WEKA YOTE (11)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Na ni muda mrefu hivyo alikuwa kama raia wa tanzania, tulipenda sana ufundishaji wake hivyo tulimpenda pia yeye kwa upole wake japo muda mwengine anakasirika na kutuchapa ila sio kwa sifa kama sir fulani, tulipenda kuficha uovu wa sir lusinde kwa kutimtaja tukiwa kwenye story zetu hasa tunatumia jina la sir fulani.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Somo lilianza topic ya kwanza life skill ndio tupo, alianza kudadavua hasa mambo ya uongozi, aliendelea na somo huku akikimbizana na muda hasa kwani muda wake ulikuwa mwisho kuisha hivyo akaacha tu maswali akiyoandika ubaoni na kuondoka baada ya kutuaga.
Yapata saa sita muda huo lunch inakaribia, nilicopy maswali na kuanza kuyafanya nikiwa nafanya mara Grace akaja pale nilipokaa tena na kiti chake kisha akaa.
"Mambo gao."
"Poa ."nilijibu kama sitaki.
"Mh,mzima wewe."
"Niko poa."
"hivi sir alikuchapa"
'Sir nani.?"niliuliza kama sijui vile.
"Jamani yani umemsahau.!"
"sir nani sasa."
"Lusinde."
"Hapana."niliendelea na majibu yangu yale yale ambayo sikujua Grace anayachukuliaje.
"Sawa mwaya ngoja niende, aaah nimekumbuka leo naomba uje jioni tutoke wote gao."alisema huku akiwa kasimama.
"Jionii.!"Niliuliza kwa kushaangaa.
"Mbona hivyi jioni ndio."
"mh haya."nilijibu tu kwa mkato hali ikiyipelekea Grace kutokuvumilia akaondoka, alijua fika kosa alilofanya hivyo najua alikuwa akitafuta njia ya kujirudi kwangu.
Niliendelea na kazi zangu mpaka kengere ya lunch kugogwa kisha tukaelekea nje, tulitoka wanafunzi nje muda huo tukizongana zongana wenyepesa wakienda kula chakula kinachouzwa kwenye mgahawa uliopo shule.
Hatimae muda ukaisha tuliingia dalasani na harakati kuendelea msaa nayo yakitutupa mkono kila mtu akiwa busy na mambo yake, kimya kilitawala baada ya saa lusinde kuamrisha tunyamaze hivyo wote kimya tukakaa mpaka muda unaisha ikagongwa kengere ambayo wanafunzi wote tulijua fika ni ya lala salama yani ya mwishi ili tuelekee majumbani mwetu.
Tulifika paredi kusikiliza matangazo, Grace alikuwa ananitazama tu akijua nitamsubir tuongozane kumbe laaah sina mpango huo.
Matangazo yalifika tamati tukaruhusiwa na mimi nikaawahi kuondoka nikiongozana na kidato cha kwanza.
Tukiwa njiani ndipo walianza, michezo yao ambayo siipendi kabisa walianza kufukuzana fukuzana huku na huko huku wakicheka.
"Samahani kaka,"alinikanyaga mmoja na kuomba msamaha kusema kweli nilikereka mno ila nikachukulia ni watoto bado.
Niliwapita wale nikachepuka mbele huko napo hivyo hivyo, kweli watoto ni watoto tu walitembea kwa kushikana mikono na kuziba njia nzima, kila nikitaka kupita wanaziba mara ya kwanza ya pili ya tatu.
"Aaah sogeeni njiani bhana ni lazma mshikane."nikisema kwa jaziba hapo wakaachiana na kukaa kando na mimi nikapita na kutembea hatua ndefu hadi kufika nyumbani nikaingia kulikuwa kimya hakuna niliyemuona sijui ni kutokana na mimi kuwahi kurudi muda huo, niliingia chumbani kwangu kubadili nguo, dakika mbili zilitosha kabisa nikabadili na kutoka kwa ajili ya kula hali ilikuwa vivyo hivyo sikuona mtu.
Nilijipakulia na kuanza kubugia upesi upesi ili nikatembeee nilikuwa tayari na kududumia maji ya baridi kisha safari ya kwenda kuzurura ikaanza.
Nilitoka mpaka nje, nikapanga kwenda kusabahi marafiki mana ni kitambo hatujaonana njiani nilitembea huku nikiimba nyimbi zozote zinijiazo kichwani.
"Gao yule pale ngoja nikuitie sawa."nilisikia sauti kwa mbali ikinitaja ndio nikageuka kuangalia nikamuona ni mkali yule rafiki yangu akiwa na msichana aliejazia maungo hasa nyuma.....
Sauti ile iligonga ndani ya ngoma za masikio yangu nilipo waangalia wao hawakuniona kutokana na kuangalia mara moja tu na kutizama pembeni, sikupenda kuwafata hivyo hata mkali alipo thubutu kuniita sikushawishika hata kumuangalia kabisa niliendelea na safari yangu nikitokea nyumbani,nilizunguka mitaa kadhaa nikiwa sina hata sababu iliyonipelekea kutembea ila kwa lugha nyengine naweza kusema ni hali ya kunyoosha miguu tu ndio kikichofanya nipoteze muda kuzunguka.
Kutokana na muda mrefu kutokutembea hiyo nikutokana na kutoka shule muda mmbaya hivyo sehemu nyingi nilikuwa sijatembea nilichukua muda huo kuzunguka zunguka hadi kufikia maskani kwa jamaa zangu, nilijumuika nao.
"Aaaa gao vip niaje mwamba upo."alinichangamkia mmoja wapo.
"niko poa tu nambie."
"Safi dogo mishe"
"safi kaka"tuliendelea na kusalimia, kisha story nyengine zikaendeleaa kijiwe kilinoga na story za hapa na pale.
"Mnamjua yule dogo flani hivi mnene kidogo aliejazia hips na bonge sambwanda mnajua,?"aliuliza jamaa mmoja katika kijiwe pale.
"Nampata yule anaekaa kwa yule mzee anaependa sana kusoma magazeti"
"Ndio huyo huyo bhana."ni maongezi yalioendelea kijiweni pale hapo mimi nikiwa msikilizaji mana sikuwa na cha kuchangia.
"Mwanangu yule demu achaa."aliongea kwa kuhamaki jamaa mmoja.
"Ana nini yule demu, mana nasikia ni moto."aliitikia mwengine,
"Yule demu achana naye juzi jamaa wamempiga mtungo wa mchangio."
"Aaah wapi huko jamaa,"waliendeleaa kuongea huku kila mmoja akionesha kushangaa sana.
"Aaah acha mwana mchopanga si unampata sasa yule nawenzake kama watano hivi yani mpaka demu kakimbia kaacha chupi palepale."
"teh,teh,teh,teh,teh,teh,aaah kakomeshwa . hahahaha"
Waliongea kwa kucheka.muda huo giza ndio lilianza kumea hivyo sikuendelea kukaa pale nilitumia muda huo kuaga kisha nikaondoka.
Nikiwa njiani nilitembea hima hima kuwahi giza lisije nikuta njiani nilitembea mwendo wa kijeshi jeshi, mpaka kufika nyumbani tayari nikaingia ndani na kufunga mlango, hapo shangazi na wanae nikawakuta wamekaa sebuleni nilisalimiana na shangazi kisha nikaingia ndani kwangu kuweka vitu vya shule sawa, vile naingia ndani nilikumbuka kitu.
"Aaaah, namba ya yule dada duuuh nilimsahau"nilikumbuka namba ya dada alietaka kunigonga na gari yake, ambayo haikuwa mbali niliiweka juu ya meza ndogo iliyopo chumbani kwangu. Baada ya kuichukua sasa nilifikilia pa kupata simu ya kumpigia sikupata jibu nilifikiria simu ya shangazi nimwibie ila sikuona kama ni sawa, tangia hapo sikupata jibu la wapi nitapata simu ya kuongea nae nilifikiria majibu hakuna nikairejesha mahala pake nilipoitoa ili kumbu kumbu isitoke mwishowe nikaipoteza kabisa.
Baada ya muda nilipomaliza kazi iliyoniingiza chumbani nikatoka na kukaa sebuleni na wakina doreen na careen, watoto waliofana karibia kila kitu cha mwilini kasoro sauti tu.
"Shangazi kaenda wapi."niliuliza hapo moja moja akanijibu doreen. "Mama kaenda kuoga,"
"ahaa, sawa"nilimwitika, kisha nikakaa kimya kuendelea na utazamaji wa runinga.
"Kaka gao, hivi una miaka mingapi"aliuliz careen swali ambalo sikujua anauliza kwanini. KIukweli walipenda kuniita kaka ila maumbile yao na yangu yana shadadiana hasa kimo changu ni kama chao sikuwazidi ila walipenda kuwa wadogo kwangu.
Swali lile lilinishinda kidogo kujibu, hapo sikuwa nasababu nikauliza tu na mimi mana kuna namna tatu za kujibu swali ya kwanza swali kwa swali ya pili swali kwa maelezo ya tatu ndio swali kwa mkato yani unajibu kwwa mkato mimi sikutaka kujibu kwa mkato au kwa maelezo nilijibu swali kwa swali.
"Kwanini unaniuliza .?"
Nilimpachika na yeye swali lake.
"Amna nimependa kukuuliz tu nijue."alinijibu ki aibu aibu hapo hata majibu yake hayajajitosheleza hivyo nilipata mashaka siku mjibu nikamjibu vyengine kabisa.
"bas usijari nitakuambia siku moja."nilisema huku nikiendelea na kuangalia runinga.
"We naye careen maswali gani hayo unamuuliza kaka"alijibu, doreen. Hapo careen akanyamaza kimya kika tawala zilipita dakika kama tano hivi kwa kukadilia ndipo mlango ukafunguliwa neema akaingia huku mgongoni na begi lake.
Alitusalimia kisha akanikonyeza pasina wakina careen kuona hapo sikumjari niliendelea na kuangalia runinga yeye akapita hapo ndion macho hayana pazia niliacha kuangalia runga macho yote nikiangusha kwake kutokana na kuvaa skin iliyompaka kiasi kwamba hata vazi la ndani kucholeka.
Macho kwa umbea hayakukubali kupitwa hata na Hatua aliyokuwa akinyanyua kutembea, macho yangu yalidumu katika maungo yake ya nyuma nikimtizama tu nae sijui alijua kama ananipagawisha mana alizidisha mwendo ule, kiasi kwamba ikafika mpaka wakati akili za kijinga zanituma nimfate alipo kule.
Niliendelea kumtazama nikimsindikiza mpaka akaingia kona ya chumbani hapo ndio nikarudisha macho, wakina careen na doreen hawakuniona kutokana na mimi kukaa nyuma pale ndio ilifanya wasinione ninachiangalia.
Tuliendelea kukaa pale mpaka muda wa chakula ulipo fika ndio wote tukajumuika mezani kupata diner.
Kila mtu alijisevia mwenyewe kisha ulaji ukaendelea na story kuanza.
Wakati hayo yote yanaendeleaa nilianza kuhisi naguswa guswa na miguu chini huku sikuweza tambua ni nani kutokana na watu waliokuepo pale hivyo nilianza kula timing nikisubilia kuangalia juu. Nikivizia mtu anaechezesha miguu kwa juu akitingishika, nilikaa kwa muda kisha ndipo nikambaini anae nigusa ni careen, sikuongea nae nilimpotezea sikumjali na yeye hakujua kama nimemgundua.
Sikumuelewa anataka nini tokea hapo hadi kufikia kugusa gusa miguu yangu chini nilipotezea tu.
Masaa yaliendelea kukatika hadi wote tukamaliza kula na kila mmoja akaendelea na jambo lake kuna walio ingia kulala na wengine kuangalia runinga na wengine kuosha vyombo,muda ulikuwa umeenda sana.
Mimi nilielekea chumbani kwangu kujipumzisha, nilingia ndani hata mwili ulisadifu nilichokuwa nazamilia kufanya mana tayari uhitaji wa kulala nilikuwa nao mwili ulikuwa umechoka kiasi kwamba hata macho yalikuwa mazito kuamka hivyo nikajitupa kitandani na usingizi kunikuta.
Kilipita kimya kifupi hapo sasa usingizi ulianz kupotezwa na joto lililoanza kuujaza mwili wangu jasho lililonitapakaa kama maji nikishindwa kuvumilia nikajikuta naamka.
Niliamka na kuvua nguo zile nilizo lala nazo kisha nikavaa taulo nikiwa na lengo la kwenda kuoga, nilifanikiwa kutoka nje hapo nikaanza kuutafuta mlango wa bafuni lililokuwa ndani, kutokana na kutoka usingizini na haraka nilizokuwa nazo, sikukumbuka hata kuangalia kama kuna mtu au laa nilichifanya ni kuusukuma mlango uliokuwa wazi na kuingia na ndani ya bafu.
"Haaaah wewe gao umefata nini kunichungulia huku.?"alishangaa sana kuniona mimi pale, hata mimi pia nilishangaa alikuwa ni careen.
Muda huo hata usingizi uliniruka tayari mana careen alikuwa hana nguo muda huo ananaliz kuoga, nilijihisi hadi aibu nikitamani ardhi ifunuke angalau nijifiche humo.
"Yani mimi naoga umekuja kunichungulia ili unione sio sasa nasema kwa mama."
"jamani sijajua kam upo nisamehe ngoja niondoke usimwite mama tafadhali."maneno yalinitoka lakini careen hakukubali alichotaka ni kumuita mama yake, muda huo kashavaa khanga yake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni