MAPENZI NA NGONO (20)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
‘’NATUMAINI WEWE NI PABLO DANIEL NAPENDA KUKUTAARIFU KUWA MWANAFUNZI MWENZAKO SAMSON HATUNAYE TENA DUNIANI’’ Nikajikuta nikipata mawenge na kizunguzungu baada ya kusoma messeji ile ambayo ilinichanganya na kuona kwamba ilikuwa imekosewa labda Halima ndio amekufa kutokana na kupata ajali na si rafiki yangu.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Haraka haraka bila ya kujishauri nikavaa haraka na kutoka nje nikifuatiwa na rukaiya ambaye hakuwa na lolote la zaidi la kusema.tulipotoka nje ya ile hoteli tukaanza kutafuta taxi huku mimi nikiwa bado nimechanganyikiwa machozi yananilengalenga.‘’vipii Pablo mara ya pili hii tunakuja unakuwa na hali hii una matatizo gani??’’ yalikuwa maneno ya rukaiya.ghafla rukaiya akanikombatia huku akiwa ananiuliza maswali kadha wa kadha lakini ghafla macho yangu yakakutana uso kwa uso nay a Rebecca ambaye………………
Taratibu Rebecca akaanza kutosegelea na kusababisha mwanaume niwe na tetemeke hali iliyosababisha hata rukaiya kushangaa taratibu nikamtoa rukaiya pale kifuani na kusababisha aanze kushangaa hali iliyosababisha pia ageuke nyuma kuangalia sehemu niliyokuwa naangalia.
‘’wee vipi’’rukaiya akaniuliza lakini sikuwa na jibu la kumpa kwa wakati huo nikabaki nikimuangalia Rebecca kwa shauku kubwa ya kutaka kujua kama akifika pale atasema nini na itakuaje.baada ya kufika pale Rebecca akabaki akituangalia kwa umakini na kuzidi kumstaajabisha rukaiya ambaye akageuka naye na kumuangalia Rebecca aliyekuwa ameshika kiuno chake akiwa amebebetua mdomo wake kwa hasira kali huku machozi yakitaka kumlenga mikono yake ilikuwa imekunja ngumi hakika ilikuwa balaa juu ya balaa.
‘’pablooo huyu nani??’’rebecca akavunja ukimya kwa kuuliza swali ambalo halikupata jibu kutoka kwangu kwa sababu nilikuwa kimya nikikodoa macho kumuangalia yeye.
‘’weee unaliza kama nani sasa??’’rukaiya akavunja naye ukimya swali nililotaka kujibu mimi akalijibu yeye kwa kuuliza swali lingine lilisababisha Rebecca acheke kicheko cha nguvu kikejeri.
‘’siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa umenisikia wewe kikaragosi.’’
‘’weee ishia hapo hapo nani mbwa hivi unavyoojiona unaweza kufikia uzuri wangu wewe eeee unaweza Malaya wewe.’’
‘’haaaa ushie hapo hapo hebu Pablo mwambie mimi ni nani Pablo mwambie nyang’au wako mimi ni nani??’’
Katika hali nisio itegemea ghafla Rebecca na rukaiya wakaanza kurushiana maneno ya nguoni yaliosababisha kiwe kivutio kwa watu waliokuwa wakipita sehemu ile licha ya kuwa na watu wachache lakini kila aliyepita na kusikia hali ile alikuwa akisimama kuangalia kinachoendelea na nini kiliku wa kisababishi cha hali ile kutokea.
‘’hebu jamani wee Rebecca na rukaiya hebu acheni kutukanana kumbukeni nyie ni watu wazima sasa mnataka kujaza watu hapa.’’mwanaume nikajikuta nikitumia uanaume wangu kuwaambia kwa sauti ya kupaza na kibesi lakini hakuna lilisaidia na hakuna hata mmoja aliyetumia masikio yake kunisikiliza.katika hali nisiyoitegemea ghafla rukaiya akamsogelea karibu kabisa Rebecca.
‘’weee mbwa tu halooo kwa uzuri gani wakujifananisha na mimi wewe.’’
‘’PAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA’’
Nikajikuta nikitoa macho baada ya kusikia kibao kikali kutoka kwa rukaiya kwenda kwa Rebecca ambaye kibao hicho kilimpata barabara katika paji la uso wake na kusababisha nibaki nikitumbua macho kwa kutoa amini nilichokiona.hakika kile kibao kilimuingia barabara Rebecca ambaye akainama chini huku akilia na kulalamika kibao kile kwa maumivu ya hali ya juu.lakini ghafla Rebecca bila ya kuuliza akanyanyuka na konde kali sana lililoenda moja kwa moja katika uso wa rukaiya ambaye akaachia ukulele mkali wa maumivu nakudondoka chini mzima mzima.baada ya rukaiya kudondoka chini haraka Rebecca akamsogelea kwa kumkalia juu na kuanza kumshindilia mangumi yasiyokuwa na idadi ya uso nakusababisha damu kuanza kumtoka rukaiya ambaye kutokana na ngozi yake nyeupe ya kiarabu kuruhusu kuutoa damu haraka.hali ikiaanza kuwa mbaya kwa rukiaya na mimi nikapiga hatua ndefu na kwenda kumtoa Rebecca alipokuwa amemkalia rukaiya ambapo ndio alikuwa akimshindilia mangumi rukaiya na kumtoa.
‘’Paaablooo niachie nimfundishe adabu huyu Malaya wa kiarabu niache nakwambia niaaache.’’kwa hali ya hasira Rebecca akalala kwa hasira huku akiwa anahangaika kujitoa mikono mwangu nilipokuwa nimeshika baada ya kumtoa.
‘’hebuuu tulia bwana.’’nikajikuta nikipayuka kwa kumuambia Rebecca ambaye kumuambia vile ilikuwa ni kama sawa sawa nakumpandisha hasira akajikunjua nakuanza kunishindilia mimi makonde mfululizo bila ya huruma lakini kutokana na kuwa mwanaume mwanaume tu nikamzuia kwa kumshikilia vizuri huku nikiendelea kumpandishia sauti ya kuwa anyamaze.lakini kama ilikuwa mchezo vile ile nahangaika kumtuliza Rebecca rukaiya naye akajikusanya nakunyanyuka na kumvamia Rebecca na kuanza kumshindilia makonde ya mgongo kwa nguvu huku akimtukana.nikajikuta nikichoka na hata nilipojaribu kuwagombelezea hali ilikuwa ile ile hakuna aliacha kutaka kupigana na mwenzake kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka kumfundisha mwenzake adabu haswa.
Uzalendo ukanishinda nikajikuta nikiwaacha na taratibu nikaanza kuondoka na kuwaacha pale huku moyo ukiwa unanienda kwa kasi kama mtu aliyekimbia mbio ndefu.nikiwa nimeshafika mbali na sehemu waliyokuwa wakipigana Rebecca na rukaiya ghafla nikamshuhudia mzee mmoja akiwa na kuanza kuwagombelezea jambo ambalo mzee Yule akalifanikisha na kupelekea kila mtu Rebecca na rukaiya achukue njia yake.mwanaume haraka nikaenda kupanda gari la kuelekea nyumbani gari ambalo nilipata mapema nakujikuta nikishusha pumzi ndefu baada ya kufanikiwa kupata siti ya kukaa.
Mawazo yakazidi kuniandama na kunisumbua mara kwa mara nikawa naisoma messeji niliyotumia ikiwa na taarifa ya habari ya kifo cha rafiki yangu kipenzi Samson rafiki ambaye alikuwa ni wa pekee niliyempenda licha ya kuwa na mikwaruzano ya hapa na pale baina yangu na yeye na kisa kikubwa kilikuwa ni mwanamke ambaye alikuw akinitaka mimi na kumkataa yeye Samson.sikuchukua hata muda mrefu sana nikafanikiwa kufika nyumbani ambapo nikamkuta mama akiwa nje na kuonekana akiwa na nyuso za majonzi sana na baada ya kuniona chozi likamdondoka taratibu katika paji lake la uso na kusababisha niwe na shauku ya kujua nini kilichokuwa kikiendelea.
‘’vipii mama shikamoo mbona unalia.??’’
‘’marhaba mwanangu kwani ulikuwa wapi mwanangu maana uliniaga unakwenda kumuona mgonjwa hospitali na hautokawia kurudi sasa nashangaa ulienda wapi kwani??’’
‘’hamna mama kuna sehemu flani nilipitia baada ya kutoka hospitali.’’
‘’anhaa sawa natumaini messeji ya taarifa ya kifo cha Samson uliipata maana kabla hajafa alikuja hapa nakuniachia bahasha ya kaki ambayo alisema wewe ukirudi uifungue na kuisoma lakini haikupita hata lisaa simu yangu ikaita alikuwa ni mama yake anakuja kunipa taarifa kuwa Samson hatunaye tena duniani eti ameejinyongaaa’’
Maneno ya mama yakanishtua na kujikuta na mimi machozi yakaanza kunitiririka na haraka nikaingia ndani nilipofika sebuleni nikakutana na bahasha ya kaki iliyowekwa kwenye meza haraka nikaichukua na kwenda nayo chumbani kwangu na kukaa katika kitanda kisha nikaichukua ile bahasha nakuifungua nakukutana na karatasi nyeupe iliyoandikwa maneno kwa wino wa bluu ambayo taratibu nikaanza kuyasoma kutaka kujua yalikuwa yanasemaje.
‘’RAFIKI YANGU KIPENZI PABLO NATUMAINI HAUTOKASIRIKIKA KWA MAAMUZI AMBAYO NAENDA KUYACHUKUA KWA SABABU PABLO MIMI NAJIUA KWA SABABU MOJA TU HALIMAA ANITAKI,ANIPENDI.HANIITAJI KATIKA MAISHA YAKE NA PIA ANAKUPENDA WEWE NA ANATAMANI UMUOE NAPENDA KUTHIBITISHA ILO KUWA ANAKUPENDA KWA SABABU LEO ALIPOANZA KUONGEA TU HAKUTAJA JINA LINGINE LOLOTE HAKUMTAJA HATA MAMA YAKE AKAKUTAJA WEWE NA ANATAKA AKUONE PABLO MIMI NAJIUA KWA SABABU SIWEZI KUVUMILIA KUONA WEWE UNATOKA NA MWANAMKE AMBAYE NAMPENDA KWA HERI NDUGU NITAKUMISI SANA’’
Yalikuwa ni maneno kutoka katika ile karatasi na kusababisha nianze kuangua kilio cha nguvu sana.niliumia kwa sababu rafiki yangu kajiua kisa mwanamke ambaye mimi sikuwa na mipango naye,
‘’Noooooooooooooooooooooooooooo’’nikajikuta nikilalamika sana huku nalia hali iliyosababisha mama haraka kuja na kuingia moja kwa moja chumbani kwangu na alipoingia akaiona karatasi ile ambayo mimi kutokana na uchungu nikajikuta nikiiweka palepale.akaichukua ile barua nakuanza kuisoma kisha akaniangalia nakushusha pumzi ndefu huku akiniangalia.
‘’pablo mwanangu nataka unijibu maswali nitakayo kuuliza lakini kabla sijakuuliza nihadithie mkasa mzima mwanangu.’’mama akaniambaia nimuhadithie na mimi sikuwa na budi ya kudanganya kwa sababu hali ilikuwa ni tete mwanaume nikajifuta machozi nakuanza kumuangalia mama aliyekuwa ananiangalia kwa shauku ya kutaka kujua……
"Mama kusema ukweli samson alikuwa anampenda sana halima kitambo sana na mara kwa mara alikuwa akinituma sana kwake kwa lengo la kwenda kumuambia habari hizo za kama yeye alikuwa akimpenda halima taarifa ambazo hata mimi nilizifikisha kwa huyo halima kwa sababu halima ni rafiki yangu sana tunashauriana kwa mambo mengi sana.lakini sasa hali ni tofauti sana kwa halima mara nyingi alikuwa ananikanya mimi kumuambia habari hizo huku akinisisitizia kuwa alikuwa hampendi samson jambo ambalo lilimuumiza sana samson ambae kuna siku moja tukajikuta tukipigana kabisa baada ya halima kuja kunikombatia mimi.
Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba mwisho wa siku halima akaja kuniambia mimi ananipenda lakini hata nilipojaribu kumkataa alikuwa akilia na kutishia kujiua na mwisho akajipeleka makusudi kwa kujigongesha katika gari baada ya kumwambia siwezi kuwa naye na ndio huyu niliyeenda kumuangalia jana Mama.kiufupi samson ameamua kujiua eti kwa sababu leo halima baada ya kuzinduka akataja na jina..l....."kabla hata sijamaliza kuongea maneno yale ambayo yalikuwa ni ya ukweli yaliochanganyika na uongo kibao nikajikuta nikishindwa kujizuia machozi kibao yakaanza kunitoka na kusababisha mama ambaye hakuna na neno sasa lolote la kusema akanisogelea na kunikombatia nakuanza kunifariji.
"Sikia mwanangu kumbuka kazi ya Mungu haina makosa na Mungu ndio mpangaji wa kila jambo na ndio alipanga hivyo itokee" yalikuwa ni baadhi ya maneno ya mama yalionifariji mimi niliyekuwa bado naendelea kulia. Siku ilikatika na kesho yake asubuhi na mapema tukadamka mimi na mama kuelekea kwa rafiki yangu kipenzi samson kwenda katika msiba wake ambao baada ya kufika tukapokelewa na vilio vya hapa na pale kutoka kwa ndugu na jamaa na sisi tukajiunga nao wakiambatana na mamia ya wanafunzi ambao wengine tulihitimu nao kidato cha nne ambacho ilikuwa si siku nyingi tumalize.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni