WEKA YOTE (8)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Nilisikia kugogwa kwa mlango ila sikujali ilikaa kimya tu, mpaka mgongaji akaacha pengine ni maumivu aliokuwa akiyapata pale anapogonga.
Nilijifanya kama sijui kilichotokea shule ilinimsahau grace hata taswira yake sikuivuta tena.
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
"Daaah mapenzi kitu gani kama ipo ipo tu, ya nini nijiumize kisa mwanamke na wakati wapo wengi."nilisema na kuamka kitandani japo nilimpenda sana ila nilijivua tu pendo.
Nilikaa ndani muda mchache nikisubiri Ester amalize kufanya usafi, ndipo nikamkumbuka mdada wa jana alietaka kunigonga na gari lake bahati mbaya, akanipa hela pamoja na namba za simu, nilianza operesheni ya kuitafuta nguo niliyovalia jana mana ndio niliweka pesa aliyonipa nilitafuta hadi nikachoka kila nguo sio ndio nikakumbuka nguo chafu nilitia kwenye ndoo na ndio ile nguo ipo humo humo na ndoo ipo nje, nilifungua mlango haraka haraka na kutoka nje hadi kufika kwenye ndoo na kuanza kupekua nguo zangu hadi kuiona ile pesa hapo roho ikatulia nikarudi ndani wakati huu sikufunga mlango nikarudishia tu.
Nakuanza kuzihesabu zilikuwa noti za elfu kumi kumi zipo kumi na mbili yani laki na ishirini nilifurahi mnoo na kuziweka ndani ya begi langu la nguo,kisha nikaanza kuvua nguo zangu za shule na kiziweka juu ya enga iliyopo chumbani kwangu zilikuwa hazikuchafuka, wakati huo nikatoka hadi valandani Ester hayupo anaosha vyombo niligundua kutokana na kusikia mgongano wa sahani za dongo na vikombe.
nikakaa na kuiwasha tv siku hiyo sikupanga kurudi shule kabisa siku hiyo niliamua kupoteza muda kwa kutizama runinga,muda nao ukaanza kusogea mpaka kufika mchana Ester alikuwa busy muda wote mpaka mchana ndio akamaliza kupika na kutenga mezani nikaenda kula.
"wewe gao mbona leo mapema alafu ulikuwa haupo sawa nini shida."alisema ester.
"amna kawaida ondoa shaka."nilimtoa wasi wasi aliokuwa nao,akatulia hakuongea tena akaendelea na shughuli zake.
Na mimi nikaendelea na kula hadi kumaliza nikaelekea chumbani kwangu kulala.
Nilikaa kwanza nilipo kosa cha kufanya nikaamua nilale tu, kikapita kimya cha muda wa masaa kadhaa hadi kujakustuka tayari nilikuwa nimelala sana niliamka na kuelekea bafuni kuoga, niliingia nikaoga hadi nikamaliza nilingia chumbani kwangu nikavaa nguo zilizo nipendeza nikachukua na zile pesa kisha nikatoka valandani muda huo saa kumi na mbili giza ndio linaingia hakuna alierudi sii shangazi na wanae wala neema kutoka chuo,aliekuwepo ni ester tu.
"ester hivi hawajarudi tu."
"hawajarudi neema aliniambia atachelewa kurudi leo."
"na shangazi nae.?"niliuliza.
"yeye hajasema ila nilipoongea nae sijui alisema atapitia sehemu na wanae"
"sawa "niliitika nakuendelea kutizama tv, tayari nikamkumbuka mama imma akili yote ikahama kwake nilikaa pale hadi kufika saa mbili usiku nikamuaga ester na kutoka nje nikiwa na nia ya kwenda kwa mama imma.
Nilitembea hadi kufika katika eneo la boda boda nikapanda ilinipeleka kwa mama imma nilipanga nisifike kwetu sikutaka nikutane na baba nilimchukia mnoo.
Mwendesha boda boda alinifikisha hadi mitaa ya kule nyumbani kwa mama imma ambako ndio kwetu, sikuenda haraka haraka nilitembea kwanza mpaka kufika saa tatu nikijua kuwa imma atakuwa kalala, nikanyata hadi dirishani.
"mama imma,mama imma, mama imma,"niliita dirishani kwake.
"weee nani hapo dirishani."nisauti ya mama iliyonitisha mpaka nusu haja ndogo inimwagike tena kibaya zaidi yupo na shangazi..
Nilisimama kama mti uliokauka unaongoja kukatwa au kidondoka,mama na shangazi walianza kunifata wakitaka kunijua mimi nani,kitendo hicho kiliperekea nichomokome haraka kama gari lililoko mwendo kasi na break kukatika, kitendo cha kukimbia ndio ikawa afadhali yangu mana ilikuwa kidogo mama anione.
Mbio nilizotoka nazo pale,zilienda kukomea karibu na barabara ya magari nikaanza kuhema juu juu mithili ya mwizi aliewaponyoka watu wenye hasira kali waliotaka kuuondosha uhai wake baada ya kuiba vyao.
Nilienda mpaka upande wa pikipiki nikapanda kurudi nyumbani,masaa machache tu ilinifikisha karibu na nyumbani nikashuka na kumlipa kisha akaondoka na mimi nikauendea mlango na kuingia ndani.
"mamboo gao watoka wapi.!"ni sauti ya neema akiniuliza,nikafikiria uongo wa kumdanganya.
"oooh nilikuwa juu hapo napiga misele tu."nilidanganya nae akakubali tukaa pamoja kwenye makochi tukipiga story na kucheka.
Dakika kadhaa shangazi akaingia na wanae wawili niliotambulishwa hapo awali kuwa ni doreen na careen.
"shikamoo kaka gao"walinisalimia kwa pamoja nami nikawaitikia kumbe walisha nijua tayari ujio wangu,nilimsalimu shangazi akaitika na kukaa kochini.
"Ester "aliita, shangazi.
"abeeeeh dada."
"niletee maji ya baridi"
"sawa dada alafu chakula tayari hamieni huku."alisema ester hapo wote tukaelekea meza ya kulia chakula,shangazi nae akapewa maji yake akaanza kunywa huku kila mmoja akijipakulia chakula chake mwenyewe kinachomtosha.
"haya mwanangu gao za tangu juzi.?"
"salama shangazi za huko utokapo."
"salama unapaonaje hapa nyumbani."
"pazuri shangazi."tulizidi kuongea na shangazi , huku vikisikika vijiko vinapo gonga sahani wakiwa kimya tu wapo busy na kutafuna,story za pamoja zikaanza.
Msimuliaji alikuwa careen alietusimulia kichekesho kilicho tuweka wote midomo wazi kwa vicheko,story ziliendelea hadi wote kumaliza kula kisha kila mtu akaelekea chumbani kwake kulala baada ya kutakiana usiku mwema.
Niliingia chumbani kwangu nikajiandaa kwa ajili ya kesho,niliweka kila kitu sawia kuanzia mavazi ya shule na vitu nyengine vihusivyo shule sanjari na kupaka kiwi viatu vyangu kisha nikajilaza kuitafuta kesho,kiza kilitawala.
Nilikuja kustuka kutokana na mlango kugongwa na jina langu kuitwa na sauti nilioinakiri kichwani alikuwa ni Ester akiniamsha.
"Gao,gaooo, amka kumekucha muda wa shule huu."niliisikia kwa mbali kama mtu anae ninong'oneza,alizidi kuita mpaka nikaamka na kuitika ,huku najivuta vuta kwa uchovu nikijinyoosha mwili.
Nikachukua mswaki na kuvaa taulo nikielekea bafuni kuoga upesi upesi nikaingia na kujiandaa haraka kukimbizana na muda dakika tano zilitosha kunifanya nitakate kisha nikatoka na kuingia chumbani kwangu kujiandaa nilivaa sambamba na upakaji mafuta mpaka namaliza nikatoka na kumuaga shangazi tulieongozana akitokea ndani kuingia chooni nilimuaga kisha nikatoka nje na kuelekea shule.
Njiani nilianza kukumbuka tukio la jana lililotokea kwangu lilizidi kuniumiza moyo,ila sina jinsi niliendelea na safari mpaka kufikia eneo la shule kengere maalum kwa ajili ya namba iligongwa nikaelekea eneo la kuhesabiliwa namba, baada ya kupata namba nikaelekea darasani siku hiyo ilikuwa ni zamu yangu katika usafi wa darasa hivyo sikufika kabisa katika eneo la nje,nilibaki darasani na usafi kuendeleaa nikiwa na wenzangu, tulimaliza kufanya usafi tayari na kukaa humo humo darasani.
"eheeeeee.!gaoo umekuja mwenyewe leo,nilisema utakuja hapa ni mtoni lazima uje kama si kunywa maji,utakuja kuchota kama si kuchota utakuja kufua."ni maneno aliyosema sir lusinde mkononi akiwa na viboko vyake hapo nilikuwa natetemeka kwa woga tu.
