nilibakaiza miezi miwili tu nijfungue. Uchungu wa maisha umepungua kwa namna moja au nyingine kwa sababu zile pesa nilizitumia vizuri tukachanganya na za rafiki yangu huyo kipenzi tukafungua duka la nguo na urembo wa kike.
Sabrina na yeye alikuwa akienda mpaka Niaraobi kuleta mzigo na mimi ikawa kazi yangu kumbwa ni kuuza duka hilo. Tulijiatahdi sana kila pesa tuliyopata kufanya jabo la maana na Mungu alitukunia nazi mambo yakawa yanatunyookea.Sabrina nay eye hakucha tabaia yake hiyo ya kutumia mwili wake kutafauta pesa.
Na sasa kila pesa aliyoipata ailitumia kuongeza mtaji. Umaarufu wa huduma yetu ukawa mkumbwa sana na tukashauriana tufungue duka lingine ambalo tutajiajiri watu wa kutusaidia.Kweli apangaye hufanikiwa.Mjini maisha mipango pia si lazima uend shule uwe na degree ndo unaweza kufanakiwa kimaisha.
Nilikuwa namshauri sana rafiki yangu atulie lakini wapi yeye na viwanja viwanja na yeye. Sasa kila mmoja aliikuwa anaju umuhimu wa mwenzake.Mimi nilimtegemea binti huyu kwa sababu alikuwa akiongeza sana mtaji kila kuitwayo leo.Na yeye alikuwa akinitegemea kwa sababu mimi niliweza kusimamia pesa zisipotee.
Hatimaye miezi tisa ilifika na ule mda wa kujifungua uliwadia. Miezi hii nayo ilikuwa na mitihani mizito kwangu mana tarehe za kujifungua zilipita bila mimi kujifungua. Sikupata uchungu kabisa jambo ambalo lilipelekea mmi kulazwa na kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Madakatri waliamua kuwa niche sindano ya uchungu ili kufanikisha zoezi.Bado maji hayo ya uchungu hayakusaida hivyo ilinilazimu kufanyiwa operesheni. Ninamshukuru Mungu kwa kweli nilijifungu salama toto la kiume, handsome boy mzuri kama mama yake.
Yeah ingawa alikuwa ni mwanaume lakini alaichukua sura yangu kwa asilimia nyngi huku akichanganya weupe wa yule mzee.Lilikuwa ni toto la nguvu lenye kilo tatu.Nilitoka hospitali na kurudi nyumbani kwa kuendelea na kuuguza kidonda na malezi. Sabrina kweli alikuwa hataki shida maana alitafuta msicha wa kazi.
Yaani huyu ni kiboko maana aliona bila hivyo atakuwa na majukuu mengi ya kunisadia.Mimi nlimshukuru kwa yote na nilimuomba Mungu aendeleee kunipigania ili nifanikiwe katika maisha.Nilijitahidi sana kufuata malezi yaiyobora na nilihudhuria kliniki na kufuata maelekezo yote ya ulezi.
Sikuwa mvivu kwa kweli nilinunua na vitabu vya amlezi bora kwa mtoto.
Ingawa Sabrina alinisihi sana eti nisimnyonyeshe mwanangu kwa madai kuwa nitaharibu matiti yangu lakini mimi nilikataa mpango huo nilimnyonyesha na mtoto alikuwa mwenye afya ya kuvutia.
Alichukua mwilii wa mama yake kwa kweli maana kila uitwayo leo alizid kuwa bonge.Nilimpa jina la Arsen jina ambalo lilipendekezwa na rafiki yangu Sabrina.Ingawa nilikuwa kwenye malezi lakini pia sikuacha kujitunza na kufanya niendelee kuonekana mrembo tena mrembo haswa.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
