WEKA YOTE (10)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Nilianza kuyachezea nae akapagawa ndipo nikatoa mkono wangu na kuichukua funguo juu ya meza, kisha bila kutazama nyuma nikafungua mlango kwa fujo, kisha nikakimbia japo mvua ilikuwa inamwagika sikujali nilichojali ni kushindana na shetani la ngono lililokuwa katika orodha ya cv yangu tendo hilo nilikimbia huku nikijishaa mwenyewe..TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
'Leo nimekuwaje, yani nimekataa kufanya hivi hivi na alikuwa uchi mmh, haya mapya "nilijiwazia mwenyewe, kweli yalikuwa mapya sidhani kama chui yupo tayari kumwacha swala hata kama kashiba. Mvua nayoo ilikuwa mbioni kuacha kunyesha kabisa, kutokana na kutembea huku mvua ikinyesha nililowanika mwili mzima hata daftali zangu sikujua zipo katika hali gani wakati huu mana sikuzijali kabisa niliujali mwendo nikikimbia kuenda nyumbani ila begi langu sikukumbuka kama ndani lina daftali, nilitembea hadi hadi kifika nyumbani mvua ikiwa imeshaacha hata kunyesha.
Niliiingia ndani baada ya kuvua viatu vyangu vyenye matope yaliogandiana chini ya soli.
Baada ya kuingia ndani nilikimbilia chumbani kwangu kuwahi kuzivua nguo zangu zilizozidi kunipa baridi iliyonitetemesha zaidi, nikaufikia mlango wangu na kuufungua kisha nikaingia ndani kitendo cha kuingia nilivua nguo zangu na kuvaa taulo ili nitafute nguo za kuvaa ndani ya begi. Nilisikia minong'ono ya watu niliwagundua ni shangazi na wanae wakipiga soga, nilianza upeku peku nikitafuta nguo ya kuvaa nilifanikiwa kuipata hapo nikavaa na kuzichukua nguo zangu za shule tayari kwenda kuzifua.
Nilitoka hadi valandani kuelekea uwani.
",Shikamoo shangazi."nilimsalimia nikiwa pale valandani napita ndio akaitika na kuniambia.
"gao vipi mvua mwanangu"
"Daaah imenikuta nimelowa kweli.
"nilisema.
"Mmh pole sana"
"Asante,ngoja nikazitie povu ndio nijakula."nilisema, baada ya kuitika nikatoka nje nikimuacha anatizama runinga alikuwa peke yake hata wale waliokuwa anaongea nao sikuwaona,siku hoji nikatoka nje, muda huo giza ndio linaanza kuvutana kutengeneza usiku.
Nilichukua ndoo na maji na kuanza kuzifua nguo zangu zote nilitamani kukaa juu ys ndoo ila niliumia hasa pale nilipojaribu kukaa.
'Aaaii aaah"niligugumia, mwenyewe, mpaka nikajuta kwanini nilikaa mana makalio yalikuwa yamevilia damu kwa fimbo za sir lusinde alienivimbisha.
"Aaaah yani huyu mwalimu nitamkomesha hawezi nionelea kiasi hichi."nilijisemea huku nikifua kwa kuinama sikukaa tena nilifuma hima hima hadi nikamaliza sanjari na kuzianika, kisha nikaingia ndani kwenda kupata chakula mana hata njaa ilianza kuninyemelea.
Niliingia ndani wakati huu nikamkuta dhangazi na wanae pamoja na neema wanatizama runinga, nilipoingia tulisalimiana kisha sikupoteza muda nikaiendea meza haraka haraka, nilifika na kujipakulia kisha nikaanza kula muda huo giza limeingia kumaanisha ni saa moja tayari.
Nilikula upesi upesi kiasi kwamba kama vile simezi chakula,nilimaliza kula baada ya kunawa na kujisafisha vyema. Nikaungana na wenzangu valandani kutizama runinga.
Masaa yalianza kukatika tukiwa tunatizama runinga story zikiendelea huku mimi nikikaa kwa shida katika masofa yale nikiugulia maumivu sikutaka wajue.
Tulikaa pale mpaka muda wa chakula ukiwa tayari, shangazi hakuenda kula akidai ameshiba hata mimi pia sikuwa na sababu ya kutaka kula tena, hivyo tukabaki wawili mimi na shangazi.
Ndipo nikaakaanzisha mada, kwa kumtandika swali shangazi.
"Hivi shangazi baba yangu ni nani.?"nilimpachika swali lililomshangaza shangazi hadi kustuka.
"Haah, wewe mbona umeuliza hivyo.?"alishangazwa na swali langu.
"shangazi shule nimeandikishwa kama gao seif na baba anaeishi na mama anaitwa juma"nilinyoosha maelezo, hapo shangazi akiwa kama mtu alipata mshtuko kwa mimi kusema vile.
"Mwanangu nitakuambia siku ni siri hiyo ambayo imefichwa."alisema shangazi hapo alinipa maswali mengi ambayo kama yangekuwa yanahesabiwa yangejaa hata gunia.
"Siri.?"niliuliza kwa kuhamaki,shangazi aliposema ni siri.
"Ndio mwanangu nitakuambia siku,aliposema hapo ndio alizidi kunipa shauku ya kutaka kutaka kutaka kujua nilianza kumlazimisha aniambie tena kea kumbembeleza alikuwa kanita aliposema kuwa ataniambia yani ilikuwa ni sawa na pale unapo soma hadithi alafu inafikia utamu unaambia itaendeleaa, hivyo sikupenda kuona itaendelea nililazimisha shangazi aniambie.
"sawa nakuambia ila usimwambie mama yako kama nimekuambia."
"Sawa shangazi sitamwambia kabisa"nilizidi pigilia msumali ili aniambie tu.
"Sawa yani ilikuwa hivi......"kabla hajamaliza wakina neema,doreen na careen wakatokea hapo hakuendelea kutokana na kuwa ile ni siri, nilichukizwa na ujio wao nikiona ndio wamenikosesha kujua ukweli kuhusu baba kuhusu baba yangu.
Sikuwa na budi ya kuendelea kukaa niliwaaga na kuondoka nilijuafika hapo hataweza kunambia tena, niliingia chumbani kwangu ilikulala kuitafuta siku nyengine, nguo niliziacha uwani ziweze kukauka. Kisha nikavuta shuka na kulala.
Kilipita kimya kirefu mpaka kunakucha ndio nikaamka muda huo haraka n kuzichukua nguo zangu nje tayari kwa pasi, nilizipasi na kwenda kuoga baada ya kumaliza kupasi.
nilioga himahima mpaka nikamaliza na kuvaa kisha kuwahi shule, nilianza kuitafuta njia ya shule nikitembea upesi upesi mpaka kufika, cha kushukuru muda huo huo ndio namba zinahesabiwa nilipata namba na kuelekea katika maeneo ya usafi.
Usafi ulifanyika mpaka muda wa paredi asubuhi ukafika tulipewa matangazo kadhaa na kuingia darasani.
Siku hiyo kipindi cha kwanza kilikuwa ni kiswahili nwalimu mhusika ni sir lusinde tuliingia darasani tukisubiri aje.
Siku hiyo ilikuwa tofauti sana Grace alianza kujipendekeza kwangu nikiwa nimekaa katika kiti changu nilimuona anataka kunirushia kikaratasi alicho andika nisome kabla hajarusha, mwalimu wa kipindi akaingia ambaye ni sir lusinde. Alisalimiwa na wanafunzi tukasimama ila mimi siku salimia, baada ya salamu wanafunzi tukakaa.
Kipindi kikaendelea, sasa Grace aliona ni muda wa muafaka ea kunitupia kikaratasi chake alicho kikunja vyema.
Kitendo cha kunirushia kumbe sir kaona.
"Gao hicho nini, ulichorushiwa njoo nacho hapa"'nilistuka kumbe kaona tena aliniita kwa jazba, nikaenda kinyonge.
",Nipe hiyo karatasi."alisema, hapo nikim tazama Grace anatapa tapa, darasa zima likinitazama sir alichukua ile karatasi na kuisoma.
"Hivi ni mimi ndio akili zenu embu soma wenzio wasikie upuuzi huu na unambie ulikuwa wamtumia nani.?"karatasi ile sir alijua mimi ndio nilikuwa namtumia mtu,hapo nilianza kutetemeka. Nikaanza kusoma.
",NISAMEHE KWA KUKUAMBIA VILE NAOMBA LEO JIONI TUTOKE WOTE NIKUAMBIE KITU KIZURI.....
NAOMBA UNISAMEHE SANA TUWE KAMA ZAMANI NIME...."nilishindwa kuongea nikiwa pale mbele sir nae akinilazimisha nisome.
"soma upuuzi wako soma"alizidi kunididimiza zaidi halo wambea wa darasa hawakuacha kucheka vicheko vyao vya kimbea.
"nipe hiyo karatasi lete."aliniambia Na kunipokonya, tangia hapo nilipata kesi ambayo haikuwa Yangu kabisa.
"sasa uupuuzi nauhifanyi kwenye wallet Yangu nikamuoneshe MKUU wako wa shule upuuzi Huu.,alisema sir Bila kuongopa akaitia ile karatasi ndani ya pochi Yake ya rangi nyeusi.
"kwanza nikukute staff sawa kanisubiri Kule.,"alisema hapo sikupingana nae nilienda moja kwa moja staff kumsubiri.
Nilikaa Masaa kadhaa nae akaja Na kuniita ndani ya ofisi Yake.
"Gao wewe siku hizi umekuwa mhuni sio,"
"hapana mwalimu Mimi sio mhuni,nilikuwa naandika mwenyewe sijamwandikia MTU."tulizozana pale nikiiomba asije kunichapa akanitonesha maumivu.
"sasa nakuuliza maswali Yangu ujibu kama ninavyotaka ole wako unidanganye napeleka Huu upuuzii wako kwa MKUU wa shule."aliniambia.
"sawa Mimi nitasema ukweli,"
"unamahusiano gain Na madam jack,"alinipachika swali ambalo ni dhahiri lilionesha ni wivu.
"madam ni kama mwalimu wangu hatuna uhusiano mwengine."nilisema kwa kujiamini.
"unanidanganya sio eh.!"alisema,
"kweli mwalimu yule ni madam wangu tu" haku kubaliana Na majibu Yangu hivyo aliendelea kuning'ang'aniza ni mwambie ukweli.
Tukiwa tunaendelea Na mazungumzo, mlango ukagogwa.
"nenda darasani."alinifukuza halo nikatoka Na kukutana mlangoni Na MKUU wa shule,nikampa heshima Yake kisha Na Mimi nikaondoka kuelekea darasani.
Nilipoingia wanafunzi wapo katika vikundi nikajiunga nao, kusoma kukaendeleaa.
Grace alikuwa ni wa kunitizama tu muda wote Na jicho lake LA mahaba sikumfatiliza tuliendeleaa kujadili mpaka muda ukaisha wa kipindi hivyo kazi zikakusanywa.
Kengere Nayo ya chai iligogwa Na wanafunzi wale wenye pesa wakatoka kwenda vibandani kunywa chai wale wasio Na kitu walibaki darasani Na kufungua daftari Zao kujisomea,Mimi nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wenye hela za chai hi yo niliwahi nisije kuta mwana so Wang yani "CHELEWA CHELEWA UTAKUTA MWANA SI WAKO"nilikumbuka methali hiyo tuliyofundishwa shule za msingi.
Nilikimbia kuelekea kwenye chain bahati nzuri sijachelewa nilifika muda Huo Huo Na kupata chai nikioigugumia kwa pupa ilisababisha niungue ulimi nikaimwaga daah nilipofikiria Kuwa watu wameikosa hiyo chai niliyomwaga, wamekaa tu darasani nilitamani angalau ningewapelekea ila tayari ilishamwagika haiwezi kurudi tena, niliamka kuelekea darasani baada ya kumpa mama muuza pesa yake na kulifata jengo la choo kujisaidia kabla ya kuingia darasani, nilimalizahaja yangu na kuekeka darasa.
Nilienda moja kwa moja nakukaa sehemu yangu ya kukalia nkitizama mbele, wakati huo hata wanafunzi walikuwa wachache bado Nilitumia muda huo kupitia daftari zangu kuzisoma kwa umakini nikimsubiria mwalimu aingie darasani,niliendelea kuzifunua nikisoma kwa kutizama kwa makini, dakika kadhaa kipindi kiligogwa hivyo kumpa nafasi mwalimu aje dalasani hapo wanafunzi wakaanza kuingia mmoja mmoja mpaka wakajaa wote ndio mwaliku nae aaja dalasani, alikuwa ni mwalimu wa somo la uraia au kwa kimombo au kisekondari tunasema ni civics, aliingia tukamsalimia kisha tuka kaa mwalimu huyo jina lake alilo kuja nalo shule anaitwa kakuma sondo nakumbukuka siku ya kwanza anajitambulisha kalibia wanafunzi wote pale paredi tulibaki midomo wazi na kucheka utambulisho wake mbele ya mkuu wa shule siku hiyo tulichalazwa na walimu wote kisa tu kucheka jina la mwalimu mgeni wa kiume, tulipendekeza tumuite sir sondo ili kuachana na adha ya kutamka neno ambalo ni tusi tayari, nakumbuka hatukuweza kuelewa maana ya jina lake kutokana na mwenyewe kutokulifafanua sisi tulijue ilikuwa ngumu kwetu kila akiulizwa anasema alitokea kenya kabla ya kuja tanzania kusoma chuo.
Na ni muda mrefu hivyo alikuwa kama raia wa tanzania, tulipenda sana ufundishaji wake hivyo tulimpenda pia yeye kwa upole wake japo muda mwengine anakasirika na kutuchapa ila sio kwa sifa kama sir fulani, tulipenda kuficha uovu wa sir lusinde kwa kutimtaja tukiwa kwenye story zetu hasa tunatumia jina la sir fulani.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni