Notifications
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…

BAMBUCHA (20)


JINA: BAMBUCHA
Mwandishi: Eliado Tarimo

SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...

“Karibu sana Bambucha na pia yapo mazoezi ya kupunguza mwili na makalio bla kuoteza muonekano wako mzuri”. “Mimi hayo siyataki nataka ya kuongeza bila kupoteza uzuri”.Akatabasamau kisha kanipa mkono. Nililipia huduma hiyo ya ushauri kisha nikaondoka zangu.

TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE

SASA ENDELEA...
Nilifikiria hayo maongezi nikajua bado kwa upande wa aina ya vyakula bado sijapata ushauri hivyo nikaona bora niendelee kutafauta wataalamu.Basi nikaenda kwa mtaalamu mmoja kupata maelekezo mengine. Huyu sasa ndo alinitisha mpaka nikaogopa kabisa.

Kwanza alinambia wazi njia zote mpaka za dawa za kupaka kuchoma sindano lakini lazima anieleze mandhara yake kwanza.“Kimsingi unenepeshaji wa kisasa wa makalio, mapaja na matiti hufanyika kwa njia ya kuweka vipandikizi (silicone implants), kupaka cream, kuchoma sindano za mafuta ya mwili kutoka katika nyama za tumbo (fat transfer injection) au kuvaa vitu vinavyotengeneza umbo linalotamaniwa na wanaume.

Matumizi ya dawa za kunenepesha makalio, mapaja na kutunisha matiti si salama kwa afya kwani zinaweza kusababisha hali ya kushindwa kupumua kutokana na mzio (allergy), kansa, kuoza kwa misuli ya makalio na miguu (gangrene), uvimbe wa misuli (lumps/granuloma), kunenepa kwa makalio au matiti bila mpangilio au ulinganifu, kupooza au kifo wakati mwingine.Dawa hizi zinaweza kusababisha kifo pale zinapoingia katika mfumo wa damu na kuharibu ini, ubongo, moyo na mapafu.

Dawa zingine kutokana na kuongezewa viambato vya steroidi, mapema au baadaye sana zinaweza kusababisha magonjwa ya vidonda vya tumbo, udhaifu wa mifupa (osteoporosis), figo kushindwa kufanya kazi na shinikizo la damu”. “Je, kuna mifano yoyote kwa mtu aliyewahi kuathirika?, ilibidi nimuulize maana nilihisi ananitisha siunajua tena wabaonge wenzetu wana vikwazo vingi tu pamoja na wivu.

Akanijibu kwa kusema “Kuna mifano mingi ya wanawake waliodhurika au kupoteza maisha kutokana na dawa hizi za urembo usiokuwa wa lazima. Mwaka 2004, mwanadada Apryl Michelle Brown mwanamitindo ya urembo wa nywele (Hair stylist) kutoka Los Angeles, Marekani alipoteza makalio, mikono na miguu yote baada ya misuli yake kuoza kutokana na kupata madhara ya sindano za kunenepesha makalio.

Mrembo wa zamani wa Argentina(1994), Miss Solange Maginano akiwa na umri wa 38, alifariki dunia mnamo mwaka 2009 katika Kliniki moja huko Buenos Aires, Argentina akiwa anapewa dawa za kuongeza ukubwa wa makalio yake.

Mwaka 2011, kulikuwa na taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa Claudia Adelotimi, mwanadada mwenye asili ya Nigeria aliyekuwa na umri wa miaka 20 akifikiri kuwa kunenepesha makalio kungemfanye awe nyota katika ushiriki wake kwenye picha za video za muziki wa kizazi kipya wa kufokafoka, alipoteza maisha kwa kuchoma sindano hizi huko Philadephia, Marekani.

Visa vya namna hii ni vingi sana miongoni mwa wasichana na wanawake wanaopenda urembo bila kujali afya kwanza. Wasichana wengi wanapotumia dawa hizi, huwa wanafikiri kuwa wanaboresha muonekano na maisha yao lakini wanapopata madhara ya kiafya, hupoteza vyote yaani ubora wa maisha na uzuri wao wa asili na kubakia na majuto ya kudumu”.

“Kwa wasichana ambao wanaona kuwa maisha hayawezi kuwa matamu bila kunenepesha makalio, mapaja na matiti yao, ni busara kufanya hivyo kwa njia za asili zisizokuwa na madhara kwa afya zao. Sehemu hizi za mwili zinaweza kunenepeshwa kwa kutumia sayansi ya lishe bora”.

Hapo sasa nikataka kujua hiyo sayansi yal ishe bora ni ipi. Akanambia “kunywa maji mengi na mazoezi ya mwili ni siri ya urembo.Pia Kula vyakula vyenye protini ya kutosha na vyakula vyenye asili ya mimea yaani mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa na mafuta yenye asili ya mimea pamoja na kupunguza sukari na chumvi kwenye chakula, husaidia sana katika uimarishaji na unenepeshaji wa misuli ya makalio, matiti na mapaja.

Kuepuka ulaji wa nyama yenye mafuta mengi au mazao ya maziwa kama vile siagi na samli pia husaidia”.Hapo kwenye vyakula nikawa nimemuelewa na akahidi kuwa nitapewa package inayoendana na mahitaji ya mwili wangu baada ya kuchukua vipimo.
Akaendelea kutoa somo kwa kusema.

“Mazoezi ya kila siku (asubuhi na jioni) ya kupunguza mafuta katika nyama za tumbo, kufanya kiuno kuwa chembamba na kuimarisha misuli ya mapaja pamoja na makalio ni njia bora ya kumpatia msichana umbo la kupendeza na kunenepesha au kutunisha makalio bila madhara ya kiafya.

Baadhi ya watafiti na wataalamu wa mambo ya urembo wanadai kuwa, kiuno cha msichana au mwanamke chenye uwiano wa 70% ya mzunguko wa mapaja yake (hips circumference) au kipimo cha 0.7 WHR (waist to hip ratio) kinaonyesha afya nzuri ya msichana au mwanamke na kinafanya makalio na mapaja ya msichana au mwanake kuonekana kuwa makubwa.

Mazoezi yanayosaidia katika jitihada za kufikia lengo hili kwa kutumia njia za asili na kwa usalama huku yakiimarisha afya ni pamoja na kuruka juu, kupanda ngazi za nyumba (stair climbing), kuinama, kuchuchumaa pamoja na kuminya au kuchua misuli ya makalio (massage) kila siku.

Ili zoezi la kuchuchumaa lilete matokeo yanayokusudiwa fuata kanuni zifuatazo: Kwanza tambua kuwa lengo lako ni kubadilisha muonekano wa umbo lako kwa njia salama, hivyo basi ni lazima ujitume kufikia lengo hilo. Anza mazoezi ya kusimama wakati miguu yako ikiwa imeachana kiasi cha upana wa kifua chako kisha taratibu kunja miguu yako kwenye magoti ili kuchuchumaa hadi mapaja yawe sambamba na sakafu au ardhi kwa dakika kadhaa kisha panda juu taratibu ili usimame kama mwanzo.

Fanya zoezi hili angalau mara ishirini kabla hujapumzika au kubadilisha mtindo wa zoezi.Fanya mtindo mwingine wa zoezi la kuchuchumaa wakati miguu ikiwa imepishana, weka mguu mmoja mbele kiasi cha umbali wa hatua moja na mguu mwingine uwe nyuma kisha chuchumaa kwa kukunja magoti yote, mguu wa mbele ujikunje na kutengeneza kona yenye 90° digrii na mguu wa nyuma uwe chini kiasi cha nchi 2 hivi juu ya sakafu.

Kisha simama na kubadilisha mguu uliokuwa nyuma uwe mbele na kurudiarudia zoezi mara kwa mara.
Zoezi jingine ni lile la kuweka magoti yote na viganja vya mikono yote sakafuni kama mtu anayetaka kusujudu, kisha inua mguu mmoja kwa nyuma wakati goti moja na mikono ikiwa sakafuni.

Badilishabadilisha mguu wa kuinua na fanya hivyo kwa dakika 20 kila siku asubuhi na jioni. Lakini pia unaweza kusimama wima na kunyoosha mikono yako yote mbele usawa wa kifua chako kisha ishushe taratibu hadi uguse vidole vya miguu yako kwa mikono yote miwili.

Baada ya hapo inuka taratibu hadi usimame wima kama mwanzo na urudierudie zoezi hili kwa dakika 20.Zoezi jingine linaloweza kusaidia ni lile la kuchua au kiminyaminya misuli ya makalio (massage) kwa dakika 30, asubuhi na jioni kila siku. Zoezi hili huimarisha misuli na kuongeza kiasi cha mzunguko wa damu katika nyama za makalio. Zoezi la kuchua misuli pia linaweza kusaidia katika utunishaji wa matiti kwa wale wanaohitaji matiti makubwa yaliyojaa.

Fanya massage ya matiti kwa kutumia vikanja vyako kila siku asubuhi na jioni na kuchezea chezea chuchu kwa dakika 30, hii itaongeza mzunguko wa damu katika matiti na kupunguza damu ya hedhi lakini pia itasababisha ongezeko la kichocheo cha prolactin na kuimarisha misuli ya matiti.

Ili mazoezi haya yalete matokeo yaliyokusudiwa ni lazima yawe endelevu na yaende sambamba na kanuni zingine za afya na urembo kama vile lishe bora, kunywa maji ya kutosha na kuwa na mtazamo chanya katika maisha”.Kwa maelezo hayo niliona kabisa hakuna haja ya kuchoma sindano zaidi ya kutumia njia za asili.

Lengo langu la kuwa msichana mwenye mvuto zaidi mjni.Nilirudi zangu kwenye biashara yangu na sasa nilikuwa nimepata taarifa ambazo mimi niliona zinajitosheleza.Niliamua kwa dhati kabisa siku inayofuata nianze mazoezi na pia kabla ya kufanya hivyo nilimua kwenda kupima afya ya mwili mzima.

Nilianza mazoezi rasmi huku nikitumia mchanganyko wa vyakulaa ambao ungesaidia kuendana na mzoezi hayo na kufanya mwili wangu uwe wa mvuto

Sikutaka eti nifanye mazoezi alafu nikomae niwe na vigimbi kama mlima magimbi. Mimi nilitaka nifanye mazoezi alafu niwe nyonyoro umbo lenye mapangilio sio makalio makumbwa yasioendana na mwili wangu. Kupanga ni kuchagua na hata kama umezaliwa mbaya ukiamua kuwa mbaya zaidi unaweza.

Ila hata kama ulinyimwa vitu fulani ukiamua kuwa mzuri unaweza.Kweli kadri siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo hivyo nilivyoongeza juhudi katika mazoezi.Katika miezi kadhaa tu mabadiliko yalianza kuonekana.Mshundundu ulianza kuongezeka hapo kiunoni ndo usiseme.

Matiti nayo kuna jinsi niliya boost kimtindo.Ukisikia namba nane hiii sasa ndo ilikuwa namba nane. Nikipita njiani watu walikuwa wakihaha na kuumiza shingo zao.Si wanaume mpaka wanawake walishindwa kujizuia na kuniangalia. Sijui na wao walikuwa wakipenda nini.

Arsen mwanangu handsome boy na yeye alishaacha kunyonya kwa hiyo mimi ilikuwa ni kujiachia tu.Na hivi alikuwa anapelekwa baby care, aahaa nilipata mda wa kufanya fujo mjini. Tamaa ya pesa za haraka haraka ndo ilianza kuniponza maana nilianza kuambatana na shoga yangu Sabri aviwanja mbalimbali.

Siku moja nikiwa zangu ofisini kwangu nikifungafunga mahesabu yangu Sabrina alinipigia simu na kuniambia kuwa kuna dili limetokea nimkute hapo Samaki Samaki. Sikujua ni ishu gani basi mimi nilifunga na kueleka sehemu hiyo maarufu kwa kula bata. Nilivyofika hapo nilimkuta akiwa mwenyewe kabisa huku akiwa anakunywa maji tofauti na siku zingine kabisa.

Swali la kwanza nililomuuliza vipi anaumwa au ndo swaga.Hakunijbu kitu alitabasamu tu na kuniambia kuna kazi anataka nimsaidaie.Nilimuuliza kazi gani akanambai nisiwe na mchecheto ebu niagize kitu nilichkuwa nataka kunywa. Niliagiza wine nyekundu kama kawaida yangu na kutegea sikio na kumsikiliza.

"Umeona wale wanaume pale mbele” Sabrina alianza kwa kuniuliza. Basi na mimi nikawaangalia kwanza na kusema “ndio alafu mbona kama washambawashamba”. “Sio washamba hayo makoti makumbwa waliovaa yasikufanye uwazarau”. “Hao mabwana wamefikia hotel moja ambayo ipo karibu tu kutoka hapo.

Hapo mabwana ni wafanyabiashara wa madini na wameingia mjini kwa ajili ya kuuzani machali wa kutoka Arusha. Sasa nataka tuwaingize mjini tuwaibie lakini kwa kutumia akili. “Jamani Sabrina wewe watu wa Arusha si nasikiaa huwa wanatembea na bastola huoni ni hatari”. “Ni kweli kabisa lakini sisi wenyewe tumebeba bunduki kwenye miili yetu yaani hawa ni kuwadatisha kimapezi kisha tuna wawekea madawa hivyo tunawaibia”.

Sikutaka kuamini kama kweli hizo ndo kazi anazozifanya Sabrina na kunileta pesa za kuendesha biashara. “Sasa unachoogopa ni nini wakati wale wapo wawili na sisi tupo wawili cha msingi ni kutumia akili kuliko nguvu. Wapo wanaotumia nguvu kutafuta pesa hizo sisi tunatumia akili zaidi”.

“Sasa tutatumia mbinu gani mpaka tuwe nao”, ilibidi niulize. “Ndio hapo sasa shosti ndo maana nimekuita hapa tujadiliane najua kwa jinsi wewe ulivyo ni rahisi sana”. “Kwa hiyo ninachotaka hapa tufanyae kitu chochote ambacho kitafanya wajue kumbe kuna wanawake wa nguvu hapa”.

“Ni kweli lakini ngoja nikuulize wewe nani alikutonya huu mtonyo”. “Aliyenitonya huu mtoyo ni rafiki yangu mmoja yeye kwa sasa ni muhudumu wa ile hotel waliyofikia”. “Basi kama ni hivyo hawa watakuwepo hapa kwa mda mrefu hivyo hatuhitaji papara naomba nipe nusu saa tu niende nyumbani nikatupie vile vitu vyangu vya kibata mzinga nikija kwa mara ya pili tu wenyewe watatufuta”.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU

26 Bambucha Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni