
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Yakakutana na careen alieambatana na doreen wakifungua fungua daftali zao pale wakiwa makini kusoma sikuwashangaa sana, mana nilijuafika kuwa nao wameanza mitihani ya nusu mhula, walikuwa kidato kama changu cha tatu, nilipita karibu yao nyuma ya sofa walizokuwa wamekaa.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
"Hah, gao mambo"ni sauti ya uchangamfu ya careen alienisalimia kwa njonjo, nami sikupenda inipite salamu ile hivyo nikaitika kwa kibesi(sauti ya mkazo).
"poa"nilitika huku nikiondoka bila kumwangalia yote ni njaa niliyokuwa nayo, nikaikaria meza ya chakuka kisha nikajipakukia na kuwaza kufukia kutokana na kutaka kula cha jioni na cha usiku nilijiwekea kiasi kidogo ilu mradi wakati wa usiku nisiwe nimeshiba,hivyo nilimaliza mapema kwa kufakamia vile .
nilipomaliza baada ya kunawa nilijumuika na wakina doreen,nikikakaa mbali nao sofa la pembeni yao, muda huo shangazi hakuwepo hapo mana kawaida yake kila siku mida kama hiyo hupenda kwenda kuoga hiyo ndio kawaida yake.
Nilikaa nikitazama runinga, kipindi ambacho hakikunivutia zaidi ya kunichosha sikukipenda kabisa kilikuwa ni taarifa ya habari ya Chanel ten ile ya saa moja,uzuri ilikuwa ikiishia yani inafika tamati,wakati nilisubiri iishe dakika kadhaa sauti ya careen ikamtoka.
"gao nakuomba mara moja unisaidie."aliita na mimi nikamfata tu walikuwa wamekaa wawili ila kila mtu na daftari yake.
"naam unasemaje,"
"nisaidie,hili swali linanisumbua sana."aliniogopesha kuniambie nimsaidie swali, mana kichwa changu chenyewe ndio hicho naenda shule sina nijifunzacho naenda ilinionekane ninaenda tu ushahidi kuondoa ujinga tu.
"swali gani hilo?"niliuliza nikijihami kama ni hesabu nijue namkimbia vip, nilipanga hata nimdanganye naenda chooni mkojo umenibana.
ila ikawa tofauti pale nilipoangalia swali lenyewe ni somo la kingereza ambalo kidogo nilikuwa nikielewa japo kidogo sio sana vya kupata mia darasani.
nilichuka daftali yake kuangslia zaidi linahusu nini.
"sasa unasimama nitaelewa vipi si uiname au kaa hapa kabisa unielekeze"alisema careen hapo nikaamua nikae baada ya kuangalia swali lenyewe ni kuhusu language use matumizi ya since na for,unless na if, although,despite inspite, niliyatazama kwa makini maswali yale,nikiwa kimya mana swali lilitaka kugeuza inspite of kwenda kuwa despite.
"mbona unatazama nisaidie pengine wakauliza hata kesho kwenye mtihani wenu,.
"nilianza kushirikisha ubongo wangu unipe jibu ila nikawa nachemka ubongo haukuonesha ushirikiano wowote kwangu ulikuwa ukiniacha nishiriki mwenyewe pengine ni kutokana na kutokuwa makini darasani pale walumu walipo kuwa wakihimiza.
swal liliuliza>> We walk on,unless it was raining.
aliniambia niigeuze sentensi hiyo, kusema ukweli sikuwa nkijua hata nikitaka kujaribu, sipati jibu sahihi hivyo ilinibidi nikodoe macho tu kama emoj ya wasap,.
"mbona hujibu nisaidie basi"alizidi nihimiza nilijibu hapo mimi sina cha kujibu nimepoa tu.
"chakula tayari njooni tule"nilishukuru pale Ester alipotuita kwa chakula ndio ikawa pona yangu nisiaibike pale.
nikawa wa kwanza kuamka kisha nikaenda, wakati huo nae neema akaja alitusalimu huku akisema kachoka, tuliendelea kuongea pale huku tukimeza chakula mpaka tunafika tamati nilikuwa nimeshiba vya kutisha nikanawa na kuamka moja kwa moja chumbani kwa nikachukua sare zangu za shule kwenda kuzifua,nilitoka nazo mpaka uwani kisha nikaanza kufua, huku muda ukisogea hima hima mpaka namaliza kusuuza kimya kishaingia,hapo nikaingia ndani, muda huo sikuwaona wote zaidi ya shangazi nikaamua kujumuika nae aliniuliza maswali kadhaa kama nimefunga mlango nilimwambia nimefunga nae alikuwa akiangalia tamthilia anayo ipenda inayoruka startv, nilianza kumchokoza na maswali yangu nikimtaka aniambie juma ni nani yangu yule baba anae ishi na mama ambaye ananitesa hasa kile kipigo cha siku ile,shangazi alionesha kikwazo mpaka akaanza kunambia sasa na mimi nikatega sikio kumsikiliza akaanza.
"gao mwanangu baba yako alikufa kipindi hicho, baada ya yeye kufa ilikuwa simanzi sana mana aliacha pengo ambalo halikuwa na wakuliziba, alikuwa tegemezi la familia, sasa alipokufa,juma ambaye alikuwa ni mdogo wake baba yako,alileta mzozo kutaka kumrithi mama yako......
"aling'ang'ania sana kuwa na mama yako mana kabira letu linaruhusu kurithi wake wa marehemu, kipindi hicho mama yako alikuwa yatima hata kwa kukaa, hata kwao alipoteza wazazi.."alipofika hapo kidogo roho iliniuma sana hata machozi yakinilenga tayari kutoka.
"mwanangu familia ilikubari juma amrithi mama yako na akarithishwa mama yako nae hakuwa na sababu ya kukataa ilimbidi akubari tu ndipo miaka hiyo wewe ulikuwa hujui kitu na umri wako wa darasa la pili."aliongea shangazi, nilihisi uchungu kumbe baba yangu kafariki na mama yangu kurithiwa na juma daah ilinisikitish japo sikuonesha wazi shangazi kuniona,nikihudhunika moyoni.
kisha tukaongea machache nikaingia kulala huku nikiwa na mawazo msururu.
Nilipoingia ndani na kujitupa kitandani usingizi haukunijia kutokana na mawazo nilikuwa nikitafari kifo cha baba yangu kiliniuma zaidi ila sina jinsi nilianza kutafakari nikifikilia kumbe juma alikuwa akinipiga vile bila huruma kwa kuwa mimi sio mwanae ndio mana hakunionea huruma hata kidogo, nilitafakari na chuki juu y juma,ikameza moyo wangu hakika nilimchukia sana mpaka nikafika mbali na kusema.
"au kamuua baba ili amrithi mama yangu,"nilizidi kujifakamiza maswali ambayo hayakuwa na majibu wakati huo, nakumbuka niliutafuta usingizi il sikuupata ulinijia usiku mwingi sana tena bila kutegemea.
Asubuhi niliamka, tayari kujiandaa kisha nikafanya kama kawaida yangu kila siku ndani ya nusu saa nishajiandaa na kuelekea shule kwa mwendo wa hatua ndefu na kutokuangalia nyuma nikitembea kama gari ya mwendo kasi, nilifika shule bila kuchelewa hata namba hazikuwa zimehesabiwa hivyo nilichukua namva pale na moja kwa moja nikaelekea eneo la usafi kama siku zote huko sasa nikakutana na frank aliekuwa anafagia baada ya kuniona akaacha na kunifata.
"oya gao vipi mwana."
"safi nambie frank"
"daah, safi tu jana lusinde si amekusanukia mwana."alisema frank hapo akanishangaza ya kutosha ikabidi nimchape na swali.
"lusinde kanisanukia vip frank"nikauliza.
"jana sijui ulitoroka bas kuna mda kabla hatukuruhusiwa kwenda nyumbani alikuja class akaanza kuku tafuta alituuliza wote tukamjibu hatujui."aliniambia frank, tangia hapo alinibebesha mzigo wa hofu niliyokuwa nayo,.
"daaah, mwanangu si msala huu lisinde hana dogo yule,liponiulizia baada ya kunikosa akasemaje."
"oooh,alikasirika hakuongea kitu ila kavimba huyo daah kama andazi lililotia hamira ya kuzidi"
"hahahahahahaha,frank acha masihara"nilicheka nikifurahi baada ya frank kumsema lusinde.
"ndio kaumuka kweli,"
"daah, kaka msala huo akinidaka yani huyu ticha anajifanya kunifatilia sana,"nilisema.
"kweli mwanangu yani siku kadhaa nimekuja namuona anakufatulia sana kama mwanae"
"huyu dawa yake ndogo sana, nitamkomesha."nilisema kwa kujiamini.
"kaka wataka umfanye nini huyu ticha."
"haha, siri ya mtungi utajua tu subiri."
"acha kunificha mwana."alisema frank.
"bas ngoja nikushirikishe nitakuambia cha kumfanya huyu."
Tuliendelea kuongea ila maongezi yetu yakakatishwa na mwalimu aliekuja eneo hilo hapo ndio tukatengana kumpumbaza mwalimu asije kujua kama tulikuwa tunaongea, baada ya kutengana killa mmoja akaokota fagio zilizokuwa chini pale kisha tukaokota ili kufagia dakika kadhaa kengere ikagongwa moja kwa moja tukajumuika paredi wanafunzi wote kusikiliza matangazo ya siku hiyo tuliamlishwa na vilanja hakukua na uwepo wa mwalimu yoyote hivyo alisasa mbele kilanja wa zamu na kuongea.
"Habari wanafunzi wenzangu kwa niaba ya mwalimu wa zamu kaniambia nimiruhusu muingie darasani kusubiri mtihani unakuja, pia anaomva mtulie amikute mmelala juu ya meza zenu,sawa"alisema kilanja yule wa zamu akiwa mbele ya hadhira ya wanafunzi hapo akaamlisha kisha akaturuhusu tuingie darasani tulimtii kwa kuingia darasani, baada ya kuingia hatukutulia kufatisha alivyosema kilanja maagizo toka kwa mwalimu, tulianza kufatana nilianza mimi kwa kumfata frank hapo tukaanza kupiga story huku tukicheka.
"mwanangu daah, jana kisanga yani nikikuka dah, natamani ijirudie ile kitu."niliongea kumwambia frank.
"nini hiyo jamaa"aliuliza frank hapo nikiwa tayari kuwambia juu ya nilichofanya na madam,ila kabla sijamwambia mwalimu akaingia hapo nikikimbia haraka sehemu yangu.
"habarini wanafunzi kaeni tayari kwa mtihani mabegi yenu na daftali zenu toa nje zote sawa"aliongea msimamizi siku hiyo alikuwa wa kiume sio madam hivyo utan utan hakuna.
Alianza kugawa karatasi hatimae tukapata wote kisha akaamuru tuanze nilianza kwa kukiamini ulikuwa mtihani wa historia nilianza kufanya kwa kuangalia maswali yenyewe kama kawaida nilikimbilia nyuma kwenye section ya mwisho nilihisi kuchanganyikiwa mana maswali yote hakuna nililokuwa nikirijua nilishia kutazama tu hasa zile essay ndio kabisa sina ufundi nazo yani naweza jifananisha na mbumbbu yani kichwani mwangu hakukuwa na kumbu kumbu yoyote ya kuhusu elimu ni vitu vichache ndio navijua ila vyengine hapana sikuvijua.
ilikuwa essay ya scramble for and partition of africa ilinishinda hapo milichoamua ni kufata section Akuchagua nako hali haikuwa tofauti maa kila nikiangalia kama yanajibika wapi haku niliamua nijilalie juu ya meza yangu eti niijiaminisha material yatakuja bila kusoma nilala muda mrefu,sana na kujisahau.
"Muda umeisha kusanya karatasi, muamshe huyo alielala."ilisema sauti ya mwalimu niliyoisikia kwa mbali hapi nikaamka tu mwenyewe, yani nilipata hasara sikujaza hata swali moja zaidi ya kuandika jina tu, yani niliullaum usingizi mana nilijihesabu nisha fail, nilikusanya kisha kuupotezea mtihani nikatoka nje bila kumstua frank hapo moja kwa moja nikakaa eneo lenye mawe nilikaa nikitafakali mustakabali wangu na wanawake wakati nikiendelea kutafakari mara viganya lain vikayafunga macho yangu, nilishindwa tambua alienifumba mpaka pale alipoamua kuniachia ndipo nikamuona sasa.
"Huyoo muone hata hakunijua kama ni mimi"aliongea Grace huku akitabasam na kutuo vishimo kwenye mashavu yake,nilikuwa sijamjua kama ni yeye hivyo baada ya kukaa story zikaanza nilimumba animalizie mkasa wake nae akakubali akaanza kuongea.
"Gao, ally ni mpenzi wangu tena yupo kidato cha nne ally nilimpenda na yeye akanambia anamipenda sikujua kama ananidanganya, niliendelea kumpenda huku kila siku tukiongozana kuja shule na pia mara moja moja kutoka, ally alichonifanyia sikuamini ila nampenda sana na nitazidi kuumpenda,"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho