WEKA YOTE (18)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
"Gao acha tu yani sijui wanaume mpewe nini,aah najuta"alisema grace hapo kidogo picha ilinijia,na kujua fika ni mapenzi hayo ndio yanamsumbua japo sijajua kwa kina tatizo lake ila nilihisi tu kutokana na maneno yake.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
"Wanaume wananini?,Grace"nikamshushia swali.
"Gao mimi siamini kama Ally kanifanyia vile."alizidi kuongea huku akilia kwa kufina fina,aliniacha na lundo la maswali ambayo nikimshushia ni zaidi ya police.
"Ally ndio nani na amefanya nini,?"
"Gao sikuwahi kukwambia, kabla kuwa nina mpenzi anaeitwa ally."
"ndio hujanambia sasa ally ni nani na unalia nini.?"niliendelea na upolice wangu, ambao haukuwa rasmi.
"Gao naomba tukakae, nikuambie ila inaniuma sana," Alisema, na kukaa sehemu kisha akaanza kunielezea, japo siku hiyo ilikuwa ya kuanza mitihani ya mwezi wa sita, hiyo haikuwa sababu ya kutoacha kuniambia , tukaa pembeni huku nikijaribu kuubana mkojo uliokuwa umenibana, ndio Grace akaanza kunielezea.
"Gao mimi siamini nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulijuana kabla sijahamia shule hii, mana nilikuwa nasoma shule jirani ila mpenzi wangu anasoma shule hii tena kidato cha nne, mwanzoni alinipenda na kunisikiliza kwa kila nitakacho mwambia tulipendana sana ila wiki mbili za nyuma hapo mwenzangu kaanza kubadilika kiasi kwamba hata simu hanipigii wala hanitumii jumbe, hali ile ilikuwa kila siku nikimwambia anachonijibu ni kuwa busy, iliniuma sana nikikumbuka upendo wake wa mwanzo na sasa haupo tena ule upendo.."akanyamaza kidogo na kuanza kulia hapo mimi nikiyafuta machozi yake kwa reso yangu nyekundu yenye picha ya nembo ya club ya manchester united, nilimbembeleza asilie mana alilia kwa uchungu sana, hali iliyonitia simanzi na mimi nikimuonea huruma.
"Gao, najuta kuwa nae pengine nisingekuwa naye leo hii nisingelia hivyi, Ally ni mwanaume wangu wa kwanza kuwa nae naweza dirikibkuswma yeye ndio alinitoa usichana wangu, kitendo alichonifanyia ally kimeniumiza sana sikuwahi kumsariti tokea niwe nae ila yeye amenisariti na kunifokea kisha kunitamkia matusi ya nguoni."alizidi kuongea huku bado akilia na kunipa kazi ya kumfuta machozi ila kabla hajaendelea tukiwa tumekaa ndipo tukasikia sauti.
"'form three wote mnaitwa mtuhani unaanza'iliita sauti ya mdada ambae ni kiongozi (kilanja) anasoma kidato cha tatu mkondo A huku mimi na Grace tukisoma mkondo B nilimwambia GRACE atangulie kisha mimi nikaelekea msalani kukinusuru kibofu changu kilichoanza kuchoma kutokana na kuubana mkojo,grace alikuwa mmyonge hata tembea yake.
Nilimsindikiza na macho kidogo kisha nikaelekea chooni kukinusuru kibofu changu kilichokuwa kikichoma kwa kukaa na mkojo muda mrefu, hivyo ilinibidi tu nikajisaidie hapo niliingia chooni na kumaliza haja yangu bila kujali siku hiyo tuna mtihani niliondoka nikitembea mwendo wa kawaida kama sio wa mtu anayewahi kwenda sehemu nilipofika kwenye korido ya madarasa ya kidato cha nne nilikuta pametulia hakuna kelele wala mwanafunzi anaezunguka pale, hali hiyo iliyofanya nitembe upesi upesi niwahi darasani mana niligundua mtihani ushaanza kama mwalimu alivyotuamhia.
Nilifika mlango wa chumba changu cha mtihani hapo moja kwa moja nilikutana na msimamizi wa kike mwalimu wa kidato cha kwanza.
Nikaomba kuingia nae bila hiyana akaniruhusu huku akiwa busy na simu yake ya kufuta, wala hakunijali ila aliniambia tu nichukue karatasi ya kufanyia mtihani zilizokuwa mbele pale na mimi nikachukua la maswali na la kujibia kisha nikaanza kukifata kiti changu na meza nikijua vipo kumbe laahasha, nilitizamana na Grace aliekuwa anasimanzi machoni,
Nilimtizama na kumpotezea kisha safari ikaendelea, nilishangazwa nilipofika eneo langu ninalo kaa akiwa amekaa mtu mwengine na meza pamoja na kiti changu havipo ambavyo niliviandika jina vyote jina la GAO DE SWAGGERBOY.
Sikuviona na eneo langu, akiwa amekaa mtu mwengine nilishindwa hata kumsumbua nikabaki nimesimama huku nimeduwaa.
"Wewe mbona umesimama hapo hukai, hujui kama muda haukusubiri nusu saa ishakatika sasa,"alisema msimamizi yule.
"Madam kiti changu na meza sivioni,"nilimjibu.
"Sasa si ukatafute unachopoteza muda ni nini."alisema madam hapo sikuwa na sababu ya kuendelea kukaa, nilitoka nje kimya kimya kwenda kutafuta kiti na meza, nilizunguka maeneo kadhaa nikitafuta meza kwanza nilikosa, ila nikatazama juu kule ofisini kwa walimu nikafanikiwa kukiona kiti nikiamua nikifate ila kabla sijakibeba alitokea sir lusinde huku kashika lim.
"Gao, mtihani ukiisha nitafute usingoje nikakutafuta hutafanya mtihani wa pili."alinitisha na kuondoka hapo akilibl yangu ilicheza nikajua ni kitendo cha kumtoroka siku ya ijumaa,niliacha kumuwaza kisha nikajibebea kiti nikawa nakishusha kuelekea darasani, kimya kimya nikatafuta eneo nikakaa nikiwa na karatasi zangu.
Kusema ukweli sikuwa nikijua ni mtihani gani tunafanya hata kusoma sijasoma kabisa, yote ni kuondoka bila lidhaa ya muda maalum wa kutoka shule, ndio mana sijapata hata kujua mtihani wa kwanza.
Wakati huo msimamizi alishatangaza imebaki nusu saa hapo sasa ndio nikauangalia mtihani ambao nilikuja ujua ni wa hisabati, hapo kichwa kilipata moto nikiangalia maswali hakuna ninalo kumbuka,nilichofanya nikayacopy maswali yote na kundika jina langu, sikujibu swali hata moja.
Mpaka muda unaisha tukakusanya kisha wote tukatoka tukiwa nje, wanafunzi wenzangu walianza kujidai kila mmoja, wakisema maswali waliyoyajibu hapo mimi nikiwa sina lolote hadi kukaa mbali nao nikimtafuta Grace, hata aniendelezee sikumuona.
Nilipokuwa nimekaa juu ya jiwe ndio nikakumbuka sir lusinde aliniita, Sikujali nilikaa tu pale nikikumbuka kisanga cha yule mkulya nikiogopa sana, ila sidhani kama ninachakupinga juu ya hisia zangu, nilikaa dakika kadhaa kisha ndio nikauliza mtihani unaofatia, nilimuuliza mwanafunzi mwenzangu aliekuwa akipita eneo lile, nae akanijibu ni kiswahili.
nilitumia muda huo kupitia tulivyosoma hasa mambo ya ngeli za maneno,vishazi, aina za maneno, historia ya kiswahili na topic ndogo nyingine, nilikuwa nikisoma ila sijaona kama naelewa, kichwa kilikataa mawazo mengi nilichoamua nibkuelekea vibanda vya chai angalau akili itakaa sawa, nilifika kweli na kunywa chai kisha kurudi juu ile kufika kikagongwa kipindi kumaanisha mtihani umeanza.
Kabla sijakifikia chumba cha mtihani lusinde alikuwa makini nilimuona akishuka haraka haraka kuja darasani kwangu na kwapani kahifadhi fimbo......
Nilikuwa sina chaguo jengine zaidi ya kujificha sehemu ambayo ilikuwa kama chumba kidogo, niliingia pale, huku nikiwa makini kuchungulua nje nikisubiri lusinde atoke ila wapi,kila nikitazama ola niliogopa kwenda yote ni kuto tii wito ambao aliniita na mimi nikapuuzi nakujifanya mkaidi mana kama ningemfuata alivyoniita pengine nisinge jificha ficha juu yake.
Niliendelea kukaa huku nikila chabo mbili tatu kumuangalia,yote haikutosha ilikuwa kazi bure mana nilichungulia mpaka nikakata tamaa huku nikiogopa kwenda nikihofia nisije kukutana nae, kitendo kile kilinifanya niendelee kukaa pale huku nikijua muda ni rafiki yangu ya kuwa utanisubiri kumbe laahasha muda hauna rafiki, hali ya kwamba ulitembea mbio mbio mpaka nikaanza kusikia mizogomo zogomo ya wanafunzi wakicheka kwa furaha, sikutaka kuamini kama mtihani wa kiswahili umenipita, mtihani ambao ulikuwa rahisi sana kwa kuwa ni lugha yetu tuliyoizoea nilijiraumu nikiwa sina cha kufanya niliona hata aibu mpaka ikapelekea moja kwa moja niondoke shule wakati huo.
Nilipita nyuma nyuma nikiogopa papalazi hasa wambea wa darasa wasije pata habari za kwenda kuongea.
Nilikuwa natembea kinyonge kama mtu anaeumwa mwendo wangu ule ulifanya nikatoka nje ya shule.
Nako mwendo haukuwa tofauti na ule niliokuwa nikitembea kule,shule mwendo ambao pengine hata ningekutana na mtu njiani asingeacha kuniuliza juu ya hali yangu, nilighafilika sana pale nilipokuwa nikitembea kisha akaja mtu na kunirukia kwenye mabega kwa nyuma kitendo ambacho kama si uwanaume wangu tayari ningeanguka sakafuni kwenye vumbi.
"Nani wewe aaah,mijitu mengine sio wastaarabu aaah,"maneno yalinitoka pale pale kabla sijamuona alienirukia.
Nilipoangalia ndipo nikakutana na sura ambayo haikuwa ngeni mbele ya macho yangu kitendo cha kumuona ndio nilitibuka ukichanganya na kisirani nilichotoka nacho shule,nilimtupia matusi mengi yasio na idadi kiasi kwamba mpaka akaondoka kwa aibu iliyomjaa, alikuwa ni loveness nilikumbuka pale nilikuwa maeneo ya kwao.
Sikuendelea kukaa pale nikaondoka haraka haraka.
"Aah, mi wanawake mingine haijielewi "maneno hayakuniisha kinywani niliyatamka kila mara nikichukizwa na kitendo chake cha kunidandia kwa kunirukia.
Safari iliendelea japo nilibadili mwendo kabisa wakati huu nilionekana mtu mwenye haraka sana, na hatua ndefu kama mwanafunzi mwenye njaa akiwahi ugali nyumbani.
Nilitembea hima hima hadi nikaufikia mtaa wetu hapo nikaanza kuchanja njia nikiisogelea nyumba yetu.
Hatua kadhaa nikaufikia mlango wetu mkuu kuu ambao ni geti nikaingia ndani kabisa hapo kuufata mlango wa kuingilia.
Nilifinya kitasa kama kawaida nikaingia ile naingia macho hayana panzia nilimshuhudia Ester akiwa kalala upaja wote upo nje kutokana nakuvaa khanga tu, runinga ilikuwa wazi hakuizima kabisa alafu aliweka miziki.
Macho yalinitoka nikajikuta nameza mafunga kadhaa ya mate hadi nikashindwa kuendelea kuondoka hali iliyopelekea nisimame kama mlinzi nikitizama tu ule upaja, hisia zangu hazikuweza kuhimili utulivu kabisa pale pale zikanituma hovyo na mimi nikazifatisha, niliamua nimfate Ester, pale alipo nia na madhumuni niimsogelee kisha niushike shike upaja wake nikijifanya namuamsha. Mawazo yangu niliyafanyia vitendo nikaenda kweli tamaa ishanijaa kweli mapenzi kitu haramu,nilumchukia Ester aiku ile lakini leo kisha nimeona paja lake likiwa wazi eti nataka kulichezea kitendo cha kusogea karibu zaidi nikagundua sio paja tu kumbe hadi hadi matiti yake yalio simama dede yalikuwa wazi, sikufikilia ni mtindo gani aliolala zaidi ya uchu kunijaa, hapo kono langu lisilo na adabu likayaendea maziwa yake kifuani ulikuwa mkono wa kushoto nililishika hali iliyopelekea Ester aruke huku akipumua kwa nguvu.
"Haah, wewe mbona tunashituana jamani nilikuwa mbali umenistua"aliongea kwa kudeka na mapozi kisha akasimama na kujifunua khanga na kujifunika vizuri hapo macho yalinitoka mana nilishuhufia alichovaa ni chupi tu tena iliyotuna eneo la tompo.
Kabla hakijaendelea kitu pale pale tulisikia ujio wa watu ambao hawakuwa wengine zaidi ya wakina Doreen na Careen.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni