Notifications
  • THE NIGHTMARE (4)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.“unanipiga mimi?...utaona!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Aliongea Karim na kuondoka huku analia.*****************************Zilipita wiki mbili bila ya Karim kuonekana nyumbani kwao. Sabra alisikitika kidogo kutokana na kuwapenda sana watoto wake japokuwa huyo mtoto mkubwa hakuwa…
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…
  • MY DIARY (50)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA HAMSINITULIPOISHIA...Nilimnongo’oneza kuwa atumie kinga ili nisimwambukize ukimwi akanijibu kwa sauti ya mahaba nisiwe na hofu yeye yupo tayari kufa kwa ajili ya penzi langu hivyo hawezi kutumia kinga kwa mke wake aliyemoa tena siku muhimu kama hiyo.Sikutaka kumbishia yeye ndo muaamuzi wa mwisho kuhusu afya yake hivyo nilimuacha aendelee kufanya yake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kumbe na…
  • MY DIARY (49)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya maneno ya kusilimu ambayo waliambiwa wayatamke kiongozi huyo alisema neno ya mwisho kabla hajashuka.” Kila alie na akili timamu, mwenye busara naa anaetaka haki, na kusimama pamoja na haki, basi akiangalia dunia ilivyo na jinsi inavyokwenda basi lazima kutakuwa na nguvu kuuu nayo ni mwenyezi mungu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuna vitu vingi sana…
  • MY DIARY (48)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NANETULIPOISHIA...Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu…
  • MY DIARY (47)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SABATULIPOISHIA...Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Candy alinisihii sana…
  • MY DIARY (46)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SITATULIPOISHIA...Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya…
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…

MAPENZI NA NGONO (10)

Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
"Wee mtoto upo wapi???,rafiki yako kaja nyumbani kasema leo haujafika twisheni je umekwenda wapi si kawaida yako kwenda sehemu bila ya kuniaga!!" weee mtoto na kupigia simu haupatikana umepatwa na maatatizo gani au ushaanza umalaya??.. heee leo utanitambua sikuogopi huo ukubwa wako unaokudanganya nitakupiga kama una nguvu tupigane na utaniambia ukweli leo umetoka wapi"

TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE

SASA ENDELEA...
Zilikuwa ni baadhi ya messeji za mama zilizonichanganya kabisa na kujikuta nikiropoka kwa nguvu mpaka rukaiya akasikia.
"Leo kazi ipo"......................
"Kwani kuna nini unavyoendelea kunificha unamaanisha nini unajua nishaanza kuogopa pablo baby??" rukaiya akaniuliza swali ambalo lilizidi kunichanganya na kunitia hasira nakujikuta nikimkata jicho kali lililomfanya aniangalia kwa uoga huku akiendelea kutembea kwa haraka haraka kama nilivyokuwa nafanya mimi kutokana na kuogopa kuweza kumuacha.

Kama kawaida niliendelea kushangaa jengo hilo ambalo lilinifanya nijiulize maswali mengi kutokana na Madhari yake kuwa kama tulivyoingia halikuwa likionyesha kama usiku ulikuwa unaingia hakika kulikuwa hakuwezi kutabirika kwa kubashiri muda mpaka uangalie muda katika kifaa cha kuangalia muda kutokana na Mataa yalikuwa yanawaka muda wote.kwa mwendo wa speed nilikuwa nakwenda nao ulifanikisha kupanda lift na kushuka chini huku safari hiyo lift hiyo haikunipa shida nikajikuta nimetulia na lift hiyo ikashuka chini kwa kasi na tukiwa humo ndani ya chumba cha lift hiyo rukaiya alikuwa ananiangalia kwa macho ya huruma kama mtu aliyekuwa anataka kuongea kitu lakini kutokana na hali yangu ilimfanya aogope kabisa kuzungumza na mimi ambaye kwa wakati huo mawazo yote yakiwa nyumbani itakuaje mapigo yangu ya moyo yaliongezeka sana kuliko awali presha ya kwenda kukwaruzana na mama ndio ilikuwa imetawala katika kichwa changu jambo ambalo kwa hakika sikuhitaji kabisa litokee.

Nikiwa bado katika dimbwi zito la mawazo ndani ya chumba kile cha lift nikajikuta nikishtuka badala ya mlio wa lift kulia ikiashiria kuwa muda wa kufika sehemu tulipokuwa tunapataka umewadia na mlango wa lift huo wenyewe ukajifungua na kusababisha watu wengine waliokuwa wanasubiria lift hiyo katika mlango huo ili nao waingie.Mimi bila ya kupoteza muda kwa mwendo wangu ule ule wa haraka haraka kama niko jeshini nikaanza kutembea kwa speed na kuzidi kutesa Rukaiya ambaye wakati huo alikuwa kimya licha ya kuwa alikuwa anatamani kuniongelesha lakini Alikuwa anashindwa kutokana na hali ilivyokuwa inaendelea.

Ghafla nikiwa katika mwendo wangu ule nikajikuta nikimvamia mwanamke aliyeonekana ni mfanyakazi wa mule kutokana na Nguo zake za sare ya hoteli ile alizovaa na kusababisha yeye pamoja na vitu alivyokuwa amebeba vidondoke na kilichonipa angalau hafueni ni kuwa vile vitu vilivyodondoka havikuwa vyombo vya udongo bali vilikuwa ni vitabu vingi vinene ambavyo kama ustarabu huku nikiwa namuomba msamaha kwa kuto muangalia usoni nikaanza kuviokota haraka haraka kutokana muda ulikuwa unakwenda kasi sana.

Baada ya kumaliza kuviokota vile vitabu nikageuka kwa kasi huku bado nikiwa nimechuchumaa kwa lengo la kumpa vile vitu vyake na kumsaidia kumuinua kutokana mpaka muda niliomaliza kuokota vile vitabu bado yeye alikuwa amekaa nakuniangalia.mshangao wa haja ukanikumba baada ya kukutanisha macho na msichana huyo ambaye yeye baada ya mimi kumuangalia naye alishtuka kidogo na kuniangalia kwa muda na kuachia tabasamu la nguvu lilionifanya nianze kumtathimini mwanamke yule ambaye baada ya kuvuta kumbukumbu kwa kasi nikamtambua na kumkumbuka kuwa alikuwa ni mwanamke ambaye alitusindikiza katika chumba alicholipia rukaiya na kutupa funguo baada ya kufika katika chumba kile na kuniacha katika mshangao kwa sababu tangia alivyoniona alikuwa anatabasamu na kudiriki hadi kunikonyeza tulipofika katika chumba alichotupeleka.

Nilimuangalia kwa muda nakujilazimisha kuunyanyua mdomo wangu kwa lengo la kumwambia pole lakini nikajikuta nikishindwa baada ya mwanamke yule tena kunikonyeza na kupelekea mimi kutabasamu pia huku macho yangu yakienda mbali mpaka katika kifua chake kilichosimamisha nido zilizosimama vizuri na kuzidi kumfanya mwanamke yule kuwa na mvuto zaidi kama ukimuangalia.yote yale yalifanyika bila ya rukaiya kujua jambo ambalo lilinifurahisha kisha nikanyanyuka na kumuangalia mwanamke yule ambaye nilimuona akiingiza mkono mfukoni katika sketi yake nzuri nyeusi aliyovaa na kuninyooshea mimi mkono wake aliouingiza mfukoni na kuutoa huku akiwa na lengo la kutaka mimi nimsaidie kunyanyuka Jambo ambalo liliniacha na maswali mengi lakini nikapotezea na kujitutuma kumpelekea mkono wangu uliomuwezesha kumuinua na bila ya uoga yule mwanamke akanifinya mkono wangu na kuniachia karatasi katika ule mkono niliomnyanyua na kuzidi kunichanganya lakini nikajitahidi kuonyesha kama nimemuelewa na kukipokea kikaratasi hicho ambacho sikujia kimeandikwa nini na kukiweka haraka mfukoni.

"Hiyo namba nipigie." kwa sauti ya chini yule mwanamke akaniambia bila ya rukaiya aliyeanza kunisogelea taratibu kusikia na mimi nikaua soo kwa kumuitikia kwa kichwa na kumuangalia kwa muda baada ya kunigeuzia mgongo na kuanza kuondoka na mimi bila ya kuchelewa nikakumbuka kuwa nilikuwa na msala mzito nikageuka na kuanza kutembea kama kawaida na kumuacha rukaiya aliyekuwa ananifata akiwa amesimama pale na kuzidi kumnyong'onyesha kabisa.Baada ya kufanikiwa kutoka nje ya hoteli ile ya serena hoteli ambayo ndio ilikuwa mara ya kwanza mimi kuingia katika hoteli ile bila ya kupoteza muda nikaanza kutafuta bodaboda kwa lengo la kuwai huku kila nikifikiria nyumbani presha ilizidi kupanda na Kushuka huku hofu ikichukua nafasi yake.

"Sasa pablo unataka kuniacha subiri tuchukue taxi."
"Hamna rukaiya wewe chukua taxi mimi nachukua bodaboda nataka niwai kufika nyumbani mapema kuna matatizo kidogo"
"Mmmh matatizo gani mpenzi"
"weee jua kuna mtatizo mbona maswali mengi rukai.." kama bahati kabla hata ya kumalizia sentensi nikaiona pikipiki ikiwa inakuja upande wangu huku ikiwa haina hata abiria jambo lililopelekea mwanaume kuishimamisha pikipiki hiyo na dereva wa pikipiki ile akitii na kuishimamisha na kuanza kuongea naye bei kwa lengo la kunipeleka nyumbani kabisa na kufanikiwa kuelewana naye na mimi nikapanda pikipiki hiyo

"Aaaa wee....pablo sasa unaondoka hata uniagi unajifanya Mjanja??"
"Aaa...dereva endesha basi hiyo pikipiki unasubiri nini??"hakika kwa muda huo sikutaka kabisa kumsikiliza rukaiya ambaye alionekana kukasirishwa na jeuri niliyomfanyia na kutokana dereva wa bodaboda au pikipiki kunisikiliza mimi mteja wake akaanza kuiendesha kwa kasi ya ajabu iliyoanza kunipa matumaini na Kama ningepanda gari ingenigharimu kutokana na foleni kubwa iliyozuka baada ya kufikia mbele kidogo.hakika usemi wa siku ya kufa nyani miti yote uteleza ni msemi ambao ni wa kweli kabisa kwa sababu kabla hata hatujafika Mbali sana pikipiki yetu ama bodaboda kwa jina maarufu ikasimamisha na traffic ambaye baada ya kuomba leseni kwa muhusika na mmiliki wa bodaboda ile akaanza Kuumauma meno na kukaa kimya akiashiria Kwamba akuwa na leseni.........................

Nikajikuta nikipandwa na hasira za ghafla baada ya hali kutokea na kumuangalia dereva yule kwa jicho baya ambalo kutokana na kuwa usiku sidhani kama aliniona.
"Nyie ndio wavunjaji wakubwa wa sheria yani unatembea na pikipiki barabarani bila ya kuwa na leseni haya twende kituoni haraka" yalikuwa ni maneno yaliotoka kinywani kabisa kwa traffic yule aliyetukamata na kutokana na dereva yule kutokuwa na Pesa mfukoni hata pale traffic alipomwambia Ampoze kidogo.Alikubali kupeleka pikipiki hiyo kituoni na Alionyesha kabisa hakuwa na ujanja Mimi nikakuta shauri ya kunyanyua mguu kwa lengo la kuondoka lakini traffic yule hakuniruhusu kuondoka na kuzidi kunipa presha kubwa hasahasa nilipoangalia saa na kugundua kuwa ilikuwa ikielekea saa tatu usiku na ndio kwanza sikuwa na dalili yoyote ya kufika nyumbani.

"Na wewe twende kituoni kwa kosa la kukubali kuendeshwa huku ukiwa haujavaa element je ungepata Ajali?? hilo ndio kosa lako na Lazima uende ukatoe ripoti kwanza kituoni la sivyo kama hautaki presha ya kwenda kituoni toa Elfu thelathini na tano hapo" hakika maneno ya traffic yule yalinichanganya na kunitoa machozi kabisa kwa sababu nilipojisachi mfukoni nilikuwa na elfu sita tu na hata nilipodiriki kumwambia nina elfu tano alikataa kabisa na hata tena nilipojaribu kumuambia pesa zangu zipo katika simu yangu niliyoizima kutokana na kuogopa labda Mama atanipigia simu pia alikataa na kushikilia msimamo wake wa kunipeleka kituoni duu ilikuwa mushkheri kweli kweli na hata nilipojaribu kugoma na kusimamia msimamo wangu na kujitetea kuwa mimi nilikuwa ni mwanafunzi Bado traffic aligoma na kupelekea kunitisha kabisa kama nikiendelea kugoma na kuniambia atanipeleka pabaya zaidi ya pale.

Sikuwa na jinsi nikakubali kwenda kituoni huku machozi yakinitoka sana na kutetemeka pia hii ilitokana na kama nikipelekwa kituoni lazima nitaambiwa nimpigie Mama yangu kuhusu sakata hilo na kupelekea hata kutozwa na pesa pia Maneno yalikuwa yanasemwa na miongoni mwa watu kuwa kituoni kuingia bure kutokana na hela ndio ilinikabili kwa hela gani nilizokuwa nazo daa ulikuwa ni mtihani ambao hata kama mama atakuja kutoa na kuniwezesha mimi kutoka bado maswali mengi yangezuka kwa mama kwamba nimefikaje kule na nimetoka wapi kwa sababu niliaga na kwenda tuition.Safari ikaanza tena Mimi na traffic yule tukapanda pikipiki ya yule dereva asiyekuwa na Leseni na kuanza kuelekea kituoni.Moyo ulizidisha kunienda Mbio hali iliyosababisha nianze kutetemeka sana huku majasho yakinitoka hali ambayo ilionekana kumuogopesha kidogo traffic.

"Wee dereeva hebu simamisha pikipiki yako"Ghafla tukiwa bado hatujafika kabisa kituoni yule traffic akaomba pikipiki isimamishe jambo ambalo sikulitegemea na kujikuta nikibaki tu nikiangalia je mchezo utakuwaje.
"Haya wee dogo unaonekana Muoga Sana haya nipe hiyo Elfu tano fasta uondoke Kwenu Usiku mnene huu"

Bila ya hata kutegemea traffic akasema vile na kufanya hata nisitegemee na kubaki nikiwa siamini amini hali ile kwa haraka haraka nikatoa ile hela huku nikitetemeka na kumkabidhi yule traffic ambaye baada tu kumkabidhi huku nikiwa tayari nishashuka nikamuona akirudi kupanda pikipiki ile tena kwa sababu alishuka na kuamuru dereva aendeshe jambo ambalo haraka dereva aliitia na kwa haraka wakaondoka na kuniacha mimi palepale huku nikiwa hali siamini amini kabisa kuwa nimeponea katika tundu kubwa la sindano na kujikuta nikishusha pumzi zito la furaha huku kukiwa na hali ya uoga yenye hofu iliyokuwa inazidi kuongezeka kila sekunde iliyokuwa inaongezeka.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU

Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho


27 Mapenzi na Ngono Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni