SEHEMU YA SABINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Simu ya jamaa ikaita, akaitoa kwenye koti lake, akaipokea nakuiweka sikioni mwake, akazungumza kwa lugha ya kiarabu, nikastukia kumuona jamaa akichomoka kwa kasi, ndani ya chumba pasipo kuniona nyuma ya mlango, ving’ora vya gari za polisi, nikaanza kuvisikia na kunifanya nishushe pumzi nyingi, na kujikalia chini, huku jasho jingi likimwagika.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Ndani ya dakika kadaa askari kadhaa wakawa wameingia katika sehemu tulipo, dorecy na phidaya wakatoka bafuni, askari na madaktari walio salimika katika vamizi la majambazi hawa
***
Wagonjwa tulio salimika tukahamishwa kwenye hospitali moja, inayo milikiwa na jeshi la nchi ya philipines, matiibabu yangu hayakuchukua muda mrefu sana, nikaruhusiwa kutoka hospitalini na kuhamia kwenye hoteli ambayo phidaya anaishi kwa siri sana, na amelipiwa gharama zote na dorecy ambaye tayari amerudi kwa mume wake.
“phidaya,itatubidi turudi tanzania”
Nilizungumza huku macho yangu yakimtazama phidaya aliye jilalia kiuvivu kwenye kitanda, huku akiwa tumbo wazi akilichezea chezea kwa kiganja chake tumbo lake lenye kiumbe ndani
“si usubiri niweze kujifungua kwanza”
“hatuwezi kuishi hapa, pasipo sisi kuwa na kazi, unadhani tutayamudu vipi haya maisha?”
“sawa mume wangu, je tukirudi huko tanzania, tutafikia wapi wakati umesha sema kwamba mama yako alitekwa na baba yako mkubwa”
Nikamtazama phidaya kwa muda, kwani kitu alicho kizungumza kinamaana kubwa sana kwangu, isitoshe sijajua ni hali gani inayo endela kati ya mzee godwin na mama yangu.Nikanyanyuka taratibu na kuisogelea computer iliyopo kwenye meza humu chumbani kwetu, ambayo imeunganishwa na huduma ya internet.Nikaiwasha taratibu, baada ya muda nikafungua mtandao wa google
“unataka kufanya nini?” phidaya alizungumza huku akipiga hatua na kuja kukaa kwenye kiti nilicho kikalia mimi
“kuna mtu nataka kumtafuta”
“nani?”
“baba yangu mzazi, anaishi afrika kusini”
“mmmm sawa”
Nikaliingiza jina la baba yangu mzazi kwenye sehemu ya kutafutia, kwenye mtandao huu ambao unasadikika ndio mtandao mkubwa duniani kote, ulio kusanya mambo mengi sana, ndani ya sekunde kadhaa nikawa nimefanikiwa kulipata jina la baba yangu mzazi pamoja na historia yake, cha kumshukuru mungu nikakutana na taarifa nyingine iliyo nipendezesha moyoni mwangu, kwani ameingia kwenye orodha ya matajiri kumi nchini afrika kusini huku yeye akiwa nafasi ya nne kutoka juu.
“inabidi twende nyumba ni kwa baba”
“sawa mume wangu”
Phidaya hakuwa na pingamizi na maamuzi yangu niliyo yachukua, nikaanza kufwatilia hati za kusafiria kuelekea afrika kusini, kutuokana na pesa ambazo dorecy anatusaidia, sikupata tabu sana katika kukamilisha maswala usafiri wa ndege.Siku ya pili tukakusanya kila kitu kilicho chetu kwenye hoteli ambayo tunaishi, tukakodi tanksi hadi uwanja wa ndege, muda wa kupanda ndege ulipo wadia, tukaungana na wasafiri wengine na kuingia ndani ya ndege, na taratibu safari ikaanza, huku moyoni mwangu nikimuomba mungu atufikieshe salama, kwani kumbukumbu za ajali iliyo tokea nchini kenya kipindi nikitokea afrika kusini, inaendelea kuzunguka ndani ya kichwa changu kama mkanda wa filamu.Phidaya kwa kudeka muda wote kichwa cheka amekilaza kifuani mwangu, huku akiimba nyimbo za kunibembeleza kwa sauti ya chini
“baby” nilimuita kwa sauti ya upole
“mmmmm”
“naomba niende msalani”
“sawa, ila usichelewe mume wangu”
Phidaya alinijibu taratibu huku akijinyanyua, kifuani kwangu taratibu, nikasimama, na kuanza kupiga hatua za kuelekea chooni, nikaingia ndani ya choo na kumaliza haja zangu zote, nikanawa uso wangu ili kuutoa uchovu na usingizi unao ninyemelea usoni mwangu.Nikafungua mlango, gafla nikastulia kitu chenye ncha kali kikinikita mgongoni mwangu, na sauti ikasikika kutoka nyuma yangu
“tulia kama ulivyo upo chini ya ulinzi, mr eddy”
Mwili ukanisisimka na kujikuta nikitulia kimya, huku kwa mbali mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ila sauti niliyo isikia nyuma yangu haikuwa ngeni masikioni mwangu, nikatamani kugeuka na kutazama nyuma ila sikuwa na uwezo kutokana nipo chini ya ulinzi wa mtu huyu.
“oya wewe bwege kweli, kijiko pia kinakutisha”
Mtu aliye nyuma yangu alizungumza huku akizunguka na kuja mbele yangu, macho yangu yakakutana na john, rafiki yangu wamuda mrefu tangu tukiwa shule ya sekondari, akiwa amevalia mavazi maalumu kama watumishi waliopo kwenye hii ndege, nikashusha pumzi nyingi na kubaki tukitazamana.Tabasamu likatawala usoni mwa john na mimi pia nikajikuta nikitabasamu na kukumbatiana naye huku tukipigana pigna migongoni kwani, nimiaka kadhaa imepita pasipo sisi kuonana
“eddy mwanangu, aahaa nikitambo sanaa”
Johna alizungumza kwafuraha huku tukiachiana
“kweli mwanangu, haya mbona huku tena kwenye ndege?”
“ndugu wee acha tuu, maisha mwanangu yanabadilika”
“ndipo unapofanyia kazi?”
“nipo training(mafunzo), napata pata ujuzi”
“pcb wewe umekuwaje, umekuja kwenye ndege huku, au ndio hiyo elimu ya tanzania, hkl anakuwa mkaguzi wa fedha, wakati mathematics amenyoosha mswaki?”
Nilizungumza kwa utani huku nikiwa nafuraha usoni mwangu
“ahaaa kaka, ndio maana yake, huku tumeingia hivyohivyo tuu, tena kwa masaada wa mama yako ndipo aliniunganisha huku”
Taarifa ya john ikanistua kidogo nakujikuta nikaanza kumfkiria mama yangu
“mama yangu yupi?”
“haaa kwani eddy wewe una mama gani mwengine?”
“hapana nimekuuliza hivyo kutokana nina maana yangu?”
“mama yako ambaye kwa sasa ni waziri wa usafirishaji, ametoka kwenye kitengo cha afya”
“unataka kuniambia kwamba mama yangu yupo hai?”
“ndio yupo hai, tena yeye anakutafuta wewe”
“john umeniacha njia panda hemb……..”
Sikuimalizia sentesi yangu, msichana mmoja aliye valia mavazi kama john, alimuita john kwakutumia lugha ya kingereza
“am coming”(ninakuja)
John alimjibu msichana aliye muita huku akimtazama usoni mwake
“sasa eddy, ngoja mimi nikaendelee na majukumu ndugu yangu”
“sawa ila kaka nahitaji tuzugumze zaidi”
“usijali kwani wewe unaelekea wapi?”
“afrika kusini, kwa mzee”
“mzee gani tena, kwa maana baba yako amefungwa?”
“eheee”
“kwani eddy ulikuwa wapi siku zote”
“john”
Sauti ya msichana aliye muita john mara ya kwanza ilisikika tena, ikimuita kwa msisitizo
“kaka baadaye”
John aliondoka kwa kupiga hatua za haraka kwenda katika sehemu alipo itwa, nikashusha pumzi kwa mara nyingine, huku kichwa changu kikiingia mawazo mapya katika maisha, kwani kwakipindi hichi, nilichokaa mbali na nchi yangu sikujua ni mambo yapi yaliyo endelea kwenye nchi yangu, na pia sikujua ni kitu gani lilichotokea kati ya mama yangu na mzee godwin, baba yangu mkubwa ambaye kwa mara ya kwanzi nilidhani kwamba ni baba yangu mzazi.Nikarudi kwenye siti yangu, huku nikiwa nafuraha usoni mwangu
“mbona umechelewa kurudi ulikuwa na nani?”
Phidaya aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikajikuta nikitabasamu kwa furaha na kumtazaka usoni mwake
“mke wangu, ninafuraha wee acha tuu”
“furaha gani tene hiyo?”
“kwanza nimekutana na rafiki yangu wa kipindi kirefu sana”
“nani?”
“nitakuambia tukitulia”
“ahaaa eheee, sawa bwana”
Phidaya alizungumza kwasauti yakudeka huku akigeukia uapande wapili wa siti yake, nikaupitisha mkono wangu mmoja kwenye kiuno chake na kumvuta karibu yangu na kichwa chake akakilaza kifuani kwangu taratibu
“umekasirika?”
“ndio”
“nisamehe mke wangu”
“sikusamehe, hadi uniambie umekutana na nani?”
Nikamuadisia phdiaya, historia fupi kati yangu na john, nikamuelezea kuhusiana na maisha ya mama yangu japo hakunieleza kwa undani, sana kuhusiana na maisha yaliyo jitokeza kwenye familia yangu ila moyoni mwangu kidogo nikipata matumaini yakumuona mama yangu, hadi namaliza kumuadisia phidaya, mwenzangu tayari usingizi umepitia nakulala fofofo.Baada yamasaa kadhaa, sauti ya msichana ilisikika kwenye vipaza sauti vilivyomo ndani ya ndege, akituomba tufunge mikanda kwani ndege ipo karibuni kutua katika uwanja wa ndege wa ‘johannesburg’.Ndani ya dakika kadhaa ndege ikatua kwenye uwanja na abiria wakaanza kushuka mmoja baada ya mwengine, john akafika hadi kwenye siti yetu, ambapo ametukuta tunatoa toa mabegi yetu katika sehemu ambayo tumeyaweka
“huyu ndio, john ambaye nilikuwa nikikuambia”
Nilimtambulisha john kwa phidaya
“john huyu ni mke wangu, anaitwa phidaya”
“ahaaaa, habari yako shemeji”
Phidaya na john wakasalimiana kwa muda huku wote wakiwa wanafuraha, john akatuomba tumsubiri nje ya uwanja, yeye nawezake wakimalizia hatua za makabidhiano ya ndege, nawahudumu wengine ambaoa watarudi kwenye safari ya mzunguko wa ndege hiyo.Tukakaguliwa mimi pamoja na mke wangu phidaya, tukatoka nje ya uwanja wa ndege na kutafuta sehemu yakukaa, ndani ya dakika kumi na tano john akaja katika sehemu tuliyo kaa, kutokana ipo wazi sana kwa watu kutuona
“jamani, sijui nyinyi wezangu munaelekea wapi?” jonh alituuliza
“sisi tunasafari yakuelekea kwenye cap town”
“munaonaje tukafikizia hotelin leo, kisha kesho muweze kwenda kwakutumia usafiri watreni za umeme”
John alitushauri, sikuwa nakipingamizi kutokana hatukumaliza mazungumzo na john juu yakitu ambacho kimetokea kwenye maisha ya miaka michache iliyo pita, tukakidisha taksi iliyotupeleka kwenye hoteli moja iitwayo ‘mondior concorder’ iliyopo pembezoni mwa barabara ya albetina sisulu, tukafanikiwa kupata vyumba viwili vyenye hadhi nzuri kwawageni kulala
“baby mimi najisikia kuchoka, nitapumzika zangu ndani”
Phidaya alizungumza mara baada ya kuingia katika chumba tulicho chukua
“kwanini?”
“ kuna chakwanini wakati nimekuambia kwamba nimechoka, hivi unadhani hili jitoto lako humu ndani halinichoshi?”
“mmmm mke wangu na wewe kwakudeka, haujambo”
“nini”
“yaishe mama kijacho”
“wewe niudhi tuu”
Phidaya alizungumza huku akijilaza kitandani taratibu, kwa jinsi mwili wa phidaya ulivyo umbika, umekuwa nikivutio kizuri kwangu ambacho sichoki kikitazama kila muda na dakika zake zinavyo zidi kukatika
“kweli hapa nimepata mke”
Nilijisememea kwasauti yachini chini, nakumfanya phidaya kunitazama kwamacho makali, akaachia msunyo mkali na kujiweka vizuri kitandani, kutoka tayari kumeshaanza kupambazuka, sikuona haja ya mimi kuendelea kulala kitandani, kusimama kwenye dirisha la chumbani chetu lenye kioo kikubwa, na kuaanza kuuangalia mji huu jinsi ulivyo jengeka kwa majengo yaliopo kwenye mpangilio mzuri
“huji kulala hapo umesimama kama mshumaa wapasaka, maana yake ni nini?”
Phidaya alizungumza huku akitumbulia macho yake, makubwa kiasi
“mke wangu saa hizi, saa kumi na mbili na nusu, nitalala nini?”
Phidaya akajifunika kwashuka gubigubi, kwa jinsi ujauzito wa mke wangu ulipo fikia, unampelekesha kama mtoto mdogo kwani kila analo lifanya nikituko kwangu.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com