MUUZA UBUYU (12)

0
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Baadae ziliungana na kuunda USA mnamo mwaka 1787 ambao walikuwa ni wakulima na wenye viwanda hii baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wakulima na wamiliki wa viwanda mwaka 1861/65 baada ya kuisha kwa vita hivyo USA iliweza kuingia katika maendeleo ya viwanda na kuiwezesha kushindana na mwingereza kwanzia karne ya 20"

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Nilipomaliza utangulizi niliona wanafunzi wakinipigia makofi

"Hongera emmy kweli unasoma, haya wengine" alinipongeza mwalimu na hii yote hakufundisha ila mimi tu nilipenda kutumia vitabu mblimbali kuandaa notes.

Baada ya mwalimu kutoka darasani wanafunzi wengi walinifata kuomba notes zangu wakaandike hivyo mmoja aliona vyema atumie ubaoni kuandika notes baada ya mwalimu kuzipitisha.
*************

Nilikuwa mkimya mno nikisoma simulizi za mejah the plan boy ambaye mara nyingi uandika ktk page yake ya dimbwi la simulizi, kila mara zote anazotoa mwendelezo nimekuwa nikifatilia maana napenda sana fasihi maana ndicho kitu ninachosoma na uwependa kukosoa baadhi ya waandishi ambao hawafati kanuni za kiuandishi na wasiopenda kubadilika. Wakati namalizia kusoma simulizi ya " utamu wa mchezo" nilisikia simu yangu nyingine inaita ya line ya halotel. Nilikimbia fasta kuipokea sikufanikiwa kuigundua ni namba ya nani maana ilikuja bila jina.

"Emmy upo wapi? Ilisikika sauti nzito

" nipo nyumbani wewe nani?
Niliuliza kwa uoga kidogo

"Mimi ni rafiki yako, napenda uniite rafiki" aliongea yule mtu

"Sikujui wewe rafiki umenifahamu wapi?

" hahaaa emmy muuza ubuyu nakufahamu napenda kukwambia kitu emmy" iliongea ile sauti na kuendelea kunitisha

" kitu gani?

" emmy una mkono wa pesa, nyota yako inang'aa na usidhani wanaume wanakutaka bure kuna kitu wanapata kutoka kwako"
Alizidi kunitisha

"Wewe mbona sikuelewi"

" unaweza usinielewe leo ila kesho utanielewa ila kuwa makini kwani huyo elly amefanikiwa mambo mengi kupitia wewe hivyo nyota yako kali sana emmy"

Nilibaki mdomo wazi na kuanza kujiuliza kuna ukweli gani juu ya anayoongea yule kaka rafiki. Nilipoita sikuweza kupata mwitikio kwani simu ilikuwa imekatwa tayari.

Nilijiuliza maswali mengi sana baada ya simu kukatika yule kaka rafiki ni nani? Ila sikupata majibu niliendelea kuwa mpole nikarudi mezani taratibu nikashika simu yangu kubwa ikabidi nizime data maana hapo awali nilikuwa nasoma simulizi za mejah the plan maker.
"Mungu wangu leo tarehe 20 siku zinazidi kwenda karibia nifanye mtihani wangu wa kumaliza kidato cha sita eeh mungu wewe ndiye unajua maisha yangu natamani siku moja nifike chuo kikuu udsm"

Nilikuwa na determinations/matarajio makubwa hasa mbele yangu ni ili la kufika chuo akili na mawazo yangu yalikuwa uko tu. Nilitazama ratiba yangu nilikuwa natakiwa nisome geography, akilini mwangu nilitaka nisome geography2 maswali ila nilitazama mzigo niliokuwa nao geography 01 nikazuta begi langu nikatoa kitabu kilichoandikwa na zisti kamili cha physical geography nikaanza kusoma theories za structure of the earth nilianza na isostancy theory, kisha plate tectonic theory nikajihisi usingizi mzito nikaegemea kwenye kiti nikapitiwa na usingizi, ilikuwa michale ya saa7 usiku.
***************

05:43
Nilishtuka kutoka usingizi ndipo nilipogundua kumbe nilala palepale nikanyanyuka huku nikihisi mgongo unaniuma sana, ingekuwa siku za kawaida ningeenda kulala lakini mitihani inakaribia sikuweza kulala kabisa niliingia bafuni nikawasha maji ya uvuguvugu nikaoga ili mwili upate nguvu kisha nikarejea tena mezani kwaajiri ya kuendelea na ratiba yangu.

Ile asubuhi nilipitia topics za pratical geography hasa map na statistics nilihisi sehemu hiyo ndiyo nilikuwa na mapungufu mno, sikupenda kupoteza muda wangu kuwaza mengine ilibidi nizime simu kisha nisome intensive/kiundani maana kama nikiacha simu on atakurupuka jimmy atapiga au willy na sasa huyu aliyenipigia jana anayenipa stress kumfikiria ni nani/kaka rafiki nae ameongezeka hivyo nikikaa kuwafatisha sitafika mbali au malengo yangu ya kufika university of dar-es-salaam hayatatimia.

Nilisoma sana na niliona raha bado ya kusoma maana kuna raha ukisoma kitu alafu ukakielewa, ilifika saa moja kasorobo nikatoka mezani kisha nikaosha vyombo vyangu na kuanza kufanya usafi nyumba nzima kabla sitoa mapazia na vitambaa kwa ajiri ya kufua. Haikuwa kazi rahisi niliitaji yamkini kupata dada wa kazi lakin naye atafanya nini pale ndani na uku kazi nilihisi naweza kuzimudu mimi mwenyewe. Wakati nafanya usafi nilikumbuka kitu kilichonifanya nikae na kutafakari "hivi mimi nina maadui wengi sana? Ni nani anayeniandama hivi kila siku yanaibuka mapya nina nini mimi? Uenda anachosema kaka rafiki kweli inawezekana nina nyota kali maana sio rahisi wanaume waning'ang'anie mimi tu haya jimmy, willy na elibariki kuna kitu hapa" nilimaliza kuwaza kisha nikasimama na kuendelea na mengine.
**********************

Nilifika eneo ambalo jimmy aliniomba nifike japo nilitoa udhuru nyingi ila alinisihi hata kwa dakika kumi tu kisha nitaendelea na ratiba yangu nilikuwa suprised/shangazwa baada ya kuona duka zuri la nguo za watoto/baby shop za kila aina ambapo pia waliuza sabuni, maziwa ya lactose, pampers na kila kinachoitajika kwa watoto kwanzia mwezi mmoja mpaka miaka 7, kila aliyeniona alishangaa sikuweza kujua kwa haraka haraka wanashangaa nini ila inaonekana ujio wangu ulikuwa tayari umeshajulikana.
Baada ya kuzunguka duka zima jimmy alianza kunieleza baadhi ya mambi kuhusu kazini kwake.

"Unajua emmy wewe ni mwanamke wa ndoto za wanaume wengi, ufanani na mazingira uliyokulia kusema ukweli toka ile siku ya kwanza nilipokuona tukishughulikia suala lako lile(kesi ya sam) nilitokea kuvutiwa na wewe nikamwambia willy naye pia alionyesha kukubaliana nalo ila kumbe naye moyoni anakupenda sikujua, akaamua kuniwahi ila kwangu sikukata tamaa nimeamua kukuonyesha ni jinsi gani nakupenda nakupa duka hili liwe lako bby"

"Wow! Nashukuru kwa kuwa muwazi hata willy pamoja
na kufanya yote aliyofanya hakuwahi nitamkia kuwa ananipenda nakushangaa wewe kwa ujasiri wako" niliongea kwa ujasiri huku namtazama usoni nilimuona akitabasamu.

"Naomba nikubalie emmy"

"Usijari ila kusema ukweli mimi nina mtu ninayempenda yule sam niliyewahi kuwaambia hivyo nisingetamani anione msaliti na hapo badonatoka na elibariki kimakosa sitamtendea haki sam na elibariki eti kisa hawapo na pia utu wangu nitaonekana kama najiuza tu"
Niliongea huku machozi yananilenga.

"Hapana emmy hii itakuwa ni siri kati yetu hakuna atakayejua"
Alibisisitiza sana huku aking'ang'ania mkono wangu

"Hapana jimmy wakina emmy wapo wengu unawexa mpata mtu mwenye sifa kama zangu cha msingi usiwe na haraka ili kumpata"
Niliongea kabla sijaingia ndani ya gari yangu tayari kuondoka

"Pleaseee emmy nakusihi"
Sikutaka kumpa tena second chance nikaondoka

Akili na moyo vikawa vinashindana moyo unasema "chukua duka na alikuahidi nyumba ya kuishi na mama yako mdogo kubali" na akili inaniambia "no kumbuka wema wa elibariki usimsahau sam mtu unayempenda kwa dhati hayo ni yakupita hata kwa nguvu zako utapata siku moja" niliendasha gari nikiwa na migogoro nafsia ni lipi nifanye lipi niache. Mara nikasikia simu yangu inaita ilikuwa kwenye handbeg, moja kwa moja nilijua ni jimmy sikupokea ikaita mara ya pili nikiwa kwenye jam nikapokea ilikuwa namba ngeni.

"Nani mwenzangu"

"Rafiki yako, naitwa kaka rafiki"

"Eeh jamani wewe unanitakia nini lakini"
Niliongea huku nalia

"Usilie emmy napenda kukumbusha hao wanaume sio wazuri kwako jitenge nao" aliongea kaka rafiki

"Kwanini unafatilia maisha yangu wewe mkaka"

"Kwasababu wewe ni rafiki yangu'

" mimi sio rafiki yako nakuomba futa namba yangu"
Nilikuwa mkali kwake

"Sawa ila willy naye ataandaa mtego kwa ajiri yako kuwa makini, jioni njema"

"Kaka rafiki, kaka rafikiiiiii" niliita bila mafanikio

Niliwaza mtego gani ambao willy anataka aandae kwa ajiri yangu sikupata jibu hapo nilikuwa fire nilisikia simu inaita tena. Niliona jina pale willy "inawezekanaje hii" niliwaza kabla sijapokea sasa cha ajabu nilitazama kushoto nikamuona willy kwenye gari la pembeni yangu nilishtuka mno...

Nilitazama pembeni yangu nikamuona willy akaniangalia na kutabasamu huku simu yake ikiita bado , nilikumbuka maneno ya kaka rafiki nikaanza kuhisi jambo juu yake. Mara taa iliruhusu tupite nikapita nikielekea kariakoo niilitaza site mirror sikuweza kuona gari la willy nikajua tumeachana palepale fire, nilipita msimbazi hapo katikati nikaona carpets nzuri za uturuki nilitafuta parking nzuri ili niingie dukani na pia nilikuwa nahitaji nipite bookshop ninunue reviews za masomo yote kwanzia geography1&2, histry1&2, language1&2 na general studies.

"Habari za leo" nilisalimia

"Salama dada karibu" aliitikia muuzaji ambaye alikuwa ni mdada km mwarabu aliyechanganyika na uswahili

"Naomba hiyo carpet ya pink yenye mistari ya reds na purple"
Alisogea kunitolea carpet mimi nilichukua simu yangu na kujaribu kuangalia maana kuna jumbe zilikuwa zinaingia wakati nipo nadrive sikupata bahati ya kuzisoma. Zilikuwa ni nyingi mno kuna wateja wangu wa ubuyu, willy, jimmy na salma zikuzifungua kutokana na muda kuwa mdogo.

"Dada iangalie" aliniita yule mdada kunifanya niachane na simu nitazame yeye.

"Hiyo ni shilingi ngapi dada? Ilisikika sauti nyingine ya pembeni ila bado ckuitilia maanani

" ni laki nne na arobaini ila bei inapungua" alijibu yule dada

"Dada nimeipenda hii nipunguzie" nilijaribu kumuomba hapunguze bei.

"Hii hapa dada nimeshamlipia" aliongea yule kaka nikashangaa mno niligeuka kumtazama vizuri alikuwa ni willy.

Nilibaki mdomo wazi nikashindwa nisemaje kwa muda ule nilimtazama nikamtazama yule mdada muuzaji aliyekuwa anamwambia mkaka mmoja anibebee lile zuria mpka nitakapomwambia aliweke.

"Dada una usafiri? Aliuliza yule mdada sikumjibu bado nilikuwa nashangaa na willy alionyesha tabasamu pana mno ila mimi nikakumbuka maneno ya kaka rafiki " willy atakuandalia mtego kuwa makini" nilipokumbuka hivyo nilimgeukia yule dada muuzaji.

"Dada nashukuru naomba mpeni aliyelipia, willy asante ila sihitaji kwa sasa" nilimjibu willy na kuondoka kuelekea garini.

"Kuna wanawake wasumbufu namna hii" aliongea willy na kuondoka pia kuja upande wangu lile zuria likabaki mgongoni kwa yule kijana.

"Please naomba usinisumbue willy nilihitaji msahada wenu wakati nina kesi yangu, mmeshindwa kunisaidia mnaleta mapenzi mwambie na mwenzako mimi sina njaa kihivyo kama mna moyo wa kusaidia mkasaidie watoto yatima msinisumbue tena" nilimaliza nikafunta gari na kulock milango yote.

Nilihisi kichwa kinauma nikamuitaji sana kaka rafiki angalau anipigie simu anielekeze cha kufanya maana nilihitaji mfariji kwa wakati huu ila ckuwa nae hivyo kaka rafiki nilihisi ni mtu anayenitakia mema mno.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)