"Jana ni nani alikupa idhini ya kuondoka shule muda ule kabla ya kuruhusiwa."alinitandika swali ambalo lilikuwa gumu kujibika haswaaa,nilishimdwa kujibu nikawa namtizama tu.
"mbona hujibu ndio dharau au umekuwa asaivi."aliniambia,na kunisogelea karibu.
"hapana sir."
"hapana nini wewe mjeuri eeh ngoja nikuoneshe ujeuri leo,nifate ofisini."akitoa kauli na kuondoka,na mimi nilianza kuzuga zuga nikisita kwenda mana shughuli yake sio ya kitoto,sikumfata nilipoteza nuda kadhaa
"gaoo unaitwa na sir lusinde."alikuja mwanafunzi wa kidato cha kwanza niliemtambua kwa sale yake ya tofauti na mimi ambayo ni ya kidato cha kwanza yake rangi ya kaki na yangu kijivu kijivu,nilizidi kuchanganyikiwa kitendo cha kutuma mtu aniite ndio haswaa kilinitisha, niliganda ganda hadi kupata uamuzi nikamfata.
"wewe nimekuita saa ngapi,hadi utumiwe mtu ndio uje sio."alisema kwa jazba sir .
"haya lala chini lala chini."alinilaza chini kwa fimbo za bega mpaka nikalala,hapo alipata uwanja alianza niteremshia fimbo zisizo na idadi hata wiki zililipita tena kwa hasira hakuchapa sehemu yake alikuwa akinipiga kiunoni.
"aaaah sir sasa unanichapa wapi huku."
"unasemaje wewe umekuwa si ndio"aliniambia na kuendelea kunichapa,alinichapa fimbo za kutosha.
"sasa adhabu yako uhamishe kifusi cha udongo ujaze pale kifusi kikubwa mikokoteni mitatu."alisema maneno mfurulizo,alinipa kazi nzito ambayo sijawahi ifikiria kabla kama nitaifanya.
"nenda store kachukue chepe jembe na ndoo"
"sawa."nilijibu kifupi,nilienda nae mpaka store ajanikabidhisha vifaa na kunionesha eneo la kuchimba.
"haya chimba hapa ukajaze kifusi ole wako usaidiwe unaanza upya sehemu nyengine."aliniambia,daah nikifikilia mikokoteni mitatu ni udongo mwingi sana na itanichukua muda mrefu kumaliza,nilianza kuchimba na jembe ili kurahisisha nikitumia chepe.
kengere ya paredi iligongwa nikiwa pale pale mpaka wanaingia darasani nipo pale pale tu.
kazi ilikuwa ngumu upande wangu sijawahi ifanya ila nilitumia jinsia mwanaume yani uwanaume wangu kuifanya unajua mwanamke na mwanaume ni tofauti sana hivyo nilitumia nguvu za kiume kuifanya hiyo kazi kila mwanafunzi anapita hakuacha kunipa pole wengine wakiuliza kosa langu nililofanya ila sikuwa nikiwaambia, kazi ili hadi kubakisha mkokoteni mmoja na nusu hapo nimechoka tayari,nikauendea mti uliokaribu na eneo lile kujituliza tu.
Madamu alikuwa anakuja eneo hilo kwa mwendo wa madaha kiasi kwamba anaogopa kukanyaga chini,alikuwa akitokea nyumbani kuja shule,alinifikia na kunishika shavu.
"oooh gao i mis you upo wewe."aliniambia mkono mmoja akiwa kauweka shavuni kwangu,nilikosa cha kumjibu nikiomba aondoke tu pale ila haikuwa hivyo alizidi kuongea maneno ya ajabu.
"gao leo usiku nataka uje kwangu si utakuja eeh,nikuandalie nini."aliongea,mara ghafla sir lusinde akatokea eneo lile madam alipomuona akazuga............
"ooooh gao adhabu kakupa nani muda wa vipindi
huu."alizuga madam na hakusubir sir afike pale
hivyo akaondoka haraka, kuniachia mimi msala, sir
nae akawa kashafika pale tayari.
"kazi yangu umemaliza"ndio swali aliloanza
nalo,pale na mimi nikajiuma uma.
"aaa bado sir."nilijibu kwa wasi wasi."
"hujamaliza?, ulikuwa unaongea nini na madam
hapa."
"hatukuongea kitu zaidi ya kuniuliza adhabu kanipa
mwalim nani muda wa vipindi."nilidanganya bila
kujua kumbe katuona kuanzia mbali.
"Ndio amekushika mpaka shavu sio,!"
"hapana sir nilimwambia najisikia vibaya kichwa
kinasumbua ndio akaniangalia joto."niliongea kwa
wasiwasi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni