MAHABA NIUE (11) JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... Kwa mbali sana Ramsey alianza kusikia kama kuna mtu ana gonga mlango ila alipuuzia mlango ule una endelea kugongwa na kumfanya Ramsey asitishe zoezi lile. KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... "Nini tena Ram?,Mbona una penda kuninyima raha?" Alilalamika Doreen "Kuna mtu ana gonga mlango" "Mtu gani Ram hakuna mtu atakae kuja sasa hivi" Sauti ya mlango ili sikika tena na kumfanya Doreen akae kimnya aki subiri tena akidhani labda ame sikia vibaya mlango ule ulizidi kugongwa tena. Jasho jembamba alihisi lina mtoka na kuanza kuhisi tumbo la kuhara bila kujua tumbo lile limeanza saa ngapi wakati alitoka kwake ubungo akiwa mzima wa afya. alifunga vifungo vya shati na kubaki kutumbua mimacho aki muangalia Doreen "Sasa ina kua kuaje? huyo ata kua nani?" "Ata kua mume wangu" Ramsey ali siikia maneno yale kutoka kwa Doreen na kumfanya azidi kupagawa sana h…