MAHABA NIUE (6) JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... "Kumbe baby ukivaa ivyo una pendeza eeeh?" "Duuu kweli leo nime pendeza" Alichukua moka na kuivaa mguuni. bila kusahau marashi aliji pulizia na kujiweka tena sawa. "Funguo uta weka pale kwa siku zote" KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... "Poa..sasa unywi chai?" "nita chelewa nita kunywa huko napoenda" Alitoka nje na kuangaliana na Mama khadija "umependeza sana wapi iyo?" "Naenda Mwenge mara moja" Ramsey alijibu huku akiendelea kuondoka alipo fika mbele kidogo alitoa wallet yake na kuonekana kama aki tafuta kitu baada ya kukiona alitoa. ilikua ni business kadi iliyo abdikwa NISSAN SALES AND BUYING . aliyo pewa na Mama yule siku ile pale baa DDC . aliangalia vizuri namba zile na kuziingiza kwenye simu ali hakikisha vizuri kama ndo zenyewe na kuzipiga. "Halloo naongea na meneja wa kampuni ya NISSAN?" Aliongea Ramsey huku akiwa han…