MAHABA NIUE (4)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
"namuona"
"Mi namfuata"
"hahahaha Ramsey kausha bana humuwezi"
"embu niangalie mimi. najiamini tulia hapa nisubiri potelea mbali hata niki sikia sauti yake nita furahi"

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII

SASA ENDELEA...
Ramsey aliinuka kweny kiti kile na kuanza kumfuata mama yule aliye kua ameshuka kweny gari la kifahari.

kitu kingine ambacho kilicho kua kina mfanya apate mademu ni ujasiri aliokua nao hakua na kitu kuogopa mtoto wa kike katika maisha yake.

"Anti anti. ndio wewe samahani kidogo"

Ramsey aliita huku akizidi kumsogelea Mama yule

"sijui naku fananisha au?"
"inawezekana YOU NEVER KNOW"
""tusha wahi kuonana mahali kuna biashara tusha wahi kufanya"
"mmmh mi ni mfanya biashara ndio inawezekana cause huwa nina meet na watu wengi ndani na nje ya nchi"
"ofisi yako iko wapi?"
"posta"
"enheeeee basi yaah nisha kumbuka tayari. sasa nipatie business card yako kuna biashara nataka tufanye tena"
"okay well wait kidogo"
Mama yule alifungua pochi yake na kumpa kadi yenye namba za simu
"asante sana"

Ramsey alita basamu na kumgeukia prosper ambae alikua ana mwangalia akiwa mbali na kumpa ishara ya dole gumba kuashiria kuwa kila kitu kimeenda sawa.

ALirudi na kukaa kwenye meza na prosper ambapo hapo tayari nyama choma ilikua mezani walianza kula huku wakinywa na bia taratibu huku stori zikiendeleana tayari ilikua ime timu saa mbili usiku
.
"hivi Ramsey?"
"nambie"
"ao mademu una otembea nao kaka una kumbuka CONDOM?"
"condom natumia ila ina tegemea na demu mwenyewe.ila mara nyingi huwa natumia. alafu badilisha stori tule nyama hapa"
"okay haina noma'"

waliendelea kula nyama zile ila Ramsey anatoa simu yake mfukoni baada ya kuita ila anaganda juu ya kioo cha simu kwa muda kidogo akiwa haamini mtu anaye mpigia aliiangalia kioo cha simu kiliandikwa EYMER KWAY.

aliipokea huku akitabasamu na kuiweka sikioni.
"kway kway vipi mwanangu ndo umeingia nini?"
"ndo nipo eapot sasa hivi"

uliongea upande wa pili wa simu iyo

"karibu Tanzania ndugu yangu nipo DDC hapa nakula vyombo"
"upo DDC ?, agiza kreti nyingine mbili za bia hapo nakuja na shemeji yako sasa hivi..naenda kumchukua home"
"poa poa mwana njoo kaka nita furahi sana"

wali kata simu na Ramsey kuonekana kufurahi sana.

"huyu mwanangu sana anaitwa Eymer Kway aisee yaani hapa akija hapa hatu toki sasa hivi? "
"ame tokea wapi kwani?"
"Uganda uganda ndo ameingia leo"

"kwaio ndo tuna msubiri"
"ata kuja we uta mwona"

Ramsey aliendelea kunywa pombe huku akiwa na furaha sana.

tayari ALTEZA nyeusi iliegeshwa pembeni ya baa hiyo na mtu aliye shuka kwenye gari hiyo alielekea moja kwa moja kwenye meza aliyo kaa Ramsey.
"Kwaaaay ayayayayaya ndugu yangu"

Ramsey aliropoka kwa nguvu na kumkombatia rafiki yake huyo huku akimpiga piga mgongoni na kufurahi huku wakizidi kuvutana vutana mikono

"Ramsey jembe langu vipi lakini?"
"safi tu.. huyo ndo nani tena?"

Ramsey ili bidi ahoji alivyo muona msichana amesimama nyuma ya Kway.

"huyu shemeji yako anaitwa Joylah,
Joylah meet my Friend Ramsey"
"nashukuru kuku fahamu shemeji Yangu Joylah mimi ndo Ramsey au Ramsoooo wana niita"

Joyla ali tabasamu kusikia vile na kufanya vishimo yaani dimpoz ziingie ndani na kuzidisha uzuri wake.

"Kway shemeji mzuri"
"kausha basi Ramsey nili kwambia uagize kreti za bia ziko wapi?"
"Mi nili jua uli kua una zingua"
"we mshamba nini, nipo sirious bana nataka leo tule gambe mpaka asubuhi"

Kweli Kway alimaanisha alicho fanya alimuita muudumu na kumwambia aweke kreti mbili pembeni yao.
"pesa kaka"
"nita kupa"
"nipe sasa hivi"
"bei gani?"
"kreti mbili elfu themanini"
Pale pale Kway alitoa wallet na kumu hesabia Ela muhudumu yule huku akimkabidhi pesa zile.
"Ila kway hii sehemu si salama unajua"
"si salama kivipi?"
"kuna kua kuna fujo sana vibaka usiku huu"

Kway alimuangalia Ramsey kwa kitambo na kupandisha tisheti yake juu kidogo na kufanya Ramsey atoe macho baada ya kuona bastola ndogo pembeni ya kiuno cha Kway ambapo baadae alifunika na tishert

"kaka una nitisha mambo yako sio madogo"
"hapa amani ipo nipo kamili gado "
"stori vipi ivi bado una tunga?"
"ndio natunga namalizia kitabu kina choitwa MAHABA NIUE niko na jamaa mmoja ana itwa SUNDAY J MUNA . facebook tafuta page story za KWAY utajua mengi.Mpigie simu shem aje basi"
"ahaaa okay poa"

Ramsey aliji fikiria kwa kitambo ampigie simu nani na kumkumbuka Monalisa msichana mwenye asili ya kiarabu kwa mbali .

huyo ndiye hupenda kuwaonesha marafiki zake wengi katika matukio kama hayo sababu moja tu msichana huyo hujua sana kupangilia nguo.

"Love njoo DDC hapa ,ndio kariakoo chukua hata taxi. eeeeh ndio pale pa siku ile .. sasa hivi mke wangu oga chap chap.. nakusubiri nakupenda pia"

Ramsey alikata simu na kumgeukia Joylah
"shemeji vipi mbona kimnya?"
"Amna mbona nipo tu"
"upo ndio ila husemi kitu"
"nasikiliza tu maongezi yenu shemeji"

"baby leo hunywi?"
Ramsey aliuliza baada ya kumuona Joylah hanywi.
"okay subiri. nishajua dawa yako. muuhudumu embu njoo mara moja"
"naam kaka"
"leta Catton mbili za reds weka hapa juu ya makreti"
"Lakini Lav"
"Noo muhudumu leta haraka"

Pombe zili letwa na wote kuanza kunywa huku Prosper akiwa tayari chakali.

Ramsey aliba ki akishangaa hasa alipo muona Esta kwa mbali ana kuja haku taka kuamini alijua wenda pombe zime mpanda kichwani ila ana fikicha macho na kumuona tayari keshafika mezani.
'huyu demu nani kamuita tena'?

aliongea kimoyo moyo Ramsey na tayari Esta alifika meza ile aliyo kaa Ramsey na kuvuta kiti.

"ume juaje nipo hapa?"

Aliuliza Ramsey huku akiweka tabasamu la uongo.

Kway aligeuka na kumuona Msichana yule na kujua ndiye aliye pigiwa simu muda mfupi na Ramsey.

"shemeji karibu vuta bia hapo tunywe"
"Asante glass iko wapi?"

Glass ili letwa pale na Esta kumimina bia ile kwenye glass.

Ramsey jasho lilianza kumtoka hasa kwa mbali alivyo muona Monalisa ana kuja meza ile walipo. alicho fanya alisimama na kuelekea chooni akikwepa balaa litakalo mkuta pale na kujua kivyovyote angewa gonganisha wasichana hao.

aliwaaga na kuwaambia kua ana elekea chooni

"Ram Ram.."
Monalisa aliita huku akiwa kwa mbali aligeuza shingo kwa Esta na kukuta akimuangalia kwa macho makali sana.

"nisubiri pale nakuja"

alitoa agizo ilo na Monalisa kwenda kukaa meza aaliyo kua amekaa Ramsey na akina Esta.

"OYA KAKA MTOE ESTA KWENYE IYO MEZA FANYA JUU CHINI ATAHARIBU SHUGHULI"
ulikua ni ujumbe wa meseji ambao Ramsey aliuandika akimtumia prosper.

"HILI ZALI UKIKIMBIA HAPA NDO UTAARIBU WEWE NJOO MIMI NITAJUA CHA KUFANYA"
"HUYO ESTA MIMI NAMUELEWA "
"KAKA WEWE NJOO"
"OKAY POA"

ili mbidi Ramsey apige moyo konde na kurudi mezani na kukaa akiwa kimnya sana na kutoweza kuongea maana alijua akiongea chochote ata julikana

"baby mbona kimya"?

tayari Esta alianza na kumfanya Monalisa akae kimya asikilize ata kacho jibu Ramsey.

"Fresh tu kwani vipi?"
"huyu nani?"
"esta siki...."
Prosper alidakia alivyosikia swali lile ili kumsubaisha
"sija kuuliza wewe funga bakuli lako"
"huyo nani Ram?"
"anaitwa Monalisa"
"kwani vipi?"
ilibidi Monalisa nayeye aliulize alivyoona mambo yabapoenda sio.
"nawewe nyamaza"
"ninyamaze ? we umevurugwa nini?"
"nani kavurugwa?"

Tayari Esta na Monalisa walianza kupandishiana maneno kwa sauti ya juu.

Ramsey alivyoona ivyo ili bidi ainuke na kuelekea msalani ili kuepuka balaa lile ambalo moto wake asingeweza kuuzima haraka.

ila alipo fika msalani anaganda baada ya kumuona msichana mmoja ametoka maeneo ya chooni huku akiwa na kimini aliji kuta akimshangaa sana kutokana na pombe alizokua nazo kichwani aliji kuta nayeye anaingia choo hiko cha kike aki mfuata msichana yule.
alimshika kiuno na kufanya msichana yule aruke kidogo ila Ramsey alimtuliza baada ya kumvuta shingo yake na kuanza kumpa denda huku akizidi kumsogeza ukutani.

alichukua mkono wake na kupandisha sketi ambapo alikutana na chupi na kuisogeza pembeni huku zoezi la kuchezea ikulu ya msichana huyo kuanza . msichana huyo alianza kutoa miguno huku akizidisha kumpiga denda Ramsey na taratibu kuanza kumvua tshirt Ramsey..

"Baby,khaaa !!"

Esta aliita baada ya kutokea nyuma yake na kumfanya Ramsey ashtuke huku akimshangaa Esta baada ya kuwafumania



Msichana yule ambae aliyetoka kupigwa denda na Ram aliona aibu na kuanza kuvuta vuta sketi chini na kutaka kutoka ila ana zuiwa na Esta na pale pale Esta kumpiga Kofi lililompata vizuri juu ya shavu na kumfanya dada yule ashike shavu lake na kuinamana chini kutokana na kofi lile kumuingia.

"Esta una mpiga msic.....puupuuu"

Ramsey nayeye alipokea makofi ya usoni bila kutegemea kutoka kwa Esta.
"Msen***** nini.! una taka kusema nini ?, Una jifanya malaya si ndio"?

"sio ivyo baby wangu"
"Mimi sio baby wako tena twende huku nika malizane na yule kahaba wako uniambie mimi na yule nani una taka ubaki nae"

Kweli esta alimvuta mkono Ramsey kwa nguvu huku

wakimuacha msichana yule akilia chooni baada ya kupokea kofi kali kutoka kwa Esta.

Ramsey alivutwa msobe msobe mpka kwenye ile meza waliyo kua wame kaa mara ya kwanza.

" wewe kahaba wa kike. huyu hapa baasha ako. una sema una mpenda sema akusikie"

Esta aliongea kwa Jazba huku akipigapiga mguu mmoja chini na kumuangalia Monalisa huku akisubiri jibu.

"Ram mbona siku elewi lakini, huyu nani mbona ana nitukana hivi"?

Ki ukweli Ramsey hakua na cha kuongea alikua kama amewekewa uji wa mtama mdomoni aliji kuta mdomo una kua mzito na kubaki kuwaangalia wote wawili.

"Lakini esta sasa si ukae chini tuya malize hapa"
Aliongea prosper kwa sauti ya chini nayeye kusimama

"nawewe fala nyamaza wewe mnafki sana wewe. Huna lolote una jua alicho kua anakifanya huko bafuni?,Fala sana wewe tena una bahati nakuheshimu hapa kuna wageni leo ningeanza nawewe matako"

Safari hii Esta alipaza sauti na watu wa baa ile kuanza kugeuka na kumuangalia anavyo ropoka.

"Ramsey nambie ukweli kama unan....."

Mona lisa aliongea ila alikatishwa uko-fi aliorusha Esta na kumpata Monalisa na kumfanya ayumbe yumbe na kufakamia meza ile iliyo kua na vinywaji na bia kuanza kumwagika.

Monalisa nayeye hakuku bali nayeye alirusha kofi na kulijibu ambalo lili mfikia pia Esta juu ya shavu.

purukushani ile ilianza makofi kuanza kurushwa huku na kule

"Esta tulia kuwa mstaarabu"
"Hakuna cha ustaarabu hapa..niache Ramsey nimuoneshe huyo kahaba wako."

Esta haku ridhika aliona chupa ya bia na kuishika ambapo aliirusha kwa nguvu usawa wa Monalisa kwa bahati nzuri Mona lisa aliiona na kuinama kidogo ambapo ilipita na moja kwa moja na kutua kichwani kwa JOYLAH demu wake kway na kumpasukia kichwani.

Joylah alidondoka chini pale pale na damu kuanza kuruka.

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAM👇BONYEZA HAPA

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)