MAPENZI NA NGONO (11)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Bila ya hata kutegemea traffic akasema vile na kufanya hata nisitegemee na kubaki nikiwa siamini amini hali ile kwa haraka haraka nikatoa ile hela huku nikitetemeka na kumkabidhi yule traffic ambaye baada tu kumkabidhi huku nikiwa tayari nishashuka nikamuona akirudi kupanda pikipiki ile tena kwa sababu alishuka na kuamuru dereva aendeshe jambo ambalo haraka dereva aliitia na kwa haraka wakaondoka na kuniacha mimi palepale huku nikiwa hali siamini amini kabisa kuwa nimeponea katika tundu kubwa la sindano na kujikuta nikishusha pumzi zito la furaha huku kukiwa na hali ya uoga yenye hofu iliyokuwa inazidi kuongezeka kila sekunde iliyokuwa inaongezeka.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Bila ya kulaza damu nikaanza kukimbia mbele kwa lengo la kupanda gari lolote ambalo litakalopita mbele yangu jambo ambalo kama Mungu tu haikuchukua hata dakika gari la kuelekea kwetu likapita na nilipolisimamisha likasimama na mimi nikapanda haraka haraka gari ambalo hakika sikuamini kama lingesimama kutokana lilikuwa tayari limejaa abiria na kusababisha baadhi ya watu kusimama tena kwa kubanana.Kutokuwa na foleni kulisaidia kwa kiasi kikubwa safari yetu kusonga licha ya kuwa gari letu lilikuwa likisimama simama kila lilipokuwa linafika katika vituo tofauti jambo ambalo lilikuwa linanikera sana.Simu yangu niliona sumu sana kama kituo cha polisi kwa sababu kama ningeendelea kuangalia ingenipelekea kuangalia saa na hata kupigiwa na Mama ambaye mpaka muda sikujua nitamdanganya vipi ili aweze kunielewa kama nilikuwa nimetoka wapi na kilichoharibu zaidi ni yule rafiki yangu aliyekuja kuniulizia nyumbani kama messeji ya mama ilivyosema.
"Eee Mungu Ahsante" Nikajikuta nikimshukuru Mungu baada ya kufika kituo cha karibu ambacho Vilibaki vituo viwili tu nifike nyumbani na kuanza kujipa matumaini Huku mara kwa mara nikiwa najuzia kuangalia saa iliyokuwepo mbele katika kioo cha dereva ambacho kilikuwa kinaonyesha ilishaingia saa nne usiku kwa wakati huo.Nikiwa katika hali ya Matumaini zaidi Baada ya gari yetu kubakisha kituo kimoja tu cha mimi kufika nyumbani huku gari ikiwa inaenda kwa mwendo wa kawaida Ghafla Tukasikia Mlio mkali wa speeda ya gari kusikika karibia kabisa na gari yetu hali iliyosababisha kila mtu angalie nyuma na hata watu walikuwa wamekaa wakasimama kuangalia je nini kinaendelea kwa gari inayokuja nyuma yetu Bila hata ya kutegemea hali ambayo ilinifanya nitumbue macho makali sana Hii ni baada ya gari lile moja kwa moja likavamia gari letu na Kutugonga kwa Nguvu hali iliyozua mtafaruku mkubwa ndani ya gari letu
"Maaaaaaaaaaaaaaaaaaaamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa"
Ilisikika sauti ya mama mmoja ambaye alipata mshtuko mkubwa na kujikuta akipiga kelele kubwa na kuzimia papo hapo baada ya ajali ile iliyosababisha kioo cha nyuma ya gari letu lile kupasuka chote na Kuwamwagia abiria waliokuwa nyuma ya siti ambao wao ndio waliokuwa wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na ajali ile ambayo haikutegemewa kabisa na watu.Baada ya kugongwa na gari lile lililokuwa speed ambalo baada ya kutugonga lilibaki palepale na gari letu pia likabaki palepale pia baada ya dereva kufunga breki kali iliyosababisha pia abiria waliokuwa wamesimama nikiwemo na mimi kuyumbayumba kisha tukadondoka.hakika mshtuko ule tuliopata ulifanya watu karibia wote wafe ganzi hata mimi pia nilikuwa nipo chini baada ya kudondoshwa na breki kali aliyofunga dereva kwa lengo la kuzuia ajali nyingine na Abiria waliokuwa nyuma wote wakazimia si dereva wala kondokta hakuna aliyeshuka kimya gafla kikatanda na kufanya kama hakukuwa na watu ndani ya gari lile.
Haikuchukua dakika nyingi gari la kutoa huduma ya kwanza likawasili likiambatana na gari la Mapolisi ambao nahisi waliitwa na watu waliokuwa wameshajaa pale wakiwa wanatuangalia kwa mshangao ambao hakuna hata mmoja aliyediriki kuja kutuangalia.Nguvu ya mapolisi na wale wa hudumu wa kutoa huduma ya kwanza hakika walifanya nguvu ya ziada kutoa huduma nzuri haraka haraka na kusababisha miongoni mwa watu kuwa sawa na kuwachukua baadhi waliokuwa taabani zaidi.hata mimi baada ya Nguvu kurudi sikupoteza muda kwa sababu nilikuwa sijaumia sehemu yoyote bali ulikuwa ni mshtuko tu ndio ulisababisha niishiwe nguvu Kwa mwendo wa kukimbia haraka haraka nikaanza kuitafuta nyumbani muda huo huku hofu iliyoipotea na kuongezeka hofu ya ajali ikanirudia tena moyo uliongezeka kama kawaida kunidunda zaidi kila hatua niliyokuwa nikipiga kwa mwendo wa kukimbia.
Nikajikuta nikishusha pumzi ndefu za kuhema baada ya kufika nje ya nyumba yetu ambayo Nilikaribishwa na mataa ya ndani kwetu yaliyokuwa yanawaka.Kitete kilizidi kupanda majasho yalizidi kuongezeka yakisaidia na yale ya kukimbia Kwa hali ya uoga niliyokuwa nayo nikaanza kuomba Mungu aweze kuniokoa kwa hali ile ambayo sio siri kulikuwa na Asilimia ndogo kabisa ya kutopigwa na Mama ambaye nilihisi atakuwa na hasira kali sana dhidi yangu.Nilinyonga kitasa cha mlango wa geti kwa staili ya aina yake na kufunguka bila ya kupiga kelele nakuingia ndani kwa mwendo mdogomdogo na kuelekea katika mlango wa kuingilia ndani kabisa na nilipofika pale pia bila ya kusita na kwa hali ya kujiamini nikaifungua mlango ule na kuingia.
"Eee..Mungu baba nisaidie"Nilisema maneno yale huku nikipiga hatua ya kuelekea sebureni kwa mwendo ule ule wa taratibu lakini kilichonisangaza kwa wakati ule ni ile hali ya kujiamini ambayo sikujua ilitokea wapi.
"Weee Mwanaizaya Njoo hapa umetoka...wapi nambie umetoka wa......."Paaaaa!!!"yalikuwa ni maneno ya mama ambaye kabla hata ajamalizia alinisogelea kwa kasi ya ajabu na aliponifikia akanitandika kibao kikali cha uso kilichosababisha nianze kuona nyota huku shavu langu kulihisi kabisa lilikuwa ni zito kabisa.mama hakuishia pale alikamata shati yangu na kunikunja shingoni na kuniongeza kibao kingine kilichopelekea sasa machozi yakianza kunilenga na kujikuta nikiangalia chini baada ya kuona mama akiwa ananiangalia kwa macho makali na ya kuogopesha.
"Wee leo lazima nikufumue kama vipi unajiona una nguvu tupigane umetoka wapii mshenzi wee au ushaanza umalaya eee si nakwambia nijibu basi ushaanza umalaya??saa tano hii usiku huu umetoka wapi Maana tuition haujaenda maana rafiki yako kaja hapa nyumbani kausema haukufika Wakati hapa nimekupa pesa ya shule na umeniaga unakwenda tuition nambie umetoka wapii??"
"sasa Mama sawa ni haki yako na ni lazima kuniadhibu ninapokosea lakini kabla hata ya kuniadhibu mama yangu ulitakiwa kuniuliza nimetoka wapi usiku huu na utakapo ona makosa yangu ndio uniadhibu nishakuwa sasa Mama ningekuambia bila ya kukuficha unajua kabisa mimi mwanao sina tabia hizo ona sasa ulivyokasirika unavyo hema mama umesahau kama wewe una presha na inakusumbua."
Hakika sikujua kabisa kwamba ningeweza kusema maneno yale ambayo yalionekana kabisa kumuingia mama ambaye aliacha kunikunja na kuniangalia kwa umakini kidogo na kuonyesha sura ya huruma ambayo katika nafsi yangu niliona ule ndio ushindi wa kwanza wa kumueleza mama kwa lengo la kujitetea ili asifike pabaya.Baada ya kusema maneno yale mama akageuka nyuma na kunishika mkono na Moja kwa moja tukaenda mpaka katika makochi na kukaa sofa moja ambalo mama aligeuka na kuanza kuniangalia na kuonyesha kabisa shauku ya kutaka kujua ilikuaje mimi kurudi Nyumbani muda ule.Nilipiga funda la mate mdomoni kama mtu aliyekuwa anakunywa kinywaji na kumuangalia mama ambaye alikua ananiangalia kwa umakini wa hali ya juu sana.
"Ni kweli kwamba leo sikuenda tuition kama nilivyoaga kwa sababu wakati naelekea huko nilipofika stendi hapo nikakutana na Rafiki yangu steven ambaye alinishawishi tukafanye mtihani shuleni kwao hakika maa sikuweza kukataa kwa sababu niliona ni moja kati ya kujipima hasahasa ili kujua uwezo wangu upo wapi ndipo nikaongozana naye mguu kwa mguu mpaka shuleni kwao Pale kinondoni Mwebe jini lakini tukiwa tupo barabarani maana tulikuwa tunatembea kwa miguu kwa sababu sio mbali tukapita njia moja Ambayo kulikuwa na mateja wanaovuta unga kabla hata hatujamaliza kuingia defender ya mapolisi ikaja na kutukamata pale wote na kuwachuka mateja wale wanaohusika wasiohusika wotee tukakamatwa na kupakizwa kwenye defender tulijaribu kujitetea wee ikashindikana mwezangu akatoka mapema baada ya kuwapa Pesa na mimi nikawapa yangu ya tuition ndio wamekuja kunitoa Saa mbili usiku mama"
"Mmmh Aisee poleni sasa mbona hakunipigia simu??"
"Hamna mama simu yangu niliificha maana wale waliokuwa na simu wote walinyang'anywa"
"Sasa mmetolewa saa mbili usiku mbona umerudi saa tano mwanangu??"
"Aaa...mama nilisahau kuna ajali imetokea hapo kati nahisi taarifa ya habari itaonyeshwa na Mimi nilikuwepo lakini hakuna aliyeumia sasa ile ilisababisha tuzuiliwe na mapolisi halafu foleni ikawa kubwa sana ndipo nilipoamua kutembea kwa mguu mpaka hapa"
"daa jamani mwanangu pole haya ngojea nikakuwekee maji ya kuoga uoge kisha ule halafu Kesho baba tunaenda kwa rafiki yangu Mama rebecca tabata"
Hakika sikuamini kwamba mama angeweza kupoa bila hata ya kuniuliza sana Nikamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia kutokumbwa na balaa la kupigwa na Mama ambaye alikuwa na hasira kali.Nikaoga baada ya kumaliza kuoga kama kawaida nikakuta mama kashanitayarishia chakula ambacho nilikifakamia kwa hasira kutokana na njaa kali niliyokuwa Nayo kisha nikaenda kulala nikiwa na Mawazo juu ya safari ya kesho yake aliyoniambia mama.Hakika sikutaka hata kugusa simu yangu niliiacha vilevile imezimika kutokana na kuogopa labda rukaiya anaweza akanipigia au zureiya ambao wote sikujisikia hata mmoja kuongea naye.
Hakika siku ile ilienda haraka sana kuliko hata nilivyotegemea kuwa nilipopatwa na usingizi tu nilikuja kushtuka baada ya Mama kunigongea Mlango ikiashiria kuwa ilishafika Asubuhi.Kama kawaida yangu nilijitayarisha na nilipomaliza nilikuta Mama tayari kashajitayarisha na ananisubiri.Safari yetu ilikuwa njema kabisa ndani ya Masaa mawili tu tulifika kwa Mama rebecca tabata mama ambaye alitukaribisha vizuri katika jumba lake ambalo sio siri lilikuwa jumba zuri na la kisasa lililosababisha mpaka mimi kushangaa shangaa jinsi lilivyokuwa limependeza
"Shoga umejitahidi kujenga wewe na mumeo daa"
"Hamna mama pablo mbona kawaida vp lakini Biashara zako maana muda Enhe na wewe Pablo haujambo"
"Ndio Mama rebecca" ghafla tukiwa katika mazungumzo mimi na Mama rebecca nikasikia sauti tamu na nzuri ya msichana akiimbia huku akija pale sebuleni tulipokaa na kusababisha mimi nikae kwa umakini kumuangalia ni nani aliyekuwa anaimba.
Nikiwa katika hali ya sintofahamu Msichana Mmoja mrembo Akatokea pale sebuleni akiwa kaachia tabasamu pana lililothibitisha kuwa alikuwa ni mzuri kweli kweli Ngozi yake nyeupe ilitosha kabisa kumfanya aonekane mrembo hasahasa na umbo lake ambalo kama mwanaume lijali akimuangalia Basi atatamani kufanya naye Mapenzi kutokana na umbo lake la Namba nane huku akisaidiwa na Mzigo mkubwa nyuma ambao uliniacha hoi na kufanya ukorofi katika sehemu yangu ya Mashambulizi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni