MAPENZI NA NGONO (2)

0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
"Pouwaaa hebu nipe namba yako ili tuongee vizuri leo" Hakika mafanikio ya kumpata zureiya msichana ambaye sio siri uzuri wake ndio ulinipagisha ukanijia kichwa changu huku nikimtumia halima ambaye aliniambia kuwa alikuwa ni rafiki wa karibu ndio ulinifanya nijipe moyo.

TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE

SASA ENDELEA...
Hakika siku hiyo iliishi haraka sana huku katika siku hiyo nikiwa shule mawazo juu ya zureiya ndio yaliniandama sana kichwa changu huku kila nifunguapo daftari kwa lengo la kusoma niliiona picha yake kubwa katika daftari langu na kunifanya nishindwe kabisa kusoma.saa ya kuondoka ili wadia huku nikiendelea kumkumbusha halima kuhusu inshu tuliyoongea na kuniahidi ikifika saa mbili usiku ndio atakuwa naye na kunifanya nijiandae.nikafika nyumbani nikiwa na shauku kubwa ya kusubiri saa mbili kufika.kama ilivyohada mida ya saa mbili kama na nusu hivi mlio wa simu yangu ukaita na kunifanya niache kula na kwenda kuikimbilia simu yangu na kuona jina la halima katika kioo cha simu yangu.kwa hali ya kudunda kwa moyo nikajikuta nikiipokea huku mapigo yangu ya moyo yakienda kasi sana

"Haloo pablo"
"halima vp"
"Pouwa basi huyu hapa zuu kama vp ongea naye"nikiwa na shauku kubwa la kusikia sauti yake ghafla simu yangu ikazima na kutokana na kuisha chaji.nilijikuta nikipandwa na hasira huku nikijilaumu na kwenda kuichomeka simu yangu katika chaji lakini kabla hata yakuichomeka simu yangu chaji umeme ukakatika na kunifanya nizidi kuishiwa nguvu huku nikienda njee na kukuta umeme kote umekatika

"Daa tanesco hawa maboya kweli"Nilijikuta nikiwalaumu tanesco huku muda mwingine nikijilaumu mimi kwa kusahau kuweka simu yangu katika chaji.Nikiwa katika shauku kubwa ya kusubiri umeme lakini mpaka mida ya saa tano usiku umeme ulikuwa bado haujarudi na kunifanya Nilale siku hiyo nikiwa na manung'uniko makubwa kutokana malengo yangu ya kuongea na mtoto mzuri zureiya kuanza kuingiwa na vikwazo vidogovidogo.kama kawaida tena Asubuhi na mapema nikaamka nakukuta umeme usharudi nikachomeka simu yangu chaji kisha nikaenda zangu shule.halima hakusita kunilalamikia kuhusu suala ya kukata simu huku akinilaumu na kutosikiliza maneno niliyokuwa najitetea.

Furaha kubwa alinionyesha halima Alinipa namba yake ya simu nakunifanya furaha yangu izidi kipimo na kumkombatia jambo ambalo yeye lilimsisimua na kubaki akiwa ananiangalia kwa macho ya kulegea kisha nikamtoa buku mbili ya kama kumpa pongezi kwa kuweza kunipa namba.Siku hiyo nilichelewa kurudi shule kutokana na kazi za kufanya kuwa nyingi za kufanya masahihisho ya mtihani tuliofanya siku hiyo.ilipofika mida ya saa mbili nikaichukua simu yangu na kuichukua namba ya zureiya iliyokuwa nimeiandika katika daftari langu nikaisave katika simu yangu kisha kwa hofu kubwa yenye kusababisha kudunda kwa moyo nikaipiga. Nilipiga namba hiyo ambayo iliita tu lakini haikupokelewa kama Mara tatu na kunifanya nibaki katika hali ya unyonge.Nikiwa katika hali ya mawazo yaliochukua nafasi kama nusu saa Mlio wa messeji ikasikika katika simu hali ilionifanya kwa haraka haraka nifungue sms hiyo

"We nanii kwani mbona usiku"Nilijikuta nikinywea baada ya kusoma messeji hiyo.nikiwa katika harakati ya kujibu messeji hiyo simu yangu ikaanza kuita na Nilipoangalia jina ilikuwa ni namba ya zureiya.kwa hali ya hofu kutokana na kuhisi yaweza kuwa labda mzazi wake nikaipokea
"hallooow...........

"Halloow we nani Mbona unanisumbua."
"m..imii....pa..b..lo rafiki yake halima"Nilimjibu zureiya aliyeonekana kuwa na ukali kidogo kwenye kuongea.baada ya kumjibu ukimya mzito ukatalawala kama dakika moja huku kila mmoja akionekana kuogopa kumuanza mwenzie
"O..oo..kumbe wewe..enhe nambie"
"Mzima wewe zureiya"
"yeah mimi mzma lete story wangu"
"Daah una sauti nzuri sana"
"Hahaahha jamani kawaida mbona sasa sikia nikuambie kitu mimi nakuawaga free kuanzia Ijumaa so usiku mwema wangu nicheck kuanzia siku hiyo"
"Ooo daah nawe pia".

Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwangu kutokana na kuongea na msichana niliyetokea kumpenda ghafla bila ya kutegemea huku kupata fursa ya kuongea ilikuwa ni kama bahati sana katika maisha yangu.furaha yangu sikusita kuionyesha kwa halima baada ya kwenda shule huku nikimuahidi kuwa ninaweza kumpata kutokana na kuongea Naye vizuri halima akusita kunipongeza kwa hatua niliyopita huku akinisisitiza na kuniambia tabia nzuri za halima.Hakika sikusita kusubiri kwa shauku kubwa baada ya kufika ijumaa ambapo ndani ya mida ya saa mbili usiku nikaweka salio na kuanza kumpigia zureiya huku nikiwa na shauku ya kuongea naye.Simu iliita sana mpaka ikakatika lakini sikusita kuendelea kumpigia huku nikiamini atakuwa labda yupo bize na kazi zake za nyumbani.Nikiwa katika hali nyingine ya kupiga ghafla sms ikaingia na nilipoiangalia ilikuwa ni ya zureiya nikajikuta kwa haraka haraka nikiifungua huku nikiwa na utayari mkubwa wa kuisoma messeji hiyo

"WE NANI?? NAKUOMBA UKOME KUNISUMBUA UMENISIKIA PLEASE NAKUOMBA NINA MUME WANGU NIPO NAYE PLEASE USHINDWE" nikajikuta Naanza kulengwalengwa na machozi kutokana na messeji hiyo iliyotumwa na Zureiya jambo ambalo lilinifanya niishiwe nguvu.nikajikuta nikizima simu yangu na kupanda kitandani huku nikianza kutokwa na machozi kutokana na kumpenda sana zureiya.hakika hali ilikuwa mbaya kwa upande wangu baada ya kuendelea kujibiwa majibu mabaya na zureiya ambaye alikataa katakata kuipokea simu yangu huku akinikataza kabisa kumpigia simu na kumtumia messeji.

Hali ile ilinitia unyonge huku nikishindwa kabisa kumueleza ukweli Halima ambaye kwa mara kwa mara alikuwa akiniulizia kuhusu maendeleo yetu mimi na zureiya jambo ambalo lilizidi kuninyong'onyesha na kunifanya nishindwe kujuzuia na kujikuta nikimuhadithia mchezo mzima halima ambaye alionekana kuhuzunika na habari hiyo na kuniahidi kunisaidia huku akiniambia shughuli nzima ataicheza yeye.siku nyingi zikakatika huku halima naye kuwa bize na masomo kwa sababu kilikuwa ni kipindi cha mwezi wa sita kipindi cha mtihani sikuendelea kumsumbua kutokana na hali hiyo.baada ya kumaliza mitihani tukafunga shule na sisi form Four tukipata likizo fupi kutokana na kujiandaa na mtihani.Nikiwa katika likizo hiyo siku moja usiku nikapigiwa simu na halima ambaye alionekana na furaha kuongea na mimi huku akiwa na taarifa kubwa ya kuniambia.

"Pabloo ee zureiya anataka kuongea na wewe Jumamosi Njoo Nyumbani" habari hizo za janeti zikanitia uoga mzito sana huku nikiwa na tahadhari kubwa ikanibidi niendee kufanya shopping kariakoo na huku nikijipanga kwenda kuonana na Zureiya.siku zilizidi kwenda haraka huku mawazo yakiendelea kunitawala kichwa changu kutoka na kuwa na bahati mbaya ya wasichana nikiwa katika umri wa miaka kumi na nane nilishatongoza wasichana karibia kumi na kuishiwa kukataliwa vibaya vibaya na jambo lilikuwa naliofia na kukataliwa na zureiya na kuamini kama nitakataliwa basi litanitesa sana na kuniaribia hata masomo yangu kutokana na ukweli kwamba zureiya alikuwa ni msichana ambaye namuhitaji
"Daa sijui itakuaje.".......

Siku ya miadi ikafika na Asubuhi na mapema kabisa nikajiandaa kwa kumaliza kufanyafanya kazi za nyumbani ambazo nilizozizoea kufanya kisha mida mida ya kama saa sita nikaanza kujiandaa.kabla hata sijamaliza kujiandaa messeji katika simu yangu ikaingia na nilipoisoma ilikuwa ni ya halima
"Oy fanya fasta basi kuja"nilikuwa naingalia angalia sana messeji hiyo huku moyo ukinienda mbio hofu kubwa bado iliendelea kutawala katika nafsi yangu huku nikiwa na Asilimia ndogo kabisa ya kukubaliwa.Bila ya kuchelewa nikamuanga mama kuwa ninaenda kwa rafiki yangu kisha kwa haraka haraka nikawai stendi na kufanikiwa kupata gari lililojazaa jambo lililosababisha kutokaa baadhi ya vituo kutokana na gari hilo kujaa watu wengi.

"konda moroko shusha"kwa kujiamini kabisa nikamwambia konda na kumpa nauli huku nikiwa nimebanwabanwa na watu na kushuka salama baada ya kushuka nikatulia kidogo pale kituoni na kuanza kujiangalia angalia na kujiweka vizuri kutokana na siku hiyo kuhisi kama nimependeza licha ya kutosifiwa na mtu yoyote mpaka nilipofika pale hata mama aliishia kuniangalia bila ya kusema chochote.kwa mwendo wa haraka haraka nikaanza kukatiza mitaa huku nikiwa na hofu sana na kuangalia kila sehemu zilizokuwa na vioo na kujiangalia angalia.Nilipoanza kukanyaga mitaa ya akina halima ndipo moyo wangu ulipozidi kunienda mbio sana huku nikijaribu kujiweka hali ya kujiamini kwa kuongea maneno ya kuwa mimi mwanaume ili niondoe hali ya uoga.nilifika mpaka katika umbali kidogo na nyumba ya akina zureiya nakuanza kuangalia angalia huku nikichukua simu yangu na kuanza kuitafuta namba ya halima kwa lengo la kumpigia.

"Pablooooooooo"sauti kutoka nyuma yangu ikanishtua na kunifanya nigeuke na kumuangalia aliniita na kumuona halima aliyekuwa katika hali ya kutabasamu kisha akanisogelea na kunishika mkono kisha nakuuanza kutembea naye kwa kumfuatisha kila sehemu anayopita.kwa kupitapita vichochoro kwa mwendo mfupi safari yetu ikagota katika kibaraza kilichopo katika kichorochoro hicho ambacho kilichokuwa akina pita pita nyingi za watu.katika kibaraza hicho nilimuona mrembo mkali aliyekuwa akiniangalia baada ya kufika ambapo baada ya kuvuta kumbukumbu ndio nilipogundua alikuwa si mwingine bali ni zureiya mrembo ambaye kama ukimuangalia huto gundua mapungufu yake katika urembo wake na uzuri kama ukimuangalia.Nikiwa katika hali ya hofu nilitoa tabasamu hafifu na kumuangalia zureiya ambaye pia naye akaachia tabasamu zito lenye madimpozz mashavuni na kunifanya nizidi kuingia.

"Jamaani eee acheni niwaache nakuja sasa hivi" halima aliaga kwa haraka haraka kisha kwa sauti ya chini chini ambayo zureiya hakuisikia akanambia muda ndio huu maliza sasa kisha akaondoka na kuniacha mimi nikiwa bado nimesimama.nikajizoa zoa na kukaa na kumsogolea zureiya aliyekuwa anaangalia pembeni kisha bila hiyana nikaanza kuanzisha mazungumzo.
"Mambo vp zureiya"
"Pooua palo nambie"
"Haha jamani sio palo ni pablo bana"
"Hahaha sawa pablo nilisikia una shida na mimi haya nambie sasa nakusikiliza"
"Oouk pouwa unajua nini yani tangia siku ya kwanza nilipokuona sio siri nilitokea kukupenda sana yani ni...n..lijikuta tu nakupenda kutokana na muonekana wako ulivyo unaonekana mkarimu,mstaarabu yani nimekupenda."
"hmmm pablo unanichekesha sana jamani sasa hivyo mkarimu sijui mstaarabu umevijuaje wakati haunijui kiundani??"
"Aaa yani siku ya kwanza tu nilipokuona niliviona katika ndani ya moyo wangu kupitia macho makali yenye kuchuja kizuri na kibaya hebu nakuomba nijibu unanipenda au unipendi zureiya au nikupe muda??"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU

Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)