WEKA YOTE (16)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
"Sio mwizi unatoka wapi peku peku hivyo."nilikuwa sijajiangalia na hata habari sina kuangalia hapo kweli viatu sina, sikuweza kuwa na kumbu kumbu sahihi juu ya nilipotupa viatu vyangu.
"Huyu ni wale wale embu nipishe"alikipenyeza mmoja aliekuwa kashika gongo, alizuliwa ila tayari alirusha gongo likanipiga la kiuno.
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
"Oooooh,aaaaaah"nilitoa ukelele wa maumivu.
"Bhana niacheni,sasa kazi gani ya kiboya hii mwizi huyo tumsurubu mwaleta ujinga"alisema kwa jazba.
"Jaman mimi sio mwizi nimekimbizwa kule wakati natoka nje kukojoa ndio wakatokea watu wenye mapanga na kuanza kunifukuza."nilitamka uongo uliofanana na ukweli kabisa,sikujua kama watanielewa wakati huo kiuno kinaleta shida nayasikia maumivu niliyoishia kuyavumilia tu.
Walizozana zozana, muda huo niligundua ni sungusungu,walinielewa kishingo upande upande ila yule mmoja wao hakuweza kuamini aliwalaumu sana wenzake na kutukana matusi kadhaa hasa upumbavu,ujinga na uboya, aliyatamka maneno yale kuwaambia wenzake baada ya kuniachia mimi.
"Sawa kwenu wapi.?"
"sipajui nilikimbia tu giza hili siwezi kufahamu"
"Umetokea wapi?"alizidi kuniuliza maswali ambayo sikuonesha ushirikiano, alikosa hata cha kuendelea kuniuliza hivyo alichofanya ni kuniekekeza njia ya kutokea kwenye kituo cha magari.
Nilimshukuru, kisha nikaachana nao hapo moja kwa moja nikaanza kuongoza kuifata barabara ile, njiani nilianza kujitisha mwenyewe na kuogopa kabisa, niliendelea kutembea na mwendo huo wa kuogopa ogopa.
Wakati nikitembea mwendo wa kulazimisha kiuno kishirikiane na miguu ili nwendo uendeleaa, nilishaangaa gari kubwa la mizigo likipita huku gurudumu zake ziligongana gongana kibaya zaidi halikuwa na taa, Lilitembea na giza lake bila kujali mashimo ba mabonde yaliyopo njiani hapo sasa nilibaki mdomo wazi liliponikaribia gari lile ambalo sidhani kama waliomo ndani waliniona nililiita ni gari kutokana na ukubwa wale ila lilinishangaza liliponifikia halikuwa gari kama nilivyotegemea.
Nilishaangaa sana hadi kukikuta nakimbilia mti uliokopembezoni mwa pale, hapo nilisitiri mwili wangu kutokana na woga ulionijaa,
Niliogopa sana lile halikuwa gari ila ni treni.
Sijasumbua kichwa kujua ni aina gani ya tren inayopita kwenye barabare ambayo sio yake.
Kwa woga niliishia kujibanza kwenye mti nikisubiria lipoteee katika ngoma za masikio yangu, sikuwa nikiliona zaidi ya ya mgongano wa gurudumu.
Sikuwa na habari kumbe muda unazidi kusogea tu, nilitoka mafichoni pale na kuanza kuifata njia ile, mwendo niliotembea ni kama roboti kiuno hakikuwa tayari kutoa ushirikiano niliendelea kukiradhimisha tu ilimradi nifike nyumbani japo naogopa.
Baada ya umbali kadhaa nilikaribia nyumbani kabisa ndio nipo kwenye njia ndogo ya kuingia nyumbani.
Kwa mwendo ule ule,
Mara hammadi bila kuonabnilijikuta nakanyaga mkia wa mmbwa hapo ikawa kama nimemchokoza alianza kupiga kelele za kuboha nilijilazimisha na kurusha teke lililompiga akakimbia, hapo nikapata nafasi ya kufika nyumbani.
Japo nimetumia juhudi zote mpaka nafika nyumbani ila bado ilikuwa kama nimecheza tu mana geti lilisha fungwa tayari hivyo njia ya kuingia ndani hakuna.
Kwa akili za haraka zisizotaka umakini wa kufikiri niliona nipande juu hata nilale uwani,nilisahau kama kiuno changu hakipo imala nilikifanya kuruka juu mzima mzima, kuruka niliruka vizuri kilichonikwamisha ni pale kuvuta mguu kuweka pale juu hapo niliamsha maumivu nikajikuta naanguka chini kabisa.
"Aiiiiiiiii"kelele hazikuacha nitoka, mithili ya mtu alievamia miba tena migunga, lazima kelele zikutoke.
Nilipoteza umaridadi wa kuamka pale chini, niliamua kupageuza kitanda na kulala nikijifunika ngumi.
Usiku ulikuwa mrefu sana, nikiwa nimelala sijui kinachoendelea.
Kilipita kimya hadi kujakukohoa,hiyo ndio ikawa sababu yangu ya kuamka niliamka nikifikicha macho, uchovu wa kuamka.
"Haaah nipo wapi hapa"nilijipa swali na kuamka kusimama nikishangaa shangaa, na kuondoka eneo lile kusubiri mlango ufunguliwe nipate nafasi ya kuingia ndani.
Muda mchache nilisikia ukifunguliwa, macho yote nikayaelekeza getini kuangalia anetoka,
Nilikodoa macho bila mafanikio kwani hakuna alietoka ilinibidi niende kwa tahadhali kwanza nilichungulia uwani hakuna mtu ndipo nikanyata hadi kujituliza kwenye mauwa.
nilijiona mjanja sana kumshinda sungura kumbe nipo mtegoni bila kujua.
Nilijitoa na kuufata mlango haraka haraka nikijua bado wamelala.
Ile kufinya kitasa na kuingia ndani kabla sijageuka mana nilipoufinya niliingia taratibu sikuangalia mbele nilimrudisha mlango taratibu sasa ile kuugeuka tu, shangazi huyo kasimama mbele....................
Alionekana amefura zaidi kwa hasira hata sura yake ilionesha, hata lile tabasamu la sikuzote linalompendezesha uso, halikuonekana.
Siku subiri aanze kuongea nilianza kibabaika peke yangu..
"Aa aa nililala uwaniii."nilibabaika mithili ya bubu aliezoea kuongea kisha akapata kilema cha ghafla huku akijaribu kuitafuta sauti ikae sawa.
"Nimekuuliza.?"alisema shangazi hapo tayari alinimezesha woga, nikimuogopa kama anatisha.
"Hivi gao kwanini unataka kunipa presha eeh kwanini.?"aling'aka vilivyo hapo sikupenda kumzidishia hasira ilinibidi ni nywee kama piriton.
"Nimechoka kulazwa macho, nimechoka utaniua na presha urudi tu kwenu."alisema, shangazi hapo sasa ikawa kama kamshitua alielala udingizi wabkukesha kibaya zaidi ametumia maji aliyoyagandisha na friji.
"Nisameee shangazi nisamehe tafadhali nakuomba nisamehe sintarudia tena"nilimwaga maneno mfululizo,nikimtaka shangazi anisamehe.
"Mimi nimechoka kitendo ilichofanya sijapenda kumbuka mara ya pili ya kwanza umeondoka bila kuaga ikiwa nakuita leo umelala huko huko, mara nyingine si utafia uko uko umeona ulivyojaa vumbi, mimi nimechoka urudi kwenu"shangazi hakuregeza kamba hakutaka kunipa msamaha kabisa, alipo niambia nimejaa vumbi ndio nikapata nafasi ya kujiangalia,nilikuwa kama kikagula au kichaa aliejiogesha vumbi.
"Nisameheme shangazi tafadhali sitarudia nisamehe tu."nilizidi kuomba msamaha ila ikawa kama natwanga maji kwani shangazi alikuwa kakasirika sana.
"Careeen, careeeen"aliita kea jazba sikujua anamwita wa nini, nae muda mchache akaja kiupole mana tayari alijua hali ya mama yake.
"Abeeeh mama"
"nenda kule ndani anakolala huyu mpuuzi ukatoe nguo zake utie ndani ya begi ulete hapa, umesikia haraka "alisema kwa jazba hapo nilitulia kimya nikiona aibu kuomba msamaha mbele ya careen.
"Mama kwani kuna nini, na mbona gao kachafuka hivyo.?"aliongea kiipole careen.
"Nawewe sitaki maswali, nenda karete harakaa." Alizidi kupiga kelele, careen aliondoka kwa kujirazimisha hadi kuingia chumbani kwangu.
Kuondoka kwa careen ndio nilipata nafasi ya kuomba msamaha.
"Shangazi nisamehe, nakuomba nisamehe nitaenda wapi nisamehe usinifukuze."niliomba msamaha kwakulalamika na magoti nikapiga kabisa kumaanisha nauhitaji msamaha.
"Utaenda kwa mama yako, sipendi kulazwa macho, nimekaa hapo kwenye makochi muda mrefu nikisubiri uingie nilikuwa macho tu sasa mimi naona ukakae na mama yako tu."alizidi pigilia msumali tena wa inch nne akizidi ushindilia, kwa hali ile niliona msamaha ni ndoto nilikosa matumaini kabisa ya kusamehewa.
"Wewe, careeen fanya haraka."
"Namalizia mama."alisema careen, sauti ikitokea ndani, niliamka tu mana msamaha hakuweza nisaidia shangazi kakasirika hadi kumfanya atishe kama chatu aliejizungusha kwenye mti huku ulimi upo nje akisubiri mpita njia amtafune.
Muda mchache Neema akaja akitokea ndani alionekana kushangazwa na hali yangu akasogea hadi pale na Careen nae akatoka ndani kwangu huku kashikilia begi langu mkononi.
"Mama nini tena mbona yupo hivi jana alikuwa wapi.?"aliuliza Neema.
"nilishakataa maswali na wewe unauliza embu nyamaza huyu aende kwao."kitendo cha kusema vile ikawa kama kamsitua Neema, alianza kuniombea msamaha careen nae alianza kuomba yani wote wakijua wapo peke yao huku kila mmoja akizania mwenzake anasaidia kuomba kumbe ni mpenzi mwenza, kama mmoja wao au wote wangejua nimetafuna mpaka Ester na wao wawili sidhani kama wangeshiriki kuniombea msamaha tena ndio wangekandamiza nifukuzwe.
"Mama msamehe tu, muulize vizuri alipolala hujui kakutana na nini huko, msamehe mama tushamzoea sasa ukimfukuza tutabaki na nani."alilalamika neema huku machozi yakimtoka, nilijua fika anachogombea nisiondoke yote ni dushelele.
"Msiniletee uchuro wenu sawa."alisema shangazi.
Wakati huo tayari Alipoa japo sio sana,nadhani maneno ya Neema aliyasikia vizuri hapo akakaa kimya huku kisha akanyanyua kinywa.
"Nenda kaoge kisha ukivaa njoo hapa, nawewe pereka begi ndani.
"Asante shangazi kwa kunisamehe asante."nilisema na kuelekea bafuni kama alivyonambia, sikungoja aongee tena haraka niliingia bafuni na kuvua nguo zangu ambazo kabla sijavua nilijitazama sikuwa na tofauti na kigagula mana nilichafuka mnoo, sikujali nikazivua na kuanza kuoga nilitumia bomba la juu linalo mwaga maji chini baada ya kujiswafi na kujihakikishia nimetaka, ila wakati huo kwa mbali nilisikia kiuno kikiuma japo sio sana hata nilipopiga magoti kiliuma ila sikutaka shangazi ajue,nilichoona wakati huo ni kujinyosha ili hata kikaesawa, nilijibunua mikono kuireta nyuma na kicgwa nacho kikiangalia nyuma, ili kujinyoosha kiuno.
"Aaaahhhhhhhhhhhhh"nililalamika maumivu ya kiuno, sauti ambayo sikujua kama wanasikia walioko nje.
Sikuendelea nikaacha ila nilijiona kidogo kimekaa sawa hapo nikajimwagia maji tena, kisha nikajifuta maji na taulo lililokuwa juu ya mlango, nikatumia kuvaa lilelile.
nikazichukua nguo zangu chafu nilizoshika kwa tahadhali zisinichafue sasa wakati napita pale sebuleni na ushikaji wangu ule wa nguo kabla sijamalizikia hele zikanguka nusu shangazi aone.
"hizo nini.?"aliuliza.
"Hamna shangazi sio kitu."nilivyomjibu hivyo hakuendelea kuongea mana nilitupa na nguo chini ili kumpumbaza hapo nikajua hakuona kabisa kisha nikaingia ndani, nilivaa sanjari na kupaka mafuta,nilipo maliza nikakaa kitandani kupangilia maneno ya kwenda kumuongopea shangazi mpaka anielewe, nilitumia muda kupangilia nikijadili na kichwa tu.
Nilipohakikishwa nimetengeneza maneno ya kueleweka ambayo nikimwambia lazima akubali tu bila kipingamizi nikatoka sasa nikionana na shangazi aliekuwa ananisubiri kwa hamu nimulezee vyote vilivyonilaza nje.
"Mhuu ushaoga sasa nadhani mwili umechangamka, haya jana ulienda wapi na ulilala nje kwanini na kwanini umekuja umechafuka?."aliniorodhoshea maswali akiyokuwa akiyatakia majibu kwa ufasaha na mimi nikaanza kushuka essay ya kuongea maneno nilianza kuporomosha maneno ya uongo na kweli.
"Shangazi mimi nilipo ondika hapa moja kwa mojanilienda pale dukani kwa mangi tunapo kaaga na na kina twite sasa tumekaa pale tukipiga story huku masaa yakienda kutokana nabkunogewa na story sikukumbuka nyumbani niliendelea kubaki mpaka wakatokea watu ambao hatukuwafahamu walianza kutukimbiza na mapanga tulikimbia kwa kutawanyika kila mmoha akielekea kwake sasa bahati mbaya mimi nilielekea kwenye mapori huko alinifata mmoja ambae haku katatamaa alinifukuza kama mmbwa kila nikanguka nilikuwa naamka mana alinikimbiza kama masubwi nilidondoka mara kadhaa na kuamka kisha naendelea kukimbia mpaka nilimpoteza, baada ya kumpoteza porini ndio nimetafuta njia ya nyumbani kisha nilitokea barabarani niliifata mpaka kufika hapa, nako ilinibidi nilale nje tena chini baada ya kujua geti limefungwa ndio asubuhi nimeingia ndani baada ya kusikia mlango umefunguliwa, kufika hapa ndio tunakutana."
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni