BAMBUCHA (19)

Jpt
0
JINA: BAMBUCHA
Mwandishi: Eliado Tarimo

SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...

Alichukua mwilii wa mama yake kwa kweli maana kila uitwayo leo alizid kuwa bonge.Nilimpa jina la Arsen jina ambalo lilipendekezwa na rafiki yangu Sabrina.Ingawa nilikuwa kwenye malezi lakini pia sikuacha kujitunza na kufanya niendelee kuonekana mrembo tena mrembo haswa.

TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE

SASA ENDELEA...
Nilionana na wataalamu na walinishauri niepuke kupaka mafuta, losheni au manukato yenye harufu kali.Kwa mujibu wa watalaamu vitu hivi si vizuri sana kuvitumia kwa sababu mtoto anatumia mda mwingi kwenye mwili wa mama.Pia baada ya kuhakikisha ule mshono umepona vizuri nilianza mazoezi mepesi mepesi kufanya mwonekano wangu uwe mzuri na wa kuvutia.

Nilikuwa natumia mafuta na losheni zisizo na kemikla na pia hata kucha zangu zilikuwa fupi na niliziremba kwa mtindo huo.Nilijitahidi sana kuwa natural na kuonekana ni mrembo wa asili.Wakati huo mimi najitunza ili nirudi kwa kishindo Sabrina yeye aliendelea kupuyangapuyanga na kuangaika na wanaume mapedeshee wa mjini.

Yaani kama wewe ni mwanaume ambaye huwezi kuhonga kuanzia laki moja kwa Sabrina hata usijisumbue utabaki kula tu kwa macho au utaambulia maneno ya shombo. Mwenyewe alikuwa na msemo mmoja usemao eti “nitakuchamba kwa maneno machafu mpak ukioga maji ya maka usitakate”.Hapa ndugu zangu wa dini ya kiislamu mtanisaidia maana mimi siyajui maji ya Maka.

Kwa hiyo sijisifii mimi ni miongoni mwa wanawake wachache ambao waliendelea kubaki warembo mara baada ya kujifungua. Ni kweli kukaa na mtoto miezi 9 ni kazi.Ni kweli kulea ni kazi mana usiku unaweza hata usilale kwa kubembeleza mtoto.Na ni kweli kuna uwezekano wa kuongezeka uzito lakini hivi vyote ndugu yangu msichana sio sababu ya kujiachia na kuwa kama furushi la mkaa.

Ngoja niwashauri wanawake wenzangu hasa mlioolewa usikubali kabisa kujiachia na kupoteza urembo wako. Mtu amekuoa mwaka jana tu ukiwa bonge la mtoto, mwanamke mwenye mvuto mwanaume akawa anaona faharii kutembea na wewe kwenda sehemu yoyote ,leo umezaa mtoto mmoja umejiachia, upo upo tu kama gunia, hufanyi mazoezi, mchafu mchafu tu.

Hiyo ndoa ndugu yangu itaharibika na utajuta maana mwanaume huyo akikutana na makurumbembe makombwa mwiko kama Sabrina ujue hapo hatarudi atalala nje ya ndoa na ukicheza ndo utaachika tu. Jamani mimi sijaolewa lakini msipuuze huu ushauri wangu na kaa ukijua kuwa kuolewa ni jambo moja jukumu la pili ni kutunza ndoa yako.

Baada ya kuzaa mpe mume sababu ya kukupenda kama alivyokupenda mara ya kwanza.Kufunga ndoa ukadhani kuwa umemaliza kila kitu ni kosa, tena si kosa tu ni kosa la jinai, sumu na shubiri ya hiyo ndoa yako.Jitunze uonekane vizuri mrembo na ndoa yako idumu.

Wewe puuzia tu subiri makomba mwiko yaje huko ndo utajua.Siku zilizidi kwenda na biashara zilikuwa zinaendelea kama kawaida.Kwa kuwa kulikuwa na binti wakunisaidi malezi mimi nilianza kutoka na kwenda kwenye miangaiko ya kila siku. Nilikuta biashara imeyumba kidogo hasa ile frame niliyokuwa nikisimamia mimi iliyumba na kuliokena kuwa kabisa yule binti tuliyemweka alikuwa hayupo makini.

Alikuwa mdokoaji sana hivyo hasara za wazi zilioneka.Sikushangaa maana Sabrina yeye alichokijua ni kuleta mzigo na kuendelea na mambo yake. Hata haulizi mapato na matumizi yaani yeye akishapewa pesa ya mzigo hataki kujua faida imeenda wapi.

Ni ngumu kwa kweli na nilichukia sana mpaka nikatamani nimfukuze huyo binti siku hiyo hiyo.Nilifanya mahesabu na niliamshauri Sabrina kama tunataka kuendelea basi binti huyo tumuondoe na mimi niendelee kusimamia biashara kama kawaida. Kwa hiyo baada ya mapungufu hayo mimi nilirudi na yule binti aliondoka.

Alivuna alichokipanda kwa sababu hakula kwa akili na sasa duka lilipwaya kabisa.Siku zilizidi kwenda na mtoto alikuwa anaendelea vizuri.Sikutaka kumuachisha ziwa mapema nilimuacha afurahie vya kutosha mpaka alipofikisha miaka miwili. Hapa sasa ndo utamu ulipoanzia. Na mimi ilikuwa ndo mda wangu wa kutumia uzuri wangu vizuri.

Nilitaka kupata maendeeo ya haraka haraka ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba kwenye kiwanja chetu tulichokinunua huko Kibamba.Kiwanja hiki kilikuwa ni kikumbwa hivyo tulikigawa katikati upande mmoja wa Sabrina na mwingne wa kwangu. Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kujaribu kupita nja zile zile alizokuwa akipita Sabrina ila mimi nilitaka kupita kwa akili zaidi.

Sasa kitu cha kwanza nilichokifanya ni kutengeneza tumbo.Nilitaka niwe na umbo la bata mzinga umbo la Bambucha, umbo la Chura umbo ambalo litakuwa kivutio kwa kila mwanaume ambaye ataniona.Nilianza kwanza kupita kwa wataalamu na kuwaulizia njia za asili za kutengeneza hili tumb liwe kivutio.

Nilitafuta njia ya kuzifanya hizi hips ziwe mara mbili.Kila nilipoenda walinishangaa maana tayari nilikwua nimejaliwa lakini eti nilitaka zaid.Wengine walidiriki kusema nilikuwa sina shukrani na nilitaka kumkfuru Mungu lakini mimi sikujali. Ujue kwenye biashara lazima ujue sreghth zako na ukishazijua lazima utumie vizuri ili uweze kuwashinda wapinzani wako.

La sivyo utakuwa unaonekana wa kawaida tu. Sabrina alishajijua kuwa hana umbo nene hivyo akawa kila siku anatafuta mbinu za kuonekana mrembo kwa hilo hilo umbo lake na mimi sasa nilitaka hivyo.Basi katika harakati zangu hizo kuna siku nilienda kwa wataalamu hasa wa mazoezi maana nilisikia kuwa mazoezi ni muhimu sana hivyo nilienda kupata ushauri.

Nikampata Mzungu mmoja ambaye anamilki Gym moja maarufu sana hapa mjini. Sijui ni mzungu koko maana alikuwa akiongea kiswahli vizuri utazani labda alikuwa ni mzaramo.Alianza kutema cheche zake kwa kuniambia “Hakuna ubaya wowote kwa mtu kutaka kupendeza.

Swala la kuonekana mzuri au kuwa mtanashati limekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu hususani upande wa dada zetu. Si kitu cha ajabu maana tangu enzi za mababu , tunasoma katika historia jinsi mwanamke alivyosifiwa kwa uzuri na urembo wake.

Swala la uzuri na urembo wa mwanamke linajadiliwa mara nyingi katika aya mbalimbali za misahafu ya dini zetu, kuonesha ni jinsi gani ambavyo hata Mungu mwenyewe anavyouthamini uzuri na urembo wa mwanamke. Si ajabu kuona jinsi ambavyo makampuni makubwa yanavyojishughulisha na utengenezaji wa vipodozi na nguo, vitu ambavyo vinachangia sana katika kumfanya mwanamke aonekane mzuri na mrembo, yanavyotengeneza faida kubwa.

Sikatai kwamba kuna uzuri wa kuzaliwa, la hasha wapo wazuri tena wazuri utazai wameshusha kutoa pepeono. Ni dhahiri kabisa wapo watu waliojaliwa kuwa na muonekano mzuri ambao wamezaliwa nao. Na mtakubaliana na mimi kwamba kuna baadhi ya vitu katika miili yetu ambavyo hatuwezi kuvibadilisha hata kama hatuvipendi, lakini habari njema ni kwamba asilimia kubwa ya muonekano wa sura na miili yetu waweza kubadilishwa, na kuendana na matakwa yetu.

Siongelei wala sishauri utumiaji wa madawa au njia nyingine zenye madhara katika mwili wa binadamu. Bali naongelea jinsi ambavyo mfumo wa maisha waweza kukusaidia kupata muonekano unaoupenda bila kuwa na madhara yeyote ya kiafya katika mwili.

Usifikirie sana, hapa naongelea vitu vya kawaida kabisa katika maisha yetu ya kila siku visivyo kuwa na gharama yeyote zaidi ya muda. Naongelea mazoezi na lishe bora”. Hapo nilitigisha kichwa maana kwenye mazoezi na lishe bora ni sehemu ambayo nilikuwa nahitaji maana nilisikia hizi njia za mchina zina madhara sana.

Akaendelea kusema kuwa “Viko vitu vingi vinavyoelezea muonekano wa mtu. Sura na umbo la mwili ni sehemu kubwa na muhimu katika muonekano. Sasa wewe unataka nini ainiuliza huku akiniangalia machoni”. “Nikamwambia umbo”. “Safi najua wanawake wengi wanaangaka mpaka kutumia madawa wenye madahara kwa afya zao.

Ndio maana mimi nimekuja kwako sihitaji hizo njia”. “Vizuri sana na habari njema ni kwamba, huitaji kutumia madawa ambayo yanaweza kuwa na madhara kwa afya yako ili kupata nyonga na makalio ya ndoto yako. Mazoezi na lishe sahihi vinaweza kabisa kukupatia nyonga na makalio uliyokuwa ukitamani siku zote. Leo hii nitakulekeza aina ya mazoezi yanayosaidia kutengeneza sehemu za nyonga na makalio na kuzipa muonekano unaoutaka”.

Wataalamu wa mambo ya mazoezi wanasema, “mazoezi mazuri kwa kina dada ni mazoezi ya sehemu ya chini ya mwili. Hapa ninamaanisha mazoezi yanayohusisha misuli ya miguu, mapaja, nyonga na makalio. Sababu ya kusisitiza mazoezi haya kwa kina dada ni kutokana na ukweli kwamba, wakati mazoezi haya husaidia kiafya, pia yanasaidia kuzipa muonekano mzuri sehemu za nyonga, mapaja na makalio”.

Nikamwambai aende moja kwa moja kwenye mazoezi yanayokuza na kuyapa makalio na nyonga muonekano mzuri. “Sawa inaoenekana una haraka sana?”, alaiuliza. “Ndio mtaalamu maana nimefunga biashara na nimekuja hapa mara moja tu. “Sawa ngoja nipunguze maelezo.

“Zoezi muhimu kuliko yote, ambalo kwa bahati mbaya kinadada wengi hulikwepa, ni zoezi lijulikanalo kitaalamu kama ’’squarts’’ yaani kuchuchumaa kwa kiswahili rahisi. Kufanya squarts, waweza tumia uzito au waweza fanya squarts bila kutumia uzito wowote.

Unachukua uzito unaoweza kuhimili, na kuuweka mabegani (kumbuka uzito huu unatakiwa uwe umewekwa pande zote kwa uwiano sawa ukiunganishwa na bomba ambalo ndiyo unaliweka mabegani). Simama wima miguu yako ikiwa imetengana kiasi, halafu chuchumaa taratibu, na kunyanyuka taratibu.

Rudia mzunguko huu mara 6 mpaka 8, kwa kila seti, na ni vema kufanya seti tatu mpaka tano. Kumbuka waweza fanya squarts bila kuwa na uzito wowote, cha muhimu ni kuikutanisha mikono yako pamoja nyuma ya kichwa wakati wote unapokuwa unachuchumaa na kusimama. Ni muhimu kufahamu kwamba, kama unataka sehemu zako za makalio kuongezeka ukubwa, basi ni vema kutumia uzito.

Zoezi lingine ni lile la kukaa mkao wa wanyama. “Kama mnayama niliuliza kwa hamak?”. “Ndio hiyo unapiga magoti na kuweka mikono yako chini kama vile unataka kutembea kama mbwa au paka. Taratibu unarudisha mguu wako nyuma kama kwamba unampiga teke mtu aliye nyuma yako (kama ng’ombe au punda anayepiga teke la kinyumenyume).

Unafanya hivyo taratibu na kuurudisha mguu bila kuweka goti chini. Unarudia mara 6 mpaka 12 kwa mguu mmoja, halafu unafanya hivyo hivyo kwa mguu wa pili. Ni vema kufanya mizunguko mitatu mpaka mitano ya zoezi hili. Muhimu ni kwamba, unaporudisha mguu nyuma, usiunyooshe kabisa, ili msukumo mkubwa usikike kwenye sehemu za makalio.

Zoezi hili ni zuri sana kuyapa makalio umbo na muonekano mzuri. Pia ni zuri sana katika kuondoa maumivu ya mgongo.Yako mazoezi mengi yanayosaidia kuongeza na kuyapa makalio muonekano mzuri (shape). Ila niliyotaja hapo juu ni baadhi tu ya mazoezi ambayo waweza fanya hata nyumbani.

Ila kama utakuwa na nafasi uwe unakauja hapa kuna mashine maalumu zinazosaidia kuyaweka makalio yako katika umbo na ukubwa unaotaka. Waweza tumia smith machine kwa squarts.Waweza fanya ``quadriceps curls’’, ´´leg press’’ na mazoezi mengi kwa kutumia mashine maalumu zinazopatikana kwenye gyms mbalimbali.

Ukweli ni kwamba kupata makalio yenye muonekano na ukubwa unaoutaka, zingatia mazoezi yanayohusisha sehemu ya chini ya mwili . Si swala la kujaribu, bali ni kitu kinachojulikana kisayansi na kiuzoefu”. “Sawa mtaalamu kwa kuwa nataka nitakuwa nakuja hapa kufanya hayo mazoezi”.

“Karibu sana Bambucha na pia yapo mazoezi ya kupunguza mwili na makalio bla kuoteza muonekano wako mzuri”. “Mimi hayo siyataki nataka ya kuongeza bila kupoteza uzuri”.Akatabasamau kisha kanipa mkono. Nililipia huduma hiyo ya ushauri kisha nikaondoka zangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)